Majibu ya Tuhuma Dhidi Yangu!

Majibu ya Tuhuma Dhidi Yangu!

Mamisamaha yote hayo ya nini? Kumbe kweli misamaha ya kodi inatumiwa vibaya nchi hii.

Wakati mwingine unaishiwa kuwa na hasira tu. Yaani bunduki za kuwalinda Tembo, ngiri, mbuni, faru, twiga, nk ambao ni wanyama wetu hazipewi msamaha wa kodi lakini akina Kigwangalla wanalundikiwa misamaha ya kodi kibao eti wanajenga kituo cha afya! Wapi!
 
Huyu dogo why are you guys calling him Dr.? Ulaya kuitwa medicine doctor lazima uwe na PhD lakini huyu mwizi na mkweoa kodi mnamwita Dr how comes?
 
Huyu dogo why are you guys calling him Dr.? Ulaya kuitwa medicine doctor lazima uwe na PhD lakini huyu mwizi na mkweoa kodi mnamwita Dr how comes?

Wewe ndio lijinga kabisa,mpuuz mkubwa hujui chochote,umeniudhi kweli maana umeonyesha utupu uliopitiliza,jinga sana wewe,kukusaidia tu,aliyehitimu shahada ya kwanza ya utabibu wa mifugo au binadamu initial name yake ni dr,alafu then any phd order,ni dr.Kigwangala is a medical doctor,graduated from Muhas 2005.Usisahau na upumbavuni kwetu,mjanja mjanja yeyote anaweza akajipachika udokta au uprof.
 
Mwizi mkubwa wewe kama katibu wako kinana jangili..
 
sawa kumbuka na wewe uliwahi kusema yule wakili aliekusaidia kesi yako ya mgomo ni mgonjwa! Ama kweli muosha uoshwa! Kumbuka ukipaka watu tope lazima nawe wakupake bila kiujali mahusiano yako na watawala! Pole na hongera kwa kujiosha (tope liko pale pale!)
 
Ndg Mbunge,Natumai hakuna aliyekushurutisha kuja hapa katika jamii kujieleza. Japo umejitetea sana, nimepata muda wa kujua pia niliyokuwa siyajui. Nimeumia sana tena sana! Hakika laana ya Mungu i katikati yenu mnaohujumu haki za watanzania wengi. Hapo hatuna pia uhakika hiyo tenda ya ujenzi uliipata kwa njia gani? Halafu ukijumlisha hisa zako na mkeo unapata 51% then you have a major say. Ni kwa nini watendaji wa kampuni hawajakanusha? Na kama umeonewa kwa nini usiende Mahakamani? Hauna tofauti na wenzio mnao hujumu inchi hii yenye utajiri mwingi. Dawa pekee ni KUWAONDOA NINYI NYOTE KWENYE UCHAGUZI UJAO ILI MCHUNGUZWE NA HAKI ITENDEKE.
 
