Majini & Mapepo 👻🤔

Majini & Mapepo 👻🤔

Sijasoma Uzi wako ni mrefu sana ila ninachokumbuka kuna ndugu yetu mmoja wa kike alikuwaga na majini miaka ya 90 yalikuwa yanapanda kabisa ila siku hizi sioni hizo mambo nahisi wale majini waliamua kurudi kwao baada ya kuona hali ngumu hapa Bongo😐
Acha uvivu soma bana😒
 
Hivi ShesRise_1 argument yako ni kuwa hakuna kabisa creator au unahisi yupo ila sivyo kama wanavyodai watu wa dini za Abraham
Nikitumia reason naona kabisa kuna mtu alikaa akaunda gari
Nyumba ikisimama kuna mtu kaijenga nk..... I mean kila kitu tunachokiona kuna muanzilishi behind

Kwa mantiki hiyo hata hii dunia inaweza kua ina creator lakini sitaki kuamini kua huyo creator ni huyo wa kwenye vitabu vya dini Ukiosoma kwa akili bila vitisho ni kama tumepigwa
 
Sio lazima kujua habari za Mungu kupitia dini.
Ahaaa sawa
I can tell you about myself. Mimi nimezaliwa kwenye familia ya dini lakini nilikua siamini hizo mambo kabisa.
Vizuri mkuu
Imani yangu ilikua ni kupata utajiri kwa njia yoyote ile. Nimekaa miaka saba sijawahi kuingia kanisani.
Aiseee sijawahi kufika huku noma
Nilikua ni mlevi, mvuta bangi na wale vijana wa makundi namimi nilikua ndio kundi lenyewe, thanks God alinipa akili ya kujitambua tuu.

Nikiwa chuo mwaka wa kwanza mimi nimeuza bangi sana, na hiyo ndio ilikua plan ya kuutafuta utajiri. Club zote maarufu Dar kwa miaka ya 2010-2014 ndio vilikua viwanja vyangu. Nimeshinda sana club sansiro, bilcanas na pale sinza africasana pamoja na ambiance.
Mambo ya kula maisha hongera na pole pia
Mungu aliingilia kati nikajikuta nimeokoka pasipo mtu yoyote kuniambia okoka. Hapa ndipo nilimjua Mungu.
Hapa kwenye kuokoka unapatengaje na dini?
Baada ya kuokoka nilipata amani ambayo sijawahi kuiona maishani mwangu, Yaani amani ambayo siwezi kumsimulia mtu akaelewa. Hicho ndicho kitu pekee Cha tofauti nilikigundua baada ya kuokoka.
Hongera sana mkuu
Niliokoka kanisani na hiyo ndio ilikua njia ya kujifunza habari za Mungu.
Hapa upo kwenye ile line uliyoikataa ya dini
Baada ya kuokoka nilikua nakwenda kanisani vizuri tuu na pia nilikua najifunza mahubiri ya mchungaji wangu. Lakini sio Kila alichokuwa anahubiri mchungaji nilikipokea kama kilivyo. Na hapa ndipo ilianza safari nyingine mpya ya Mimi kumjua Mungu zaidi.
kubali tu kua uokovu wako ulikua sambamba na dini licha ya kua kule juu umesema unaweza kumjua Mungu bila dini
Nilianza kusoma biblia Mimi binafsi na pia nilianza kuyachunguza maandiko.
Mimi pia hufanya hivyo na ndio maana napata maswali na mashaka kuhusu
Maandiko ya hivi vitabu vya dini
Wachungaji wengi wanafundisha watu habari za mbinguni tuu kitu ambacho sio kweli. Mungu angekua anataka twende mbinguni basi angetuua wote ili twende mbinguni tukapumzike na kukuthibitishia hili wewe nenda kasome biblia Kuna mahali katika kitabu Cha Yohana Mtakatifu YESU anatoa ripoti kwa baba yake ambaye ni Mungu anamwambia "SISEMI KWAMBA UWATOE DUNIANI LAKINI WAPE USAIDIZI" hivyo tunapookoka ni kwamba tunafanyika watoto wa Mungu na kwa hilo tunapewa usaidizi wa kutenda jambo lolote hapa duniani, Sawa sawa na neno katika Wakorinto linasema "NAYAWEZA MAMBO YOTE KATIKA YEYE ANITIAYE NGUVU".
Kwahiyo injili ya kwenda mbinguni ni batili?
Maana umesema kama Mungu angetaka angetuua wote na tukaenda mbinguni
Kuhitimisha naweza kusema kwamba dini ni msingi wa kumjua Mungu lakini sio lazima ujifunze kupitia dini, wewe soma biblia na Roho Mtakatifu akuongoze bhasi.
Roho mtakatifu nampataje?
Nasema soma biblia kwasababu hapa katika maisha ya kawaida ni Kuna watu wanajua vitu vingi na shule hawajaenda Wala Nini.
naunga mkono hoja
Nimalizie kwa kukuuliza swali kwani alieandika mitaala ya shuleni na vitabu yeye alifundishwa na nani? Ukipata jibu hapa bhasi jua kwamba hata Mungu unaweza kumjua pasipo kupitia hiyo njia ya dini.
mitaala ya shule iliandikwa na mtu mmoja?
nitafatilia kuhusu hili sitaki kutoa jibu bila uhakika

