Makamba Jr, DSTV Wamewashinda Kuhusu Channel 5 Za Bure?

Makamba Jr, DSTV Wamewashinda Kuhusu Channel 5 Za Bure?

Kiukweli hili swala linaniuma sana. Wahusika wamenyamaza kama vile hawalioni, mimi naweza kukaa hata siku tatu siangalii TV kwa sababu ya DSTV unakuta pesa huna na Dstv tayari washakata.
 
Nadhani ipo haja ya kufungua darasa humu JF. Labda niwasaidieni:

DSTV na ZUKU TV zinatoa matangazo yake kwa mfumo wa Pay TV kama itakavyokuwa AZAM TV inayoanza soon mwezi ujao. Hizi haziingiliani na mfumo ambao ni wa Free-To-Air (FTA) ambao ndio unaozihusisha Star Times, Ting, Digitek na Continental. Wote hawa wanatoa matangazo kwa njia ya Digital lakini tofauti ni kwmaba hao ZUKU na DSTV wako kibiashara 100% na ndio maana wanaitwa Pay TV. Hawalazimishwi na sheria ya nchi yoyote kuzibeba TV za ndani isipokuwa pale wenyewe wanapoona kuna biashara kwao.

FTA ndipo utazikuta Star TV, TBC na hizi nyingine maana kuonekana kwake sio kwa kibiashara. Leo hii DSTV anaweza akaamua kuiondoa Star TV na akaiweka ITV akiona itamlipa zaidi na akikubaliana na ITV pia. TCRA hawana la kufanya hapo maana haiwahusu kama ilivyo kwa ving'amuzi vya Star Times et al.

Naamini walau mtakuwa mmeelewa wewe na wenzio ingawa mnaweza kuwa mnahitaji maelezo zaidi ili kuelewa kikamilifu

Asante kwa darasa
hii ina maana AZAM TV hawatalazimishwa na sheria za TCRA zinazobana tbc na startv?
sio ndio?

au startv leo wakiamua kuwa na wao ni paytv sio tena free to air tv hawalazishwa kuwemo Startimes sio?

na je na mimi nikiamua kuanzisha my own pay tv kwa mujibu wa sheria zilizopo kuna pingamizi?

je ctv na cable za mikoani?

na easy tv je? wapo makundi gani?
 
Zuku kila wakati ina upgrade software yaani ukiwa unatizama TBC habari kitu kinajizima kila baada ya muda na kujiwasha ati ZUKU Satellite
 
Kwa hiyo hawa pay tv kwa vile hawabanwi na sheria wanaweza kurusha vipindi vyovyote wanavyoona vinafaa na hawawezi kuwa censored? Hata kama ni vya maadili mabovu au hatarishi kwa taifa kwa vile sheria haiwagusi basi ni twende tuu?
 
f so basi TCRA hawajui wajibu wao kaka, nchi zite duniani wanakotumia cable lazima uingize tv zote ambazo ni free to air katika mfumo wako ili wanachi waangalie bure na zile za kulipia ndio watalazimika kulipia.
Like umeipata kwa sababu ya hayo maneno tuu ila kukusahihisha tuu ni kuwa tuliahidiwa Local Channel zitakuwa free on air.Alafu
"DSTV ni Digital Satelite Television, Mfumo wao wa usajili na udhibiti hauhusiani la Local providers bali ni international providers"Ivi ukiwa una operate internationally unaruhusiwa kuvunja sheria/taratibu ambazo inchi husika imejiwekea?
Haingii akilini kwa mwananchi kuwa na vingamuzi zaidi ya vitatu kisa eti apate plus local channel huitaji PHD kujua kuwa huu ni upumbuvu na kuna watu are being paid for this as result tunapoeza mda wetu kuwadiscuss nao wanaona mfumo uliopo wako OKEY.
Are you people of TCRA serious kweli.
Niko na DSTV ambako napata STAR NA TBC na ili kupata CH10 na ITV naitajika kupata vingamuzi vyengine.Ivi huu uhuru wa kupata habari kama ilivyoainishwa kwa katiba uko wapi?
 