MBUNGE wa Nzega, Dk. Hamisi Kigwangalla (CCM), amejikanganya katika maelezo aliyoyatoa kukanusha tuhuma za kutumia vibaya misamaha ya kodi ya mamilioni ya shilingi kwa ajili ya ujenzi wa Chuo cha Afya eneo la Uchama, wilayani ya Nzega.
Katika taarifa yake aliiweka kwenye mitandao ya kijamii na vilevile mazungumzo yake na gazeti hili kwa simu, Dk. Kigwangalla alitoa maelezo ya kukinzana ambayo yanatofautiana na yale yaliyoko kwenye nyaraka za kampuni yake ya Emergent Africa Ltd.
Wakati Kigwangalla akisema msamaha wa vifaa hivyo ni kwa ajili ya Ujenzi wa Chuo Cha Afya Nzega (kitakachoitwa International Institute for Health Tabora), nyaraka za TRA na Kituo cha Uwekezaji (TIC) zinataja kituo hicho kama Taasisi ya kisasa ya Kliniki ya Madawa, Afya ya Jamii na Elimu ya Biashara.
Sambamba na hilo, mbunge huyo anadai kuwa na hisa asilimia 40 na mkewe Dk. Bayoum Kigwangalla ana asilimia 11 wakati nyaraka za TIC zinaonyesha kuwa anamiliki asilimia 78 na mkewe 22.
Nyaraka hizo zinaonyesha kuwa kampuni ya Emergent Africa Ltd, ilisajiliwa TIC Septemba 27, 2011 na iliruhusiwa kupata misamaha hiyo kuanzia Septemba 2011 hadi Agosti 2014.
Hata hivyo, akizungumza na gazeti hili, Dk. Kigwangalla alishindwa kufafanua kuhusu utata wa nyaraka kutofautiana tarehe za kuagiza na kupokea bidhaa.
Wakati nyaraka nyingine zikionyesha kuwa manunuzi yalifanyika nchini China Oktoba mosi 2012, nyaraka za TRA zinaonyesha kuwa bidhaa hizo zilishaingizwa nchini tangu Aprili 14 mwaka huo, kupitia kampuni ya Innovative Freight yenye TIN 100-145-596, risiti namba 2012/0000002986.
Pia utata huo, unaonekana katika taarifa za Shirika la Viwango Tanzania (TBS) ambazo zinaonyesha bidhaa hizo zilikaguliwa Machi 28, 2012 kwa fomu Na 40381.
Kuhusu hilo, Dk. Kigwangalla alisema, “Suala la tarehe ni suala dogo sana, na haliwezi kuathiri bidhaa zilizoingizwa nchini. Wewe unakimbilia kujadili tarehe tu, hilo hata watu wa TRA hawakuangalia tarehe bali bidhaa ndiyo maana wakaruhusu. Pengine tarehe zimekosewa China.
“Na wewe una uelewa mdogo wa mambo ya biashara nakuvumilia tu,” alisema.
Dk. Kigwangalla alisema, “Niliwahi kuibiwa bidhaa na nyaraka za dukani, ingawa mke wangu alinizuia kuripoti polisi na sasa nitachukua hatua, we nenda katoe taarifa unayojua, mimi nitakuja tena kuongeza ufafanuzi. Sina uadui na wewe hata Mbowe, nitawashtaki mahakamani kadiri mnavyonichafua.”
Aliongeza kuwa bidhaa zilizoingizwa tangu Aprili mwaka jana, hazijauzwa; kwamba ziko katika stoo Dar es Salaam kwani anasubiri kupata mkopo ili aweze kuzisafirisha kwenda wilayani Nzega.
Tanzania Daima ilidokezwa kuwa hata kampuni ya Innovative Freight Forwarders Co. Ltd iliyoshughulikia upakuaji wa mzigo huo na kuutoa bandarini haijalipwa hadi leo.
Akizungumza na gazeti hili kwa simu jana, meneja wa kampuni hiyo, Queen Mwasanguti, alisema: “Kwa kweli wewe ni mtu wa nne kuniulizia suala hilo, ni kweli sijajua kuna nini, ingawa ni kweli sijalipwa ila kila nikimuuliza Kigwangalla anasema yeye atakuja anikutanishe na vijana wake waliosimamia mizigo hiyo ili aweze kunilipa.”
Aliongeza, “Bidhaa ziliingia ndio, sisi tulikabidhiwa nyaraka hizo unazotaja tukashughulikia mizigo hiyo kwa taratibu za kawaida, ingawa ni kweli ‘bill of lading’ na ankara za manunuzi ya biashara zilitofautiana.”
Kwa mujibu wa makubaliano kati ya kampuni ya Emergent Afica Ltd na TIC, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) iliombwa kuisamehe kodi kampuni hiyo ya Dk. Kigwangala vitu mbalimbali vyenye orodha toka namba 1 hadi 390.
Bidhaa hizo kwa uchache ni kompyuta 1042, mashine za kutolea kopi 12, Printa 12, mashine za kufungia (binding machines) 12, vikokotozi (calculators) 640, projekta 12, ‘video camera’ 12, feni 30, vifaa vya simu, maboksi 28, jenereta moja, magari aina ya Toyota 13, malori matatu, Nissan Navarra Pik up nne, Mitsubishi Canter mbili na mabasi madogo manane.
 