licha cha kua huenda ni wazo lilovumbuliwa na mtu na pengine akaamua kushirikisha wengine

Kwahiyo unasema Mungu mwenyewe anaweza kujifunua kwako si ndio

kama ni hivyo basi ajifunue kwangu pia
Mkuu ni lazima uelewe kwamba dini ni Mpango wa mwanadamu kumtafuta Mungu. Lakini pia katika dini yamejaa maslahi ya mwanadamu kwa kutumia jina la Mungu. Nitakupa na mifano yake

Mosi: Wakoloni walitawala Africa pamoja na America kwa kutumia njia ya dini. Kasome historia ya Marekani na ukoloni.

Pili: Dini zinatumika kwa maslahi ya watu ili kuuza silaha, Zingatia wale watu walioaminishwa kwamba wakifa wanapigania dini wataenda peponi.

Tatu: Dini ni chanzo Cha mapato hasa hasa nchi za Africa, angalia wachungaji wanavyomiliki Mali za ajabu huku waumini wao wakikosa nauli na wengine wanalala njaa. Waumini wanajenga shule, mahospitali lakini wanashindwa kusomesha watoto wao wala kutibiwa katika hospital walizozijenga wao wenyewe.

Nne: Dini zinatumika kama chanzo Cha taarifa za kijasusi. Zamani wakati wa utawala wa Roma ilikua ngumu sana kupata taarifa za mauaji na hasa hasa mauaji ya Siri hivyo wakaja na mbinu inaitwa kitubio. Kwamba waumini wa Roman Catholic wanatakiwa kwenda mbele ya padri na kukiri dhambi zake zote na huu utaratibu Hadi Leo unaendelea katika kanisa la Roman. Hii ilikua ni mbinu ya kupata taarifa za uhalifu pasipo watu kujua. Zingatia zamani hizo dini ilikua ni Moja tuu ambayo ndio Roman Catholic church

Tano: Serikali za Dunia nzima zinafaidika sana na uwepo wa dini kwasababu dini zinawapa watu matumaini hivyo kupunguza mzigo wa mashinikizo kwa serikali na pia wanasiasa wanapata unafuu. Ndio maana hapa bongo utaona wanasiasa wetu hawaishi kwenda makanisani na Kuna muda unasikia serikali imewapa kanisa Fulani fedha au Kuna wachungaji Fulani Fulani wamepata milungula. Zingatia fedha za Escrow mpaka wachungaji na mapadri walipata gawio😂😂😂🤗

Yapo mengi sana ya kuandika lakini naomba niishie hapa, huku nilipo mvua inanyesha sana Leo na shughuli zangu zinasuasua.
Kwa maelezo yote haya upo sahihi lakini kumbuka na wewe uliokoka huko huko kanisani kwa wapiga dili😅😅😅
Hapana dini ndio zimetumia vitabu vitakatifu kujianzisha. Binafsi sijawahi kuisoma kuruani ila nikisikiaga baadhi ya mahubiri ya masheikh huwa naona kuruani na biblia tofauti yake ni ndogo sana.

Kwenye biblia anaitwa YESU kwenye kuruani wanamwita Issa bin Mariam.
Manabii wengine wote pia waliopo kwenye biblia wanatambulika katika kuruani pia.
Bibilia ni kitabu kikongwe kuliko Qur’an
QUR’AN ni copy ya bibilia hasa agano la kale kwenye bibilia
Ni kama mtu aliamua kuboresha tu kuondoa vitu Fulani kuongeza vitu fulani
Ukitaka kujua historia ya dini inabidi ukasome historia ya Roma Empire. Roma empire imetawala Dunia muda mrefu sana na Roman Empire ndio chanzo Cha dini na dini ya kwanza kabisa ni Roman Catholic Church.

