Makamba Jr, DSTV Wamewashinda Kuhusu Channel 5 Za Bure?

Mkuu kwann Serikali na hao TCRA hawaliongelei hili? Walichotuambia na kutuaminisha ni kuwa as nchi Tupo tayari kwa ajili ya digitali na pia Kampuni zote za ving'amuzi zitarusha FTA tv. Kumbe ni Yale Yale fullu propaganda hii nchi hii mpaka tumwondoe CCM ndo tutatulia

Tatizo serikali kupitia TCRA haijatoa elimu maridhawa katika kuelewesha wananchi tofauti ya Pay Tv na FTA ili wananchi wasichanganyikiwe kama hivyo. DSTV haihusiki na wala sio Multiplex aliyepewa haki ya kurusha matangazo ya digitali kama ilivyo kwa StarTimes, Digitek na wengineo. DSTV ana taratibu na sheria zake tofauti kabisa mkuu
 
wote tunasaga lami kaka kutafuta tu elimu kisha turudi kuendeleza gurudumu
kwa post hii tunapeana elimu nimeelewa vingi kutoka kwako.
tuwaelimishe walaji yaani wateja kuhusu haki zetu..
tcra wakiwa makini bado dstv wangeingiza walau hata channel 6 za tanzania kwa lazima
tcra in uwezo wa kublock matangazo yao tz wasipotii agizo
na serikali inge revoke license yao
what i heard though not proved kuna vigogo wana hisa dstv na makampuni mengine ya vingamuzi
ndio maana hawajali kelele za wananchi.. how awkward tulipie local channels ???

Nadhani umenilisha maneno mkuu, nilisema TCRA ni Local regulator sio local Operator kama ulivyoelewa, naomba ukasome vema post yangu utaona hilo. Kutokana na kutokunielewa katika hilo, ndio sababu content nzima katika post yangu ukashindwa kuielewa. mie nipo Tanzania wewe uko Ulaya, tuna mifumo tofauti ya utangazaji na sheria tofauti. Laiti ungekuwa Tanzania ungezungumza lugha nyingine.

Ushauri wako kwa watendaji wa TCRA watakuwa wameusoma na wataufanyia kazi. Kila la kheri na maisha ya Ulaya mkuu sie tunasaga lami na Tanzania yetu
 
Tatizo serikali kupitia TCRA haijatoa elimu maridhawa katika kuelewesha wananchi tofauti ya Pay Tv na FTA ili wananchi wasichanganyikiwe kama hivyo. DSTV haihusiki na wala sio Multiplex aliyepewa haki ya kurusha matangazo ya digitali kama ilivyo kwa StarTimes, Digitek na wengineo. DSTV ana taratibu na sheria zake tofauti kabisa mkuu

Afadhali mkuu umetoa somo. Maana raia wa Chadema sijui wanamuogopa JMakamba. Wallshaanza kufungua madesa yao ya matusi.
 
wote tunasaga lami kaka kutafuta tu elimu kisha turudi kuendeleza gurudumu
kwa post hii tunapeana elimu nimeelewa vingi kutoka kwako.
tuwaelimishe walaji yaani wateja kuhusu haki zetu..
tcra wakiwa makini bado dstv wangeingiza walau hata channel 6 za tanzania kwa lazima
tcra in uwezo wa kublock matangazo yao tz wasipotii agizo
na serikali inge revoke license yao
what i heard though not proved kuna vigogo wana hisa dstv na makampuni mengine ya vingamuzi
ndio maana hawajali kelele za wananchi.. how awkward tulipie local channels ???

Tusitafune maneno. Mwenye hisa nyingi dstv ni ndugu ami mpungwe. huyu alikuwa balozi wetu huko bondeni.

Maelezo ya mwana mpotevu kidogo yanatupoteza. Ni kama anatuambia Tanzania sio sovereign state. Yaani lijamaa litoke huko maporini na sheria zake za porini na kuzitumia ndani ya nyumba tena kwa gharama na madhara makubwa kwa wenye nyumba. Kama si ujuha ni nini?

Hata mimi nimeona kule Norway. Ni Canal+ ndiyo kila kitu kimekuwa pay to watch. Na hii ni ya michezo zaidi. Lakini hizi za habari hapana. Hapa lazima tutofautishe mambo ya msingi, muhimu na yasiyo muhimu sana.

Hata malipo ni kwa dola hapo dstv. Na hii nayo watasema ni sheria zao, na haziguswi na sheria za Tanzania. Ya kweli hayo jamani? Hapa tunachezewa tu ndugu zangu.
 
Nadhani ipo haja ya kufungua darasa humu JF. Labda niwasaidieni:

DSTV na ZUKU TV zinatoa matangazo yake kwa mfumo wa Pay TV kama itakavyokuwa AZAM TV inayoanza soon mwezi ujao. Hizi haziingiliani na mfumo ambao ni wa Free-To-Air (FTA) ambao ndio unaozihusisha Star Times, Ting, Digitek na Continental. Wote hawa wanatoa matangazo kwa njia ya Digital lakini tofauti ni kwmaba hao ZUKU na DSTV wako kibiashara 100% na ndio maana wanaitwa Pay TV. Hawalazimishwi na sheria ya nchi yoyote kuzibeba TV za ndani isipokuwa pale wenyewe wanapoona kuna biashara kwao.

