Swali zuri sana, ila serikali yetu haijawa wazi na wananchi unless ni operation ya siri. Wataalamu wa kijeshi mko wapi?
Majeshi yameanza kwenda last year kulinda amani wakati mjadala kati ya serikali na waasi unaendelea. Kwanza walienda 100. Baadaye wakawa wanaongezwa. Hizi habari zimetangazwa sana na haikuwa siri. Hadi wiki mbili zilizopita,mjadala umekuwa na umri wa miezi 8 na hakuna maendeleo, na Rais wa Comoro akaomba AU ivamie kisiwa kile na kumkamata jamaa, au la basi jeshi lake ingawa dogo lakini itabidi livamie.
Tanzania na South Afrika zimekuwa zikishughu;ikia suala la Comoro kwa muda mrefu sasa. Lakini nchi za Libya, Senegal Sudan na Tanzania ndo zimekubali wito wa AU kupeleka vikosi kwa ajili ya kumvamia Bacar. Jumla wanaweza kuwa 1900, na Tz imetoa kwenye 700 hivi, na kuifanya ndo kiongozi wa operesheni.
Hivyo basi, mejeshi yetu yamekwenda kule chini ya mandate ya AU, licha ya ukweli kuwa Rais wetu pia ni mwenyekiti wa AU. Vile vile, tuna uhusiano wa damu na Comoro, kwani watu wetu wengi hapa wametokea kule na vice versa, kitu kinachotufanya tuhitaji kuwasaidia.
Kama kweli kuna watu wamekufa, basi hizo ni hatari zinazohusishwa na mapigano. Kuna mwanajeshi ambaye hajui kuwa anaweza kufa vitani? wao wanaelewa vuziri zaidi dhana ya kufa wakati wowote. Kama tunafikiri hili ni jambo baya (kumsaidia jirani) basi ubaya wake tusiuone sasa, ilibidi tuuone wakati vikosi vinapelekwa. Vikosi vya kwanza vilikwenda kule miezi nane iliyopita.