Majibu ya Tuhuma Dhidi Yangu!

Majibu ya Tuhuma Dhidi Yangu!

Kigwangala usituchanganye kwa maandishi yako marefu namna hii.
Hivi kama wewe unamiliki hisa 40 na mke wako hisa 11 which is equal to 51 unadahani hiyo Kampuni ni ya nani?Tayari mnamiliki zaidi ya Nusu ya Hisa zote.Hapo ni ukweli kabisa hiyo kampuni yenu ni ya ki-wizi na yote hayo yalisemwa ni ya kweli. Nijuavyo mimi mmiliki wa hisa nyingi ndie mwenye maamuzi ya juu.

Unakana halafu unakubali una akili nzuri kweli?Magamba mnalo ila mwisho wenu 2015.
 
if you don't need to prove anything then delete your non sense which you have blindly posted to the public, take your case to your family and do not involve the public in any of your mess again.

Sasa kama huna sababu ya kuthibitisha lolote kwa yeyote humu nini kimekufanya uandike mgazeti wote huo na kuuweka humu? Si ungeandika na kubandika huko kwenye litovuti lako la www.hamisikigwangalla.com....

Umesema kuwa hujihusishi na uendeshaji wa biashara ya kampuni kama mtendaji wa kila siku.

Kwamba kampuni ya Emergent Africa Ltd ina watumishi wake sehemu mbalimbali.

Anayetakiwa kukanusha hayo madai ni wewe mwenye hisa 40% au ni kampuni ya Emergent Africa Ltd?

Could this be another one man company or a family company?

Could this company be a sham or mere a façade concealing the truth facts?

Would you mind us piercing the corporate veil to know what is going behind?

UCHAGUZI 2015 sio mbali. Wewe na wenzako kama MAIGE, NGELEJA etc. Mutakiona cha mutema kuni. Ni aibu sana kwa vijana kama nyinyi toka kanda ya ziwa kufanya ufisadii kiasi hiki wakati majimbo yenu yana shida tupu. Unategemea kushinda 2015? Majibu yako marefu sana, ningekuwa wewe ningejibu very simple ila sababu wewe muongo umetuandikia ngojela. AGAIN 2015 coming soon.

Kigwangala umetoa utetezi dhaifu sana. Umedai kuwa wewe si mtendaji mkuu kwenye hiyo kampuni lakini hapohapo umeahidi kuwashughulikia watakaokuwa wamehusika katika uuzaji wa vifaa hvyo.. Unajielewa kweli?

JF kuna watu makini wa kuhoji vitu vya msingi kama mlivyofanya nyie, anyway mie sina shida sana kwa viongozi kufanya biashara ila ingependeza kama hizo kampuni walikuwa nazo miaka 3 kabla ya kuwa viongozi tena kwa kuongezea wawe wamefanya kazi yenye ukubwa sawa na hiyo kazi inayofanywa, na si mtu kwa kuwa kiongozi anafungua kampuni leo kesho anapewa kandarasi kubwa. All in all ni mwanzo mzuri kwa Kigwangala kujibu tuhuma kuliko kukaa kimya huenda atafunguka zaidi.
 
Ningependa kumuamini mtu huyu lakani mhhh sijui!! Ndio maana mwalimu alionya uongozi na biashara huishia ufisadi.
 
Ningependa kumuamini mtu huyu lakani mhhh sijui!! Ndio maana mwalimu alionya uongozi na biashara huishia ufisadi.

Siku hizi uongozi ni daraja la kutaka kujua yaliyomo serikalini ili tenda na mambo mbalimbali mazuri yanayokuja uyajue na kujipanga na ikiwezekana kutafuta watu wenye uzoefu na hiyo kazi kisha mnaingia kwa mgongo wa kufanya kazi kwa ushirikiano kwa kununua hisa chache kwenye kampuni huku nyuma ya pazia una push mambo yaende na kampuni linapata kazi. NDIO MAANA WALISEMA SERIKALI ISIFANYE BIASHARA ILI VIONGOZI WA SERIKALI WAFANYE BIASHARA
 
Hii stori inashabihiana na ile ya Maige. Ilianza hivi hivi, mara ana mkopo CRDB, mara ana magari ya mafuta yanayomuingizia dola elfu kadhaa kwa trip. In the end akaishia pabaya.

Kigwangala amejieleza sana lakini still kuna facts zina miss......

Kwa sasa nakubaliana na media unless mheshimiwa takes the matter to the court.
 
