CBS NEWS
Wakati Mbunge Edward Cruz akishutumiwa vikali kwa kujijali mwenyewe na familia yake kwa kuwakimbia wananchi wenye majanga kwenda safari ya mapumziko kisiwani Cancun Mexico maelfu ya wakazi mkoani Texas Marekani wamejikuta hawana maji kufuatia mabadilko makubwa ya tabia nchi.
Baadhi ya wananchi wamelazimika kuokota barafu na kuchemsha ili kupata maji kwa ajili ya matumizi ya msingi.
Kukatika kwa maji mkoani Texas kunakuja siku chache baada ya kutamalaki kwa mgao wa umeme uliotangazwa na Shirika la Ugavi wa Umeme mkoani humo kufuatia kuelemewa kwa mahitaji ya nishati hiyo katika gridi ya mkoa.
Katika majiji makubwa likiwemo la Houston mkoani humo raia weonekana wakipanga foleni kwa ajili kugawiwa maji ya chupa kwa hisani ya taasisi za misaada.
Mbunge Cruz ambae alirejea nchini Marekani siku mbili baada ya mapumziko yake nchini Mexico alilazimika kuomba msaada wa ulinzi kutoka jeshi la polisi la uwanja wa ndege baada ya wananchi wenye hasira kali kutishia kumshushia kichapo.