Majibu ya Tuhuma Dhidi Yangu!

Majibu ya Tuhuma Dhidi Yangu!

Mkuu HKigwangalla,
Nakubaliana na wewe kwa mambo mengi uliyosema....kwamba si dhambi kwa Mbunge kupata misamaha ya kodi na si za dhambi kwa yote uliyosema kwamba si dhambi! In fact, si dhambi vile vile hata kama ingekuwa ni kweli unamiliki 78% ya hisa na Shemeji akawa anamiliki 22%......NARUDIA, sio DHAMBI na yeyote anayeona hayo ni dhambi basi hatupe hoja za maana hapa!!

Hata hivyo, bado hapa umetenda dhambi, tena dhambi iliyotajwa hata kwenye Misahafu ya Dini; dhambi ya UONGO!
VOICE......SAUTI inakushitaki! Waandishi wa Riwaya/Tamthilia/Scripts(sana sana Scripts ambazo zinabeba Dialogue nyingi zaidi) nazani watanielewa zaidi ninapozungumzia suala la SAUTI! Unaweza kujiona kwamba kilichopo mbele yako ama unachokitoa mbele yako ni MAANDISHI tu lakini kwa mwandishi wa Script anaweza kuisikia kabisa sauti yako kutokana na maandishi yaliyopo mbele yake!

Hapa nilichogundua ni kwamba umedanganya kusema wewe unamiliki 40% na Wife anamiliki 11%. Hapa wala siwezi hitaji uthibitisho wa BRELA coz' I know huko BRELA ndivyo inavyosomeka, Kwamba HK anamiliki 40% na Mrs. HK anamiliki 11%! Swali ni dogo tu; je, 49%(au sehemu yake) umemmilikisha nani kwa niaba yako? Kuwa mkweli hapa ili upunguziwe madhambi ya Uongo ingawaje bado nitataka kufahamu ni kwanini ummilikishe mtu mwingine kwa niaba yako! Unakwepa nini?
 
Last edited by a moderator:
chuo ni chake, na ni binafsi. kampuni ni yake. then anapata msamaha wa kodi. apa kuna walakini. PCCB wanatakiwa kufanya uchunguzi wa kina
 
Wewe ni mtumishi wa watu, umechaguliwa na watu, unawakilisha watu, umebeba taadhima kubwa sana.

Sasa unapoanza kuhamaki na wananchi wa kawaida unajionyesha kukosa kifua, kukosa maarifa, kukosa kujua kwamba unajibizana na watu usiowajua,unajionyesha kutofikiri kwa kina.

........

Waswahili wanasema [Al] muhitaji hanith.i walau kama rijali

Sasa yeye anahitaji watu kisha anajitia urijali kwao watu hao hao

Au ndio shukurani ya punda?
 
The truth is always short and brief, haya maelezo marefu ukiwa na akili timamu unajua mwandishi ni muongo, make it brief and precise otherwise hii ni longolongo. CCM hakuna muadirifu, bandika nyaraka za kodi ulizolipa wakati umeagiza hiyo SUV.
Wewe ni on purpose defaulter kwenye moja ya tasisi za fedha na kama BOT ingekuwa na credit bureau wewe ungekuwa blacklisted kukopa toka tasisi yoyote ya fedha, sijui uadirifu wako uko wapi? huko kwenye udaktari huwezi hata kutunza siri za wagonjwa, nani anaweza kukuamini?

Kama mimi niko bize na kupiga mahesabu kodi ya mapato serikali imepunguza ngapi
 
Hivi hii emegent africa ltd. ni kampuni ya ujenzi? Swali kwako ndugu hamisi

Kwa jinsi alivyo chakazwa hapa sidhani kama atakuwa na guts za kurudi hapa na kujibu hata swali moja alilo ulizwa.....Gingwala umelikoroga zaidi sasa itabidi ulinywe..
 
