Mkuu kwa jinsi ulivyoandika hii mada yako naweza kuona busara na utu uzima ulioko kwenye maandishi yako
Ninachotaka nikushauri ni kuwa mabinti aina ya
lara 1 wanakuwa na mitizamo hii kwakuwa wanakuwa wanapambana na hofu zilizoko ndani mwao kuhusiana na suala zima la ndoa,wanaiogopa
Sasa wanadhani kupambana kwa kuipaka matope wataokoka nayo
Nadhani unajua kabisa kuwa mtu kama anakuogopa atashinda mtaani kwenu akikukashifu kila uchao,anapofanya hivyo sio kwamba anafanya hivyo kwakuwa na lengo la kukupaka matope,hapana,anakuwa anapambana na hofu zilizoko ndani mwake kwakuwa anajua kabisa anakuogopa sana
Huyu mwache na akiendelea kukua atakuja kugundua kuwa alichokuwa anakiogopa hakikufaa kuogopwa hata kidogo kwani ni cha kawaida,nilipokuwa na umeri fulani hivi nilikuwa napambana na vijana wenzangu ambao walikuwa wanajiingiza kwenye ndoa
Lakini zaidi nilikuwa nashauriwa na watu wazima kuwa kinachonisumbua ni hofu ya ndoa na umri tu lakini sikuwaelewa,waliniambia kuwa siku nikija kuoa au kukua mambo yatabadilika sana
Leo hii sijaoa lakini nimekua na nayaona mambo kwa mapana yake na sina haja ya kuikashifu au kuisema vibaya au kuigopa ndoa kwakuwa huo ni utoto!!