Achana na Uyahudi, uyahudi ilikua ni tamaduni za watu wa Israel na ndio maana hata Pilato alikataa kumuhukumu Bwana YESU.

Kwa kifupi dini ya kwanza ni Roman Catholic church, ikafuatia dini ya Lutheran, Martin Luther alianzisha Lutheran church baada ya kuona Roman inatumika kukandamiza watu. Yaan Roman ilitumia biblia kuwatumikisha watu na ndio maana waumini wa Roman Catholic hadi Leo hawana utamaduni wa kusoma biblia. Yaani wao biblia anaisoma padri tuu bhasi.

Baada ya Martin Luther dini iliofuatia ni Anglican na hii dini alikuja baada ya Mfalme wa Uingereza kutaka kuoa mke mwingine na Roman Catholic church wakamkatalia hivyo Mfalme wa Uingereza aliamua kuanzisha kanisa lake na kuwaamuru waingereza wote kusali katika kanisa lake. Anglican church ndio kanisa la kwanza duniani kuruhusu ndoa za jinsia moja binafsi hata sikushangazwa kutokana na historia yake.
Ahaaaaa we mjuzi wa mambo kweli kweli nimeipenda hiii 🔥🔥
Hivyo dini hazikuleta vitabu vitakatifu Bali dini zinatumia vitabu vitakatifu.
Vitabu vitakatifu vilikuja kujaje mkuu
 
Shukran mkuu 🙏
Karibu sana
Ninachoweza tu kusema kuna mambo mengi sana tunapigwa kwenye hizi Imani zetu. Mi kuna wakati nachukulia haya mambo ya mapepo, majini, sijui moto wa milele nk ni wajanja wachache tu waliamua kutukondoosha ili tujikute tunayatafakari na wakati mwingine kuyaamini mawazo Yao.

Nadhani unapofariki dunia kila kitu kinakoma hapo labda kama Mungu au nature itaamua kukutumia vinginevyo huko baadaye. Maana chukulia unapokuwa umelala fofofo hakuna kitu unachokuwa unakumbuka hujui jinsia yako, hujui kama una familia, unaishi wapi, umelala wapi, jina lako Nani, Una elimu gani nk yaani kila kitu haujui hata kama una watoto 1000 humjui hata mmoja usingizini, sasa kama huo ni usingizi tu ebu fikiria juu ya kifo.
 
Nikitumia reason naona kabisa kuna mtu alikaa akaunda gari
Nyumba ikisimama kuna mtu kaijenga nk..... I mean kila kitu tunachokiona kuna muanzilishi behind

Kwa mantiki hiyo hata hii dunia inaweza kua ina creator lakini sitaki kuamini kua huyo creator ni huyo wa kwenye vitabu vya dini Ukiosoma kwa akili bila vitisho ni kama tumepigwa
Kama Una amini kuna creator basi huoni kuwa kuna haja ya kuweka guidelines na Sheria za jinsi ya kuishi, maana kama ameweza kuweka ulimwemgu vizuri basi vyovyote vile lazima atakuwa ni intelligent being na lazima aweke Sheria kwenye nyumba yake na hizo Sheria kuna Ambazo zitakuwa ni strict na punishment inahitajika ili kuweka balance
 
Ninachoweza tu kusema kuna mambo mengi sana tunapigwa kwenye hizi Imani zetu. Mi kuna wakati nachukulia haya mambo ya mapepo, majini, sijui moto wa milele nk ni wajanja wachache tu waliamua kutukondoosha ili tujikute tunayatafakari na wakati mwingine kuyaamini mawazo Yao.
Kabisa mkuu mie zamani nilikua mnazi wa dini sana
Mtu akiona hivi anadhani naongea kitu nisichokijua naelewa sana ninachosema

Mashaka yangu tu yamebaki kwenye ndoto mara nyingi sana nikiota ndoto hua kweli nikiwaza kitu hua mara nyingi kuna ukweli nikija kugundua baadae inakua too late
Nadhani unapofariki dunia kila kitu kinakoma hapo labda kama Mungu au nature itaamua kukutumia vinginevyo huko baadaye. Maana chukulia unapokuwa umelala fofofo hakuna kitu unachokuwa unakumbuka hujui jinsia yako, hujui kama una familia, unaishi wapi, umelala wapi, jina lako Nani, Una elimu gani nk yaani kila kitu haujui hata kama una watoto 1000 humjui hata mmoja usingizini, sasa kama huo ni usingizi tu ebu fikiria juu ya kifo.
Wanasema ukilala ni nusu ya kifo sasa ukifa itakumbuka nini?
Ni kama wajanja walianzisha dini ili watutawale
 
Ahaaa sawa
🤝
Vizuri mkuu
🙏🙏🙏🙏
Aiseee sijawahi kufika huku noma
Ni maisha tuu, and still this dream live in me.

Mambo ya kula maisha hongera na pole pia
Siwezi kupokea Hongera mpaka uniambie pole ya Nini hii. Tafadhari niambie kwa upole mkuu😊😊🫣

Hapa kwenye kuokoka unapatengaje na dini?

Kuokoka sio dini, kuokoka ni kumkiri YESU Kristo kuwa ni Bwana na mwokozi wa maisha yako. Kumkiri YESU hakuhusiani chochote na kanisa lolote wala dini yoyote. Na ndio maana Bwana YESU hakuacha kanisa Wala hakujenga kanisa na wala hajawahi kuwaamuru watu wejenge kanisa.

Bwana YESU hajawahi kukaa nyumbani kwa makuhani Wala kwa wazee wa kanisa, Bwana YESU hakuwatoa wanafunzi wake hekaluni wala kanisani Bali wanafunzi wa YESU walipatikana kutoka katika shughuli zao. Mfano Petro alikua mvuvi na YESU alimuita kutoka katika uvuvi.

Bwana YESU alikwenda nyumbani kwa mtoza ushuru akala chakula na kunywa. Zingatia mtoza ushuru alionekana kama mtu mbaya na asiyefaa kabisa mbele za uso wa watu wa makanisani lakini YESU ndio alikwenda kwake, Pia watu walimsema vibaya Bwana YESU kwamba anaketi na kula pamoja na watoza ushuru na jibu lake lilikua jepesi tuu kwamba nimekuja ili kukitafuta kilichopotea.

Mfano wa mwisho ni yule mwanamke kahaba, yeye alikubalika mbele za Yesu. Lakini je! alikua ni mtu wa kanisani? Unaona kwamba ili kumpata YESU hakuitaji kwenda kanisani au kuwa Mtakatifu sana bali kunahitaji kuwa na moyo wa utayari wa kumjua Bwana YESU.

Hongera sana mkuu
🙏🙏🙏🙏

Hapa upo kwenye ile line uliyoikataa ya dini
Labda nitolee maelezo kidogo, binafsi nimemjua Mungu kupitia dini lakini watoto wangu au watu wengine waliokaribu namimi siwezi kuwashauri wapitie katika dini ili kumjua Mungu.

Nitawaambia wamkiri YESU Kristo kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yao alafu nitawashauri waanze kusoma biblia na Mungu atajidhihirisha kwao.

kubali tu kua uokovu wako ulikua sambamba na dini licha ya kua kule juu umesema unaweza kumjua Mungu bila dini
Mkuu nimesali kanisani miaka 5 tuu, kwasasa nakwenda mwaka wa3 sijawahi kuingia kanisa lolote, lakini siachi kusali na Mungu HAACHI kujibu maombi yangu.

Mimi pia hufanya hivyo na ndio maana napata maswali na mashaka kuhusu
Maandiko ya hivi vitabu vya dini
Sahihi, lakini unaweza kuwa unasoma biblia kama story.

Okoka kwanza alafu ndio uanze kusoma biblia.

Kwahiyo injili ya kwenda mbinguni ni batili?
Maana umesema kama Mungu angetaka angetuua wote na tukaenda mbinguni
Unakosea kusema ni batili.

Mungu alipomuumba mwanadamu hakumuumba ili akaishi mbinguni HAPANA, mwanadamu aliumbwa ili atawale na kumiliki hapa duniani. Hivyo injili ya kwenda mbinguni sio batili Bali ni kwamba tutakwenda mbinguni na kurudi kuishi hapa duniani tena.

Ukisoma biblia kuna sehemu Yesu anawafundisha wanafunzi wake kusali anasema salini hivi " BABA YETU ULIYE MBINGUNI JINA LAKO LITUKUZWE, UFALME WAKO UJE, MAPENZI YAKO YATIMIZWE HAPA DUNIANI KAMA HUKO MBINGUNI, UTUPE LEO RIDHIKI YETU NA UTUSAMEHE MAKOSA YETU KAMA NASI TUNAVYOWASAMEHE WALIOTUKOSEA, USITUTIE MAJARIBUNI LAKINI UTUOKOE NA YULE MWOVU, KWA KUWA UFALME NI WAKO NA NGUVU NA UTUKUFU NA HATA MILELE AMEN."