HKigwangalla
JF imeharibiwa na watu wenye roho za husda; nadhani wameshtushwa sana na jitihada zako unazozifanya badala ya kuomba ushauri nao wafanye kitu gani wamegeuka ni watu waliokata tamaa ya maisha hasira zao wanataka kuzimaliza kwako; nakupa pole sana kwa hilo endelea na jitihada zako mradi ukifanikiwa hautawasaidia wana CCM peke yao naamini lengo ni kuwasaidia watanzania wote hususani kina mama na watoto
Chama
Gongo la mboto DSM

Naona wewe JF inakukosesha usingizi kabisa hizo tuhuma zimetolewa kwenye magazeti huyo GAMBA HK kaamua kuzijibu umu sasa JF imeharibiwa kivipi unataka tukubaliane na utetezi wake wa kitoto unatakiwa kujua tuliopo umu tuna bongo nzuri za kufikiria hatuwezi kusikiliza utetezi wa kipuuzi kama wa HK.
 
jamani CCM tuoneeni huruma muda mwingine... kuna life after death..wananchi wenu mnawaomba kura vizuri wakati wa uchaguzi na baada ya hapo mnawasulubisha..so far,ukifa huendi na kitu my dear!!!!i feel sorry for you
 
halafu kinachosikitisha zaidi ni mtu kupost kitu halafu hajibu chochote after that..its better kukaa kimya kuliko kuleta thread ambayo huwezi kujibu watu later..damn
 
Mbunge wa Jimbo la Nzega,
Taarifa kwa vyombo vya habari
Bungeni, Dodoma, Mei 1, 2013.

Nawasalimu kwa heshima na taadhima.




Ya ukweli: ni kweli kwamba ninamiliki hisa kwenye kampuni ya Emergent Africa Ltd. Nina hisa 40% na mke wangu Dr. Bayoum Kigwangalla anamiliki hisa 11%. Sijihusishi na kuendesha biashara hii kama mtendaji wa kila siku – kampuni ina watumishi wake sehemu mbalimbali. Ni kweli kwamba kampuni ina mradi wa kujenga chuo cha afya Nzega (International Institute for Health Tabora), eneo la uchama, na ni kweli imepewa orodha ndefu ya vitu ilivyosamehewa kodi na serikali kwa kuwa ni vitu/vifaa vya mtaji (deemed capital goods). Ni kweli kwamba kampuni imewahi kuingiza nchini kontena moja lenye vifaa vichache sana katika vinavyotajwa kwenye habari ile, na vingi kati ya hivyo vipo aidha kwenye stoo ya kampuni iliyopo Nzega ama ya Dar es salaam, Kigamboni. Kwa kuwa vipo, wanahabari wanakaribishwa kwenda kuvitazama vitu hivi kama wanapenda.



Kuwa na hisa kwenye kampuni inayofanya biashara halali siyo dhambi. Kupata msamaha wa kodi siyo dhambi. Dhambi ingekuwa kuviuza baada ya kupata msamaha. Kama kuna mtu anaamini kuwa kuna vifaa vimeuzwa na kampuni yangu, kati ya hivi vilivyoingizwa nchini kwa msamaha, anakaribishwa kuleta uthibitisho wa nyaraka za mauzo (cash sale receipts, tax invoice ya mauzo, pay-in slip ya benki ya malipo, delivery note, ama receipt yoyote ile ya kampuni hii inayoashiria kuwa mauzo yamefanyika) ili niweze kufuatilia kujua ni nani aliyeuza na kwa nini alifanya hivyo ili niweze kuchukua hatua za kinidhamu dhidi yake ikiwa ni pamoja na kumpeleka mbele ya vyombo vya sheria.

Watanzania tuache kushabikia uongo. Kufanya hivyo kunaziba mianya ya ukweli kutamalaki. Tuache kutazama mambo kwa macho ya wivu, husda na majungu. Tusimame kwenye misingi ya ukweli daima. Nchi hii itaendelezwa na watu wenye kuchukua maamuzi thabiti na hatua za maksudi za kuleta mabadiliko – kama miradi ya namna hii (ya chuo cha afya Nzega kule!). Nchi yetu bado ina watu waaminifu na waadilifu na tunaamini tutafanikiwa kuwadhibiti walio waovu. Hata siku moja kweli haijawahi kushindwa vita na uongo. Si kila mtu aliyeko kwenye uongozi ndani ya CCM basi ni fisadi, watu wazuri na wasafi wapo pia. Tusimuangalie kila mtu kwa sura ya ‘ufisadi' na ‘ubadhirifu' tu! Tuaminiane jamani. Tusifedheheshane na kukatishana tamaa. Safari kuelekea mapinduzi ya maisha ya watanzania kiuchumi na kijamii bado ni ndefu lakini tutafika. Tufanyeni kazi.
Taarifa hii nimeiandika na kuitoa mimi mwenyewe, Hamisi Andrea Kigwangalla, M.D., Mbunge, Jimbo la Nzega. (simu yangu ya kiganjani ni 0782636963 na email yangu ni hkigwangalla@gmail.com, website: www.hamisikigwangalla.com )


Mhe.Mbunge.
Kama unadhani haya ndiyo majibu dhidi ya wanaokutuhumu/kusema uongo kama ulivyojitetea basi kuna uwalakini.

