Mwenyekiti mwenza wa UKAWA Dr Emmanuel Makaidi amewataka wafuasi wa UKAWA kote nchini kutojishughulisha na mchakato wa kumpata mgombea Urais ndani ya CCM.
Dr Makaidi ambaye pia ni Mwenyekiti wa NLD amesema badala yake wanachama wote waendelee kuijenga UKAWA huku wakisubiri kutangazwa mgombea mmoja atayepeperusha bendera ya UKAWA kugombea Urais ambaye pia akishatangazwa kuna uwezekano mkubwa wa kuwa Rais wa Tanzania.
Dr Makaidi aliyekuwa akihutubia mkutano mkubwa wa hadhara mjini Masasi ametangaza pia nia ya kugombea Ubunge Masasi mjini kwa tiketi ya UKAWA.
Ikumbukwe Watanzania wana Imani kubwa na UKAWA na pia wanaamini umoja huo unaoundwa na vyama vya NLD,CHADEMA,NCCR na CUF utapendekeza mgombea mwenye ushawishi mkubwa na uwezo wa kupambana na rushwa na kuwaondolea umaskini.
Chanzo: Chanel ten Habari.