FTA ndipo utazikuta Star TV, TBC na hizi nyingine maana kuonekana kwake sio kwa kibiashara. Leo hii DSTV anaweza akaamua kuiondoa Star TV na akaiweka ITV akiona itamlipa zaidi na akikubaliana na ITV pia. TCRA hawana la kufanya hapo maana haiwahusu kama ilivyo kwa ving'amuzi vya Star Times et al.

Naamini walau mtakuwa mmeelewa wewe na wenzio ingawa mnaweza kuwa mnahitaji maelezo zaidi ili kuelewa kikamilifu

Wacha KUPOTOSHA,
Ilishasemwa nilazima hizi Channel 5 zionyeshwe na kila MULTPLEX atakaye pewa Leseni na TCRA. Pasco saidia hapa.
 
Last edited by a moderator:
Sijawahi kuona mtu muongo kama MwanaMpotevu. Yaani anaongea uzushi na umbeya tu. Hajui chochote.
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Majuzi tulisikia mgogoro kati ya kituo cha Television cha Star na Kampuni ya Startime na tishio la Startv kujitoa. Wizara na Tume ya mawasiliano wakaingilia kati na kuwalazimisha Startv wapitishe matangazo yao Startimes ili kukidhi kigezo cha kampuni zenye ving'amuzi kurusha matangazo ya Bure ya vituo vitano kitaifa ambvyo ni TBC1, ITV,STAR TV,CHANNEL 10 na CHANNEL 5.

Ajabu ni kuwa mbona jambo hilo limeshindikana kwa DSTV? Mwenye kutumia kutumia kingamuzi cha kampuni ya Multichoice (DSTV) ni lazima uwe na kingamuzi kingine maana kama fedha imekata DSTV HUWEZI pata matangazo ya hizo channel za bure bila malipo.

Je, wizara yako na tume ya mawasiliano mumewashindwa hao wawekezaji? Maana kama suala hilo kwao halipo mbona channel za kichina zinaonyeshwa bure?

Hii inamaanisha serikali yetu ina katabia ka kuwaogopa wawekezaji bila kujali maslahi ya wananchi wao?

ngoja waje wajibu
 
Mwana Mpotevu wewe umepotea, hvyo usipoteze wengine.. Hata suala la malipo kwa dola nalo utasema kuwa hao dstv hawatakiwi kuingiliwa?
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: EMT
Nadhani ipo haja ya kufungua darasa humu JF. Labda niwasaidieni:

DSTV na ZUKU TV zinatoa matangazo yake kwa mfumo wa Pay TV kama itakavyokuwa AZAM TV inayoanza soon mwezi ujao. Hizi haziingiliani na mfumo ambao ni wa Free-To-Air (FTA) ambao ndio unaozihusisha Star Times, Ting, Digitek na Continental. Wote hawa wanatoa matangazo kwa njia ya Digital lakini tofauti ni kwmaba hao ZUKU na DSTV wako kibiashara 100% na ndio maana wanaitwa Pay TV. Hawalazimishwi na sheria ya nchi yoyote kuzibeba TV za ndani isipokuwa pale wenyewe wanapoona kuna biashara kwao.

FTA ndipo utazikuta Star TV, TBC na hizi nyingine maana kuonekana kwake sio kwa kibiashara. Leo hii DSTV anaweza akaamua kuiondoa Star TV na akaiweka ITV akiona itamlipa zaidi na akikubaliana na ITV pia. TCRA hawana la kufanya hapo maana haiwahusu kama ilivyo kwa ving'amuzi vya Star Times et al.

Naamini walau mtakuwa mmeelewa wewe na wenzio ingawa mnaweza kuwa mnahitaji maelezo zaidi ili kuelewa kikamilifu

Mkuu nadhani hapo umepotosha. Nafikiri mleta mada ana hoja.

Ni kweli kwa hali ilivyo sasa, kama decoder yako ikiwa suspended baada ya subscritption yako ku-exprire huwezi kupata hata zile FTA channels.

Hii ni kwa sababuFTA channels zimekuwa pegged kwenye package yako uliyo-subscribe (which is wrong). Kwa hiyo, kama subscription ikiisha basi na zenyewe zinakuwa disconnected automatically.

Hii inamaanisha as if the local channels are not free at all and in that case ni vigumu basi kusema kuwa they are FTA channels hasa kwa wale wenye DSTV.

Ilitakiwa iwe kwamba kama subscription yako ikiisha basi wakate zile channels ambazo ni encrypted tuu na kuacha FTA channels.

FTA channels should be free hata kama zinarushwa na digital satellite television. Anaye decide channel fulani iwe FTA siyo anayeirusha hewani bali anayeimiliki.

