Majini & Mapepo 👻🤔

Majini & Mapepo 👻🤔

huwa nasema siku zote, unaweza sifia sana ukuu wa Mungu kwa kuangalia sayari,milima, bahari , mito, majangwa nk... lakini ukichunguza maisha ya viumbe hai , kwanzia bacteria,miti mpaka wanyama tunateseka hapa duniani,....UUMBAJI unaanza kutia mashaka 😮‍💨
 
Sikubani mbavu nataka fact tupu undugu hukoo hapa ni fact zitembee wewe umesema unaamini majini na mapepo yapo nimekuuliza

Je kuna faida gani kuamini kitu huna uhakika nacho?
Kama ninavyoamini nilizaliwa na Mama yangu basi na hayo mambo ya majini na mapepo naamini yapo bila hata faida, kuna Waalimu humu jamvini sitaki kuwa mention itakuwa sio vizuri wakiuona huu uzi watachangia.
 
kuna wanaozaliwa wafupi wengine warefu wengine weusi wengine weupe walemavu wengine wazima hakuna cha usawa wala nini
Sasa ulitaka watu wote tufanane kama Panya 🐀 ? Ukichunguza sana kanuni za uumbaji utaishia kuchanganyikiwa, hebu jiulize Haji Manara angekuwa mweusi ungeonaje ? 🤣
 
Niliwahi kuwa na rafiki wa kihindi na nilikuwa najaribu kuelewa imani yake kuhusu kuabudu ng'ombe ........ alisema wao hawaabudi ng'ombe tuu bali wananuiya vitu vikitimia wanaweka maagano... kuhusu Mungu alisema hawamwabudu ila wanaamini katika Nguvu ya asili inayotawala viumbe vyote kupitia iyo nguvu ndio wanaitumia katika vitu. Kwangu kumwelewa Huyu Muumbaji/Mungu hautakiwi uwe na fixed mind maana asili yake ni roho kamili utakayoiona kwenye maji,moto,hewa,udongo,viumbe,mimea,mwanga,giza ,nyota hivyo sidhani kuwa na maana moja itatosha kumweleza .Ukishamweka Mungu/muumbaji kwenye kipimo cha size au umbo umekosea.
Kwahiyo na wewe unaamini vipi
 
Imani mdogo wangu, Kusikia, kusoma na kutafakari uumbaji wake ni lazima kuna Muumbaji. Ishi kwenye kumuamini Mungu hii ni Tanzania sio Dunia ya kwanza 😉
Una uhakika uumbaji ni wa huyo Mungu unaemuabudu na kumuamini
 
huwa nasema siku zote, unaweza sifia sana ukuu wa Mungu kwa kuangalia sayari,milima, bahari , mito, majangwa nk... lakini ukichunguza maisha ya viumbe hai , kwanzia bacteria,miti mpaka wanyama tunateseka hapa duniani,....UUMBAJI unaanza kutia mashaka 😮‍💨
Hakika mkuu maswali ni mengi sana
 
Kama ninavyoamini nilizaliwa na Mama yangu basi na hayo mambo ya majini na mapepo naamini yapo bila hata faida, kuna Waalimu humu jamvini sitaki kuwa mention itakuwa sio vizuri wakiuona huu uzi watachangia.
Huyo unaetaka kum mention usijaribu maana hatatia mguu😆😆
 
Hello great thinkers 🫡

Sometimes huwa najiuliza, hivi kweli majini na mapepo wapo, au ni chai tu? 🤔

Waislamu wanayaita majini, huku Wakristo wakitumia majina kama mapepo wanapozungumzia viumbe wa kiroho wanaohusishwa na uovu
(Nadhani hivi viumbe wanaviita vya kiroho kwa sababu havionekani sijui sana kuhusu hili)

Twende nalo sasa 👇

1. Majini kwa mujibu wa Uislamu

Kwa mujibu wa mafundisho ya Kiislamu majini ni viumbe ambao Allah aliwaumba
Baadhi yao ni Waislamu na wengine si Waislamu
Hii ni kwa mjibu wa Qur'an yenyewe

Qur’an, Suratul-Jinn 72:14 inasema:

Na hakika miongoni mwetu wapo Waislamu na miongoni mwetu wapo walio madhalimu
Basi wale waliosilimu, hao wameifuata njia iliyo sawa

Pia, Qur’an 55:15 inasema kwamba majini waliumbwa kutokana na mwali wa moto usio na moshi

Hivyo, kwa mujibu wa Qur’an, majini ni viumbe walioumbwa na Allah, na wanaweza kuwa na imani tofauti

Pia baadhi waislamu kuna wanaodai kwamba majini wanaweza kuwa marafiki wa binadamu, na wengine husema kwamba binadamu anaweza hata kushiriki nao ngono(Sex)

Hapo nimeweka rejea ya hizo Aya ili anataka akapitie mwenyewe kuona ukweli ulivyo

2. Mapepo kwa mujibu wa Ukristo

Kwa upande wa Wakristo, tunasikia kuhusu mapepo (demons)
Shetani na malaika walioasi, ambao wanahusishwa na uovu, majaribu na kuwapotosha wanadamu

Kwa mfano, 2 Petro 2:4 inazungumzia malaika waliotenda dhambi na hukumu yao
Pia, Ufunuo 12:7–9 inasimulia kuhusu Shetani na malaika zake kutupwa duniani

Hata hivyo kitu cha ajabu na cha kushangaza
Dini hizi zina mitazamo tofauti kuhusu hawa viumbe wa kiroho
Unaweza ukagundua tofauti iliyopo kwa MAJINI wa Kiislamu na MAPEPO ya wa Kristo

Tena Muslim wao hao majini wana mpaka majina

Ex: kuna majina ambayo tumekuwa tukiyasikia, kama Jini Subiani, Makata, Daruweshi, Sultani na Maimuna nk....

