Maji ya kuoga...!

kaka we badili nyumba ya kuishi tu.. maji ya kuoga unayakuta hukohuko hata ya moto ukitaka kitu cha shower... hutagomba na mkeo milele
 
Majibu ya wanawake wengi ktk hili imenipa picha ya kwanini ndoa zinawashinda. hili ni moja ya jukumu la mwanamke wa kiafrika kwa mmewe . Mnataka wanaumme lakini kazi iko kuiboresha ndoa. Mbona wakati hamjafunga ndoa yote haya mnafanya. Mkisha rekebisha viburi juu.. haya kazi kwenu. Mimi nikijipelekea maji bafuni hapakaliki mpaka niulizwe sababu ya kufanya hivyo.mnahalibiwa na mashoga kwenye hizo saloon.

excellent point of view. Kweli kwa majibu haya ya wanawake wengi yanaonesha sababu za kulegalega kwa ndoa nyingi. Wengi wao wakishaipata hiyo ndoa waliyoililia kwa miaka mingi huleta madharau na kutupilia mbali hata waliyofundwa. Kweli mazoea huleta dharau!
 
na nsiolewe! Kwanza wanaume wa cku hz wanaoa au wanatafuta watu wa kuwapa frustration! Hapa JF ndo kabisaaa...ningekuwa kipofu sioni wadada wanavolia hapa ungentisha! Jamani mume wangu atajiandaa kufua, kupika, aniogeshe, ajiwekee maji ya kuoga ile ya kubeba mimba ndio itakuwa kazi yangu tu! Museven umeckia?!

nimesikia sabri. Ila wanaume wa sampuli ìyo wanapatikana akhera tu!
 
na nsiolewe! Kwanza wanaume wa cku hz wanaoa au wanatafuta watu wa kuwapa frustration! Hapa JF ndo kabisaaa...ningekuwa kipofu sioni wadada wanavolia hapa ungentisha! Jamani mume wangu atajiandaa kufua, kupika, aniogeshe, ajiwekee maji ya kuoga ile ya kubeba mimba ndio itakuwa kazi yangu tu! Museven umeckia?!

nimesikia sabry. Kila la kheri. Ila wanaume wa sampuli hìyo wanapatikana akhera tu!
 
si maji tu!
ati unakuta janaume yeye na mkewe wanafanya kazi na kurudi usiku lakini ati lazma mkewe apike ndo ale.....akipika mfanyakazi hali!
hovyo!!!!!!!!!!!!!!
maji aweke nikiweka msaada tu!
 
excellent point of view. Kweli kwa majibu haya ya wanawake wengi yanaonesha sababu za kulegalega kwa ndoa nyingi. Wengi wao wakishaipata hiyo ndoa waliyoililia kwa miaka mingi huleta madharau na kutupilia mbali hata waliyofundwa. Kweli mazoea huleta dharau!

museven baada ya kupitia hii thread nimegundua kuwa kuna variations nyingi sana za mapenzi.... na ninaamini kabisa kuwa kwenye ndoa/mapenzi ni vitu vichache sana ambavyo ni wajibu na vingi ambavyo si wajibu bali mtu anavifanya kwa kuwa kuna mapenzi, anampenda mwenzi wake. Nitakuwekea maji ya kuoga bafuni (na kuoga wote) kwa kuwa tunapendana, nakupenda na kwangu ni sehemu ya mapenzi. Lakini haimaanishi kuwa ni wajibu wangu kwa sababu kama sina mapenzi na wewe haitotokea kwani hatutokuwa pamoja i.e. kwangu mie kwa mtu nimpendaye kumwekea maji bafuni ni wajibu KWANGU katika mapenzi na katu hatakiwi wewe kuichukulia kama ni WAJIBU WANGU. Kwa sababu nitafanya kwa kuwa ninapenda na si kwa kuwa tu ni mkewe au hawara.
The same applies kwenye kufua vitasa n.k
 
kama unyumba anakupa nafikiri boresha kwa kuweka
shower yako mwenyewe uondokane na kuomba omba.
vinginevyo tafuta nyumba ndogo maji yanawekwa hadi iliki
 
Naomba msaada wanaJF. Hivi mwanamke kumwekea maji mumewe bafuni ni wajibu au ni fadhìla tu? Nauliza hivi sababu mke wangu haniwekei maji mpaka nimgombeze au siku akipenda mwenyewe. Siku nyingi nalazimika kujibebea mwenyewe. Nimeshagombana naye mara kadhaa lakini habadiliki. Nifanyeje?

unajua museven, ngoja nikwambie kitu kimoja,

kwa mila na desturi zetu za kiafrika, hususan Tanzania..........

mapenzi na hayo maisha mnayoita romantic love ya mume na mke....

yameelekezwa zaidi katika majukumu, na wala sio katika muelekeo wa kizungu, ule wa kukisiana hadharani na kukumbatiana publically,

Having said that, mapenzi ya kiafrika yameboreshwa zaidi na majukumu yanayofanywa na wanandoa wenyewe...