Mheshimiwa Mbunge.
Hivi inawezekana watu wote wakaamua kukuchukia wewe tu?
Kwani ni Mbunge peke yako hapa nchini? Kwani uliwafanya nini? Una nini wewe ndugu yangu?
Maudhui ya utetezi wako yanaeleza kuwa ulicho nacho sio kiasi kikubwa kama ilivyoripotiwa, lakini unacho. Wakati mwingine kukaa kimya ni kuzuri zaidi kuliko kujiongezea maswali ya kujibu kama ulivyofanya. Pole wewe! Pole wana Nzega!
 
kwa taarifa yako ata kama ungeandika ukweli, humu utabishana na makamanda wasio amini kama kuna Mungu. sasa watakuamini wewe? wenzako wanabishana na redio.
 
Kabla hujawa mbunge three years ago ulikuwa na nini na sasa una nini? Kwanini unatoa maelezo ya miaka hiyo badala ya ku-stick on point?

Jiangalie kama vipi kafungue kesi ya kusafisha jina lako kwani kuna ushaidi mkubwa dhidi yako.

Mwisho jipime!!
 
Kuwa na hisa kwenye kampuni inayofanya biashara halali siyo dhambi. Kupata msamaha wa kodi siyo dhambi. Dhambi ingekuwa kuviuza baada ya kupata msamaha. Kama kuna mtu anaamini kuwa kuna vifaa vimeuzwa na kampuni yangu, kati ya hivi vilivyoingizwa nchini kwa msamaha, anakaribishwa kuleta uthibitisho wa nyaraka za mauzo (cash sale receipts, tax invoice ya mauzo, pay-in slip ya benki ya malipo, delivery note, ama receipt yoyote ile ya kampuni hii inayoashiria kuwa mauzo yamefanyika)

Msamaha wa vifaa hivi ni kwa ajili ya Ujenzi wa Chuo Cha Afya Nzega (kitakachoitwa International Institute for Health Tabora), ambacho nilikianza kwa fedha zangu mpaka pale kilipofikia na sasa tunasubiria majibu ya benki ya maombi yetu ya mkopo ndipo tuendelee.

Tuache kutazama mambo kwa macho ya wivu, husda na majungu. Tusimame kwenye misingi ya ukweli daima. Nchi hii itaendelezwa na watu wenye kuchukua maamuzi thabiti na hatua za maksudi za kuleta mabadiliko – kama miradi ya namna hii (ya chuo cha afya Nzega Si kila mtu aliyeko kwenye uongozi ndani ya CCM basi ni fisadi, watu wazuri na wasafi wapo pia. Tusimuangalie kila mtu kwa sura ya ‘ufisadi' na ‘ubadhirifu' tu! Tuaminiane jamani.

Taarifa hii nimeiandika na kuitoa mimi mwenyewe, Hamisi Andrea Kigwangalla, M.D., Mbunge, Jimbo la Nzega. (simu yangu ya kiganjani ni 0782636963 na email yangu ni hkigwangalla@gmail.com, website: www.hamisikigwangalla.com )


Koligi Kigwangalla, naomba nikupongeze kwa kujitokeza hapa Jf kujibu/kutoa tamko juu ya tuhuma za ufisadi zinazo kukabili si jana tu ila ni mara kwa mara kama ulivyojieleza kwenye hoja yako. Na kama ulivyoeleza vizuri sana kuwa si chombo kimoja tu cha habari kilichowahi/kinachopendelea kuweka front page tuhuma zako.

Ninaandika haya nikiwa kama mdau wa sekta ya afya na nimeshafika Hospitali ya wilaya ya Nzega na kufanya kazi karibu kwa wiki mbili, nilipata wasaa wa kuliona hilo jengo ambalo unasema kitakuwa chuo cha Afya Nzega, nilipata wasaa wa kuzungumza na baadhi ya wfanyakazi wa hospitali ya wilaya ya Nzega na kupata historia ya ujenzi unaosua sua wa hicho chuo!

Ukiwa kama Mdau/Daktari wa sekta ya afya, na pia mbunge wa wilaya ya Nzega, Je unayajua haya
1. DMO wako (Mwombeki) ni kama Mungu mtu, haambilikia au amejenga mtandao na mkurugenzi hivyo kila mtumishi atayehoji mambo ya msingi ikiwepo matumizi ya fedha anahamishwa?
2. Taratibu za uendeshaji wa ofisi ya DMO zinakiukwa? Mathalani DMO akisafiri ofisi anakaimu Katibu wa afya? Kwa nini anaogopa kuwakaimisha madaktari wenzake ambao kisheria na kanuni ndio wanaostahili?

Naomba nije kwenye hoja zako ambazo nimeziquote na nimezifayia formatting, nina maswali yafyatayo
1. Gazeti la Tanzania daima wanaamini kuwa kweli Kampuni yako imeuza vitu ambavyo havijalipiwa kodi, Je huoni kuwa ingekuwa ni busara uende mahakamani kuwashtaki Tanzania daima kwa kukuzushia na kuwadai wakuoneshe hivyo vielezo ambavyo wewe unataka sisi members wa Jf tukuletee kama uthibitisho? Tahadhari, najua vitu vya dili vingi havina risiti

2. Ujenzi wa chuo- unaweza kutuambia hatua ya ujenzi iliyofikiwa na jengo halijaendelezwa kwa muda gani? Unaweza pia kutuambia hilo jengo lilikadiriwa kugharimu shilingi ngapi na msamaha ulipaswa kuwa ni wa shilingi ngapi na utuambie mpaka sasa ni asilimia ngapi ya msamaha imeshatumika? Na kiasi gani kimebakia?

3. Wivu, husda na Majungu- Jiulize katika Wabunge wote wa Mkoa wa Tabora au wa CCM kwa nini uonewe wivu na husda koligi HKigwangalla? Na bahati mbaya Wengi wenu na chama chenu mnakimbilia kutamka hayo maneno bila kujenga hoja, wewe si wa kwanza

4. Hoja ya si kila Mtu aliye CCM ni fisadi- Umetajwa wewe kama HKigwangalla, na si CCM, sasa kwenye hoja yako CCM imekujaje? Haya tuache hili, lakini kumbuka kuna kada moja mkongwe wa CCM aliwahi tamka kuwa hakuna msafi ndani ya CCM, Koligi, unaweza kunitajia kwa kadiri ya uelewa wako angalau Kada mmoja tu wa CCM aliyemsafi? Ukishindwa uje hapa Jf uombe tukupe list of shame ya wabunge na makada wa CCM

Naomba kuwasilisha comrade!!
 
Last edited by a moderator:
Hamisi Kigwangallah ni Mbunge, Kitendo chakuja jamvini kudanganya watu kwa sababu ya stori iliyoandikwa na gazeti la Tanzania daima, na kumbeza Mwandishi wa stori hiyo kuwa amedanganya. Sijui Mwandishi huyo kama ataendelea au ataacha, ila kwa sababu ya uongo uliozushwa na Kigwangalla anayejiita Mwadilifu. Huyu kijana ni Mwizi, anadharau watanzania kwa kuwaona ni wajinga, wasio na akili. Kwa maneno yake mwenyewe kwenye tamko lake amesema anamiliki 40%, na 11% ni za mke wake. Aje jamvini kama alivyofanya jana aseme amedanganya TIC au amedanganya jamvini, na kwa manufaa gani anahadaa watu jamvini.......... sio mwadilifu, ananitishia maisha sasa. angalieni mnaomwona Kigwangalla kuwa wa maana kumbe ni wale wale tu, anamtukana mwandishi wa Tanzania daima, kale kajamaa ka Tanzania daima kako makini Kigwangalla omba radhi jamvini, jiuzulu utumishi wa umma, umejivunjia heshima
 

Attachments

  • UONGO WA KIGWANGALLAH.jpg
    UONGO WA KIGWANGALLAH.jpg
    98.8 KB · Views: 105
Nimefuatilia post hii lkn inasikitisha huu u- c-quine ( CCM/CHADEMA) umeshadhuru wengi sana humu JF. Ingekuwa na faida kubwa kama hoja ingejibiwa kwa hoja, lkn ni mipasho kwa kwenda mbele tu huku watu wakijisifia kuwa na akili au werevu, ujinga zaidi ni kujikita kwenye Kulazimisha watu waamini yale wanayoyaamini wao!!! mfano mdogo ni mtu kushauri '' kama si kweli kawashitaki mahakamani'' wanasahau kuwa '' kama shutuma ni za kweli kwa nini nao wasiende kushitaki mahakamani ila sinatolewa hadharani?'' So hata majibu nayo yaje hadharani basi...au?...lol. Ni waulize mlio lewa Ccmquine na Chademaquine hivi shutuma mnazopeana kila siku kwa msisitizo kuwa USHAHIDI MNAO, Je kesi ngapi ziko mahakamani? kwa nini? au mnatuzugazuga tu siku ziende? wakuu USIKU HAUWEZI kufananishwa na MCHANA japo kuna sehemu duniani hawaupati usiku kwa maana ya GIZA... tafakari.......
 
chuo ni chake, na ni binafsi. kampuni ni yake. then anapata msamaha wa kodi. apa kuna walakini. PCCB wanatakiwa kufanya uchunguzi wa kina
PCCB gani mkuu!km wangekuwepo nchi isingefikia hatua hii kwa wizi wa namna hii,wote ni wezi tu.


