DOKEZO Harufu mbaya ya kuudhi ndani ya stendi ya Magufuli

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,194
4,115
Leo alfajiri saa 10 usiku nilikuwa Stendi ya Magufuli kupanda basi nasafiri kuelekea Mkoa fulani. Nilisikia harufu mbaya kama chemba inayovuja eneo wanaposimama Abiria wanaosubiri basi la Happynation au jirani na yanakosimama mabasi ya Abood ili kupakia abiria.

Eneo hilo lina mtaro ambao umefunikwa kwa zege na kuacha vitundu vidovidogo, sasa kupitia vile vitundu kuna harufu kali sana inatoka ambayo ni kama shimo la choo linavujisha maji machafu na yanapita humo au mrundikano wa taka na maji yameoza sana na kuanza kutoa harufu ya uozo wa ajabu.

Baada ya kusikia hali hiyo niliwauliza baadhi ya watu wanaofanya biashara pamoja na watu wa mabasi kadhaa kwa wakati tofauti, lengo langu nilitaka kujua iwapo ni hali iliyojitokeza ghafla siku hiyo au ipo zamani.

Majibu ya watu hao yalikuwa, "hapo pana muda mrefu pananuka, ni kutokana na kupitisha taka humo bila kufanyiwa usafi wowote" aliejibu mtu mmoja wa mabasi.

Nikawauliza iwapo wametoa taarifa kwa uongozi wa stendi juu ya adha ya harufu hiyo, swali hili niliwauliza watu wa mabasi wakajibu viongozi wanajua kwa kuwa wamekuwa wakifika hapo mara nyingi tu na wanasikia hiyo harufu ila hawajali lolote.

Uongozi wa stendi ya Magufuli mjitafakari, ile hali ya harufu inatesa sana abiria wanaopanda mabasi hapo, kama ni chemba za choo zimepasuka na kutiririsha maji machafu kwenye mtaro huo, mzizibe na kama ni mrundikano wa taka basi mfanyie utaratibu wa usafi kwenye mtaro huo msije sababibisha mlipuko wa magonjwa.

Nitarudi tena kuona kama pamerekebishwa.

1688298419277.png

1688298450890.png

1688298479838.png

1688298619713.png
 
Hii imerudiwa tena Mara ya Pili wahusika wanakusanya Pesa tu hawafanyii kazi yoyote kazi kuongeza ukubwa wa matumbo yao tu

404: Page Not Found
 
Leo alfajiri saa 10 usiku nilikuwa Stendi ya Magufuli kupanda basi nasafiri kuelekea Mkoa fulani. Nilisikia harufu mbaya kama chemba inayovuja eneo wanaposimama Abiria wanaosubiri basi la Happynation au jirani na yanakosimama mabasi ya Abood ili kupakia abiria.
HILI NI TATIZO LETU WATANZANIA KARIBU WOTE NI WAZEMBE NA SIO WAWAJIBIKAJI...KILA SEHEMU NI UZEMBE NA UPIGAJI...

NINI SISI CHA MAANA TUNAWEZA KUKISIMAMIA KIKASIMAMA SAWASAWA.?
 
Mkuu wa mkoa yupo, yeye anachojua ni kukataza mabasi kwenda Shekilango tuu, huduma bora ndani ya stendi haimuhusu!
 
Leo alfajiri saa 10 usiku nilikuwa Stendi ya Magufuli kupanda basi nasafiri kuelekea Mkoa fulani. Nilisikia harufu mbaya kama chemba inayovuja eneo wanaposimama Abiria wanaosubiri basi la Happynation au jirani na yanakosimama mabasi ya Abood ili kupakia abiria.
Dar 70% inanuka 🤣🤣 HIMARS
 
Back
Top Bottom