Katika hiyo sala tunaona kwamba UFALME wa Mungu unatakiwa kuja hapa duniani, Je? ni nani wa kuuleta huo UFALME? Unadhani huo UFALME unakuja kwaajili ya nani?

Pia ukisoma biblia inasema Mungu hatofanya jambo lolote hapa duniani pasipo mwanadamu. Sasa huo UFALME nani atakae uleta hapa duniani kama Mungu hawezi kutenda jambo hapa duniani pasipo mwanadamu?

Mwisho utakubaliana namimi kwamba wachungaji wengi wanahubiri habari za mbinguni either kwa kujua au kutokujua. Wengi wa wachungaji wanahubiri hivi ili kuwavunja watu moyo na kuchukua fedha zao bhasi.

Ndio maana Bwana Yesu alisema kwamba siku za mwisho wengi watakuja kwa jina langu. Na endapo yakitukia haya na wakasema Yesu ameonekana huku au kule wewe usiende. Hivyo kupitia hili andiko utakubaliana namimi kwamba hatuupati wokovu katika dini Bali tunaupata wokovu kwa kumuamini Bwana Yesu na kusoma maandiko ya biblia.

Roho mtakatifu nampataje?
Baada ya kumpokea Yesu kuwa Bwana na mwokozi wa maisha Yako. Kwa kufanya hivyo utampokea Roho Mtakatifu.

naunga mkono hoja
🙏🙏🙏

mitaala ya shule iliandikwa na mtu mmoja?
nitafatilia kuhusu hili sitaki kutoa jibu bila uhakika

Chanzo cha elimu ni huko ugiriki, wao walifanya hivyo kwaajili ya falsafa zao. Ukisoma historia ya ugiriki na hao akina Plato, Aristotle na wenzao utaelewa vizuri.

Mantiki ya swali langu ni kwamba nilitaka ujiulize Isaac Newton alifundishwa na nani kuhusu physics and Law's?

licha cha kua huenda ni wazo lilovumbuliwa na mtu na pengine akaamua kushirikisha wengine

Kwahiyo unasema Mungu mwenyewe anaweza kujifunua kwako si ndio

kama ni hivyo basi ajifunue kwangu pia

Exactly, Mungu anaweza kujifunua kwako pia na hata sasahivi anaweza kufanya hivyo.

Cha msingi ni kwamba umkiri YESU KRISTO KUWA NI BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YAKO, kubali kutoka moyoni mwako kwamba Bwana Yesu aliacha enzi na mamlaka akashuka duniani akateswa, akasulubishwa na akatundikwa msalabani kwaajili yangu. Hivyo kupitia kifo chake na kufufuka kwake Mimi (taja jina lako) nimesamehewa dhambi zangu na nimefanyika mwana wa Mungu, hivyo ninahaki zote kutoka kwa Mungu kwasababu nimehesabiwa kuwa mwana wake kupitia Kristo YESU.

Tangu saa hiyo utakapo tamka maneno hayo amini lolote utakalomuomba Mungu amini kwamba amekupatia, haijalishi ni gumu kiasi Gani au Lina uzito kiasi Gani wewe amini kwamba limekwisha kuwa. Kama unahitaji kufanya kitu wewe nenda kakifanye utamuona Mungu huko huko.

Kwa maelezo yote haya upo sahihi lakini kumbuka na wewe uliokoka huko huko kanisani kwa wapiga dili😅😅😅
Ilikua ni njia tuu ambayo ilibidi nipitie, hata YESU alikwenda katika masinagogi na ni hao hao waliomsurubisha.

Bibilia ni kitabu kikongwe kuliko Qur’an
QUR’AN ni copy ya bibilia hasa agano la kale kwenye bibilia
Ni kama mtu aliamua kuboresha tu kuondoa vitu Fulani kuongeza vitu fulani

Anhaa nimekuelewa hapa🙏🙏🙏, sitaki kuongeza neno.

Ahaaaaa we mjuzi wa mambo kweli kweli nimeipenda hiii 🔥🔥
Asante mkuu, nakukubali sana pia nakubali sana maada zako.

Thanks much and much appreciation to you.
Vitabu vitakatifu vilikuja kujaje mkuu
Kwangu Mimi naamini biblia ni mafunuo ya Mungu kwa wanadamu, lakini pia mengine ni historia ya yale Mungu alitenda kupitia manabii,.mitume na Bwana Yesu.
 