na ni kwa jinsi gani , jamii inavyochukulia na mafundisho au aina ya maisha ambayo wanandoa wenyewe wamekuzwa nayo....

kitanzania, mwanaume anaonekana kichwa cha nyumba

na ataonekana ni mwanaume halisi anaeipenda familia yake na kumjali mkewe,

kama tu anatekeleza wajibu wake wa kimsingi, yaani kumjali mke wake kwa lishe, afya, mavazi na mahitaji mengine ya kimaisha,

kumbuka kuwa hapa, unaweza usionekane ni baba bora kama tu unadhani kwa kumkiss mkeo kila wakati, kumhug na kumshika mikono kwa mbwembwe, ndio suluhisho...........wakati mambo ya kimsingi katika maisha hujayatekeleza.

kwa wanawake, kule kumjali mumeo, kwa mambo kama hayo aliyosema museven, yaani kuweka nyumba katika usafi, kumwandalia mumeo maji ya kuoga, kuongea nae kwa lugha ya mahaba, kumheshimu,kumwandalia chakula kizuri ndo ya msingi sana.

Kitanzania bado hatuoni kuwa mwanamke anaejua kukata kiuno na kukupelekesha kwenye kungonoka ndo mke bora........hpana hii dhana kwenye jamii yetu bado ni ndoto!.......na hii ni sababu ya mfumo wa kimaisha tunaouishi...............

Lo.......nilisahau kuwasalimia wapendwa wangu!habari za masiku tele wapendwa, JF, long time............................

nipo nimefichwa huku South Sudan, karibuni kwa tahadhari lakini.

Tchaooooooooooooooooooo.................
 
mapenzi mnayaona kwenye kufanyiwa tu?
Siku mkeo akikwambia uinamishe kitambi chako upige deki nyumba utakubali?
Vyombo utaosha? Nguo utafua? Kama mkiwa na utaratibu wa kusaidia wake zenu mambo kama hayo basi mjue na nyie mtafanyiwa mazuri zaidi ya kupelekewa maji ya kuoga.

Ha,ha,ha,ha.Tuoneane huruma jamani.Kuinamisha kitambi kupiga deki ni kama corporal punishment kwa mwanaume.
 
Duh! Yaani mnatufanya wanawake kama ni watumwa wa ndoa! Hivi kuna kitu chochote ambacho mwanamke anapaswa kuenjoy kwenye ndoa?! Kufua hadi vyupi,kupika kutumikia penzi mara sijui gogo,mara chai,mama mkwe,ndugu, watoto! Mwanamke role yake ni ipi na mwanaume yake ipi?

Sio kweli . Hii dhana ya utumwa ndio inharibu kabisa akili za wamama. Kama una maji bafuni kwako huhitaji msaada wowote. Lakini fikiria maji ni ya kuchemsha jikoni kwa mkaa au kuni. Hebu fikiri pia mkeo haendi kazini halafu hakusaidii uwahi mafoleni. Hata akiwa anafanya kazi , hizo hela si anakulga mwenyewe ?" Ashindwe hata kuweka maji jamani?
 
Umejibu bila kufikir..... mke yuko nyumbani mme ana mizunguko ya kupata hata hizo pesa za matumizi hom kwani yy hachoki majibu ya wanawake wengi ktk hili imenipa picha ya kwa nn ndoa zinawashinda hili ni moja ya jukumu la mwanamke wa kiafrika kwa mmewe

katika wanawake walioshiriki mjadala huu so far ni mmoja tu amekubali hali halisi ya mila na heshima katika ndoa, ni Mamamkwe pekee
 
Tafuta nyumba yenye choo, bafu na maji ndani kwa ndani, uondokane na karaha, kama unaona unakarahishwa, japo mimi sioni tatizo ni nini hapa maana hii kazi hakupangiwa mke au mume. wewe kazi yako nini kama mwanamme ndani ya nyumba? kuvaa Suruali au? hebu tuondokee hapa cha uvivu!
 
museven baada ya kupitia hii thread nimegundua kuwa kuna variations nyingi sana za mapenzi.... na ninaamini kabisa kuwa kwenye ndoa/mapenzi ni vitu vichache sana ambavyo ni wajibu na vingi ambavyo si wajibu bali mtu anavifanya kwa kuwa kuna mapenzi, anampenda mwenzi wake. Nitakuwekea maji ya kuoga bafuni (na kuoga wote) kwa kuwa tunapendana, nakupenda na kwangu ni sehemu ya mapenzi. Lakini haimaanishi kuwa ni wajibu wangu kwa sababu kama sina mapenzi na wewe haitotokea kwani hatutokuwa pamoja i.e. kwangu mie kwa mtu nimpendaye kumwekea maji bafuni ni wajibu KWANGU katika mapenzi na katu hatakiwi wewe kuichukulia kama ni WAJIBU WANGU. Kwa sababu nitafanya kwa kuwa ninapenda na si kwa kuwa tu ni mkewe au hawara.
The same applies kwenye kufua vitasa n.k

washindwe tu kuelewa!
 
Back
Top Bottom