Sababu za Majini/Mapepo Mengi kutopatana na Nyama ya Nguruwe

GuDume

JF-Expert Member
Jan 18, 2015
6,652
14,247
Mashaka ni jamaa yangu sana anafanya biashara ya Magari.(mashaka si jina lake halisi) anaishi kwenye apartment flan huko kijitonyama. Amekuwa akilalamika sana kuwa mmoja ya jamaa wanaoishi naye kwenye compound moja amekuwa kila mara akichoma udi/ubani na kumsababishia maumivu ya kichwa kila siku flan mida ya mchana na usiku.

Anasema hali amekuwa akijaribu kumwelewesha jirani yake huyo ambaye ni mpemba ba amekuwa akipokea majibu yasiyo mazuri. Alienda hosp wakamwambia kinachosababisha aumwe kichwa ni allergy.

Baada ya kufikiria sana jamaa yangu anasema aliamua naye kujipatia ufumbuzi.akawa naye anakuja na pork/kitimoto anakaanga pale nyumban.

Anasema siku ya kwanza yule mpemba hakuwepo ila aliporud sijui alijuaje alikuja kwa mashaka anafoka anatokwa jasho sana kuwa kwa nini anachoma nyama haramu mle ndani.mashaka alimjibu tu kuwa kila mtu ana nyumba yake so ashike hamsini zake.

Siku nyingine mashaka akakaanga/choma tena kitimoto muda ule ule ambao jamaa alikuwa anachoma udi/ubani... Yule mpemba alipandisha mashetani mule ndani kwake ikawa issue kweli akilalamika na kuongea kwa lugha isiyofahamika ila si ya kibantu.

Mashaka anasema toka hapo akagundua hizo kitu zina athari flan kwa watu flan akachukua na mifupa akaenda nayo ofisin kwake. Anasema mmoja ya wafanyakazi wake alipandisha mashetani na kukimbia eneo ile. Keshoye yule dada alikuja amevimba sana mashavu. Baada ya kuulizwa anasema wafalm walimtandika sana makofi usiku ule sababu ya ile mifupa ya kitimoto pale ofisin

Nashindwa kuelewa kuna uhusiano gani mbaya wa kitimoto na mashetan/majini/mapepo?

Nikakumbuka sir nature ktk wimbo wake wa mzee wa busara pia aliuliza kuwa au sasa aanze kulala na mfupa wa nguruwe na ganja?ili mzee wa busara asimdhuru.
 
Anasema siku ya kwanza yule mpemba hakuwepo ila aliporud sijui alijuaje alikuja kwa mashaka anafoka anatokwa jasho sana kuwa kwa nini anachoma nyama haramu mle ndani.mashaka alimjibu tu kuwa kila mtu ana nyumba yake so ashike hamsini zake.

Siku nyingine mashaka akakaanga/choma tena kitimoto muda ule ule ambao jamaa alikuwa anachoma udi/ubani... Yule mpemba alipandisha mashetani mule ndani kwake ikawa issue kweli akilalamika na kuongea kwa lugha isiyofahamika ila si ya kibantu.
Binadamu bana,yeye kuchoma udi ni sawa na jamaa kuumwa kichwa ni sawa pia....

Lakini jamaa kukaanga kitimoto ni mbaya kwasababu tu ni haramu kwa mpemba,binadamu bana......
 
kitimoto.jpg


Jama jama, pepo lisipande hapa kweli?
 
Kwa nini huyo aliyesikia harufu ya nyama ya nguruwe na yeye,isiwe ni aleji.Yeye pia itakuwa ni aleji,hakuna suala la majini hapo.Wapo ambao hata vumbi,harufu kali ya chemicals,harufu ya maua,perfume,vumbi,joto,nyama ya ng'ombe nk.,hupata aleji.Huu ni ulimwengu wa wa kuthihitisha kitu kwa njia sahihi za kisayansi,sio kuleta story za vijiweni.
 
Wazungu, nao ni wahenga sema uhenga wao siyo kama wa huku afrika.

Hivi majini wanapatikana Africa tu

Mbona Europe,Asia,Antarctica hawapo na stori hizi hakuna

Wa Afrika tunapenda stori za kusadikika mara fisi mtu,mara mti unaongea ,mara popobawa ,mara majini

 

Similar Discussions

Back
Top Bottom