Wewe na ccm wenzako wote ni mafisadi tu! Blabla nyingi wakati wenzako wanazo facts zote mikononi! Kubali uliyotenda wanacnhi na taifa litakusamehe. Kwani wewe ni wa kwanza mkufisadi nchi hii? Jana bila aiubu ccm mmemtetea jangili wa tembo Kinana.... ila hakuna kati yenu (ccm) aliyetetea mali asili zetu zinazoendelea kugemwa. Hivi nyie wote ccm ni kundi lilelile, wezi watupu!!

Ukishamwona mtu huku ni Daktari , huku mwanasiasa. huku mjenzi. huku mfanya bihashara ogopa sana mtu wa aina hiyo mwizi tu , fisadi , mzandiki, mla rushwa. opportunist ,
Hao ndo wanasiasa wetu , waganga njaa mafisadi kesho utamkuta kafunguoa kanisa ni mzee wa upako, askofu nabii na mtume
OGOPA VIROBOTO HAWA WATAKUCHUNA HATA NGOZI
 
We best fake kweli, jiandae kuwa maskini 2015. Dakitari na construction wapi na wapi! Ugamba unakusumbua!
 
Mamisamaha yote hayo ya nini? Kumbe kweli misamaha ya kodi inatumiwa vibaya nchi hii.

Wakati mwingine unaishiwa kuwa na hasira tu. Yaani bunduki za kuwalinda Tembo, ngiri, mbuni, faru, twiga, nk ambao ni wanyama wetu hazipewi msamaha wa kodi lakini akina Kigwangalla wanalundikiwa misamaha ya kodi kibao eti wanajenga kituo cha afya! Wapi!

Weka mbali na TEMBO!
 
HKigwangalla
JF imeharibiwa na watu wenye roho za husda; nadhani wameshtushwa sana na jitihada zako unazozifanya badala ya kuomba ushauri nao wafanye kitu gani wamegeuka ni watu waliokata tamaa ya maisha hasira zao wanataka kuzimaliza kwako; nakupa pole sana kwa hilo endelea na jitihada zako mradi ukifanikiwa hautawasaidia wana CCM peke yao naamini lengo ni kuwasaidia watanzania wote hususani kina mama na watoto
Chama
Gongo la mboto DSM

mi naomba anishauri jinsi ya kujenga 'NYUMBA YA KUISHI NZEGA TABORA NA DAR ES SALAAM' niache kumuonea husda wivu na kijicho.

...ina sound kama kirundi ingawa sina uhakika ni cha wapi
 
Last edited by a moderator:
Maelezo mareeeeeefu lakini hayana hata chembe ya ushahidi.
 
Du.,Unajenga nyumba tatu (Nzega, Tabora and Dar es Salaam) kwa mpigo! Asante kwa taarifa. Kweli ubunge unalipa!
 
Haya tena Mh. Hamisi Kigwangala Bagaile Andrea! Una habari kuwa leo mitaa ya Parking pale yalipokuwa yanapaki maroli ya Transit, majira ya mchana kutakuwa na Mkutano wa hadhara wa wapinzani wako? Si ajabu wakachukua nondo za humu. Unao hao mkubwa, sidhani kama watakupotezea.
 
