Miongoni mwa ustaarabu wa mtu ni jina analompa mwanawe. Ukisikia jina la mtoto fulani unaweza kujua baba au mama yake au aliyempatia jina yu mwenye fikra gani. Waswahili wana tabia ya kuita majina kulingana na kipindi na mazingira aliyozaliwa mtoto. Kwa mfano, Jumapili, Jumanne. Majina mengine ya uswahilini, Sikitu, siwajui, sikudhani, siwajali, sikutegemea, sikutaraji, chausiku na cha ajabu mengi kati ya majina haya ni ya kike sijui kuna mfungamano gani kwa kweli. Yamkini baadhi ya majina hayo yakawa yanaashiria masaibu aliyopata mama wa mtoto huyo, au kukaaa muda mrefu bila kupata mtoto halafu akaja kushika mimba, hivyo akaamua kumweita mtoto wake sikudhani. Any way, kila amwitae mtoto wake jina fulani huwa na sababu zake nadhani wakiulizwa wazazi wenyewe wenye watoto wenye majina hayo wanaweza kuwa na majibu mazuri. Kuna wale mashabiki kama wa akina gaddafi, saddam, scud, hitler na majina mengine au Nejad (Rais wa Iran), au majina ya wachezaji mashuhuri na kadhalika. Hivyo kila mtu huwa na msukumo na sababu zake katika kumpa jina mwanae. La msingi unapochagua jina la mwanao hakikisha ni jina zuri na ambalo limezoeleka katika jamii anayoishimkwani kinyume na hivyo huenda akagezwa kichwa cha utani na masikhara.