Kama Una amini kuna creator basi huoni kuwa kuna haja ya kuweka guidelines na Sheria za jinsi ya kuishi, maana kama ameweza kuweka ulimwemgu vizuri basi vyovyote vile lazima atakuwa ni intelligent being na lazima aweke Sheria kwenye nyumba yake na hizo Sheria kuna Ambazo zitakuwa ni strict na punishment inahitajika ili kuweka balance
Kwani dosho si ni mpaka sasa hapa duniani tunaishi kwa sheria na kanuni ?

Au wewe unataka musema bibilia na Qur’an ndio ziwe sheria?
 
🤝

🙏🙏🙏🙏

Ni maisha tuu, and still this dream live in me.
Sawa mkuu
Siwezi kupokea Hongera mpaka uniambie pole ya Nini hii. Tafadhari niambie kwa upole mkuu😊😊🫣
Kwa kuruka viwanja kula maisha mkuu maana umekula starehe zote umeridhika ukageukia wokovu kwahiyo ladha ya maisha unaijua na ladha ya wokovu unaijua

We ni mnomaa sana
Kuokoka sio dini, kuokoka ni kumkiri YESU Kristo kuwa ni Bwana na mwokozi wa maisha yako. Kumkiri YESU hakuhusiani chochote na kanisa lolote wala dini yoyote. Na ndio maana Bwana YESU hakuacha kanisa Wala hakujenga kanisa na wala hajawahi kuwaamuru watu wejenge kanisa.

Bwana YESU hajawahi kukaa nyumbani kwa makuhani Wala kwa wazee wa kanisa, Bwana YESU hakuwatoa wanafunzi wake hekaluni wala kanisani Bali wanafunzi wa YESU walipatikana kutoka katika shughuli zao. Mfano Petro alikua mvuvi na YESU alimuita kutoka katika uvuvi.

Bwana YESU alikwenda nyumbani kwa mtoza ushuru akala chakula na kunywa. Zingatia mtoza ushuru alionekana kama mtu mbaya na asiyefaa kabisa mbele za uso wa watu wa makanisani lakini YESU ndio alikwenda kwake, Pia watu walimsema vibaya Bwana YESU kwamba anaketi na kula pamoja na watoza ushuru na jibu lake lilikua jepesi tuu kwamba nimekuja ili kukitafuta kilichopotea.
sasa mkuu wewe habari za Yesu ungezijuaje bila watu wadini maana wao ndio hufundisha habari zake
Mfano wa mwisho ni yule mwanamke kahaba, yeye alikubalika mbele za Yesu. Lakini je! alikua ni mtu wa kanisani? Unaona kwamba ili kumpata YESU hakuitaji kwenda kanisani au kuwa Mtakatifu sana bali kunahitaji kuwa na moyo wa utayari wa kumjua Bwana YESU.


🙏🙏🙏🙏


Labda nitolee maelezo kidogo, binafsi nimemjua Mungu kupitia dini lakini watoto wangu au watu wengine waliokaribu namimi siwezi kuwashauri wapitie katika dini ili kumjua Mungu.

Nitawaambia wamkiri YESU Kristo kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yao alafu nitawashauri waanze kusoma biblia na Mungu atajidhihirisha kwao.
Sasa wao watamjuaje Yesu na kumkiri bila msaada wa watu wa dini maana wao ndio hutoa mafundisho
Mkuu nimesali kanisani miaka 5 tuu, kwasasa nakwenda mwaka wa3 sijawahi kuingia kanisa lolote, lakini siachi kusali na Mungu HAACHI kujibu maombi yangu.
Mungu haachi kujibu maombi yako ?
Basi niombee nina shida na 500k leo leo mkuu 😢🤣
Sahihi, lakini unaweza kuwa unasoma biblia kama story.
Hapana nasoma na kuchambua kwa kina
Okoka kwanza alafu ndio uanze kusoma biblia.
Bila wokovu siwezi kujua ?

Unakosea kusema ni batili.

