😂 word, kujitunza na kula vizuri.
Mimi na kazi nazofanya muda mwingi nakua ndani, nikitoka nje ni mara chache sana niwe na ishu ya msingi, ikiwemo na kuonana na sadali nichukue stock yangu ya mwezi nitulie.
Watu wanaojua natumia ngwai ni wachache sana, wife hana noma yeye shida alikua analeta nikinywa mitungi na hata hivi zilinikataa ikabidi nitemane nazo.
Hata nyumbani napewa sana kesi za bangi za madogo watoto wa mabinamu niwashauri waache kuvuta bangi, ni neema za mwenyezi tu zinafanya nikubali hiyo kazi lakini deep down natumia nguvu kubwa sana kujizuia nisiwaulize hao watu (mashangazi na madingi) "kwani bangi ina tatizo gani?" 😂