Kama TBC ni FTA, then it should be free to any television network. Cheki kwa mfano link hapo chini, Sky ni pay TV, lakini ukiwa na dish na box la sky unapata FTA channels zote hata kama huna subscription. Nilidhani ingekuwa hivyo hivyo kwa DSTV

Freesat from Sky - Wikipedia, the free encyclopedia

cc The Boss
 
Now this sounds better. Nimefuatilia argument yenu head.to.toe, am now convinced with this. Hata Egypt pamoja na Fb kuoperate internationally, waliweza ku'establish local com. laws za kui'ban such that getting access to it by local people (who were on movement) were illegal. What's special on DSTV? Huu ni uzembe wa TCRA tu.
 
Wakuu nimewasoma vizuri,sasa nini kifanyike? Ujumbe huu utamfikiaje Makamba na TCRA?
 
Yes inabidi uwafikie wahusika kama TCRA (though Makamba anawezasema tuwaulize wabunge wetu) angalao watupe maelezo kwa nini FTA channels hazionekani kama free channels kwenye DSTV?

Kwa nini subscription ya DSTV inapoisha wanakata pia hata zile FTA channels? Ina maana nazo zinalipiwa?

Na hapa isiwe tuu FTA local channels bali pia FTA channels kama CNN, Al Jazeera, n.k ambazo pia ni free channels.

In fact kama hizi FTA channels zingekuwa zinapatikana free on DSTV basi probably wangeweza kupata wateja zaidi.

Wengine labda wanapenda kulipia DSTV kwa msimu. Kwa mfano, kwa mimi mpenda soka kwa sasa sioni umuhimu wowote wa kuwa DSTV wakati hakuna mechi za ligi. It is a waste of money.

Na kwa kuwa FTA channels zimekuwa pegged na kwenye package subscription package, then mtu anayetaka kulipia kwa msimu hataona umuhimu wa kuwa na DSTV.

Nadhani ipo haja ya kufungua darasa humu JF. Labda niwasaidieni:

DSTV na ZUKU TV zinatoa matangazo yake kwa mfumo wa Pay TV kama itakavyokuwa AZAM TV inayoanza soon mwezi ujao. Hizi haziingiliani na mfumo ambao ni wa Free-To-Air (FTA) ambao ndio unaozihusisha Star Times, Ting, Digitek na Continental. Wote hawa wanatoa matangazo kwa njia ya Digital lakini tofauti ni kwmaba hao ZUKU na DSTV wako kibiashara 100% na ndio maana wanaitwa Pay TV. Hawalazimishwi na sheria ya nchi yoyote kuzibeba TV za ndani isipokuwa pale wenyewe wanapoona kuna biashara kwao.

FTA ndipo utazikuta Star TV, TBC na hizi nyingine maana kuonekana kwake sio kwa kibiashara. Leo hii DSTV anaweza akaamua kuiondoa Star TV na akaiweka ITV akiona itamlipa zaidi na akikubaliana na ITV pia. TCRA hawana la kufanya hapo maana haiwahusu kama ilivyo kwa ving'amuzi vya Star Times et al.

Naamini walau mtakuwa mmeelewa wewe na wenzio ingawa mnaweza kuwa mnahitaji maelezo zaidi ili kuelewa kikamilifu

Haya maelezo yalipaswa yatolewe mwanzoni kabisa ili kuondoa maswali kama ya mleta mada, na kwa sababu mpaka sasa hakuna mserikali hata mmoja aliyepata ujasiri wa kujitokeza na kutoa majibu ya namna hii hata wewe unapaswa kujiuliza kigugumizi hiki kinatokea wapi?

Back to your points.
Kwamba Zuku na DSTV ni Pay TV kwani kwenye hivyo ving'amuzi vingine tunaangalia bure? toa maelezo ya kutosha katika hili.

Fikra zangu binafsi katika hili ni kwamba, ZUKU na DSTV wanavilipa vituo vyote vya TV wanavyoonyesha ndio maana wanaitwa Pay TV na ndio maana Bwana Mengi hayuko tayari TV zake zionekane huko mpaka na yeye wamlipe kama wanavyolipa hivyo vingine.na ndio maana subscriptions zao ziko juu.

Hao wakina start Times wameamua kujitengenezea ka business niche kao (wakiwa backed up na politics kama hizi zetu), kwamba watawacharge wateja pesa kidogo ili waweze kuenhance muonekano wa channels kwenye luninga zao and they pay no body.

Hivyo Majibu ya kwanini maelekezo ya wizara hayajatekelezwa bado yanahitajika tena haraka.
 
Ukisoma post zangu nyingine nilizokuwa nikiwajibu wenzio, naamini utakuwa umeelewa na maswali yako yote yatakuwa yamepata majibu
 
Nicas Mtei huwa nakuheshimu sana naomba nisikujibu. Asante kwa kutambua kuwa nimepotea mkuu na ninakuomba radhi sana.

Mkuu usikasirike, tunajaribu kuelimishana kisha tutaona nini sisi kama walaji tufanye ili tunufaike. Mchango wako ni muhimu sana hivyo kama kuna kupishana kauli basi watu wasameheane.
 
Last edited by a moderator:
starehe gharama jamani waacheni makaburu watese ila mbona tbccm inaonekana ata kama ujalipia!
 
Back
Top Bottom