MAKAMBA vs SHY-ROSE UVCCM Dodoma, Kulikoni?

MAKAMBA vs SHY-ROSE UVCCM Dodoma, Kulikoni?

hivi shyrose nae ni kijana? sijui katiba ya ccm inavyoprovide kuhusu umri wa kuwa uvccm.

nisaidieni wadau isije ikawa wanachakachua kila kitu

ninavyojua shyroz ni mjumbe maalum kwenye mabaraza ya vijana na uwt kama vile francis issack dc bunda anavyowakilisha uvccm akitokea baraza la wazazi....
 
hivi shyrose nae ni kijana? sijui katiba ya ccm inavyoprovide kuhusu umri wa kuwa uvccm.

nisaidieni wadau isije ikawa wanachakachua kila kitu
Ongelea hoja iliyopo usiongelee vitu au mtu,

mimi sikubaliani na hoja ya Makamba kutimuliwa abaki hadi 2015.
 
Wajumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) wa Dar es Salaam katika kikao chake kilichofanyika jijini leo April 2, 2011, wamemtaka Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba, kujiuzulu kwenye nafasi hiyo kwa kuwa mzigo kwa chama tawala.

Kikao hicho kimefanyika kwenye ofisi kuu ya CCMn ya wilaya ya Kinondoni.

Wajumbe hao wa UVCCM Dar es Salaam wamemkataa Makamba na kusema kuwa utendaji kazi wake ni mbovu ndani ya chama.

Hatua hiyo inafuatia tathmini ya uchaguzi mkuu wa 2010 ambapo CCM ilifanya vibaya na kupoteza kura nyingi za Urais na majimbo mengi ya Ubunge kwa vyama vya upinzani.

Pia, wajumbe hao wa UVCCM walirejea hotuba ya Mwenyekiti wao wa taifa, Jakaya Kikwete, kuwa CCM inahitaji mabadiliko na kuvua gamba, na kusema kuwa mabadiliko yaanze kwa Makamba kung'oka kwenye nafasi yake ya uongozi.

Katika kikao cha leo, wajumbe wengi waliochangia walimnyooshea kidole Makamba kutokana na utendaji usioridhisha.

Mjumbe wa UVCCM, Shy-Rose Bhanji, alisimama tena kama alivyofanya hivi karibuni Dodoma mbele ya Makamba mwenyewe na kuendelea kumchana kiongozi huyo.

Bhanji alisisitiza kuwa muda umefika sasa kwa Makamba kuachia ngazi kwa vile hatoshi kwenye nafasi ya katibu Mkuu wa CCM.

Nao wajumbe wengine wa UVCCM walisimama na kuunga mkono moto uliowashwa na Bhanji na kusema kuwa Makamba amekuwa mzigo kwa chama na sasa ni muda muafaka kwake kupisha damu mpya ili kuleta uhai kwenye chama.

(Source: Wajumbe wa UVCCM Dar es Salaam)
Kwani Shy-Rose ana umri wa miaka mingapi na kikomo cha umri kwa UVCCM ni miaka mingapi mi nadhani Shy-Rose anasitahili kuwemo kwenye UVCCM,huko kuna wafaa akina Jaffarai
 
jaman 2angalie huku na huku! Shyrose co kjana! Sura imemkongoroka vle ana ujana gn jaman? Labda km ni mcmamiz wa hao vjana! Yule ss ni m-mama!
 
Subirini Makamba atakavyomjibu huyo Shyrose wenu, last time alimwambia anavaa nguo fupi sana na ana hawara CHADEMA!!. Tusubiri safari hii atatoka vipi huyu mgosi. Makamba bwana!!!
Heheeee na kweli Shy si mfano wa kuigwa kwa vijana,matendo lazima yaendane na heshima ya mtu kwa hilo Makamba alisema ukweli japo ukweli unauuma mtu mzima anayevaa kihuni hastahili kupewa uongozi,
 
wakilisha dada tunataka vijana kama wewe wenye ujasiri wa kuongea ukweli. Usiyumbishwe na comments ambazo hazina kichwa wala miguu.
 
CCM wajipange vizuri ili kuanzia mwaka 2015 kiwe chama kizuri cha upinzani.
 
hivi shyrose nae ni kijana? sijui katiba ya ccm inavyoprovide kuhusu umri wa kuwa uvccm.

nisaidieni wadau isije ikawa wanachakachua kila kitu

Shy-Rose Bhanji ni mjumbe maalum wa UVCCM anayeingia kwenye Baraza la umoja huo kwa kuiwakilisha UWT mkoa wa Dar es Salaam. Ni kama Yusuf Makamba pia ni mjumbe wa Baraza Kuu la Taifa la UVCCM kupitia nafasi yake kama Katibu Mkuu wa CCM.
 
hivi shyrose nae ni kijana? sijui katiba ya ccm inavyoprovide kuhusu umri wa kuwa uvccm.

nisaidieni wadau isije ikawa wanachakachua kila kitu

nadhani umri si zaidi ya miaka35 ili kuwa uvccm. Ushangai akina Riz1 wanaitwa vijana? Ccm bana! Mi nataka abaki ktk ukatibu ili ccm ipotee kabisa.
 
Waacheni wakabane koo wakati sie tunaandika katiba mpya na 2015 tunachukua nchi swaaafi
 
hivi shyrose nae ni kijana? sijui katiba ya ccm inavyoprovide kuhusu umri wa kuwa uvccm.

nisaidieni wadau isije ikawa wanachakachua kila kitu
NA KINGUNGE JE!?? Tehe tehe!!!
 
Kwani Shy-Rose ana umri wa miaka mingapi na kikomo cha umri kwa UVCCM ni miaka mingapi mi nadhani Shy-Rose anasitahili kuwemo kwenye UVCCM,huko kuna wafaa akina Jaffarai

Huyu Shy-Rose ana zaidi ya 44yrs. Kwa wazazi wake alikokulia ni mtaa wa Miti Mirefu Mwanza, alisome Nyakahoja P/School miaka hiyo ya '80. Yeye alikuwa amenitangulia madarasa na mimi nina over 40yrs sasa, yeye je? Kamekula chumvi kibao anastahili kuitwa Bibi kama angekulia kijijini!

Tulikuwa naye kwenye kikosi cha "chipukizi wa mkoa wa Mwanza" enzi hizo za kamanda Marehemu Gupta, baada ya vita vya Kagera! Sijajua CCM vijana ukomo wa umri ni miaka mingapi! Enzi za Mwalimu limit ilikuwa 35yrs. Kwa sasa sijui!
 
jaman 2angalie huku na huku! Shyrose co kjana! Sura imemkongoroka vle ana ujana gn jaman? Labda km ni mcmamiz wa hao vjana! Yule ss ni m-mama!

Switi taratibu, jadili hoja siyo mtu. Una comment yeyote kuhusu UVCCM Dar kutaka Makamba ajiuzulu? Ndivyo JF inavyotakiwa ukitaka ukijana mbona hata Ngombare ni kamanda wa Vijana mkoa wa ..............................
 
Pia, wajumbe hao wa UVCCM walirejea hotuba ya Mwenyekiti wao wa taifa, Jakaya Kikwete, kuwa CCM inahitaji mabadiliko na kuvua gamba, na kusema kuwa mabadiliko yaanze kwa Makamba kung'oka kwenye nafasi yake ya uongozi.
hii kauli haitakua ya kinafiki kama na wale watuhumiwa wa ufisadi kama akina RA na EL nao watafukuzwa kwani kutakua ndio kuvua gamba, kama hawata liona hilo basi ni kweli sikio la kufa halisikii dawa.
 
Back
Top Bottom