Majini & Mapepo 👻🤔

Majini & Mapepo 👻🤔

Kwani dosho si ni mpaka sasa hapa duniani tunaishi kwa sheria na kanuni ?

Au wewe unataka musema bibilia na Qur’an ndio ziwe sheria?
Ndio tunaishi Kwa kanuni lakini nyingi zinebase kwenye utaifa na ukabila Inatakiwa Sheria moja ya kuunganisha ulimwemgu wote, na most ya Sheria hizo si zipo kwenye vitabu vya dini
 
Ndio tunaishi Kwa kanuni lakini nyingi zinebase kwenye utaifa na ukabila Inatakiwa Sheria moja ya kuunganisha ulimwemgu wote, na most ya Sheria hizo si zipo kwenye vitabu vya dini
Yoooo bro vitabu vya dini vipo aina mbili kuna Waislamu na wa Kristo sasa itakuje?
 
Yoooo bro vitabu vya dini vipo aina mbili kuna Waislamu na wa Kristo sasa itakuje?
Utofauti wao Sana upo kwenye Aina ya kusali ila almost zipo Sawa ndio maana zimewekwa kwenye category ya Abrahamic religion
 
Kuna energy inaitwa NISHAT YA UFAHAM
Bado haijulikan sana, nadhan iyo ndo inayobishaniwa sana kama ipo au haipo ila neno linalotumika n Roho, kwamba Roho ipo au haipo maana ata Mungu ndo iyo iyo Roho.

Nishati hii ipo kwenye damu.
Kwenye damu kuna hewa-pumzi-Uhai-Roho
Pumzi ikikata mtu anafarik-Uhai unatoweka-Roho inaacha mwili.
Sasa hii Roho au nishat inayotengeneza uhai nnn,
Kama imeweza kutengeneza uhai wa mwili wangu inashndikanaje kuwa chanzo cha uhai wa ulimwengu!!?.
 
Nafafanua kama utanielewa.

Mapenzi ya Mungu hayakua binadanu aishi kwa kutafuta pesa
Mapenzi ya Mungu hayakua mwanadamu aishi kwenye gholofa
Mapenzi ya Mungu hayakutaka mwanadamu anywe pombe
Mapenzi ya mungu hayakutaka binadam apike chakula
Mapenzi ya Mungu hayakua binadamu awe msomi
N.k

Nina amini.
Mapenzi ya mungu yalikua
Binadanu wazaliane kama wanyama wengine tena kwa kuzingatia racing husika. Mfano Mzungu kwa mzungu ndo maana kuna namna DNA za sasa za mwafrika huenda zisiwe sawa na wale wa karne ya zamani katika ubora.

Binadam ilipaswa kutembea sio kutumia magari na vingine, ndo maana utaona saiv watu wengi wanafanya jogging sababu ni nature tumeiacha.

Binadamu hatukupaswa kutumia dawa za kizungu, ilibidi tutegemee mazingira na vyakula vilivyotuzunguka maana Mungu alie ruhusu ukae equator region ndo alikupa melanin ya kukomaza ngozi yako ila tunatumia sabuni zenye kemikali kuogea na mwisho tunauziwa vipodoz ili kufanya kazi ya kile tulichokiondoa wenyewe kwa ujuaji wetu

Inshort huenda tungekua wenye nguvu zaidi au wenye afya zaidi kama tusingekua na haya tunayiyaita maendeleo tulionayo.

Emu ondoa akili ya kawaida na jaribu kufikiria out of box.
..May be Mungu karuhusu kifo kwa kitu kisichofaa au kilichovuka mipaka yake ndo maana tunakufa kilasiku na tunazaliana tena sababu Dunia inataka kitu pure na fresh kilichokwenye mipaka yake na ili kisurvive inabidi kikutane na yale mazingira ya asiri ambayo yalishakufa sababu ya hiki tunachoita maendeleo ndo maana kila siku life expectancy inazidi kupungua!!
Mimi siamini katika Mungu mkuu…………. Na kwa sababu umetaja kwamba ni IMANI yako basi Naheshimu maoni ya IMANI yako ambayo kimsingi sio FACT ni Imani tu
 
Mimi siamini katika Mungu mkuu…………. Na kwa sababu umetaja kwamba ni IMANI yako basi Naheshimu maoni ya IMANI yako ambayo kimsingi sio FACT ni Imani tu
Mkuu upo ulimaliza vipi na yule jamaa kuhusu uchawi😅
 
Viumbe vyote viliumbwa kwa hekima , vilikua kuasi baada ya kuumbwa ila wote walikuwa chini ya mamlaka ya Mungu ..Huyo shetani anasingiziwa, wapo binadamu wanafanya unyama kuliko hata shetani , shetani
 
Hello great thinkers 🫡

Sometimes huwa najiuliza, hivi kweli majini na mapepo wapo, au ni chai tu? 🤔

Waislamu wanayaita majini, huku Wakristo wakitumia majina kama mapepo wanapozungumzia viumbe wa kiroho wanaohusishwa na uovu
(Nadhani hivi viumbe wanaviita vya kiroho kwa sababu havionekani sijui sana kuhusu hili)

Twende nalo sasa 👇

1. Majini kwa mujibu wa Uislamu

Kwa mujibu wa mafundisho ya Kiislamu majini ni viumbe ambao Allah aliwaumba
Baadhi yao ni Waislamu na wengine si Waislamu
Hii ni kwa mjibu wa Qur'an yenyewe

Qur’an, Suratul-Jinn 72:14 inasema:

Na hakika miongoni mwetu wapo Waislamu na miongoni mwetu wapo walio madhalimu
Basi wale waliosilimu, hao wameifuata njia iliyo sawa

Pia, Qur’an 55:15 inasema kwamba majini waliumbwa kutokana na mwali wa moto usio na moshi

Hivyo, kwa mujibu wa Qur’an, majini ni viumbe walioumbwa na Allah, na wanaweza kuwa na imani tofauti

Pia baadhi waislamu kuna wanaodai kwamba majini wanaweza kuwa marafiki wa binadamu, na wengine husema kwamba binadamu anaweza hata kushiriki nao ngono(Sex)

Hapo nimeweka rejea ya hizo Aya ili anataka akapitie mwenyewe kuona ukweli ulivyo

2. Mapepo kwa mujibu wa Ukristo

Kwa upande wa Wakristo, tunasikia kuhusu mapepo (demons)
Shetani na malaika walioasi, ambao wanahusishwa na uovu, majaribu na kuwapotosha wanadamu

Kwa mfano, 2 Petro 2:4 inazungumzia malaika waliotenda dhambi na hukumu yao
Pia, Ufunuo 12:7–9 inasimulia kuhusu Shetani na malaika zake kutupwa duniani

Hata hivyo kitu cha ajabu na cha kushangaza
Dini hizi zina mitazamo tofauti kuhusu hawa viumbe wa kiroho
Unaweza ukagundua tofauti iliyopo kwa MAJINI wa Kiislamu na MAPEPO ya wa Kristo

Tena Muslim wao hao majini wana mpaka majina

Ex: kuna majina ambayo tumekuwa tukiyasikia, kama Jini Subiani, Makata, Daruweshi, Sultani na Maimuna nk....

Kama kweli majini wapo kama vitabu vya dini vinavyosena je, kuna namna binadamu anaweza kuwaona au kukutana nao ana kwa ana?

Sasa wana JF mjadala wetu upo hapa 👇

Kama Mungu ndiye aliyewaumba, hakujua kama wataasi?
Kwa sababu Mungu hupewa sifa ya kujua vyote

Kwa mujibu wa imani ya Kiislamu, Allah ndiye aliyewaumba majini. Qur’an 7:27 inawaonya wanadamu kuhusu Shetani na kabila lake ikisema kwamba wao wanawaona wanadamu kutoka mahali ambapo wanadamu hawawezi kuwaona.

Sasa, kama Mungu ndiye aliyewaumba majini na ana ujuzi wa kila kitu, hakujua kwamba baadhi yao wangekengeuka na kuja kuwapotosha binadamu?

Kama alijua hilo kabla hawajaumbwa, kwa nini aliwaumba akijua kwamba baadhi yao wangeasi na kuwa chanzo cha upotoshaji kwa viumbe wengine?

Na kama alikuwa na uwezo wa kuzuia jambo hilo lisitokee, kwa nini hakulizuia tangu mwanzo?

Kwa upande wa Wakristo, Biblia pia inazungumzia malaika walioasi. Katika 2 Petro 2:4, malaika waliotenda dhambi wanatajwa pia

Sasa mkanganyiko kama Mungu aliumba malaika na anajua kila kitu kabla hakijatokea, hakujua kwamba baadhi yao wangeasi?
Kama alijua, kwa nini aliwaumba akijua mwisho wao ungekuwa huo?

Na kama alijua kwamba Shetani angekuja kuwashawishi na kuwapotosha wanadamu, kwa nini alimruhusu aendelee kuwepo na kufanya hivyo?

Kwa nini Mungu aruhusu uovu, halafu aadhibu wanaoufanya?

Kwa mujibu wa mafundisho mbalimbali ya dini, mwanadamu akifanya maovu akatenda dhambi anaweza kuhukumiwa na kuadhibiwa adhabu ya Jahannamu au moto wa milele katika baadhi ya mafundisho

Mimi nazidi kujiuliza

Kama Mungu alijua tangu mwanzo kwamba Shetani, majini au viumbe wengine wangeasi na kujaribu kuwapotosha wanadamu, kwa nini aliruhusu mfumo huo uwepo?

Kwa nini atuache katika mazingira yenye vishawishi na uwezekano wa kupotoshwa, halafu atuhukumu kwa kushindwa kuvishinda?

Kama Mungu ana uwezo wa kuzuia uovu, kwa nini anaruhusu uovu huo uwepo na baadaye kuwaadhibu wale wanaoufanya?

Je, binadamu ni sahihii kuingizwa kwenye mtego mkali hivi?


Na kama Mungu alijua matokeo yote kabla ya kuumba viumbe hivi, kwa nini hakupanga mfumo ambao uovu huo usingetokea, au ambao usingewaweka wanadamu katika hatari ya kupotoshwa?

Mwisho akaahidi kutuchoma moto?

Je, huu ni mtihani wa haki?

Tuchukulie mfano halisi kwamba mtu ametengeneza mfumo, anajua kila kitu kitakachotokea ndani ya mfumo huo kabla haujaanza, na ana uwezo wa kubadilisha matokeo yake
Lakini anaamua kuuacha uendelee, huku akijua kwamba baadhi ya watakaokuwa ndani yake wataanguka na kushindwa

Sasa, ikiwa Mungu ndiye aliyeumba mfumo mzima alijua mwisho wake tangu mwanzo na ana uwezo wa kuzuia matokeo fulani yasitokee, kosa la binadamu liko wapi hasa?

Kwa nini tuwekwe katika mazingira yenye uwezekano wa kupotoshwa na viumbe ambao Mungu mwenyewe alijua wangekengeuka, halafu tuhukumiwe kwa matokeo ya maamuzi yetu?

NB :Kama kweli Mungu yupo kwanini akaumba dunia kwa namna hii
Kwanini atuahidi moto na ni yeye alianzisha
Kosa letu binadamu liko wapi?

ShesRise_1 ✋️


Kwanza nikupongeze kwa kuibua maswali haya. Haya ni maswali ya msingi katika falsafa ya dini, na hata wanatheolojia, wanafalsafa na wanazuoni wa dini wameyajadili kwa karne nyingi.

Lakini nadhani kuna mambo kadhaa ambayo tunapaswa kuyatofautisha kabla ya kufikia hitimisho kwamba Mungu hana haki kwa sababu aliumba viumbe ambao alijua wangekengeuka.

1. Je, kujua jambo kabla halijatokea ni sawa na kulisababisha?

Hapa ndipo kuna msingi wa kwanza wa mjadala.

