Maji nayo yakatika mkoani Texas, Marekani, wananchi Wachota barafu kwa matumizi

Kwameh

JF-Expert Member
Dec 3, 2011
1,483
2,000
merlin_183904809_31960c07-4ee3-4c8c-a938-22c48fb689b1-articleLarge.jpg

1613817010921.jpeg

CBS NEWS

Wakati Mbunge Edward Cruz akishutumiwa vikali kwa kujijali mwenyewe na familia yake kwa kuwakimbia wananchi wenye majanga kwenda safari ya mapumziko kisiwani Cancun Mexico maelfu ya wakazi mkoani Texas Marekani wamejikuta hawana maji kufuatia mabadilko makubwa ya tabia nchi.

Baadhi ya wananchi wamelazimika kuokota barafu na kuchemsha ili kupata maji kwa ajili ya matumizi ya msingi.

Kukatika kwa maji mkoani Texas kunakuja siku chache baada ya kutamalaki kwa mgao wa umeme uliotangazwa na Shirika la Ugavi wa Umeme mkoani humo kufuatia kuelemewa kwa mahitaji ya nishati hiyo katika gridi ya mkoa.

Katika majiji makubwa likiwemo la Houston mkoani humo raia weonekana wakipanga foleni kwa ajili kugawiwa maji ya chupa kwa hisani ya taasisi za misaada.

1613817689907.jpeg


Mbunge Cruz ambae alirejea nchini Marekani siku mbili baada ya mapumziko yake nchini Mexico alilazimika kuomba msaada wa ulinzi kutoka jeshi la polisi la uwanja wa ndege baada ya wananchi wenye hasira kali kutishia kumshushia kichapo.

1613818142227.jpeg
 

LPG Man

Member
Feb 12, 2021
37
125
Texas siyo mkoa ni Nchi Kama ilivyo Tanganyika sawa dogo acha kuharibu kwa kuifananisha Texas na mkoa
 

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
11,055
2,000
Cruz sio mbunge ni Seneta na Texas haina mgao wa umeme, habari zako kuhusu Marekani ni za kupotosha sana.
 

LPG Man

Member
Feb 12, 2021
37
125
Texas siyo mkoa ni Nchi Kama ilivyo Tanganyika sawa dogo acha kuharibu kwa kuifananisha Texas na mkoa
 

Freiston

Senior Member
Oct 25, 2020
131
250
Unaelewa maana ya "major disaster"?
Labda kwa ufupi soma hapa chini sehemu ya taarifa hiyo...

".....What is happening in Texas?​

The Southwestern state's energy grid has been overwhelmed by a surge in demand for heat as temperatures plummeted to 30-year lows, hitting 0F (-18C) earlier this week.

As of Friday, about 180,000 homes and businesses in Texas still had no electricity. Amid freezing temperatures earlier this week, as many as 3.3 million were without power.

Around 13 million people - close to half of the state's population - have faced some disruption of water services as hundreds of water systems have been damaged by the freeze.

Austin, the state's capital, lost 325 million gallons (1.2 billion litres) of water when pipes burst, the city's water director told reporters on Thursday..."
 

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
11,055
2,000
Muambie sasa huyo mwanapropaganda mwenzako aliyeanzisha huu uzi aweke hiki kipande kwa kiswahili, maana kukosekana hiki kwenye hii taarifa yake kunaifanya kuwa upupu mtupu.
Labda kwa ufupi soma hapa chini sehemu ya taarifa hiyo...

".....What is happening in Texas?​

The Southwestern state's energy grid has been overwhelmed by a surge in demand for heat as temperatures plummeted to 30-year lows, hitting 0F (-18C) earlier this week...
 

Freiston

Senior Member
Oct 25, 2020
131
250
Hakuna haja maana tumetumia vyanzo viwili tofauti vya taarifa mimi BBC wakati mleta mada katimia CBS News na kila shirika limeandika kile ilichoona katika eneo husika. Usipinge bila kufanya tafiti kidogo kwanza.
Muambie sasa huyo mwanapropaganda mwenzako aliyeanzisha huu uzi aweke hiki kipande kwa kiswahili, maana kukosekana hiki kwenye hii taarifa yake kunaifanya kuwa upupu mtupu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom