MAKAMBA vs SHY-ROSE UVCCM Dodoma, Kulikoni?

MAKAMBA vs SHY-ROSE UVCCM Dodoma, Kulikoni?

Shy-Rose is an opportunist just like vibaraka wengi tu ndani ya CCM
In reality she does not care she just want any kind of a tittle to feed her empty stomach

* I know her for a long time way back... JUST ANOTHER OPPORTUNIST; Huyu sio kiongozi tunaotaka kuiongoza nchi hii na nieona watu wanataka ajiunge CHADEMA 4 what reason? let her stay CCM please...
 
Hata Makamba ni mzee, sasa naye alifuata nini hapo? mkutano wa vijana, wazee wanazozana. Kweli mwaka huu tutasikia mengi.

At least Makamba ni CCM Secretary General anaruhusiwa kuhudhuria mikutano yote ya jumuia ya chama cha CCM per CCM Manifesto
 
Shyrose is not type ya Wanawake/wasichana wa CHADEMA, Huwezi kumfananisha na Regia Mtema/Halima Mdee na wengine. She is an opportunist. Hatumhitaji.
 
sasa watamruhusuje kuhudhuria kikao wakati age yake ishapita huko si ndio kubebana kwa vigogo au katiba yao inaruhusu?
1st Shyrose is no more kijana she's 42yrs old so the topic bogus
 
Sunday, 20 March 2011 13:17 Habel Chidawali,Dodoma

KATIKA kile kinachoonyesha kuwa hali ni tete ndani ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), jana mkutano wa umoja huo ulitawaliwa na jazba huku, Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba na Mjumbe Shy Rose Bhanj wakitupiana maneno makali.

Habari zilizopatika kutoka ndani ya mkutano huo uliofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa White House mjini hapa, zinaeleza mvutano wa Makamba na mjumbe huyo uliibuka wakati Shy Rose alipokuwa akichangia mada kuhusu hali ya kisiasa na kusema viongozi ndani ya CCM ndiyo chanzo cha CCM kunyang'anywa baadhi ya majimbo katika Uchaguzi Mkuu uliopita.

Hali hiyo ilionekana kumkera Makamba ambaye alisisimama bila kufuata utaratibu wa kikao hicho na kumkatiza Shy Rose akisema kauli hiyo haina ukweli.

Naye Shy- Rose naye akitoa maneno ya kumpinga Makamba kabla katibu mkuu huyo wa CCM naye kuendelea kuzuia kuwatupia lawama viongozi.

Kuona hivyo, Kaimu Mwenyekiti wa UVCCM, Beno Malisa aliingilia kati na kuyazima huku kila mmoja akionekana kuwa na hamu ya kuendeleza ubishi baina yao, hata hivyo kikao kikaendelea na utaratibu wake.

Hivi katika hali kama hiyo ya kujibizana bila ustaarabu mbele ya watoto wake tena wanajibizana na mwanamama anayemweleza ukweli na tena pasipokufuata utaratibu wa kuzungumza kwenye kikao, sisi tuendelee kusema kuwa Makamba ana busara ya kuongoza chama tawala? Busara ya mzee huyu iko wapi hapa? Hivi hapo hakumdharau mwenyekiti wa kikao hicho?
 
Ndani ya suruali yake!!
 
huyu mzee bor apumzike , itamsaidia yeye binafsi, chama chake pamoja na taifa kwa ujumla, inaonekana maamuzi yake mengi watu wanayachukulia vibaya, kwa hali hiyo inakua vigumu yeye kukiongoza chama chake
 
Na hii kamati ya Bashe nikiiangalia ndio inaenda kumwaga Petrol kwenye jiko...ngojeni muone watakapomaliza round zao hapo July

(Mtoto uvccm? kumwelekeza baba nini afanye, Mama UWT? kumwelekeza Baba nini afanye)
Hivi kweli huyo Baba ni mjinga kiasi hicho?

UVCCM kupambana na kina Sitta, Sumaye

Sunday, 20 March 2011 21:40
Waziri wa Ushirikiano wa Afrika mashariki Samwel Sitta
Habel Chidawali, Dodoma na Ramadhani Semtawa
UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), umesema utahakikisha kwamba vigogo ambao wamekuwa wakizungumza nje ya utaratibu wa vikao wanatupwa nje ya ulingo wa siasa za chama hicho tawala.Kauli hiyo ilitolewa na Kaimu Mwenyekiti wa UVCCM, Benno Malisa wakati akisoma maazimio ya Mkutano wa Baraza Kuu uliomalizika jana mjini Dodoma.

Katika siku za karibuni baadhi ya makada wa CCM wakiwamo, Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk Harrison Mwakyembe, Mawaziri Wakuu wa zamani, Frederick Sumaye na Edward Lowassa wamekuwa wakinyooshewa vidole na baadhi ya wanaCCM wakiwatuhumu kuzungumza mambo ya chama hicho nje ya vikao.
Bila ya kuwataja majina vigogo hao, Malisa alisema tabia ya baadhi ya vigogo wa CCM kuropoka mambo nje ya utaratibu wa vikao vya chama, inaonyesha kuota mizizi hali inayokifanya kidharauliwe.Alisema wakati ukifika vijana watawataja kwa majina na kuwaambia Watanzania kuwa hao wamepoteza sifa za kuchaguliwa kwa kuwa hawana nidhamu ndani ya chama.

"Sisi vijana tunasema kuwa watu kama hao wasipewe nafasi kabisa ndani ya chama hiki. Nasema tutapigana ndani na nje ya vikao vya chama kuhakikisha kuwa watu wa aina hiyo hawapati nafasi yoyote ya kuchaguliwa," alisema na kuongeza,"Kama ni utovu wa nidhamu basi ni afadhali tuitwe sisi kwenye vikao vya maadili tukasutwe ila msimamo ni kuwa hatutakubali kulala usingizi na kuruhusu watu hao wapewe nafasi."

Alisema katika vita hiyo, wapo viongozi ambao ni wakorofi na ambao hawatakubali hivyo mkakati wa vijana ni kuwapinga hadharani kuanzia ngazi ya vikao vya chini hadi vya uteuzi na ikishindikana majina yao yakapitishwa basi vijana watazunguka nchi nzima kuwaambia wanaCCM wasiwape kura.

Sumaye azungumza
Kwa upande wake, Sumaye, alisema anajiandaa kutoa kile alichokiita msimamo wake kuhusiana na kauli za UVCCM.Sumaye akinekana kuwa mwenye taarifa za ‘makombora' hayo ya vijana alisema ataitisha mkutano wa waandishi na kutoa msimamo wake."Nataka nitafute siku rasmi niitishe mkutano na ninyi mkiwa wengi kutoa msimamo wangu kuhusu jambo hilo," alisema.

Hivi karibuni, Sumaye alikitaka chama hicho tawala kujibu hoja za Chadema na kiache kutumia dola kuzima hoja.
Sumaye alisema hayo alipozungumza na Gazeti dada la Mwananchi Jumapili kwamba, hoja za Chadema ni za kisiasa kwa lengo la kukamata dola hivyo zinapaswa kujibiwa kisiasa na si vinginevyo.

Kauli hiyo iliwachefua viongozi wa CCM na kupitia kwa Mkuu wa Kitengo cha Propaganda, Hizza Tambwe kilitoa kauli kikimwelezea Sumaye kama mtu anayesaliti chama kutokana na kushindwa kutoa kauli ndani ya vikao husika.Hata hivyo, Sumaye alijibu shutuma hizo akisema tatizo CCM kwa sasa ni kuwa na baadhi ya watu wenye upeo mdogo na wasiojua historia ya chama kilikotoka.

Kupambana na Chadema
Akizungumzia maandamano yanayofanywa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), alisema UVCCM kitapambana na chama hicho kikuu cha upinzani kwa madai kuwa sasa kimevuka mipaka.

Alisema kwa hali ilipofikia kwa sasa ni wazi kuwa vitendo vya Chadema haviwezi kuvumiliwa na akaitaka Serikali kukichukulia hatua za haraka chama hicho cha upinzani, vinginevyo jeshi la vijana wa CCM litapambana nao.
Kauli hiyo imekuja siku chache baada ya baadhi ya viongozi waandamizi wa CCM na Serikali kutoa vitisho kwa Chadema kuhusu maandamano kinayoyaendesha.

Chadema kilianza kuendesha maandamano Kanda ya Ziwa kwa kupinga mfumuko wa bei pamoja na malipo kwa Kampuni ya kufua umeme ya Dowans. Kilitangaza kufanya maandamano nchi nzima.Lakini jana, Malisa alisema kuwa Chadema watashughulikiwa kwa namna yoyote ingawa vijana wa CCM watafanya hivyo bila ya kuvunja sheria za nchi.

Hata hivyo, hakutaja mikakati wala njia zitakazotumika kukishughulikia Chadema: "Hatuwezi kutaja mikakati yetu kwani mtu hawezi kutangaza mbinu zake za kivita lakini tutafanya maajabu bila ya kuvunja amani ya nchi."
Alisema Baraza Kuu la UVCCM liliwapa maagizo vijana wote nchini kupambana na Chadema kwa kuwa Serikali inaonyesha kusuasua kuwadhibiti.

Kamati ya kurejesha uhai
Katika hatua nyingine, Baraza Kuu la UVCCM limeunda kamati maalumu ya kushughulikia uhai wa Umoja huo ambao lilisema kuwa unaanza kupoteza mwelekeo.

Kamati hiyo ya watu wanane itakuwa chini ya uenyekiti wa Hussein Bashe. Pamoja na mambo mengine, itazunguka nchi nzima katika kipindi cha miezi minne kupata maoni ya watu mbalimbali juu ya namna gani jumuiya hiyo inaweza kurudisha heshima yake kwa Watanzania kama ilivyokuwa mwanzo.

Kamati hiyo inatarajia kumaliza kazi yake na kuiwasilisha Julai mwaka huu, wakati baraza hilo litakapokutana kupitisha jina la mgombea uenyekiti wa UVCCM ambaye uchaguzi wake utafanyika Agosti mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutangazwa, Bashe alisema kamati yake itakutana na makundi mbalimbali likiwamo Jukwaa la Wahariri wa vyombo vya habari ili kupata maoni yao.

