Majini, Mapepo, Maruhani, Uchawi na Kitimoto/Nguruwe; ukweli ni upi?

Usisingizie chakula hata siku moja, chakula hakina shida. Wanaosema mambo ya chakula ni wale wanaofuata au mlengo wa kiyahudi kabla ya kuja Kristo. Chakula hakina shida kabisa shida ni maisha yetu kama hayaambatani na aliye juu. Ndio tabu inaanzia hapo,na kumsaidia mtu huyo ni kumleta amjue yule aliye juu. Usijidanganye kuyatuliza kwa kufuata mapepo. No. Bali nenda tofauti na yanavyo taka kwa kumpokea yule aliye juu. Uwe mkweli ndani usidanganye nafsi yako na mpokee kwa imani. Full stop...'shida ni mwalimu lakini mkali'.take care.

Tatizo ni kujifananisha na MUNGU na si kingine.
 
Kasome biblia agano jipya, Yesu amemkuta mtu ana bonge na mapepo, yule mtu akalia sana, akamuuliza Yesu una nini nasi? kwanini unataka kutuua? akaomba twakuomba bas usitufanye kitu, turuhusu tuwaingie hao nguruwe, Yesu akauliza wewe pepo mchafu jina lako nani? yule mtu akajibu, tuko wengi sisi ni jeshi. Yesu akawaruhusu wakaenda na kuwaingia nguruwe. yule mtu akawa huru. sasa mimi sitaki kutoa ufafanuzi zaidi, mjumbe hauwawi, kila mtu sijui akisomaga apa ua anaelewaje, ila wewe kwa mujibu wa swali lako tafakari.....................................!!!!!!!

Km Yesu aliruhusu mapepo yawaingie nguruwe maana yake hawaruhusiwi kuliwa?,tafakari nyingine ni za kitoto sana.
 
Unasumbuliwa na wanga kila usiku? Unaona mauzauza ulalapo? Mapanya na mapaka yenye sauti za ajabu ajabu vinakusumbua? Unaamka na uchovu na kuota ndoto za ajabu? Lala na mfupa wa kitimoto, sio kitandani weka uvunguni au ufungie kwenye kona ya chumba unacholala...wakija jamaa watasepa...hiyo ndio kiboko yao

Kuna uhusiano gani na hao watu na mfupa wa mdudu?
 
Unasumbuliwa na wanga kila usiku? Unaona mauzauza ulalapo? Mapanya na mapaka yenye sauti za ajabu ajabu vinakusumbua? Unaamka na uchovu na kuota ndoto za ajabu? Lala na mfupa wa kitimoto, sio kitandani weka uvunguni au ufungie kwenye kona ya chumba unacholala...wakija jamaa watasepa...hiyo ndio kiboko yao

Hivi kwanini wakiona mfupa wa kitimoto usepa ni kwanini?
Ndo mana kuna mtu alikua anapandisha mashetani akisikia harufu ya kitimoto anaanza kulia na kusema bangi.
 
Bado sijapata jibu hadi sasa, kwanini kila killichokatazwa kuliwa au kutumia ni kitamu sana au kizuri sana? ? Haswa vilivyo kwenye vitabu hivi Biblia Takatifu na Quran Tukufu.;):)
 
Hivi kwanini wakiona mfupa wa kitimoto usepa ni kwanini?
Ndo mana kuna mtu alikua anapandisha mashetani akisikia harufu ya kitimoto anaanza kulia na kusema bangi.

Ni kwakuwa kitimoto yenyewe ndio makazi makuu ya mashetani, sasa hivi vishetani vidogovidogo vikianza fujo zao vikaletewa lile phantom vinatoka nduki
Yale mashetani Bwana Yesu aliyoyaamuru yamtoke yule mwanamke na kuwaibia lile kundi la nguruwe na kukimbia baharini hawajawahi kutoka
 
Hii post inaweza kuwakera wengi, hasa wale wapenzi wa kitu/kitimoto, aka safisha nyota aka mnyama lakini kwakuwa slogan ya JF inatuhamasisha kuongea kwa uwazi basi naomba tuvumiliane.

Nyama yake ni tamu hasa na kwa nchi kama china ndio inayoongoza kwa kuliwa, na sehemu nyingi duniani ndio nyama ghali zaidi pengine ukilinganisha na wanyama wa kundi lake.

Lakini nguruwe ni pepo au naweza kusema nguruwe wana mapepo na wameendelea kuzaliana katika hali hiyo kwa miaka elfu nyingi.

Ilikuwa hivi Bwana Yesu katika pitapita alikutana na mwanamke mwenye mapepo na Bwana Yesu akayaamuru yale mapepo yamtoke yule mwanamke, mapepo yakamjibu Bwana Yesu kuwa yakimtoka yatakosa kikao/makazi ndipo Bwana Yesu alipoona kundi la nguruwe wakichungwa, akayaamuru yamtoke yule mwanamke na kuwaingia wale nguruwe, ambapo baada ya kundi lile la nguruwe kuingiwa na mapepo lilikimbilia baharini na kupotelea huko.

Sasa tujadili

Dhana ya kwanza, Mapepo kwa kupitia nguruwe yalikimbilia baharini na kupotelea huko, lakini kimsingi hayakupotea bali yalibaki huko na ndio maana mpaka leo hii mapepo makazi yake ni baharini.

Bwana Yesu ndie aliyeyachagulia sehemu ya kwenda kukaa, kumbuka pepo kama pepo haliwezi kuishi bila mwili, hivyo yakachaguliwa mwili wa nguruwe na hii haijawahi kusitishwa.

Dhana ya pili
Kwanini mapepo yale yalikuwa mwilini mwa mwanamke na sio mwanaume?.

Pepo ni shetani na shetani kupitia nyoka ndie alimshawishi mwanamke mpaka akakubali kwenda kinyume na maagizo ya Mwenyezi Mungu pale Eden, kwahiyo kuanzia wakati huo shetani hupenyeza ushawishi wake kupitia mwanamke na ambaye hata hivyo ndio mhanga mkubwa wa mapepo.

Ni nadra sana kukuona mwanaume ana mapepo(hii ina maelezo yake).

Dhana ya tatu
Mazao ya nguruwe(nyama,kinyesi na mfupa) kutumika kama kinga ya majini nk.

Jini ni roho msafi sana anayechukia uchafu wakati pepo siku zote huambatana na vitu vibaya na vichafu, hivyo mtu mwenye maruhani mapepo wasafi, majini na uchawi akiletewa tu zao la nguruwe hakai anatimka, havichangani hata siku moja.

Ndio maana ukiona nyumba haieleweki au kuna vitu vya kishirikina kinaendelea hushauriwa kutumia mazao ya kitimoto.

Kumbuka

Kitimoto ana vimelea visivyokufa hata kwa joto Kali kabisa.

Paka hali nyama ya kitimoto.

Ndio mnyama mchafu zaidi duniani, na anayekula chochote, hachagui.

Kifo chake ni cha mateso hasa marungu mpaka anakata roho. Unajua ni kwanini?

Ni kwa sababu kitimoto ni pepo.
 
Nguruwe wenye majini ni wale waliorushiwa na yesu si wa huku kwetu majini hayawausu..mshana acha kuendeleza masimulizi ya kiroho
 
Paka hali kitimoto????? mshana jr umechemsha. Nina mabucha ya kitimoto na pia Nina majiko ya kitimoto...... paka wanashinda Kwenye biashara zangu wakila na kusaza
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom