MAKAMBA vs SHY-ROSE UVCCM Dodoma, Kulikoni?

MAKAMBA vs SHY-ROSE UVCCM Dodoma, Kulikoni?

Subirini Makamba atakavyomjibu huyo Shyrose wenu, last time alimwambia anavaa nguo fupi sana na ana hawara CHADEMA!!. Tusubiri safari hii atatoka vipi huyu mgosi. Makamba bwana!!!
Duu, hii sikuwahi kuipata. Makamba alisema lini kwamba Shy Rose anavaa nguo fupi na ana mahawala CHADEMA?
 
mimi sikubaliani na hoja ya Makamba kutimuliwa abaki hadi 2015.

Na hapo CDM hata hawatahitaji miujiza, ikulu mwaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
Kikaango cha mafisadi in da haus
 
Makamba anafaa wacha aendelee kuiharibu sisiem ili tondo yetu itimie
 
Huyu Shy-Rose ana zaidi ya 44yrs. Kwa wazazi wake alikokulia ni mtaa wa Miti Mirefu Mwanza, alisome Nyakahoja P/School miaka hiyo ya '80. Yeye alikuwa amenitangulia madarasa na mimi nina over 40yrs sasa, yeye je? Kamekula chumvi kibao anastahili kuitwa Bibi kama angekulia kijijini!

Tulikuwa naye kwenye kikosi cha "chipukizi wa mkoa wa Mwanza" enzi hizo za kamanda Marehemu Gupta, baada ya vita vya Kagera! Sijajua CCM vijana ukomo wa umri ni miaka mingapi! Enzi za Mwalimu limit ilikuwa 35yrs. Kwa sasa sijui!

Hivi Gupta alikuwa mwanza vile ama! mimi nilimkta Kilimanjaro miaka ya 84!
 
Makamba alisema ukweli hawara yake ni MR II wa cdm!
 
Mimi huwa sipotezi muda kusoma mambo ya Umoja wa Vichaa wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM).
 
Jamani wameanza tena? Yaani hawataki tujadili hoja za msingi wanataka tuwajadili wao...shit..WATANZANIA TUWAKATAE HAWA...
 
Wajumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) wa Dar es Salaam katika kikao chake kilichofanyika jijini leo April 2, 2011, wamemtaka Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba, kujiuzulu kwenye nafasi hiyo kwa kuwa mzigo kwa chama tawala.

Kikao hicho kimefanyika kwenye ofisi kuu ya CCMn ya wilaya ya Kinondoni.

Wajumbe hao wa UVCCM Dar es Salaam wamemkataa Makamba na kusema kuwa utendaji kazi wake ni mbovu ndani ya chama.

Hatua hiyo inafuatia tathmini ya uchaguzi mkuu wa 2010 ambapo CCM ilifanya vibaya na kupoteza kura nyingi za Urais na majimbo mengi ya Ubunge kwa vyama vya upinzani.

Pia, wajumbe hao wa UVCCM walirejea hotuba ya Mwenyekiti wao wa taifa, Jakaya Kikwete, kuwa CCM inahitaji mabadiliko na kuvua gamba, na kusema kuwa mabadiliko yaanze kwa Makamba kung'oka kwenye nafasi yake ya uongozi.

Katika kikao cha leo, wajumbe wengi waliochangia walimnyooshea kidole Makamba kutokana na utendaji usioridhisha.

Mjumbe wa UVCCM, Shy-Rose Bhanji, alisimama tena kama alivyofanya hivi karibuni Dodoma mbele ya Makamba mwenyewe na kuendelea kumchana kiongozi huyo.

Bhanji alisisitiza kuwa muda umefika sasa kwa Makamba kuachia ngazi kwa vile hatoshi kwenye nafasi ya katibu Mkuu wa CCM.

Nao wajumbe wengine wa UVCCM walisimama na kuunga mkono moto uliowashwa na Bhanji na kusema kuwa Makamba amekuwa mzigo kwa chama na sasa ni muda muafaka kwake kupisha damu mpya ili kuleta uhai kwenye chama.

(Source: Wajumbe wa UVCCM Dar es Salaam)

Hivi huu ni mpambano ukweli au fix? Wana ubavu gani hao? Makambaq ni mteule wa rais/ mwenyekiti wa chama kwa nafasi hiyo. Si wamwabie mhusika amtoe? Mbona wanazungukazunguka?
 
Acha wajitengenezee uadui ndani ya chama??wakipasue!!
 
Ongelea hoja iliyopo usiongelee vitu au mtu,

mimi sikubaliani na hoja ya Makamba kutimuliwa abaki hadi 2015.

Precisely!!! Nakuunga mkono mkubwa!!! That will quicken the CCM death!!
 
jaman 2angalie huku na huku! Shyrose co kjana! Sura imemkongoroka vle ana ujana gn jaman? Labda km ni mcmamiz wa hao vjana! Yule ss ni m-mama!
kweli yaelekea wewe mdada ni mrembo sana, yaani mpaka unamponda shyrose! du. Natamani ningepata number yako ya simu

kila siku huwa naombaga makamba abaki hapohapo CCM mpaka 2015, ili JK atakapofikia mwisho wa uongozi wake basi na CCM iishie hapo.
Mh. Jakaya tunaomba usimtinui makamba kwenye ukatubu mkuu ili utakapomaliza muda wako iwe pia mwisho wa chama dhalim la CCM, Amen!
 
..Mzee Makamba awe mwangalifu ktk majibu yake.

..Shy Rose ukimtibua hachelewi kukutwanga masumbwi.

..aliwahi kumpiga mgombea ubunge mwenzake ktk ccm primaries zilizopita.
 
Ujenzi wa nyumba kila mtu na fito yake kivyake! Bado kitambo kidogo tu, jahazi litatota watu watagawana mbao. Hii kali kwelikweli, dau moja dua tofauti!!?
 
...Nahisi saaasa hivi Shyrose Bhanji 'atagundulika' kuwa kumbe sio Raia !
 
Natamani Makamba aendelee kuwa katibu wa Chukua Chako Mapema ili kazi iwe rahisi 2015 CHADEMA kushika dola kwani itashinda kiulaini uchaguzi mkuu.
 
Back
Top Bottom