Maji ya kuoga...!

Duh! Yaani mnatufanya wanawake kama ni watumwa wa ndoa! Hivi kuna kitu chochote ambacho mwanamke anapaswa kuenjoy kwenye ndoa?! Kufua hadi vyupi,kupika kutumikia penzi mara sijui gogo,mara chai,mama mkwe,ndugu, watoto! Mwanamke role yake ni ipi na mwanaume yake ipi?

Asanteeee King'asti!!
Ajabu.... watu wanapenda "maendeleo" na "mabadiliko yake" lakini inapokuja kubadilisha yale yenye kuwaondolea "mteremko" ni back-peddling ya nguvu!
Kwani kama unapenda kutumikiwa kwanini nawe usitumikie? Ukimfanyia mkeo naye atakufanyia maradufu.
Kanishangaza ati mkewe hamwekei maji hadi amgombeze.....kwani huyo ni mke au mtumwa?
 
Mnapoanza kukwaruzana juu ya kuwekeana maji au kufuliana vitasa, jichunguzeni lazima kuna mahali mapenzi yamepungua kwa sababu haina ugumu wowote kama mnapendana na hamjaudhiana kwa mtu kumfanyia kitu mwenzie au hata asipofanya kuelewa na kuchukulia simple. Kama mimi MJ1 ninakuwekea maji ya kuoga bafuni, jua ninafanya hilo kwa kuwa ninakupenda na nategemea na wewe kama unanipenda kweli hutojenga hoja siku nisipofanya hivyo. Vile vile hata wewe siku ukiniwekea maji ya kuoga nitachukulia kuwa ni mapenzi na katu siktokushangaa wala kujigamba.
 
Naomba msaada wanaJF. Hivi mwanamke kumwekea maji mumewe bafuni ni wajibu au ni fadhìla tu? Nauliza hivi sababu mke wangu haniwekei maji mpaka nimgombeze au siku akipenda mwenyewe. Siku nyingi nalazimika kujibebea mwenyewe. Nimeshagombana naye mara kadhaa lakini habadiliki. Nifanyeje?

kuna wanaowekewa maji lakin amani ndani ya nyumba haipo hata kidogo!
So we kama kuna amani hilo usikwazike kaka. Ni makubaliano2
 
jamani sabri usiseme ivyo,upendo ndio nguzo ya ndoa na kupenda sio kusema i love you,ni matendo madogo.kwa msimamo huo mwezi mmoja atakukimbia.

mama mkwe mmebaki wanawake wachache sana kama nyie hawa vishankupe wa dot com ni balaa tupu
 
tatizo lao wanakopy kutoka nje
Umejibu bila kufikir..... mke yuko nyumbani mme ana mizunguko ya kupata hata hizo pesa za matumizi hom kwani yy hachoki majibu ya wanawake wengi ktk hili imenipa picha ya kwa nn ndoa zinawashinda hili ni moja ya jukumu la mwanamke wa kiafrika kwa mmewe
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom