if you don't need to prove anything then delete your non sense which you have blindly posted to the public, take your case to your family and do not involve the public in any of your mess again.
if you don't need to prove anything then delete your non sense which you have blindly posted to the public, take your case to your family and do not involve the public in any of your mess again.
if you don't need to prove anything then delete your non sense which you have blindly posted to the public, take your case to your family and do not involve the public in any of your mess again.
Mkuu Tukundane
Kama hoja ya misamaha imetokana na sheria zilizopo; na kwa maelezo ya mh. HKigwangalla hajengi hoteli ni chuo cha afya ambacho kinaendana na taaluma yake; sasa kosa lake ni lipi kama sheriaa inamruhusu kufanya? Ningepingana naye kama ametumia misamaha ya kodi kujitarisha kwa kuuza mali iliyosamehewa kodi; wengi huu uchangiaji wenu ni wa kisiasa ambao umeegemea zaidi siasa za maji taka; kama ni kweli mna hoja ya kupinga maelezo ya HKigwangalla njooni na data ambazo zitasuta kauli yake; magazeti ya bongo yamegeuka ni uwanja wa mipasho na majungu wataandika chochote ili wauze magazeti; lile gamba lilojipa milioni 140 au lile gamba lilojipa tenda kwa mlango wa uani wa zaidi ya milioni 350 mbona mmeyanyamazia? Mngeanza na nyumbani kabla ya kupiga kelele kwa jirani
Chama
Gongo la mboto DSM
HKigwangalla njoo ukanushe na hiyo.
Bwana mbunge.
Wewe ni mtumishi wa watu, umechaguliwa na watu, unawakilisha watu, umebeba taadhima kubwa sana.
Sasa unapoanza kuhamaki na wananchi wa kawaida unajionyesha kukosa kifua, kukosa maarifa, kukosa kujua kwamba unajibizana na watu usiowajua,unajionyesha kutofikiri kwa kina.
Kama mtu uliyepewa heshima na watu ningetegemea heshima kutoka kwako, hata kwa waliokukosea heshima ili wao wapate kujifunza na kuona aibu.
Na hata kama wameumbwa bila aibu, waja wengine watakaotembelea jukwaa hili waone tu kwamba hapa kwa kweli mbunge wetu kakosewa heshima.
Ukimaka unajionyesha hujakomaa.
Ukiandika "why do you think and believe that I need to prove to you anything?!!" unajionyesha hutambui kwamba wazo la kuja kutoa taarifa kutoka upande wako hapa JF tu ni kutaka ku prove kitu.
Maadam wewe ni mtumishi wa umma, kauli hii haifai. Kwa sababu si ya kiungwana na haiendani na utumishi wa umma.Hususan kwa sababu hujui huyo unayejibizana naye ni nani.
we unalilia PAYE ishushwe wakati mwenzako anapigana kuanzisha kampuni..... ..kinachosikitisha sana huwezi kumwona huyu mbunge hata siku moja anapigania PAYE ishushwe.....pamoja na kwamba naye alishawahi kuajiriwa na kuathirika na PAYE.....hawa wabunge wengi wako hivyo....wanapopata nafasi wanasahau hata walikopitia.....hii ndio aina ya wabunge tulionao......wamejaa ubinafsi uliokithiri......inasikitisha napoona watu wanawatetea wabunge aina hii......Huwa najiuliza hivi huko bungeni huwa mnakimbilia nini? kumbe mna agenda zenu za nyuma ya pazia mnaanzisha makampuni halafu mnatafuta tiketi za kuingia bungeni ili biashara zenu mziendeshe kwa kutuibia sisi wananchi. Wakati huku wenzenu PAYE inatumaliza na nyie hata hii haiwagusi. Kweli aliyeshiba hamjui mwenye njaa.
Si kweli kwamba nina hisa 78% na mke wangu Dr. Bayoum Kigwangalla ana hisa 22% - ni uongo.
Ya ukweli: ni nina hisa 40% na mke wangu Dr. Bayoum Kigwangalla anamiliki hisa 11%. Sijihusishi na kuendesha biashara hii kama mtendaji wa kila siku.
Watanzania tuache kushabikia uongo.
Taarifa hii nimeiandika na kuitoa mimi mwenyewe, Hamisi Andrea Kigwangalla, M.D., Mbunge, Jimbo la Nzega. (simu yangu ya kiganjani ni 0782636963 na email yangu ni hkigwangalla@gmail.com, website: www.hamisikigwangalla.com )
Kigwangallah, mi siyo shabiki wako lakini pia sikumaindi na kila kitu kutokana na mambo yako. Lakini mnyonge mnyongeni haki yake mpeni. Nakupa big up sana kwa kujibu. Wanasiasa wengine wangemyuti upepo upite. Nawashangaa wanaoyapinga maelezo yako. Gazeti limekukashifu. Wewe umejisafisha. Sasa ambaye hakubaliani nawe ana jukumu la kututhibitishia kuwa wewe mwongo. Pia nikupe pongezi. Bila shaka hicho chuo kitatoa fursa ya ajira kwa Watanzania directly na indirectly. Directly ni kwa wale watakaoajiriwa hapo. Indirectly ni kwa wale watakaopata ujuzi hapo na kuajiriwa kwingine.
Watakuita fisadi poa. Lakini bora wewe unayerudisha kwa wananchi kuliko wanaoficha Uswisi.
Lakini jamani sisi Wabongo tunapenda sana kuona wenzetu wakisota. Wakifanikiwa tu ni maneno.
Hamisi, kila la heri. Ila basi kwa kuwa wewe ni kijana jitahidi uwe na mwenendo mzuri kwa jamii. Nyie ndo tunawategemea mshike nchi baadaye. Yaliyopita achana nayo. Kila mtu ana background yake. Wanaokuponda wajibu kwa kuchapa kazi.