Maelezo yako hayaonyeshi kushawishi kujenga ukweli na zaidi umejenga maswali mengine kuliko majibu na hujaguzia baadhi ya madai yaliyotolewa na gazeti husika hivyo unaongeza nguvu ya hoja kwa tuhuma zilizoandikwa dhidi yako.


Mfano mdogo wa baadhi ya maswali mapya angalia maneno yenye uwekundu kwenye bandiko lako.
Pili unataka kushawishi watu eti wapi risiti kweli unazungumza kwa hadhi ya Udokta/Mbunge-Wapi umeona mlipa rushwa anadai Risiti ? au mpokeaji anatoa Risiti? acha utani labda umeteleza mawazo.
 
Kigwangala hana makosa tatizo ni mfumo tulio nao, jakuna jinsi ya kuzuia conflict of interest, je mheshimiwa ametaja kampuni hiyo.
 
HKigwangalla
JF imeharibiwa na watu wenye roho za husda; nadhani wameshtushwa sana na jitihada zako unazozifanya badala ya kuomba ushauri nao wafanye kitu gani wamegeuka ni watu waliokata tamaa ya maisha hasira zao wanataka kuzimaliza kwako; nakupa pole sana kwa hilo endelea na jitihada zako mradi ukifanikiwa hautawasaidia wana CCM peke yao naamini lengo ni kuwasaidia watanzania wote hususani kina mama na watoto
Chama
Gongo la mboto DSM

Mkuu CHAMA na wewe unaunga mkono upuuzi huu.Ifike mahali tuweke pembeni itikadi zetu za kisiasa kwa ajili ya kuliokoa Taifa letu.Mbali na tuhuma anazo tuhumiwa nazo ziwe za kweli zisiwe za kweli.Ukiyasoma maelezo yake inaonekana ni mtu mwenye uwezo mkubwa sana kifedha.Mtu ambae hakusitahili hata kusamehewa kulipa kodi na serekali yetu kama ingekuwa makini kama alisamehewa kweli kwa mjibu wa maelezo yake yasiyo na ushahidi.Huu ni upuuzi mwingine tunao upinga unaofanywa na serekali yetu.Mtu mwenye uwezo mkubwa kabisa wa kulipa kodi anasamehewa kulipa kodi huku mwananchi ambae ni masikini kabisa ambae anatakiwa kusaidiwa anapelekewa mgambo kupigwa mabuti ili aweze kulipa kodi kwa nguvu pengine na kufungwa kabisa.Eti tajilri mkubwa kabisa mwenye nazo anasamehewa kulipa kodi na yeye bila hata chembe ya aibu anajitokeza hadharani nimesamehewa kulipa kodi na serekali kwa kisingizio cha kujenga Chuo cha afya.Hicho chuo cha afya kitakuwa kinatoa huduma bure kwa mwananchi?.
 
Last edited by a moderator:
umemjibu vizuri sana huyu jamaa anayetuhumiwa kuwa ni mrundi,ila nami nimemshangaa ameyataja magazet matatu tu,mbona hayo magazet mengine yalomwandika hakuyataja?na kama Kigwangala anahis hana sababu ya kutujibu basi angekaa na tamko lake akasoma na huyo mwanahisa mwenzie,
pia amesema yeye ana hisa 40% mkewe 11% je hizo asilimia nyingine anamiliki nani?

Ambazo ukizijumlisha ni 51% ambazo kwa pamoja zinawafanya wawe majority shareholders wenye ku influence maamuzi ya kampuni, ukiacha zake pekee 40%. Mh. Hamis hajui hata elementary company law & corporate governance ndiyo sababu anatoa majibu mepesi hivi!
 