Kama kweli majini wapo kama vitabu vya dini vinavyosena je, kuna namna binadamu anaweza kuwaona au kukutana nao ana kwa ana?

Sasa wana JF mjadala wetu upo hapa 👇

Kama Mungu ndiye aliyewaumba, hakujua kama wataasi?
Kwa sababu Mungu hupewa sifa ya kujua vyote

Kwa mujibu wa imani ya Kiislamu, Allah ndiye aliyewaumba majini. Qur’an 7:27 inawaonya wanadamu kuhusu Shetani na kabila lake ikisema kwamba wao wanawaona wanadamu kutoka mahali ambapo wanadamu hawawezi kuwaona.

Sasa, kama Mungu ndiye aliyewaumba majini na ana ujuzi wa kila kitu, hakujua kwamba baadhi yao wangekengeuka na kuja kuwapotosha binadamu?

Kama alijua hilo kabla hawajaumbwa, kwa nini aliwaumba akijua kwamba baadhi yao wangeasi na kuwa chanzo cha upotoshaji kwa viumbe wengine?

Na kama alikuwa na uwezo wa kuzuia jambo hilo lisitokee, kwa nini hakulizuia tangu mwanzo?

Kwa upande wa Wakristo, Biblia pia inazungumzia malaika walioasi. Katika 2 Petro 2:4, malaika waliotenda dhambi wanatajwa pia

Sasa mkanganyiko kama Mungu aliumba malaika na anajua kila kitu kabla hakijatokea, hakujua kwamba baadhi yao wangeasi?
Kama alijua, kwa nini aliwaumba akijua mwisho wao ungekuwa huo?

Na kama alijua kwamba Shetani angekuja kuwashawishi na kuwapotosha wanadamu, kwa nini alimruhusu aendelee kuwepo na kufanya hivyo?

Kwa nini Mungu aruhusu uovu, halafu aadhibu wanaoufanya?

Kwa mujibu wa mafundisho mbalimbali ya dini, mwanadamu akifanya maovu akatenda dhambi anaweza kuhukumiwa na kuadhibiwa adhabu ya Jahannamu au moto wa milele katika baadhi ya mafundisho

Mimi nazidi kujiuliza

Kama Mungu alijua tangu mwanzo kwamba Shetani, majini au viumbe wengine wangeasi na kujaribu kuwapotosha wanadamu, kwa nini aliruhusu mfumo huo uwepo?

Kwa nini atuache katika mazingira yenye vishawishi na uwezekano wa kupotoshwa, halafu atuhukumu kwa kushindwa kuvishinda?

Kama Mungu ana uwezo wa kuzuia uovu, kwa nini anaruhusu uovu huo uwepo na baadaye kuwaadhibu wale wanaoufanya?

Je, binadamu ni sahihii kuingizwa kwenye mtego mkali hivi?


Na kama Mungu alijua matokeo yote kabla ya kuumba viumbe hivi, kwa nini hakupanga mfumo ambao uovu huo usingetokea, au ambao usingewaweka wanadamu katika hatari ya kupotoshwa?

Mwisho akaahidi kutuchoma moto?

Je, huu ni mtihani wa haki?

Tuchukulie mfano halisi kwamba mtu ametengeneza mfumo, anajua kila kitu kitakachotokea ndani ya mfumo huo kabla haujaanza, na ana uwezo wa kubadilisha matokeo yake
Lakini anaamua kuuacha uendelee, huku akijua kwamba baadhi ya watakaokuwa ndani yake wataanguka na kushindwa

Sasa, ikiwa Mungu ndiye aliyeumba mfumo mzima alijua mwisho wake tangu mwanzo na ana uwezo wa kuzuia matokeo fulani yasitokee, kosa la binadamu liko wapi hasa?

Kwa nini tuwekwe katika mazingira yenye uwezekano wa kupotoshwa na viumbe ambao Mungu mwenyewe alijua wangekengeuka, halafu tuhukumiwe kwa matokeo ya maamuzi yetu?

NB :Kama kweli Mungu yupo kwanini akaumba dunia kwa namna hii
Kwanini atuahidi moto na ni yeye alianzisha
Kosa letu binadamu liko wapi?

ShesRise_1 ✋️
Binafsi siamini kama hayo mambo yapo, kwangu ni nadharia tu.

oh my god omg GIF (1).gif
 
Ilikuaje kuaje mpaka ukaamini?
Long story madam! Nimekutana na mengi since nko mdogo niliugua sana nakumbuka nilikuwa std 3 nilipona tuu kwenye maombi kwakushika radio mchungaji akiwa anaomba kupitia hilo Jina la Yesu. Hata sasa within two weeks ago nilikuwa na hali mbaya kwa sasa amefanya na namwamini atafanya zaidi. Ukitaka kumjua Mungu pitia kwa Yesu Mungu ni waajabu sana na utamjua kulingana na unavyoilisha akili yako kumhusu.
 
Long story madam! Nimekutana na mengi since nko mdogo niliugua sana nakumbuka nilikuwa std 3 nilipona tuu kwenye maombi kwakushika radio mchungaji akiwa anaomba kupitia hilo Jina la Yesu. Hata sasa within two weeks ago nilikuwa na hali mbaya kwa sasa amefanya na namwamini atafanya zaidi. Ukitaka kumjua Mungu pitia kwa Yesu Mungu ni waajabu sana na utamjua kulingana na unavyoilisha akili yako kumhusu.
Huko kwa Yesu pia nimepita mkuu
Haya kila la kheri sana
 
Back
Top Bottom