Makamanda mbona hamsomeki?

Makamanda mbona hamsomeki?

Nothing new hapo, Nyalandu alikuja Chadema kwa mapenzi yake na ameondoka kwa mapenzi yake, hakuna kesi, zaidi yeye ndio nimemuona mshamba kwa zile pumba alizoongea, ngoja aje dikteta mwingine huko CCM tuone atakimbilia wapi.
Aweza kuja cdm na atapokelewa vizuri sana. Ndo siasa za Tz.
 
Watapata tabu sana!

Mpaka mama atoke watakuwa wamepauka kama ndoo za kuogea za uswahilini

Kibaya zaidi kwao akitoka mama atamrithisha mwanademokrasia mwenzake
Sasa chadema wataenda ikulu lini?

Maana hiyo ndio point muhimu
 
Vipi Nyarandu atakuwa kanunuliwa ee?

Nyalandu hana sababu ya kubaki cdm maana huko ccm alimkimbia dhalimu, na sasa dhalimu yuko motoni. Ifahamike Nyalandu mwenyewe anajua hana mvuto huko cdm, na anajua akirejea ccm ana nafasi ya kuendelea na ufisadi wake maana huko ndio nyumbani.
 
Ili Mama yuko vizuri.
Ile siku watu wameambiwa wanademka.

Wacha waanze kucheza mle ndani.
Bila shaka hata maana ya kudemka waliipata siku ya pili.

Mwingine katika TV alisema sasa tumefurahi zaidi kuthibitisha furaha japo ilikuwepo ilikuwa ya kiwango cha chini.

Ni baraka iliyoje kuwa mwananchi wa JMT.
 
Kama Hana mvuto ilikuwaje akashinda uenyekiti Kanda ya Kati?
Kamanda kubali tu kuwa mmepigwa d......le
Mvuto hana, ila hela za kuhonga wajumbe huko kanda ya kati alikuwa nazo. Fuatilia alipokuwa anataka kupata sign za kumdhamini agombee urais kwa tiketi ya cdm alikutana na nini.
 
Ni kitambo kidogo sijalonga na hawa washikaji zangu ‘makamanda’.

Lakini leo nadhani ni siku muafaka ya kulonga nao.

Sasa nyie makamanda, tokea Rais Samia ameshika hatamu za uongozi, nyie ndo mmekuwa mstari wa mbele kabisa kuimba mapambio kwake.

Mmekuwa na furaha isiyo na kifani! Furaha yenu hiyo inatokana na imani yenu ya kwamba yale mazonge mliyokuwa nayo enzi za hayati Rais Magufuli, sasa yamekwisha.

Kwamba eti yeye alikuwa mkali sana. Yeye alikuwa katili sana. Yeye alikuwa mshamba sana. Yeye alikuwa fisadi sana. Yeye alikuwa hivi na vile sana.

Sawa. Hayo ni maoni yenu tu. Na maoni yenu si lazima yawe ndo uhalisia wa hali au mambo.

Leo ngoja niwaulize swali: kama nyinyi sasa hivi ndo mmekuwa viongozi wa kuimba mapambio ya Rais Samia na CCM yake, kwa nini sasa leo mmenuna, mmevimba, na mmefura kisa tu ex-kamanda mwenzenu aitwaye Lazaro Samweli Nyalandu karudi CCM ili aweze kuunga mkono uendeleaji wa kazi za Rais Samia?

Kama nyie mnamuunga mkono Rais Samia, na yeye anamuunga mkono Rais Samia, wote nyie lenu si ni moja?

Mapovu ya nini sasa?

Ndo kusema hamjielewi kiasi hicho au?

Nimalizie kwa kuwaaga kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania…..

Au niwaage kwa People’s……

Teh teh teh
Kikwetu hawa tunawaita Ng'ombe waliye katika mikia, Baba alisemaga Ng'ombe akitoroka zizini akaenda zurura akirudi zizini tunamkata mkia ili wenzake wajue kuwa alitorokaga
 
Niliisikia hii.

Huyu Mama ana maneno fulani ya taarabu za mipasho sana tu, ila anajua kujiweka kama mtaratibu kwa siasa za bongo on balance akilinganishwa na mtu mwenye maneno ya kunya kama Jiwe anaonekana huyu mama kama Mtakatifu fulani.
Welp! Check this out 🤣

Na kakuwekea na mkono kiunoni kabisa!

 
Back
Top Bottom