Hizo local TV zinazopitia kwenye visumbuzi vya bongo vinaonekana vibaya la quality mbovu sana..... ukiacha kidogo ITV star tv huwa siwezi kabisa kuitizama huwa nafikisha mamcho muda wote muonekano wake kama nimevaa miwani ya macho wakati siumwi pata picha hapo
 
kwa kweli hili naliunga mkono kwa nini waweke chanel mbili tu star tv na tbc wapi other local chanels, serikali ya ccm kweli double standard kha
 
Mkuu

DSTV ni Digital Satelite Television, Mfumo wao wa usajili na udhibiti hauhusiani la Local providers bali ni international providers. Hapo ndipo unapochanganya mambo na ndio maana TCRA ambaye ni Local regulator anapokuwa hahusiki nao. Kumbuka DSTV wana miaka zaidi ya 20 wakiwa tayari wako Digital mkuu. Hili kidogo ni darasa refu sana na naweza kuchukua muda mrefu sana kukuelimisha hadi ikakukaa vema. Bahati nzuri au mbaya hiii ndio area yangu ninayoifanyia kazi.

Hapo kwenye Bluu, tofautisha Cable Television na Digital Satelite Televisions mkuu. Vi vitu viwili tofauti kabisa. DSTV sio Cable Television wala sio FTA. Hii ni Digital Satellite wakati StarTimes na wenzake sio Digital Satelilte.

Mkuu bado tunapishana kidogo
kwanza TCRA sidhani kama ni local operator bali ni national regulator. TCRA haopereti bali ana regulate
MISSION YAO NI
"To develop an effective and efficient communications regulatory framework, promote efficiency among the Communications Services Providers, and protect consumer interests with an objective of contributing to socio-economic and technological development in the United Republic of Tanzania.

Ok huku nilipo natumia cable canal digital ambao ndio servicer provider hapa europe kama ilivo DSTV kwa africa.
huku wanatumia cable kwani ndio teknolojia ya kisasa zaidi inayotumia fibres na ndani yake unapata both TV signals,simu na internet.. wanachukua channels kwenye sattelites na zingine local then wanatransmit wenyewe kwa ubora zaidi kuliko wanaotumia madish kama DSTV
na unaweza kuona channels za HD au HQ bila kuwa na PVR decorder/......
Hawa wako subjet na sheria ya kila nchi walipo na local channels ni bure
kama ukitaka za kulipia ndio unapewa decorder unachomeka waya wa cable yako au unatumia card kwa wale wenye flat screens zenye kukubali card. No dish required
Wenye kuwekewa madish ni wale walio mbali na cables au nje ya mji.
Kwa afrika ni ngumu kutumia cable since mipago miji tushaivuruga labda baadae tutumie mkonga wa taifa kuweka cable kila nyumba na kuweza kutumia cable kama wengine tuachane na madishi..

Nimeshangazwa na ukimya au kutowajibika kwa TCRA since DSTV wanatoa service kwetu hivo ni communication service providers whether wanatumia satelite au local broadcast kwani ina wateja ndani ya nchi na tunawalipa
na wanatakiwa kuwa subject na sheria zetu...
haingii akilini kusema kwa vile wanatumia satelites TCRA haihusiki hata makampuni ya simu yanatumia pia satelites hata radios etc. Kwa vile mission ya TCRA iko wazi sielewei kwanini DSTV haiko subject to our laws
na sielewi kama wanasheria wa TCRA wanafanya nini ofisin wakasome ICT laws wataelewa zaidi kuhusu
electronic communications and the role ya national regulators
wanaweza kuiga mfano Europe wana directives on electronic communications

Kusema DSTV wana miaka 20 kuwa digital sio hoja
Hoja hapa ni je kwanini hawako subject to our laws while they are providing communication services in our country na role ya TCRA ni national communication regulator whether local or international???
 
Wakuu ili kuelewa hili somo labda nili-tackle kwa alternative method:-

Hivi mtu anapojiunga na Cable au DSTV anajiunga ili aangalie local channels au premium channels ?

Kumbuka kabla ya kuingia Digital (Cable na DSTV zilikuwepo) na mtu ili upate channels za ziada ndio ulikuwa unajiunga na hizi huduma.