Mungu alipomuumba mwanadamu hakumuumba ili akaishi mbinguni HAPANA, mwanadamu aliumbwa ili atawale na kumiliki hapa duniani. Hivyo injili ya kwenda mbinguni sio batili Bali ni kwamba tutakwenda mbinguni na kurudi kuishi hapa duniani tena.
Haya ulisema wewe kua wachungaji wanakosea kufundisha habari za kwenda mbinguni
ndio na mimi ni kakuuliza je kufundisha injili ya kwenda mbinguni ni ubatili?
Ukisoma biblia kuna sehemu Yesu anawafundisha wanafunzi wake kusali anasema salini hivi " BABA YETU ULIYE MBINGUNI JINA LAKO LITUKUZWE, UFALME WAKO UJE, MAPENZI YAKO YATIMIZWE HAPA DUNIANI KAMA HUKO MBINGUNI, UTUPE LEO RIDHIKI YETU NA UTUSAMEHE MAKOSA YETU KAMA NASI TUNAVYOWASAMEHE WALIOTUKOSEA, USITUTIE MAJARIBUNI LAKINI UTUOKOE NA YULE MWOVU, KWA KUWA UFALME NI WAKO NA NGUVU NA UTUKUFU NA HATA MILELE AMEN."
Hapa nina story ila leo naiweka kapuni
Katika hiyo sala tunaona kwamba UFALME wa Mungu unatakiwa kuja hapa duniani, Je? ni nani wa kuuleta huo UFALME? Unadhani huo UFALME unakuja kwaajili ya nani?

Pia ukisoma biblia inasema Mungu hatofanya jambo lolote hapa duniani pasipo mwanadamu. Sasa huo UFALME nani atakae uleta hapa duniani kama Mungu hawezi kutenda jambo hapa duniani pasipo mwanadamu?

Mwisho utakubaliana namimi kwamba wachungaji wengi wanahubiri habari za mbinguni either kwa kujua au kutokujua. Wengi wa wachungaji wanahubiri hivi ili kuwavunja watu moyo na kuchukua fedha zao bhasi.

Ndio maana Bwana Yesu alisema kwamba siku za mwisho wengi watakuja kwa jina langu. Na endapo yakitukia haya na wakasema Yesu ameonekana huku au kule wewe usiende. Hivyo kupitia hili andiko utakubaliana namimi kwamba hatuupati wokovu katika dini Bali tunaupata wokovu kwa kumuamini Bwana Yesu na kusoma maandiko ya biblia.


Baada ya kumpokea Yesu kuwa Bwana na mwokozi wa maisha Yako. Kwa kufanya hivyo utampokea Roho Mtakatifu.
Sawaaa mtumishi 😊
🙏🙏🙏



Chanzo cha elimu ni huko ugiriki, wao walifanya hivyo kwaajili ya falsafa zao. Ukisoma historia ya ugiriki na hao akina Plato, Aristotle na wenzao utaelewa vizuri.

Mantiki ya swali langu ni kwamba nilitaka ujiulize Isaac Newton alifundishwa na nani kuhusu physics and Law's?



Exactly, Mungu anaweza kujifunua kwako pia na hata sasahivi anaweza kufanya hivyo.

Cha msingi ni kwamba umkiri YESU KRISTO KUWA NI BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YAKO, kubali kutoka moyoni mwako kwamba Bwana Yesu aliacha enzi na mamlaka akashuka duniani akateswa, akasulubishwa na akatundikwa msalabani kwaajili yangu. Hivyo kupitia kifo chake na kufufuka kwake Mimi (taja jina lako) nimesamehewa dhambi zangu na nimefanyika mwana wa Mungu, hivyo ninahaki zote kutoka kwa Mungu kwasababu nimehesabiwa kuwa mwana wake kupitia Kristo YESU.

Tangu saa hiyo utakapo tamka maneno hayo amini lolote utakalomuomba Mungu amini kwamba amekupatia, haijalishi ni gumu kiasi Gani au Lina uzito kiasi Gani wewe amini kwamba limekwisha kuwa. Kama unahitaji kufanya kitu wewe nenda kakifanye utamuona Mungu huko huko.


Ilikua ni njia tuu ambayo ilibidi nipitie, hata YESU alikwenda katika masinagogi na ni hao hao waliomsurubisha.
Aiseeeeee
Anhaa nimekuelewa hapa🙏🙏🙏, sitaki kuongeza neno.
Shukran usiongeze
Asante mkuu, nakukubali sana pia nakubali sana maada zako.

Thanks much and much appreciation to you.
Nakukubali pia mtumishi wa bwana
Kwangu Mimi naamini biblia ni mafunuo ya Mungu kwa wanadamu, lakini pia mengine ni historia ya yale Mungu alitenda kupitia manabii,.mitume na Bwana Yesu.
Oooh sawa sawa
 
Sawa mkuu
🙏🙏🤝
Kwa kuruka viwanja kula maisha mkuu maana umakula starehe zote umeridhika ukageukia wokovu kwahiyo ladha ya maisha unaijua na ladha ya wokovu unaijua

We ni mnomaa sana
Asante mkuu, lakini wokovu kwangu ndio top notch. Raha ya wokovu hakuna kujutia kama hizo starehe zingine.

