Makala: Haya ya Rose Muhando ni mapito au anguko?

Makala: Haya ya Rose Muhando ni mapito au anguko?

Mshana Akili kubwa! UnaKINA kwenye kila nyanja ya maisha! Nawaza siku JF ikifungwa tutapotezana na watu kama wewe Doh, Mwenyezi Mungu aepushie mbali kabisa.
Itakuwa Vipi JF bila Mshana? Ameeleza vizuri sana. Wachache wataelewa. Mambo ya ulimwengu wa roho na ulimwengu wa giza.
 
Rose mwezi uliopita alikuwa mwanza kazunguka sana kwa show za milioni na usu per show zilikuwa kama 5 hivi nyumba ya dodoma bado anayo,UTAPELI MTUPU,aache UNGA cocaine na heroine zinamsumbua
 
Itakuwa Vipi JF bila Mshana? Ameeleza vizuri sana. Wachache wataelewa. Mambo ya ulimwengu wa roho na ulimwengu wa giza.
Huyu jamaa anauwezo Mkubwa, JF imetufanya tunajuana kupitia hizi hizi ID fake, yaani kuna ka"jumuiya" flani hivi tumekatengeneza kwahiyo kuivuruga JF ni kuivuruga familia yetu.
 
Tutafute hela, tuwekeze ili tuwe salama. Sanaa za maigizo zinakua kila mahali kisa hili tumbo hili!
 
Mungu ndie ajuaye yote.Anaigiza au haigizi yeye tayari asha mjua Rose.
 
Rose alialikwa kuja kuimba kanisani kwetu alilipwa ila hakutokea kwenye huduma. Naona sasa hiyo ni mshahara wake wa dhambi
 
Mshana Jr umeanza vizuri ila umemaliza vibaya umemuattack rose direct, rose ana matatizo na hakuna haja ya kumungunya maneno rose anatumia unga hilo lipo wazi hata aliyekuwa meneja wake msama anajua hilo suala lililopo kwa sasa ni jinsi gani rose anasaidiwa siyo kumtupia lawana,

Uzuri wewe unajua mambo ya nguvu ya giza na bianadamu wanavyotumia katika kujitafutia ridhini kwaiyo kwa jinsi rose alivyojua vizuri kimziki wa dini hata angeacha kuimba akamua kukaa tu mjini na kuwa muumini wa imani yake rose asingekufa njaa kutokana na kazi aliyoifanya anauwezo wa kupata unafuu wa maisha yake mpaka kufa kwake yeye angekuwa anapishana na barua za mwaliko tu wa semina nje ya inchi na ndani ya inchi,

Tujiulize ilikuwaje rose akaanza kubwia unga hapo ndio tatizo kuna source ambayo miye na wewe hatuijui ila watu wake wa karibu wanaijuia waseme

Meneja wake msama atakuwa anajua asimtelekeze rose leo kisa hana maslahi naye rose au kisa hawadaiani akumbuke mchango alioutoa rose kipindi hana matatizo amsaidie
 
Mshana Jr umeanza vizuri ila umemaliza vibaya umemuattack rose direct, rose ana matatizo na hamu na haja ya kumungunya maneno rose anatumia unga hilo lipo wazi hats meneja wake masama anajua hilo suala liliopo ni jinsi gani rose anasaidiwa siyo kumtupia rawana,

Uzuri wewe unajua mambo ya nguvu ya Giza na bianadamu wanavyotumia katika kujitafutia ridhini kwaiyo kwa jinsi rose alivyojua vizuri kimziki wa dini hats angeacha kuimba akamua kukaa tu mjini na kuwa muumini wa imani take rose asingekufa njaa kutokana na kazi aliyoifanya inauwezo wa kumpa unafuu wa maisha take mpaka kufa kwake yeye angekuwa anapishana na barua za mwaliko tu wa semina nje ya inchi na ndani ya inchi

Tujiulize ilikuwaje rose akaanza kubwia unga halo ndio tatizo kina source ambayo miye na wewe hatuijui ila watu wake wa karibu wanaijuia waseme

Meneja wake msama atakuwa anajua asimtelekeze rose leo kisa hana maslahi naye rose au kisa hawadaiani akumbuke mchango alioutoa rose kipindi hana matatizo amsaidie
@utandu nisome tena uelewe... Nakubali kabisa Rose ana mapito makubwa na hili linaweza kumtokea yeyote kati yetu.... Ninachopinga ni kule kukubali kutumika na kufanya maigizo ya uongo kwa manufaa ya mtu mwingine
 
@utandu nisome tena uelewe... Nakubali kabisa Rose ana mapito makubwa na hili linaweza kumtokea yeyote kati yetu.... Ninachopinga ni kule kukubali kutumika na kufanya maigizo ya uongo kwa manufaa ya mtu mwingine
Yupo katika stress wote wamemkimbia na kama unavyojua mameneja wa kitanzania na wasanii wetu akifanya kazi anamuuzia kila kitu meneja pengine leo hii tunazijua nyimbo nyingi za rose na tunaona kabisa rose jamii bado inamuitaji kwa hizo nyimbo kwanini akate tamaa mapema hivyo unakuta kumbe asilimia 98 ya kazi zake ni haki ya meneja wake rose hana chake kumbuka sakata la mwana mama saida kaloli kuhusu haki miliki zake, hili suala pengine ndio linamtafuna mwanadada rose akijiona anajiona mkubwa anapata mialiko mingi lakini sheria ya mikataba inambana hawezi inabidi awe mpole tu

Wito wangu waziri wa habari utamaduni na michezo akae na mwanasheria mkuu wangalie ni jinsi gani watasaidia wasanii walioingiaga mikataba mibovu maana inawatesa wasanii wengi sana yani ikiwezekana itungwe sheria kazi yoyote ile itakuwa Mali ya meneja kwa mda upi baada ya hapo iyo kazi ni mali ya msanii
 
Wasalam waleikhum..!