Kiongozi makini na ambaye anajua kile anachokifanya haikuwa na haja ya kuja na taarifa hii bali tungesikia kwenye vyombo vya habari kuwa unalishitaki gazeti kwa kusema uongo na unataka uombwe msamaha na kulipwa kama ikiwezekana,kuja na kukanusha madai haya ni hoja nyepesi sana na haina mashiko na huwezi kubadili maziwa kuwa maji.
 
The truth is always short and brief, haya maelezo marefu ukiwa na akili timamu unajua mwandishi ni muongo, make it brief and precise otherwise hii ni longolongo. CCM hakuna muadirifu, bandika nyaraka za kodi ulizolipa wakati umeagiza hiyo SUV.
Wewe ni on purpose defaulter kwenye moja ya tasisi za fedha na kama BOT ingekuwa na credit bureau wewe ungekuwa blacklisted kukopa toka tasisi yoyote ya fedha, sijui uadirifu wako uko wapi? huko kwenye udaktari huwezi hata kutunza siri za wagonjwa, nani anaweza kukuamini?

Ni kweli................Ukiona mtu anaandika kurasa nyingi kuzungumzia kitu huyo anakuwa muongo!!!!! Mfano, ili kudhihirisha kile linachokisema, gazeti la Tanzania Daima limeandika "mistari miwili tu......" habari ya Mh. Kigwangalla!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Ngoma drooooo......
 
MBUNGE wa Nzega, Dk. Hamisi Kigwangalla (CCM), amejikanganya katika maelezo aliyoyatoa kukanusha tuhuma za kutumia vibaya misamaha ya kodi ya mamilioni ya shilingi kwa ajili ya ujenzi wa Chuo cha Afya eneo la Uchama, wilayani ya Nzega.
Katika taarifa yake aliiweka kwenye mitandao ya kijamii na vilevile mazungumzo yake na gazeti hili kwa simu, Dk. Kigwangalla alitoa maelezo ya kukinzana ambayo yanatofautiana na yale yaliyoko kwenye nyaraka za kampuni yake ya Emergent Africa Ltd.
Wakati Kigwangalla akisema msamaha wa vifaa hivyo ni kwa ajili ya Ujenzi wa Chuo Cha Afya Nzega (kitakachoitwa International Institute for Health Tabora), nyaraka za TRA na Kituo cha Uwekezaji (TIC) zinataja kituo hicho kama Taasisi ya kisasa ya Kliniki ya Madawa, Afya ya Jamii na Elimu ya Biashara.
Sambamba na hilo, mbunge huyo anadai kuwa na hisa asilimia 40 na mkewe Dk. Bayoum Kigwangalla ana asilimia 11 wakati nyaraka za TIC zinaonyesha kuwa anamiliki asilimia 78 na mkewe 22.
Nyaraka hizo zinaonyesha kuwa kampuni ya Emergent Africa Ltd, ilisajiliwa TIC Septemba 27, 2011 na iliruhusiwa kupata misamaha hiyo kuanzia Septemba 2011 hadi Agosti 2014.
Hata hivyo, akizungumza na gazeti hili, Dk. Kigwangalla alishindwa kufafanua kuhusu utata wa nyaraka kutofautiana tarehe za kuagiza na kupokea bidhaa.
Wakati nyaraka nyingine zikionyesha kuwa manunuzi yalifanyika nchini China Oktoba mosi 2012, nyaraka za TRA zinaonyesha kuwa bidhaa hizo zilishaingizwa nchini tangu Aprili 14 mwaka huo, kupitia kampuni ya Innovative Freight yenye TIN 100-145-596, risiti namba 2012/0000002986.
Pia utata huo, unaonekana katika taarifa za Shirika la Viwango Tanzania (TBS) ambazo zinaonyesha bidhaa hizo zilikaguliwa Machi 28, 2012 kwa fomu Na 40381.
