Maji yakipwa huenda wapi?

Haya maelezo ni ya kitaalam sana. Na moja ya vitu visivyoeleweka au kuaminiwa au vyenye kasoro ni kuwa na maelezo ya kitaalam mengi sana ambayo mtu wa kawaida ni ngumu kuyaelewa au kuyafanyia practical. Maana yake ni kuwa elimu au maarifa ya hilo jambo yamefichwa kwa kutokujua au kwa makusudi. Binafsi linapokuja suala universe na mambo yake naonaga nadanganywa sana. Sijui labda ni elimu duni niliyonayo au uwezo wangu mdogo wa kuyaelewa.
 
Hukujiandaa tu kuyaelewa ila yanaeleweka
 
Kuna jitu kubwa huwa linakunywa hayo maji. Likikojoa ndo maji yanarudi
 
Kuyaelewa mpaka ufanye meditation
 
Mwezi unasababishaje maji kupwa na maji kujaa?
Kila kitu kinavutana na kingine (ngoja tusubiri ufanisi wa quantum entanglement, inaweza kutufumbua macho zaidi). In a nutshell, hii ni kwa sababu ya uwepo wa electromagnetic sub-atomic particles ndani ya maada (kama electrons, protons, etc) ambazo ndizo zinaleta matokeo hayo.

Sasa kadiri vitu hivi vinapokuwa na mass kubwa na kukaribiana sana, kani ya uvutano kati yao inaongezeka. Mwezi ndilo gimba kubwa zaidi lililo karibu na dunia.

Pamoja na kwamba dunia inakabiliwa na kani mbalimbali kulingana na magimba yaliyoko angani (jua, sayari zingine, nyota zingine, nk), kani ya mwezi ndiyo kubwa zaidi.

So, maji yanavutwaje? Ama kupwa na kujaa kunafanyikaje? Imagine kani hiyo ya uvutano kati ya mwezi na dunia kama vile mwezi unajaribu kufyonza ama kunyakua maji duniani na kuyavutia ama kuyaelekeza kwenye uso wake.

Kimsingi, dunia yote inavutwa, lakini kwa vile maji ni kimiminika kisicho intact (kisichoshikamana) kama ardhi, basi yako flexible (less viscous) kuhamia upande mmoja ama mwingine katika chanzo cha maji (like bahari).

Kwa hiyo, kwa sababu kani hiyo siyo kubwa sana (like blackhole 🙂) kiasi kwamba haiwezi kuyanyanyua na kuyahamisha maji mazima yatoke duniani, basi maji yanaishia kuburutwa na kuhamishiwa upande mmoja hadi mwingine wa ziwa, bahari, nk. kulingana na uelekeo na position ya mwezi angani wrt the earth.
 
Ndio maana huwa sipendi kufuatilia sana habari za hii dunia,mwishowe tunaishia kutiana hofu tu.Yani imagine li body likubwa kama hili linaelea hewani huku linayumba yumba,huku linachomwa na jua upande mmoja huku upande mwingine unakuwa na giza,huku kuna mi force kibao inalipeleka kulia-kushoto juu-chini...
 
Nadhani hiyo ni paranoia ya kawaida tu, sawa na mtu anayesafiri kwa ndege (au hata gari) mara ya kwanza. Lakini akielewa na kuzoea utendaji na raha husika, anaweza hata kujisahau aka-book ndege za mashirika mawili kwa mpigo.

Hapa pia, ukielewa kwamba hizo kani zimeratibiwa na zinafanya kazi zake kwa uhakika na uaminifu 100%, wala hakuna sababu ya kuwa na hofu yoyote.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…