Kidogo tumepumzishwa kwenye zile sinema zetu.... Tumepata msimu mdogo wa mwanadini muimba nyimbo za injili mwanadada na mama wa watoto Rose Muhando.

Hii inaweza kuwa mada ya NNE kumhusu... Japo nyingine zilizotangulia zikimjadili Rose wa sasa kama celeb na kile kinachomtokea...

Kwanza itambulike kuwa hii ni vita ya kiroho, falme za giza dhidi ya falme za nuru, wakuu wa mbingu dhidi ya wakuu wa anga...

Rose ni catalyst tu katika vita kubwa ya kiroho na ya kidunia... Nuru dhidi ya giza... Alikuwa jemadari msimu wa kwanza akapambana vilivyo, akazishinda falme za giza katika maeneo mengi.. Lakini kwakuwa ana mwili wa damu na nyama, alilemewa... Akazidiwa akampa adui nafasi... Sasa anatengenezwa...!

Rose Muhando ni nani?

Kwa wale waliobahatika kusoma habari zake huko nyuma... Aliingia kwenye uimbaji wa nyimbo za injili akitokea kwenye ndoa iliyojaa mateso (kwa mujibu wake) akiwa na karama ya uimbaji na mahitaji ya nyakati kumbeba aliibuka kuwa mmojawapo wa nyimbo za injili mwenye kipaji na mafanikio mengi... Lakini mafanikio yake yalikuwa kwenye hatari kubwa kwakuwa aliyapata kwa kupambana na shetani (kimtazamo)

Kuna wakati tunaweza kusema kwa hakika Rose alikuwa mlokole kamili na nyimbo zake zikiwaokoa na kuwabariki wengi....

Misukosuko ilipoanzia

Zaburi ya 23 kuna mstari unasema... Nijapopita katika bonde la uvuli wa mauti....! Kila mmoja wetu ana mapito yake ... Hata waimbaji wenzake walishapitia anayopitia... Si wa kwanza yeye na hatakuwa wa mwisho... Shida iko hapa, je unapopitia kwenye mapito unasimama upande gani? Wa nuru au giza? Anguko lako ama kusimama tena vitategemea ulikuwa upande gani... I mean upande gani uliupa airtime kubwa....! Ni wazi Rose alipojaribiwa aliingiwa na upofu na kumpa Mungu wake kisogo akaenda kufanya kolabo na upande wa giza... Sasa anasulubiwa.. Msimu huu wa pili anamsaidia adui.. Na huu ndio ushindi uliokuwa unatafutwa na falme za giza

Imekuwaje aibukie Kenya?

Kwanza kiuhalisia Rose ni kweli kabisa anaumwa na hayupo sawa.. Ni kama mwaka sasa tumekuwa hatusikii habari zake nzuri.. Amepitia mapito mengi, amechapwa akachapika.. Anaonekana live ana POP mkononi vidonda na makovu.. Na kwa maneno yake mwenyewe kwa takriban siku 90 alikuwa hajui anatoka wapi anaenda wapi... Amekuwa kama chizi fresh, zinatoka zinarudi... Alifikaje Kenya kwa hali ile? Alipelekwa? Alifikaje kwa yule mtume nabii?
Kisanga kinaanzia hapa!

Dunia ya leo watu hupenda kuyatumia matatizo ya wengine kujinufaisha ama kuwatumia wao wenyewe pia...

Rose Muhando ni jina kubwa Afrika mashariki. Habari zake zikisikika popote ndani ya jumuiya hii si jambo geni

Mtume na nabii kwa kuiona fursa... Anamuahidi kumsaidia Rose kwa masharti hasa la kutaka amuombee mbele ya waumini wake kukiwa na camera zinazochukua video na picha.. Lakini la zaidi anamfundisha cha kuongea..

Nimeangalia kwa makini video ile.. Sijui misa ilianzaje lakini anaonekana mtumishi wa Mungu akimwita Rose aliyechoka na kuanza kumuombea.

Ghafla Rose anaanguka na mapepo yanaaza kuongea kuwa kuna wivu juu ya mafanikio yake, hawataki aimbe, wamechukua magari yake wanataka kumuua nknk... Lakini ni wakati huu mapepo yakiongea Rose ana ufahamu wa kuondoa mkono wa mtumishi mdomoni mwake aweze kuongea vizuri....

Baada ya maombi mafupi mapepo yanatimka na hapo hapo Rose anazinduka na kuanza kuongea yaleyale yaliyokuwa yakiongelewa na mapepo... Halafu anaendelea kuelezea changamoto za familia yake, watoto kukosa ada nk.. Halafu anamalizia kwa kumshukuru Mungu...

Rose, Mungu hadhihakiwi... Mapepo hayatoki kivile na fahamu hazirudi kivile.. Nguvu ya pepo kutoka si ya kitoto (nitaelezea kwenye mada nyingine)

Umetumika vibaya kwenye mapito yako... Angalia wanaokutumia wasikuongoze kwenye anguko kuu
aiseee nimetazama ile video kuna mambo mengi sijayaelewa...........


anyway, ndio dunia!
 
Back
Top Bottom