Kuhusu hilo, Dk. Kigwangalla alisema, "Suala la tarehe ni suala dogo sana, na haliwezi kuathiri bidhaa zilizoingizwa nchini. Wewe unakimbilia kujadili tarehe tu, hilo hata watu wa TRA hawakuangalia tarehe bali bidhaa ndiyo maana wakaruhusu. Pengine tarehe zimekosewa China.
"Na wewe una uelewa mdogo wa mambo ya biashara nakuvumilia tu," alisema.
Dk. Kigwangalla alisema, "Niliwahi kuibiwa bidhaa na nyaraka za dukani, ingawa mke wangu alinizuia kuripoti polisi na sasa nitachukua hatua, we nenda katoe taarifa unayojua, mimi nitakuja tena kuongeza ufafanuzi. Sina uadui na wewe hata Mbowe, nitawashtaki mahakamani kadiri mnavyonichafua."
Aliongeza kuwa bidhaa zilizoingizwa tangu Aprili mwaka jana, hazijauzwa; kwamba ziko katika stoo Dar es Salaam kwani anasubiri kupata mkopo ili aweze kuzisafirisha kwenda wilayani Nzega.
Tanzania Daima ilidokezwa kuwa hata kampuni ya Innovative Freight Forwarders Co. Ltd iliyoshughulikia upakuaji wa mzigo huo na kuutoa bandarini haijalipwa hadi leo.
Akizungumza na gazeti hili kwa simu jana, meneja wa kampuni hiyo, Queen Mwasanguti, alisema: "Kwa kweli wewe ni mtu wa nne kuniulizia suala hilo, ni kweli sijajua kuna nini, ingawa ni kweli sijalipwa ila kila nikimuuliza Kigwangalla anasema yeye atakuja anikutanishe na vijana wake waliosimamia mizigo hiyo ili aweze kunilipa."
Aliongeza, "Bidhaa ziliingia ndio, sisi tulikabidhiwa nyaraka hizo unazotaja tukashughulikia mizigo hiyo kwa taratibu za kawaida, ingawa ni kweli ‘bill of lading' na ankara za manunuzi ya biashara zilitofautiana."
Kwa mujibu wa makubaliano kati ya kampuni ya Emergent Afica Ltd na TIC, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) iliombwa kuisamehe kodi kampuni hiyo ya Dk. Kigwangala vitu mbalimbali vyenye orodha toka namba 1 hadi 390.
Bidhaa hizo kwa uchache ni kompyuta 1042, mashine za kutolea kopi 12, Printa 12, mashine za kufungia (binding machines) 12, vikokotozi (calculators) 640, projekta 12, ‘video camera' 12, feni 30, vifaa vya simu, maboksi 28, jenereta moja, magari aina ya Toyota 13, malori matatu, Nissan Navarra Pik up nne, Mitsubishi Canter mbili na mabasi madogo manane.

Hivi wewe uliyetoa maelezo yooooooooooooooooooooooooooote haya unajiona kuwa uko sahihi? Na wewe ni miongoni mwa ma-great thinkers???? Mbona maelezo yako nawewe ni stori tu..............Hakuna facts zinazoonesha tatizo. Kwani kama mtu ameomba msamaha wa kodi na akapewa tatizo ni nini? Tatizo sheria ama aliyepewa msamaha ama au aliyetoa msamaha??? Au Mh Kigwangalla ALIHONGA mpaka akapata msamaha????? Kama aliyehonga mnamlaumu na je aliyehongwa????? Au kwa kuwa aliyehongwa ni "jamaa yenu???" Mimi naona Jamii forum imekuwa ni kichaka cha ushabiki wa CHADEMA....Au ni mahala watu wanachafua majina ya watu ili wakagombee ubunge eneo linaloshikiliwa na CCM. Yes, hizi ni kampeni lakini mimi naziita ni kampeni chafu!!!!!!!!!!!!!!!
 
Nchi yetu Bana msamaha hata NISSAN NAVARA?hii ni gari starehe sii yakazi.gari za kazi landrover 110,landcruiser hardtops
 
Back
Top Bottom