Katika kamati hiyo Bashe atasaidiwa na wenyeviti wa mikoa Antony Mavunde (Dodoma), Rogers Shemwelekwa (Tanga) na Fadhili Ngajilo (Iringa). Wengine ni Riziki Pemba na Daudi Ismail kutoka Zanzibar na Ashura Seng'ondo na Zuberi Bundara kutoka Bara.

Kuzozana na Makamba unaonekana wewe ni bogus tu. Makamba alishapoteza credibility, kuzozana naye yaani unaoneka wewe ni mwehu tu. Sijui wengine wanapata huo muda wapi wa kulumbana na Makamba?
 
hahaa kazi ipo mwaka huu..yaani nyumba ikikosa baba hayo ndo madhara yake
 
Makamba janga la Kisiasa Tanzania, jamani na ninyi mkiona Mambo kama hayo msihangaike, inueni macho yenu juu tumshukuru Mungu maana UKOMBOZI WETU UNAKARIBIA!!!
Halafu inasikitisha kuona kijana anahangaika na CCM ndo maana hata umri wanaibia ili waendelee kijifuza ufisadi.
 
kwani umri si kigezo kuwa mwana uvccm? Nilitegemea hoja ya shy-rose iwe tofauti ya lawama. Kushindwa kwa ccm uchaguzi kunakera kuliko kushindwa kwao kutatua matatizo ya nchi? Huko walikoshinda wamefanya nini?

Ndio vijana wanaotaka kuleta mabadiliko. It is pathetic!
very smart comment.thanks
 
kazi hipo nadhani sisi wanamapinduzi wanatakiwa wamtetee makamba kwani anawasaidia kuvunja ccm na shy-ni binti aliyepoteza uelekeo nadhani wote tunajua ktk uchaguzi uliopita baada ya zungu kumchezea rafu shy , shy alimpigia simu makamba lakini hakukuwa na jipya toka kwa makamba so bifu likaanza hapo

Huyu hajajua mbinu wanazotumia akina mama wengine wa CCM kufanikiwa ndani ya chama? Mimi namshauri nawaulize akina mama wazoefu wenye vyeo ndani ya CCM wamweleze walifikaje hapo walipo kisha atumie mbinu hizo hizo. Mwanamke AKIWEZESHWA anaweza.
 
Sunday, 20 March 2011 13:17 Habel Chidawali,Dodoma

KATIKA kile kinachoonyesha kuwa hali ni tete ndani ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), jana mkutano wa umoja huo ulitawaliwa na jazba huku, Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba na Mjumbe Shy Rose Bhanj wakitupiana maneno makali.

Habari zilizopatika kutoka ndani ya mkutano huo uliofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa White House mjini hapa, zinaeleza mvutano wa Makamba na mjumbe huyo uliibuka wakati Shy Rose alipokuwa akichangia mada kuhusu hali ya kisiasa na kusema viongozi ndani ya CCM ndiyo chanzo cha CCM kunyang'anywa baadhi ya majimbo katika Uchaguzi Mkuu uliopita.

Hali hiyo ilionekana kumkera Makamba ambaye alisisimama bila kufuata utaratibu wa kikao hicho na kumkatiza Shy Rose akisema kauli hiyo haina ukweli.

Naye Shy- Rose naye akitoa maneno ya kumpinga Makamba kabla katibu mkuu huyo wa CCM naye kuendelea kuzuia kuwatupia lawama viongozi.

Kuona hivyo, Kaimu Mwenyekiti wa UVCCM, Beno Malisa aliingilia kati na kuyazima huku kila mmoja akionekana kuwa na hamu ya kuendeleza ubishi baina yao, hata hivyo kikao kikaendelea na utaratibu wake.

Hivi katika hali kama hiyo ya kujibizana bila ustaarabu mbele ya watoto wake tena wanajibizana na mwanamama anayemweleza ukweli na tena pasipokufuata utaratibu wa kuzungumza kwenye kikao, sisi tuendelee kusema kuwa Makamba ana busara ya kuongoza chama tawala? Busara ya mzee huyu iko wapi hapa? Hivi hapo hakumdharau mwenyekiti wa kikao hicho?

Hapa mimi sioni tatizo la Makamba kujibizana na Shyroze Bhanji. Mwandishi unakosea kutumia mfano wa baba na wanaye hapa. Huu ulikuwa ni mkutano na wote walikuwa ni wajumbe wa mkutano huo. Hivyo ilikuwa ni ruksa kwa wajumbe hao kutofautiana mawazo na hata kubishana ili kuwekana sawa. Nadhani hiki kilichotokea kwenye mkutano huu ndicho kinachokosekana kwenye mikutano mingi ya ngazi za juu ya CCM ambapo mara nyingi hugeuzwa kuwa vijiwe vya kuyapamba mawazo ya mwenyekiti bila kukosoana kunakolenga kujenga chama.
 
Back
Top Bottom