Issue / Kosa linakuja kwa hawa wauzaji wa hizi decoder (Star Times et al) kama wakilazimisha watu kutoa pesa ili kuonyesha channels ambazo ni za bure anyway (FTA); kumbuka kwamba kuna tv zipo zina built in decoder watu watakapoanza kununua hizi nadhani shida za hizi vingamuzi zitakwisha sababu hapo ndio issue itabakia choice ya mtu kulipia extra ili kuangalia anachotaka kulingana na what is provided.

Kumbuka kwamba huenda sio DSTV ambae hataki kuonyesha hivyo vipindi labda wenye vipindi ndio wanataka gharama ya juu ya yeye kulipia hivyo vipindi ili aonyeshe kwa watu wake (which maybe kwa yeye does not make economic sense, kulipia gharama kwa kitu ambacho sio value for money(
 
Mkuu

DSTV ni Digital Satelite Television, Mfumo wao wa usajili na udhibiti hauhusiani la Local providers bali ni international providers. Hapo ndipo unapochanganya mambo na ndio maana TCRA ambaye ni Local regulator anapokuwa hahusiki nao. Kumbuka DSTV wana miaka zaidi ya 20 wakiwa tayari wako Digital mkuu. Hili kidogo ni darasa refu sana na naweza kuchukua muda mrefu sana kukuelimisha hadi ikakukaa vema. Bahati nzuri au mbaya hiii ndio area yangu ninayoifanyia kazi.

Hapo kwenye Bluu, tofautisha Cable Television na Digital Satelite Televisions mkuu. Vi vitu viwili tofauti kabisa. DSTV sio Cable Television wala sio FTA. Hii ni Digital Satellite wakati StarTimes na wenzake sio Digital Satelilte.

Mkuu kwann Serikali na hao TCRA hawaliongelei hili? Walichotuambia na kutuaminisha ni kuwa as nchi Tupo tayari kwa ajili ya digitali na pia Kampuni zote za ving'amuzi zitarusha FTA tv. Kumbe ni Yale Yale fullu propaganda hii nchi hii mpaka tumwondoe CCM ndo tutatulia
 
Asante kwa darasa
hii ina maana AZAM TV hawatalazimishwa na sheria za TCRA zinazobana tbc na startv?
sio ndio?

Azam TV haitalazimishwa kuziweka local channels kama TBC, ITV, Star TV and other local TV channels isipokuwa kama wao wataona kuwa channel hizo zinawalipa kibiashara basi wataweza kuziweka kwa mapenzi yao na kwa makubaliano maalum na wamiliki wa hizo TV channels.

na je na mimi nikiamua kuanzisha my own pay tv kwa mujibu wa sheria zilizopo kuna pingamizi?
Hakuna Pingamizi, fuata sheria tu mkuu


je ctv na cable za mikoani?
Hizo zina categories zake ambayo inaitwa Cable Television hivyo hivyo. Ni sehemu ya Pay TV ingawa mfumo wao wa usambazaji matangazo ni tofauti na Pay TV kama DSTV, Zuku ambazo zinatumia dishes.


na easy tv je? wapo makundi gani?

Ni Pay TV kama Zuku TV na DSTV na Azam TV

au startv leo wakiamua kuwa na wao ni paytv sio tena free to air tv hawalazishwa kuwemo Startimes sio?

Unachanganya mambo. Kumbuka DSTV inakusanya channels nyingi ambazo mpaka ulipe ndipo utaziona. Ndani yake ndipo kuna Star TV na TBC na CNN, na Supersport channels, Africa Magic na nyinginezo nyingi. Star TV haiwezi kujigeuza kuwa Pay TV unless waamue kuanzisha king'amuzi ambacho kitasajiliwa kama Pay TV na kisha ndani yake ndipo kuwe na Star TV na channels zake nyingine ambazo hazitaonekana hadi hapo utakapolipa. Kwa sasa haiwezi kujibadili na kuwa Pay TV.

Nadhani Itakapoanza Azam TV utaweza kupata mfano mzuri zaidi wa namna Pay TV ilivyo. Azam watakuwa na king'amuzi chao na pia channels zao nyingi ndani yake ambazo hazitapatikana katika king'amuzi kingine zaidi ya Azam decorder. Nadhani walau umenielewa
 
Azam TV haitalazimishwa kuziweka local channels kama TBC, ITV, Star TV and other local TV channels isipokuwa kama wao wataona kuwa channel hizo zinawalipa kibiashara basi wataweza kuziweka kwa mapenzi yao na kwa makubaliano maalum na wamiliki wa hizo TV channels.