A lie has speed,but truth has endurance
 
Haya ya yamenikumbusha mbali sana....Mwalimu aliona mbali juu ya kazi ya siasa na biashara.....
''Kila ninapotembea ninakuwa na vitabu viwili...Biblia pamoja na Azimio la Arusha...Ninakisoma hiki cha Azimio la Arusha mara kwa mara lakini hadi sasa sijaona tatizo lolote ndani yake'' - Mwalimu JK Nyerere (Hayati Baba wa Taifa)
 
Mkuu Tukundane
Kama hoja ya misamaha imetokana na sheria zilizopo; na kwa maelezo ya mh. HKigwangalla hajengi hoteli ni chuo cha afya ambacho kinaendana na taaluma yake; sasa kosa lake ni lipi kama sheriaa inamruhusu kufanya? Ningepingana naye kama ametumia misamaha ya kodi kujitarisha kwa kuuza mali iliyosamehewa kodi; wengi huu uchangiaji wenu ni wa kisiasa ambao umeegemea zaidi siasa za maji taka; kama ni kweli mna hoja ya kupinga maelezo ya HKigwangalla njooni na data ambazo zitasuta kauli yake; magazeti ya bongo yamegeuka ni uwanja wa mipasho na majungu wataandika chochote ili wauze magazeti; lile gamba lilojipa milioni 140 au lile gamba lilojipa tenda kwa mlango wa uani wa zaidi ya milioni 350 mbona mmeyanyamazia? Mngeanza na nyumbani kabla ya kupiga kelele kwa jirani
Chama
Gongo la mboto DSM

Mkuu CHAMA ni halali kumsamehe mtu mwenye uwezo wa kulipa kodi?Huku ukitumia nguvu kubwa kumulipisha kodi mwananchi masikini ambae anahitaji kusaidiwa?.Chuo cha afya kitakuwa kinatoa msaada kwa mwananchi bila kutozwa kitu chochote?.Je unauhakika gani kuwa mh hautumii vibaya msamaha aliopewa kwa kujitajirisha yy mwenyewe?.Sheria ya msamaha wa kodi inaruhusu kutoa msamaha kwa makundi yapi?na kwa mwenye uwezo wa kiwango gani?.
 
Last edited by a moderator:
Siku hizi uongozi ni daraja la kutaka kujua yaliyomo serikalini ili tenda na mambo mbalimbali mazuri yanayokuja uyajue na kujipanga na ikiwezekana kutafuta watu wenye uzoefu na hiyo kazi kisha mnaingia kwa mgongo wa kufanya kazi kwa ushirikiano kwa kununua hisa chache kwenye kampuni huku nyuma ya pazia una push mambo yaende na kampuni linapata kazi. NDIO MAANA WALISEMA SERIKALI ISIFANYE BIASHARA ILI VIONGOZI WA SERIKALI WAFANYE BIASHARA
Hii ni dunia ya dot com, usipofanya hayo hapo juu, iwe kibiashara au kisiasa utaishia kuwa wa kutumwa tu!!! nimewaza tu.... hebu waangalie waheshimiwa walioingia bungeni haswa hawa majanki CCM/CHADEMA kwa sasa wote wanaitwa VIGOGO ki mapato na hadhi.. kwa heri...
 
Aise mchango wako umenivutia zaidi.


A lie has speed,but truth has endurance
 
Kabla hujawa mbunge three years ago ulikuwa na nini na sasa una nini? Kwanini unatoa maelezo ya miaka hiyo badala ya ku-stick on point?

Jiangalie kama vipi kafungue kesi ya kusafisha jina lako kwani kuna ushaidi mkubwa dhidi yako.

Mwisho jipime!!

Mkuu Arushaone,
kama umemsoma vizuriHKigwangalla amekiri kuwa anajenga nyumba tatu, Nzega,Tabora na Dar , halafu anabisha si fisadi?

Na msamaha huo upo na hautotumika kwa mambo mengine ya binafsi kama nilivyoeleza hapo juu kwenye ununuzi wa gari langu binafsi la kutembelea na ujenzi wa nyumba yangu binafsi ya kuishi Nzega, Tabora na Dar es salaam (ambako ninajenga).
 
Last edited by a moderator:
moto2012 Kigwa hawez kujibu hayo maswali.. Ataishia kusema kuwa wewe ni Bashe kwa hiyo unataka kumchafua. Huwa anatememea kutetea uovu wake kwa kudai kuwa mahasimu wake wa kisiasa wanamjengea tuhuma kutokana na wivu..
 
Back
Top Bottom