Nitumie nafasi hii kuwakaribisha ndugu, vijana na watu wote wampokee Kristo YESU maana yeye ni kweli na njia ya uzima.

sasa mkuu wewe habari za Yesu ungezijuaje bila watu wadini maana wao ndio hufundisha habari zake
Nikianza kuelezea hapa itabidi nipewe siku nzima, lakini elewa kwamba everything change.

Roman Catholic church ndio dini ya kwanza na Hawa walitumia dini kwa maslahi yao, akaja Martin Luther akarekebisha kidogo mpaka Leo tumefikia kupata injili ya kweli lakini imejaa ulaghai wa kula sadaka za waumini.

Bwana Yesu anasema katika biblia kwamba walikwenda lakini sikuwatuma.

Sasa wao watamjuaje Yesu na kumkiri bila msaada wa watu wa dini maana wao ndio hutoa mafundisho
Nimekwisha kukueleza hapo kabla, nitawaambia waokoke wakishaokoka watampokea roho Mtakatifu huyu roho Mtakatifu ndio atawafundisha na kuwaelekeza.

Labda unasoma biblia pasipo kuielewa, Ingekua Hawa wachungaji ndio YESU aliwaachia kondoo wake bhasi kusingekua na haja ya kupewa Roho Mtakatifu au Bwana Yesu asingemuomba Mungu kwamba atupatie msaidizi ambaye ni Roho Mtakatifu.

Wachungaji wanapiga sadaka kutokana na watu kutokujua Roho Mtakatifu.

Mungu haachi kujibu maombi yako ?
Basi niombee nina shida na 500k leo leo mkuu 😢🤣

Yes, mkuu Mungu haachi kujibu maombi yangu.

Hapa inabidi uwe na Imani, lakini kwa Leo kwasababu umeniamini natangaza kwamba hiyo fedha umekwisha kuipokea. Muamini Mungu wangu atakufanyia njia just relax and wait.

Hapana nasoma na kuchambua kwa kina

Bila wokovu siwezi kujua ?
Ndio, kwani utaweza kuingia darasa la kusomea uda
Haya ulisema wewe kua wachungaji wanakosea kufundisha habari za kwenda mbinguni
ndio na mimi ni kakuuliza je kufundisha injili ya kwenda mbinguni ni ubatili?

Hapa nina story ila leo naiweka kapuni

Sawaaa mtumishi 😊

Aiseeeeee

Shukran usiongeze

Nakukubali pia mtumishi wa bwana

Oooh sawa sawa
 
🙏🙏🤝

Asante mkuu, lakini wokovu kwangu ndio top notch. Raha ya wokovu hakuna kujutia kama hizo starehe zingine.
Hongera sana furahia
Nitumie nafasi hii kuwakaribisha ndugu, vijana na watu wote wampokee Kristo YESU maana yeye ni kweli na njia ya uzima.


Nikianza kuelezea hapa itabidi nipewe siku nzima, lakini elewa kwamba everything change.

Roman Catholic church ndio dini ya kwanza na Hawa walitumia dini kwa maslahi yao, akaja Martin Luther akarekebisha kidogo mpaka Leo tumefikia kupata injili ya kweli lakini imejaa ulaghai wa kula sadaka za waumini.

Bwana Yesu anasema katika biblia kwamba walikwenda lakini sikuwatuma.


Nimekwisha kukueleza hapo kabla, nitawaambia waokoke wakishaokoka watampokea roho Mtakatifu huyu roho Mtakatifu ndio atawafundisha na kuwaelekeza.

Labda unasoma biblia pasipo kuielewa, Ingekua Hawa wachungaji ndio YESU aliwaachia kondoo wake bhasi kusingekua na haja ya kupewa Roho Mtakatifu au Bwana Yesu asingemuomba Mungu kwamba atupatie msaidizi ambaye ni Roho Mtakatifu.

Wachungaji wanapiga sadaka kutokana na watu kutokujua Roho Mtakatifu.



Yes, mkuu Mungu haachi kujibu maombi yangu.

Hapa inabidi uwe na Imani, lakini kwa Leo kwasababu umeniamini natangaza kwamba hiyo fedha umekwisha kuipokea. Muamini Mungu wangu atakufanyia njia just relax and wait.


Ndio, kwani utaweza kuingia darasa la kusomea uda
Shukran sana kaka ake 🙏🙏🙏
 
Back
Top Bottom