Hkingwangala

Ni kweli jina unalotumia sio lako.
Ni kweli unaasili ya nje ya Tanzania na uraia wako unawalakini.
Ni kweli unahisa kwenye kampuni tajwa.
Ni kweli kampuni tajwa ni ndogo hivyo wewe na mke wako mnashiriki moja kwa moja kwenye utendaji wa kila siku.

Ni kweli kabisa uliichongea mchongo kupata tender husika.
Ni kweli ilikwepa ushuru na kuagiza vitu vingi vya biashra yako visvyokwenye tender.

Malezo yako marefu yamethibitisha ufisadi mkubwa kwenye kampuni yako unayoyafanya ukitumia kofia ya ubunge. Hakuna ulichokataa.

H kingwangala ni Fisadi kama RA, EL nk mnatofautiana kwenye tarakimu tuu.

Huna uadilifu wala hadhi ya kuwa Mbunge. Mwizi ni mwzi hata akiiba kalamu.
 
Wewe na ccm wenzako wote ni mafisadi tu! Blabla nyingi wakati wenzako wanazo facts zote mikononi! Kubali uliyotenda wanacnhi na taifa litakusamehe. Kwani wewe ni wa kwanza mkufisadi nchi hii? Jana bila aiubu ccm mmemtetea jangili wa tembo Kinana.... ila hakuna kati yenu (ccm) aliyetetea mali asili zetu zinazoendelea kugemwa. Hivi nyie wote ccm ni kundi lilelile, wezi watupu!!

katiba mpya mtasusia? au mlikuwa mnapima hali ya hewa?
 
Huyu jamaa amewai kutishia kujiuzulu ubunge.
Kumbe ilikua mkwara tu, ccm ndio inayombeba.
 
Mbunge wa Jimbo la Nzega,
Taarifa kwa vyombo vya habari
Bungeni, Dodoma, Mei 1, 2013.

……………………………..
Nimesikitishwa sana na habari hii hususan kwa kuwa ilichapishwa bila kunipa fursa ya kueleza kwa mapana uhusika wangu. Niwapongeze gazeti la Nipashe kwa kupuuza uzushi huu mara baada ya kunipigia na kueleza upande wangu wa hadithi.

………………………………………….
Yote haya kwa ujumla wake yalikuwa ni mambo ya uongo na yasiyo na chembe ya ukweli hata kidogo. Mara zote nimekuwa nikiyadharau na kuongea na wahariri wa vyombo husika vya habari kwa namna inayoashiria urafiki na weledi wa kushirikiana na kufanya kazi pamoja na si vinginevyo;

Kumbe hata hivyo ulipewa nafasi ya kueleza – japo si kwa mapana, Mbunge wangu! Umenisikitisha kwa kutuonyesha kuwa mara zote umekuwa ukiyamaliza na wahariri – japo swali ni je maongezi haya hayakuhusu ‘bahasha’ ili wasiendelee kukuanika?

…….ushauri ambao niliupata mwaka 2009 kutoka kwa moja ya wanasheria wa kampuni yangu (wa kampuni ya Marando, Mnyele & Co. Advocates), wakili nguli Mzee Mabere Nyaucho Marando, ambaye alisema ‘wasamehe tu hawa gazeti la Sauti Huru maana ni vema kujenga marafiki wengi zaidi na media kwa kuwa wewe ni kijana, kuliko kujenga maadui – na niliwasamehe bila gharama yoyote ile’.
Nimependa unavyowaingiza CDM kiaina ili ku-win sympathy yao, I suppose!

……Ya ukweli: ni kweli kwamba ninamiliki hisa kwenye kampuni ya Emergent Africa Ltd. Nina hisa 40% na mke wangu Dr. Bayoum Kigwangalla anamiliki hisa 11%. Sijihusishi na kuendesha biashara hii kama mtendaji wa kila siku – kampuni ina watumishi wake sehemu mbalimbali. Ni kweli kwamba kampuni ina mradi wa kujenga chuo cha afya Nzega (International Institute for Health Tabora), eneo la uchama, na ni kweli imepewa orodha ndefu ya vitu ilivyosamehewa kodi na serikali kwa kuwa ni vitu/vifaa vya mtaji (deemed capital goods). Ni kweli kwamba kampuni imewahi kuingiza nchini kontena moja lenye vifaa vichache sana katika vinavyotajwa kwenye habari ile, na vingi kati ya hivyo vipo aidha kwenye stoo ya kampuni iliyopo Nzega ama ya Dar es salaam, Kigamboni. Kwa kuwa vipo, wanahabari wanakaribishwa kwenda kuvitazama vitu hivi kama wanapenda.

Ya uongo: Si kweli kwamba nina hisa 78% na mke wangu Dr. Bayoum Kigwangalla ana hisa 22% - ni uongo. Si kweli kwamba kampuni imeagiza vitu na kuvipitisha bandarini na forodhani kwa msamaha kwa nia ya kuuza na hivyo kuiibia serikali kwa njia ya kukwepa kodi. Si kweli kwamba kampuni ya Emergent Africa Ltd imeingiza vifaa vyote ambavyo imepewa msamaha, kama habari inavyotaka kuwaaminisha waTanzania. Sijawahi kuuza bidhaa zozote zile za kampuni hii zilizoingizwa nchini kwa njia ya msamaha wa kodi. Kampuni ya Emergent Africa Ltd haina mradi wa kuuza tiles na hivyo haijawahi kufanya biashara hiyo.
Mwaga ushahidi tuliouzoea wa documents!

……….. Si kila mtu aliyeko kwenye uongozi ndani ya CCM basi ni fisadi, watu wazuri na wasafi wapo pia. ……………………

Taarifa hii nimeiandika na kuitoa mimi mwenyewe, Hamisi Andrea Kigwangalla, M.D., Mbunge, Jimbo la Nzega. (simu yangu ya kiganjani ni 0782636963 na email yangu ni hkigwangalla@gmail.com, website: www.hamisikigwangalla.com )
Sijui huu ujumbe unawapa CCM au watu gani na kwa nia ipi! Nawaachia wachambuzi makini watudadavulie zaidi
 
Kaka Saidi Bagaile, unathibitisha mwendelezo wa kifo cha ccm, kama yule RC wa Arusha. Umeanza kuzikana kampuni zako, halafu baada ya kutuorodheshea uharam wa utajiri wako umekuja kukiri kwamba wewe ndo "Major Stakeholder" Yaan ni sawa na Dowans tu ya Rostam Aziz kutuambia kwamba yeye sio mmiliki ila amepewa "Power of Attoney 100%" Halaf wewe na huyu jamaa wote hamna asili ya Tz. Watz tuamke. Mwanamke wa JF amka
 
FROM BEN SAANANE POST

3:VIJANA WALIOPEWA DHAMANA


Kuna vijana waliopewa dhamana lakini wameishia kuwa mafisadi wakubwa.Hawa ni wasaliti na ni kikwazo kwa vijana wengi kuaminiwa na kupewa dhamana.

Gazeti moja leo limeripoti Dr.kigangallah kutumia vifaa vilivyolipiwa ushuru kwa ajili ya kujengea hospitali na badala yake akafungua dukaa la vifaa vya ujenzi kupitia kampuni anayomiliki hisa asilimia 78 inaitwa emergent african Limited na kuuzia wafanya biashara mbali mbali na miongoni mwao ambaye ni mojawapo wa wanachama wa kundi la Stop Ben Saanane (SBS) ni MRISHO GAMBO.Huyu ni Mkuu wa wilaya ya Korogwe

Inashangaza sana mkuu wa wilaya tena kijana kama huyu anashirikiana na mafisadi kuhujumu Afya ya walalahoi

Vigae (Tiles zilizoingizwa nchini) na Emergent Africa ya Dk Kigwangala tokea China na kupewa msamaha wa kodi Mrisho Gambo Mkuu wa Wilaya ya Korogwe aliuziwa mabox 114 kwa shilingi 22,OOO. Mtu ambaye anashirikiana na Mbunge wa CCM kuibia nchi, kununua bidhaa haramu zisizolipiwa ushuru, zilizoonekana ni mali za kituo cha afya ana usafi gani wa kuendelea kuongoza wananchi? Aseme arudishe vigae vya Kituo cha afya cha Nzega alivyotumia kujengea nyumba yake.


Sasa aje hapa abishe tulete ushahidi.Nashangaa watu wanajifaragua na ID humu kutusi watu kumbe wao ndiyo mafisadi wakubwa.Wao wanasema uongo juu yetu,Sisi tutasema ukweli juu yao hadi watakapoweka makombora yao ya uongo chini
 
Back
Top Bottom