Majina ya uswahilini vs Masaki & Oysterbay

Majina ya uswahilini vs Masaki & Oysterbay

Majina kama pamela ruby heaven rarely sana kuyapata uswahilini.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums

hii sms ya sent from blackberrY 93
00 wakat natumia lism la chinesse hakuna cha bibi demu wala bibi M hahaha!
 
Kweli lakini maanake mtu anaitwa Mashaka, Tabu Havijawa sasa ndio nini?
 
na lingine utasikia SIjali...........majina gani haya jamani

Nimeishi Mikocheni na Msasani kwa miaka mingi, lakini sikubahatika kumsikia msichana akiitwa Chausiku au Havijawa. Sana sana niliwajua kina Karen, jacquline, Linah, nk. Kwanini kuwepo tofauti kubwa ya majina kwa wasichana wa uswahili na kwenye mageti makali?😛hone:
 
Afadhali majina ya wari ,majina ya mitaa uswahilini jee?. Nilidhani mchamba wima fungakazi kumbe wavumao wapo wengine. Dunga unuse jina la kitongoji mombasa kenya.
 
Kuna mama mmoja tandale kwa tumbo alitafuta jina la kizungu akakosa kaamua kumuita mwanae wa kumzaa 'sadoline'
 
Nimeishi Mikocheni na Msasani kwa miaka mingi, lakini sikubahatika kumsikia msichana akiitwa Chausiku au Havijawa. Sana sana niliwajua kina Karen, jacquline, Linah, nk. Kwanini kuwepo tofauti kubwa ya majina kwa wasichana wa uswahili na kwenye mageti makali?😛hone:

Inaweza kumaanisha kuwa wazazi wa watoto wa mageti makali waliweza kukumbwa na utandawazi mapema zaidi kuliko wa sehemu nyengine

Is it a good thing? Inategemea unavyoichukulia;

wengine wanaweza kusema wazazi wa watoto wa mageti makali walikuwa malimbukeni, na kudharau kwao na kukumbatia majina ya kigeni yaliyokosa maana katika jamii zao kwa vile walidhani kila cha kigeni ni bora zaidi

wengine wanaweza kusema wazazi wa watoto wa mageti makali were more open minded na kuweza kuvutiwa na majina ya kigeni japo kama hayakuwa na maana kwa jamii zao

Take your pick
 
Nimeishi Mikocheni na Msasani kwa miaka mingi, lakini sikubahatika kumsikia msichana akiitwa Chausiku au Havijawa. Sana sana niliwajua kina Karen, jacquline, Linah, nk. Kwanini kuwepo tofauti kubwa ya majina kwa wasichana wa uswahili na kwenye mageti makali?😛hone:

Emancipate yourselves from mental slavery,non but ourselves can free our mind-Bob Marley
 
Hivi mtoa mada unajua uswazi ya msasani? Kuna uswazi za kutosha tu, just behind the namanga frames, na nyuma ya noah's ark, kuna sehemu ukiingia huko njia ya kurudia barabarani lazma mwenyeji akurudishe.

Opposite kanisa la kkkt kuna uswazi inaitwa bonde la mpunga. Huko ni kwingine. Im just saying hata kwetu wapo.

Huko mikocheni ndo uswazi kibao mvua ikinyesha mnavua kambale.
 
Mwl NYERERE hali hiii, huiita kasumba, kujali majina ya kimagharibi na kudharau majina ya jamii yetu, masaki, oysterbay na mikocheni si makazi ya wazawa wa jiji la Dar es salaaam, majina hayo uliyoyataja ya maeneo ya uswazi ni majina ya asili ya Wazaramo, wandengereko,wakwere na wazigua, hata usukumani hakuna majina ya kimagharibi nakupa tano shujaa wangu wa leo, rais wa zamani kongo[zaire] marehemu MOBUTU SESESEKO KUKU MBANGA, alilitambua hilo na kufutilia mbali kasumba hiyo, eti leo hii mtu anasagia YANGA na SIMBA na kudai kuwa timu yake ni MANCHESTER UNITED/ARSENAL/LIVERPOOL NK , mmmmh kasumba kasumba kasumba basi ondoka bongo nenda hukohuko au lipia uhamiaji kibali cha kuishi hapa nchini, vilevile hata hao wazazi wako siyo maana hawana ubora wa wazazi wa huko mbele, kama utadai eti vitu vyetu havifurahishi ndo maana huvishabikii basi ondoka nenda hukoo kabisa na badili mpaka jina lako na kana wazazi wako.
 
Hivi mtoa mada unajua uswazi ya msasani? Kuna uswazi za kutosha tu, just behind the namanga frames, na nyuma ya noah's ark, kuna sehemu ukiingia huko njia ya kurudia barabarani lazma mwenyeji akurudishe.

Opposite kanisa la kkkt kuna uswazi inaitwa bonde la mpunga. Huko ni kwingine. Im just saying hata kwetu wapo.

Huko mikocheni ndo uswazi kibao mvua ikinyesha mnavua kambale.

Tatizo amekariri toka huko mkoani kwamba DSM uzungun ni O Bay,msasani hajui kuwa kuna uswaz pia maeneo hayo,ndo tatizo la kuja mjini ukashukia UB terminal na sio kisutu
 
Tusimlaumu kuna kitu kizuri anataka kuuliza,ila kakosa arts of building arguments..pia tusiendekeze spoon feed hapa JF..tuna mambo mazito ya kujadili mf namna gan rosources katika nchi yetu zitakavyotumika kuinua taifa,ni viongozi gan wenye uwezo wa kuorganize hizi resources kusaidia ktk elimu,afya na maji. Tuna katiba mpya mbele yetu. Mtoa maada tunatambua umuhimu wa kujadili vitu tofaut tofauti, na tunaheshimu swali lako lakin tunakuomba nenda kafanye research(u got research question) then utuletee majibu! Ila kwa sasa macho na akili zetu ni kwenye ujenzi wa taifa!

Mnajenga taifa Chit-Chat?
Swali lake ni la ki Chit-Chat na nadhani hakuna kosa alolifanya.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom