Majibu kwa lara 1

Majibu kwa lara 1

Basi nachelea kusema sikumwelewa Lara1, mie niliona mantiki ya sred ile ilikuwa ni kwamba, wanawake kati ya 30-40, walio wanaopata pressure katika jamii kuolewa, wawe makini, wasikubali kuwa bullied. Sababu kubwa ikiwa ni kuwa si kila ndoa ina furaha(japo wengi hawasemi), na maisha yote yana changamoto.

Kwani wa miaka 20-30 wana exception gani ya kukumbana na mambo ambayo wenye 30-40 watakumbana nayo?

Generally, ndoa haina umri.
 
Jana lara 1 alianzisha mada inayosema, wanawake above 30 hata 40 marriage is a hypocrytical institution. Kilichonishitua ni kuita ndoa ni hypocrytical institution tafsiri isiyo rasmi ni taasisi ya kinafiki/unafiki.

Mimi nimeoa na nina mtoto mmoja sikubaliani kabisa na mtazamo huu wa lara 1























Lara 1 ni binti ambaye hajawahi kuwa kwenye ndoa hivyo kujifanya anayajua mambo ya ndoa kwa undani ni uongo,ni sawa na mtu aliyeishia kidato cha sita na kujifanya anajua sana matatizo ya chuo kikuu ili hali hajatia mguu pale.

Anatahadharisha wale ambao ndoa zao zinaonekana ziko vizuri kwa sasa kwamba na wao ndoa zao zaweza geuka kuwa kilio,anasema kwamba kwani ndoa zao zina uspecial upi.

Ukweli ni kuwa ndoa haziwezi kufanana hata siku moja kama anavyotaka yeye ziwe. Si lazima ndoa zote ziwe na migogoro hata kidogo,kuna ndoa zinaanza vizuri zinaishia vizuri.

Zingine zinaanza vizuri zinaishia vibaya,zingine zinaanza vibaya zinaishia vizuri,zingine zinaanza vibaya na kuisha vibaya,kutegemea na wanandoa wenyewe wanavyoendesha ndoa yao.

Anashangaa wana ndoa wa jf hawatoi ushuhuda wa ndoa zao au kuomba ushauri wakati mambo yanapoharibika.kwa vile binti huyu hajawahi kuwa kwenye ndoa sishangai kuona akiuliza kitu kama hiki ndoa ina maadili yake mojawapo ni kutotoa siri nje ya ndoa.

Hii haimaanishi kwamba wafe na tai shingoni kuna taratibu zake akiingia kwenye ndoa ataambiwa ndiyo maana wapo na wasimamizi wa ndoa kuwaelekeza nini cha kufanya.

Lakini hata wale mambo yao yako salama kabisa wanaogopa kutoa ushuhuda wao kuogopa kejeli,dharau kutoka kwa watu wenye mtazamo kama wa huyo dada. Lakini ajue pia walioko kwenye ndoa hasa wanawake wana majukumu mengi ya kifamilia tofauti na walio single.

Anadai kuwa wanawake walioko kwenye ndoa ni wanafiki kwa sababu waume zao wanazini nje ya ndoa na wengine wana watoto nje ya ndoa,wengine hawatoi matumizi nyumbani lakini hawawakatazi,hvyi anauhakika gani hawawakanyi waume zao?

Yeye mwenyewe wapo watu walishamshauri aache tabia yake ya kuchuna wanaume lakini hajaacha lakini si kwamba hajashauriwa.

Anaelekea kuhitimisha kwa kusema ndoa ni safari hivyo wanaofurahi sasa wajiandae kwa lolote mbeleni yaani kufiwa na mwenza,kupata ajali,mwenzi kulogwa.

Hapa amenishangaza zaidi ina maana walio single hawafiwi hata na wazazi,ama rafiki kufiwa ni mpaka awe



Its very true,she biased on the negative part of it which isn't always the case.Although marriage journey is not always honeymoon at Hawaii
 
Ndoa ni taasisi nzito, iheshimiwe.

Kama huiwezi kaa kimya usiwavunje wenzako moyo wanaotamani kuifuata.

Sio busara pia kutoa mifano ya negative sides za wazazi hasa kwenye maisha ya ndoa, inawezekana ulitaka upitie maisha ya kishua yasio na dosari ndo maana kila siku unampondea mzee wako kwa makosa alofanya. SIO ISHU.
 
umeona na wewe mkuu eenh tuko pamoja ndoa lazima iheshimiwe na watu wote

Kwa jamii yeyote duniani huwa inakuwa na maadili(morals) ambazo ndizo huwa zinawaongoza with katika masuala mbali2 ya maisha kwa afrika nikiongea kwa mapana kuiacha Tanzania ndoa ndiyo msingi wa chini wa familia kwa mjibu was maadili yetu familia kamili inahusisha baba na mama nguzo ukivunja ungo ama kubarehe wengi wanategemea hatua ya ndoa (kuoa ama kuolewa) usipofanya hivyo jamii LA IMA ijiulize kulikoni has a km hauna tatizo na c mtawa hapa lala1hauna cha maana zaidi ya kujifanya unaiga mifumo usiyo ijua misingi yake. Kwa lugha ya kisaikolojia unaweza kuitwa mmame(kinyume cha mbabe) kimatumizi katika mfume dume.
 
KIM JONG UN THE SECOND! ALIAS lara 1 (WHAT A CHEMISTRY!!)
images
images
 
Wengine wanaona tofauti, wanaona kama 30-40 ni less advantaged, so they have to grab anything that comes in their way.

Bold ndio point ya sred ile

Kwani wa miaka 20-30 wana exception gani ya kukumbana na mambo ambayo wenye 30-40 watakumbana nayo?

Generally, ndoa haina umri.
 
Ulimpata kabisa bro na majibu yako ni sahihi kabisa...

ila huyu Lara 1 ana influence kubwa humu hata wanandoa utashangaa wanakukana

ndio maana ili jukwaa nilishahama...limepoteza hadhi yake...nimeamua kutembelea international forum nikaangalie news za ndege ya Malaysia...


tehetehe kwamba siyo majibu ni kweli siyo majibu yako ila ni majibu yangu na mtazamo wangu,hitimisho nimeshafanya kazi ukipata muda pitia usiogope urefu kuna cha kujifunza.
 
Kwani wa miaka 20-30 wana exception gani ya kukumbana na mambo ambayo wenye 30-40 watakumbana nayo?

Generally, ndoa haina umri.[/QUOTE]

Ni ukweli tupu mkuu ndoa haina umri wengine wako bussy kutafuta maisha kwanza, kuoa/kuolewa baadaye.
 
Ndoa ni taasisi nzito, iheshimiwe.

Kama huiwezi kaa kimya usiwavunje wenzako moyo wanaotamani kuifuata.

Sio busara pia kutoa mifano ya negative sides za wazazi hasa kwenye maisha ya ndoa, inawezekana ulitaka upitie maisha ya kishua yasio na dosari ndo maana kila siku unampondea mzee wako kwa makosa alofanya. SIO ISHU.

Ni kweli mkuu mtu kama amekata tamaa aache wengine wajaribu bahati zao si kuaminisha watu kuwa ndoa ni matatizo mwanzo mwisho.
 
Back
Top Bottom