Tuchukulie unajua rafiki yako ana tabia ya kufanya uamuzi fulani kila anapokutana na mazingira fulani. Ujuzi wako kuhusu atakachofanya haukumlazimisha kufanya uamuzi huo.

Kwa hiyo, katika mtazamo wa kiteolojia, Mungu kujua kwamba Shetani au majini fulani wataasi hakumaanishi kwamba Mungu ndiye aliyewalazimisha kuasi.

Kuna tofauti kati ya kujua kitendo na kusababisha kitendo.

Hata hivyo, nakubali kwamba swali la kwa nini Mungu aliamua kuwaumba huku akijua matokeo yake bado linahitaji kujibiwa. Hapo ndipo mjadala wa hiari ya viumbe na hekima ya Mungu unapoanzia.

2. Kwa nini Mungu aumbe viumbe wenye uwezo wa kufanya maovu?

Katika mafundisho ya Kiislamu, mwanadamu na majini wamepewa uwezo wa kuchagua. Qur'an 18:29 inazungumzia suala la kuchagua kuamini au kukataa.

Hoja ya hapa ni kwamba dunia si mahali ambapo kila kiumbe kimepangiwa kutenda jambo moja bila hiari.

Kama mtu hana uwezo wa kuchagua kati ya kutenda haki na kutenda uovu, je, tunaweza kusema ana sifa ya kimaadili ya kuchagua kutenda mema?

Fikiria mtu ambaye hawezi kabisa kusema uongo kwa sababu hana uwezo wa kufanya hivyo. Je, tunapaswa kumpongeza kwa kuwa mwaminifu kwa kiwango sawa na mtu ambaye anaweza kusema uongo lakini anachagua kusema ukweli?

Hivyo, katika mtazamo huu, uwezekano wa kufanya uovu una uhusiano na uwezekano wa kuchagua mema kwa hiari.

3. Je, Shetani ndiye anayemlazimisha mwanadamu kufanya dhambi?

Hapa kuna Aya muhimu sana ambayo ningependa uisome.

Qur'an 14:22 inasimulia mazungumzo ya Shetani na watu baada ya hukumu. Shetani anasema kwa maana kwamba hakuwa na mamlaka ya kuwalazimisha, bali aliwaita na wao wakamuitikia.

Hili ni jambo muhimu sana katika teolojia ya Kiislamu: Shetani anashawishi, lakini mwanadamu anabaki na wajibu wa maamuzi yake.

Kwa hiyo, si sahihi kusema kwamba mtu anafanya dhambi kwa sababu tu Shetani yupo.

Vivyo hivyo, Yakobo 1:13 katika Biblia inafundisha kwamba Mungu hamjaribu mtu kwa uovu. Hivyo hata katika Ukristo kuna tofauti kati ya Mungu na chanzo cha majaribu.

4. Kwa nini Mungu asimwangamize Shetani tangu mwanzo?

Hili ni swali zuri. Lakini tunapaswa kujiuliza pia: je, kuondoa kila uwezekano wa uovu ndilo suluhisho pekee linalowezekana?

Katika mtazamo wa dini, maisha ya duniani ni kipindi cha uwajibikaji na mtihani. Mungu kuruhusu jambo litokee hakumaanishi kwamba ameliridhia.

Kwa mfano, mahakama inaweza kumruhusu mtuhumiwa kuendelea kuishi hadi siku ya hukumu, lakini hilo halimaanishi kwamba mahakama imeunga mkono kosa lake.

Tofauti ni kwamba katika mafundisho ya dini, hukumu ya Mungu inahusishwa na ujuzi kamili, haki na kutokosea kwake.

5. Je, ni haki kumuadhibu mwanadamu wakati Mungu alijua angefanya dhambi?

Hapa ningependa uangalie Qur'an 2:286:

"Mwenyezi Mungu haikalifishi nafsi yoyote ila kwa kadiri ya iwezavyo."

Pia Qur'an 17:15 inafundisha kwamba Mungu haadhibu mpaka ujumbe ufikishwe.

Hizi ni kanuni muhimu katika uelewa wa Kiislamu kuhusu uwajibikaji. Mwanadamu hahukumiwi kwa sababu tu alizaliwa duniani, bali kwa matendo yake, nia yake na wajibu wake.

Mungu anajua mazingira ya kila mtu, kiwango cha ufahamu wake na uwezo wake. Hivyo, hukumu ya Mungu haiwezi kulinganishwa na hukumu ya mwanadamu mwenye taarifa chache.

Na kuhusu moto wa Jahannamu, katika Uislamu si kila mtu anahukumiwa kwa kiwango kimoja. Kuna tofauti kati ya makusudi, kulazimishwa, ujinga, toba na mazingira ya mtu. Pia rehema ya Allah ni sehemu kubwa sana ya mafundisho ya Kiislamu.

6. Lakini kuna jambo ambalo nataka ulifikirie zaidi.

Unasema kama Mungu alijua kwamba viumbe fulani wataasi, basi asingewaumba.

Lakini kwa nini tunachukulia kwamba ulimwengu ambao hakuna kiumbe anayeweza kuchagua kufanya uovu ndio ulimwengu pekee ambao ungekuwa na maana?

Kwa nini tusifikirie uwezekano wa ulimwengu ambao una viumbe wenye uwezo wa kuchagua, kuwajibika, kupenda, kusamehe, kujitolea na kutenda haki, ingawa pia wanaweza kufanya kinyume chake?

Hii si kusema kwamba kila mateso yanayoonekana duniani yanaelezeka kwa urahisi. Kwa mfano, vipi kuhusu mtoto anayezaliwa na ugonjwa, majanga ya asili au mateso ya watu wasio na hatia? Haya ni maswali mazito ambayo hoja ya hiari pekee haiwezi kuyajibu kikamilifu. Wanazuoni wa dini huyajadili kupitia hekima, mtihani, maisha ya Akhera na haki ya mwisho.

Lakini kutokuwa na jibu kamili kwa kila aina ya mateso si ushahidi wa moja kwa moja kwamba Mungu hayupo.

7. Mwisho, kuhusu majini na mapepo.

Kisayansi, hakuna uthibitisho wa majaribio unaokubalika kwa pamoja unaothibitisha kuwepo kwa majini kama wanavyoelezwa katika vitabu vya dini. Hivyo mtu anaweza kuhoji suala hilo kwa mtazamo wa ushahidi wa kisayansi.

Lakini ni muhimu kutofautisha dai la kisayansi na imani ya kidini. Kutokuonekana kwa kiumbe hakuthibitishi moja kwa moja kwamba hakipo, wala hakuthibitishi kwamba kipo.

Pia, majini katika Uislamu si sawa kabisa na mapepo katika mafundisho ya Kikristo. Katika Qur'an 72:11-15, majini wanaelezwa kuwa na makundi yenye misimamo tofauti, wakiwemo wanaoamini na wasiotenda haki. Hii ni tofauti na dhana ya mapepo katika baadhi ya mitazamo ya Kikristo.

Kwa hiyo, tusichanganye mafundisho haya.

Kuwa na maswali kuhusu Mungu si kosa. Hata watu wa imani wamekuwa wakiuliza maswali hayo. Lakini pia hatupaswi kudhani kwamba kwa sababu hatujaelewa sababu ya jambo fulani, basi jambo hilo halina sababu.

Unaweza kuhoji kwa nini Mungu aliumba viumbe wenye uwezo wa kuasi, lakini ili uwe na hoja kamili, unahitaji pia kujibu swali hili:

Je, uwepo wa hiari, uwezo wa kuchagua, uwajibikaji na uwezekano wa kutenda mema una thamani yoyote ya kimaadili, au ungekuwa bora zaidi kama Mungu angeumba viumbe wasioweza kufanya uchaguzi wowote?

Hapo ndipo mjadala wa kweli ulipo.
 
Back
Top Bottom