Hakuna Pingamizi, fuata sheria tu mkuu



Hizo zina categories zake ambayo inaitwa Cable Television hivyo hivyo. Ni sehemu ya Pay TV ingawa mfumo wao wa usambazaji matangazo ni tofauti na Pay TV kama DSTV, Zuku ambazo zinatumia dishes.




Ni Pay TV kama Zuku TV na DSTV na Azam TV



Unachanganya mambo. Kumbuka DSTV inakusanya channels nyingi ambazo mpaka ulipe ndipo utaziona. Ndani yake ndipo kuna Star TV na TBC na CNN, na Supersport channels, Africa Magic na nyinginezo nyingi. Star TV haiwezi kujigeuza kuwa Pay TV unless waamue kuanzisha king'amuzi ambacho kitasajiliwa kama Pay TV na kisha ndani yake ndipo kuwe na Star TV na channels zake nyingine ambazo hazitaonekana hadi hapo utakapolipa. Kwa sasa haiwezi kujibadili na kuwa Pay TV.

Nadhani Itakapoanza Azam TV utaweza kupata mfano mzuri zaidi wa namna Pay TV ilivyo. Azam watakuwa na king'amuzi chao na pia channels zao nyingi ndani yake ambazo hazitapatikana katika king'amuzi kingine zaidi ya Azam decorder. Nadhani walau umenielewa


asante
kuhusu star tv nilikuwa namaanisha king'amuzi chao cha continental
thru that hawawezi jibadili?
 
Nijuavyo, DSTV hai operate kutokea Tanzania na hata hawapo, hapa kuna wakala tu anaitwa Multi Choice.

Sahihisha kama nimekosea.
 
Hii ndo TZ bwana, non of them walks their talks. Hili la Multichoice ndo hawaliwezi kabisa. Amri ya kuvunja jengo lile la mhindi Dar imeshindwa kutekelezwa, wataweza kulazimisha jamaa walioko Bondeni??? Chezea Tanzania weye!!!!!
 
Mkuu bado tunapishana kidogo
kwanza TCRA sidhani kama ni local operator bali ni national regulator. TCRA haopereti bali ana regulate

Nadhani umenilisha maneno mkuu, nilisema TCRA ni Local regulator sio local Operator kama ulivyoelewa, naomba ukasome vema post yangu utaona hilo. Kutokana na kutokunielewa katika hilo, ndio sababu content nzima katika post yangu ukashindwa kuielewa. mie nipo Tanzania wewe uko Ulaya, tuna mifumo tofauti ya utangazaji na sheria tofauti. Laiti ungekuwa Tanzania ungezungumza lugha nyingine.

Ushauri wako kwa watendaji wa TCRA watakuwa wameusoma na wataufanyia kazi. Kila la kheri na maisha ya Ulaya mkuu sie tunasaga lami na Tanzania yetu
 
Majuzi tulisikia mgogoro kati ya kituo cha Television cha Star na Kampuni ya Startime na tishio la Startv kujitoa. Wizara na Tume ya mawasiliano wakaingilia kati na kuwalazimisha Startv wapitishe matangazo yao Startimes ili kukidhi kigezo cha kampuni zenye ving'amuzi kurusha matangazo ya Bure ya vituo vitano kitaifa ambvyo ni TBC1, ITV,STAR TV,CHANNEL 10 na CHANNEL 5.

Ajabu ni kuwa mbona jambo hilo limeshindikana kwa DSTV? Mwenye kutumia kutumia kingamuzi cha kampuni ya Multichoice (DSTV) ni lazima uwe na kingamuzi kingine maana kama fedha imekata DSTV HUWEZI pata matangazo ya hizo channel za bure bila malipo.

Je, wizara yako na tume ya mawasiliano mumewashindwa hao wawekezaji? Maana kama suala hilo kwao halipo mbona channel za kichina zinaonyeshwa bure?

Hii inamaanisha serikali yetu ina katabia ka kuwaogopa wawekezaji bila kujali maslahi ya wananchi wao?

binafsi nasema kwamba hao serikali walishindwa hata kuwakemea DSTV wanaotoza thru dolali
 
Back
Top Bottom