Maji ya kuoga...!

nimerudi aisee. Network zinaniletea uzushi uzushi bana ila usikonde nitafanya mambo tena very soon. ( kuna majitu yanakodolea macho maongezi yetu ujue).
Ngoja nitoke hapa.

hahahahahah lol! Haya banaa baadaye basi.
 
Mwambie huyo banaa kama anataka mtu wa kumfanyia kazi si aajiri house girl atambebea maji asubuhi na jioni/usiku.

Kaka hapo mwisho si ataomba mchezo kwa housegirl. Kwa kutembea na housegirl huwa kunaanzaje?
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Husni sikiliza ile kolabo ya FA,NGWEAR na JIDE 'skiza me'
kwenye hiyo bold haija kaa vizuri mtakuja kuletewa vicheche ndani
Unapenda ubosi eeh! We kupeleka maji bafuni vinakushinda? Kabla hujaoa ulikuwa unapelekewa na nani?
Acheni kukera na kuchosha wake zenu. Kwanza hata unyumba ni hiari yake akupe au akunyime.
 
ndio mijanaume ya kiafrica ilivyo inataka hadi viatu ibrashiwe....nyooooo!
 
sio kosa lako lakini ,kosa la wazazi wako tangia upo mdogo umeonyeshwa hizo ni kazi za kike nawe umejijengea hivyo in reality hakuna kazi ya mwanamke na mwanaume,fanya ili ufanyiwe!!!!wazazi wako wangekutrain kujioshea chombo chako mwenyewe kupika etc usingeona tabu.greti thinks tujifunze hapa kuwatrain watoto wetu hasa wa kiume ili wakikuwa wawe independent na useful kwa society.
 
Kaka hapo mwisho si ataomba mchezo kwa housegirl. Kwa kutembea na housegirl huwa kunaanzaje?

Hahahahahah lol! nimeshaziona hizo tena hapa hapa jamvini kwamba HG ndiye anaamka asubuhi sana kutengeneza breakfast na kuiweka mezani kisha kumkaribisha baba mwenye nyumba tena kwa adabu zote ili apate kifungua kinywa, kama kuna shati au suruali ambayo inahitaji pasi basi HG ndiye atakayeifanya kazi hiyo. Jioni Baba mwenye nyumba akirudi basi anapokewa kwa heshima zote na HG, msosi wa jioni pia anayepika, kuutenga mezani na kumkaribisha Baba mwenye nyumba ni yule yule HG mama ama yuko mbele ya TV busy na kufuatilia "vipindi vyake" au "katoka kidogo" ukaribu wa Baba mwenye nyumba na HG unazidi kuongezeka. Baba mwenye nyumba anaanza kumuangalia HG mara mbili mbili tofauti na ilivyo siku za nyuma anaanza kuyaona yale ambayo hakuwahi kuyaona siku za nyuma hahahahah lol! anasema kimoyomoyo kumbe haka kabinti kazuri eeh! nilikuwa sijakaangalia vizuri :):):) majaribuni yanaingia kichwani kwa Baba mwenye nyumba na kufikiria yale ambayo hastahili kuyafikiria :):):)
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Husni sikiliza ile kolabo ya FA,NGWEAR na JIDE 'skiza me'
kwenye hiyo bold haija kaa vizuri mtakuja kuletewa vicheche ndani

wanaume mnapenda kujiangalia nyie tu. Na sisi mnavyotuchosha tutawaletea vismol hauz.
 
Unapenda ubosi eeh! We kupeleka maji bafuni vinakushinda? Kabla hujaoa ulikuwa unapelekewa na nani? Acheni kukera na kuchosha wake zenu. Kwanza hata unyumba ni hiari yake akupe au akunyime.
husninyo umechangia vizuri lakini mwishon umeharibu suala la unyumba ni haki kwa wanandoa mwenzio akihitaj hampaswi kunyimana
 
Tatizo la wanume wengi wa kiafrica hawajui ugumu wa kazi za nyumbani, jaribu siku moja kumpa mkeo off halafu msaidie kazi zote za siku hiyo kuazia kumpelekea maji bafuni hadi siku iishe halafu uone kama kukupelekea maji bafuni ni lazima au hiyari.
 
I think ni fadhila tu, kwani hana mikono huyo mwanaume? Kuoga aoge yeye maji apeleke mwingne! Tena anakuamsha alfajiri,mama naniliuh kaniwekee maji nataka kuoga...2mbavu! Wanaume tumewaendekezaaaa, mpaka favors wanaona ni right yao sasa! Kuna mambo yani ukifikiria sana unaweza usiolewe manake ni full utumwa....! Mungu ampe ujasiri wa kuamka na kujitengea maji ya kuoga atakaefanikiwa kunioa otherwise atakuwa anakoma! Lol!
 
ndio mijanaume ya kiafrica ilivyo inataka hadi viatu ibrashiwe....nyooooo!

Napata picha hapa kuwa hapo ulipo hujaolewa na hujafundwa kwa ajili ya maisha ya ndoa, vinginevyo yasingekutoka maneno ya dharau na kejeli dizain hiyo kwa wanaume! Na wallah nakuapia, kama huo ndio msimamo wako halisi hutakuja pata mume. Utaishia kumegwa na kusherehekea ndoa za mashoga zako tu!
 
I think ni fadhila tu, kwani hana mikono huyo mwanaume? Kuoga aoge yeye maji apeleke mwingne! Tena anakuamsha alfajiri,mama naniliuh kaniwekee maji nataka kuoga...2mbavu! Wanaume tumewaendekezaaaa, mpaka favors wanaona ni right yao sasa! Kuna mambo yani ukifikiria sana unaweza usiolewe manake ni full utumwa....! Mungu ampe ujasiri wa kuamka na kujitengea maji ya kuoga atakaefanikiwa kunioa otherwise atakuwa anakoma! Lol!

na hutaolewa kamwe otherwise ubadili msimamo wako. Mwanamke mbabe hana nafasi ktk ndoa. Ni wanyenyekevu tu ndio hupata baraka hiyo!
 
Back
Top Bottom