Majeshi yetu Comoro: Who is responsible?

Status
Not open for further replies.

Game Theory

JF-Expert Member
Sep 5, 2006
8,546
845
Tanzania, Sudan na Libya wako bize kuandaa majeshi yaende Comoro , Lakini mbona hiii mipango kabambe inayofanyika inamaana kuwa ilipitishishwa na nani?na mbona suala hili la kupeleka wanajeshi wetu kule halijazungumzwa/ Halizungumziwi?


Na mbona hakuna taarifa zozote kuhusu risk analysis juuu ya maeneo ambayo wanajeshi wetu watakuwa iliyofanyika? Je role yetu sisi ni ipi?Kwa nini FOREIGN wametuweka gizani kuhusu hili?

MOD nao mbona kimya?
 
Majeshi yetu yamekuwa yakipelekwa nchi mbali mbalibila sisi kuambiwa.Yaliwahi huko nyuma kupelekwa Sychelles na hata juzi juzi Lebanon.Sasa yanapelekwa Comoro kwa mtindo huo huo.
 
mengine yako nchini congo wanafanya kazi ya kulinda amani , wengine waliwahi kupelekwa siera lione bila taarifa rasmi kutolewa na hata ukiulizwa si unajua mambo ya wanajeshi ?
 
nakhofia wasije pelekwa aghanistan tu maana nato wanataka wapelekwe majeshi wengine tz wakipewa mshiko tu watapelekwa na serekali itakaa kimya hadi pale talaban wawakamate na kuonyesha kwenye tv ndio watasema maana talabani wakiwakamata ndio vichwa vitakua halali yao hilo ndio ninalo khofia mimi
 
Nadhani kuna wakati sisi watanzania tunasukumwa tu. Ninajua kuwa miaka ile ya sabini, Nyerere alikuwa akipeleka majeshi kusini mwa Afrika kwa hiari yake. Lakini hii ya kuepeleka majeshi sehemu za mbali zeenye migogoro siku hizi nadhani kwetu haifanyiki kwa hiari. Mwanzoni mwa utawala wake, rais Kikwete aliwahi kusikika akisema kuwa serikali yake haingepeleka majeshi Somalia kwa vile haina uwezo wa kuyagharamia; je sasa hivi uwezo huo unatoka wapi kama siyo kuwa tumepewa shinikizo fulani.
 
Hivi hali ya wanajeshi wetu Lebanon ikoje?
Maana wahusika wako kimya kama hakuna kinachoendelea vile!
 
Hivi tukiamka siku moja na kukuta JK kapeleka majeshi Iraq tutasemaje?

Katiba yetu inaelekea inampa madaraka raisi kufanya atakalo maana kama tulivyoshuhudia majeshi yetu yamepelekwa Comoro bila ya Bunge wala baraza la mawaziri kupitisha uamuzi huo. Angalau baraza la mawaziri waliarifiwa baada ya majeshi kuondoka, na wala sio kuwa walijadili au kupiga kura kupitisha uamuzi huo. Lakini bunge inaelekea halikuwa na maana yeyote kuarifiwa au halikuwa na madaraka yoyote kwenye maamuzi kama haya. Ndio maana JK wala hakujali kuwafahamisha bali alitaka wasikie hizo habari kama wananchi wengine wa kawaida, nafikiri kuna walakini hapa.

Kwa hiyo, kwa uwezo huu mkubwa alio nao raisi, sio ajabu TZ tungekuwa Iraq kama urafiki wa JK na Bush wa hivi sasa ungekuwa vivo hivyo kwa Mkapa mwaka 2001, japokuwa asilimia kubwa ya waTZ wasingekubaliana na uamuzi huo. Hii ni hatari kubwa kwa nchi hasa huko tunakoelekea, ambapo tunaweza pata raisi kichaa kwa vile tu ana pesa nyingi ya kuhonga au ameangukia katika kundi jema. Mfano mzuri ni Lowassa, mtu asiyeambilika na mwenye maamuzi ya kisifa-sifa angeweza kuwa raisi wa TZ ki urahisi kabisa, na pengine bado anaweza kuwa, kwa vile tu wana mtandao wamejipanga vizuri serikalini na chamani kwa hivi sasa.




JWTZ kuongoza ukombozi Comoro

2008-03-15 09:02:14
Na Sammy Polly


Umoja wa Afrika (AU) umeiteua Tanzania kuwa kamanda wa jeshi la AU litakalohusika na operesheni maalumu kukikomboa kisiwa cha Anjouan ambacho kwa sasa kinakaliwa kimabavu na kiongozi aliyejitangazia madaraka mwenyewe,
Kanali Mohamed Bacar.

Akizungumza katika mkutano na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam jana, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe, alisema tayari sehemu ya askari wa Tanzania watakaojiunga na kikosi hicho waliondoka nchini Jumanne wiki hii kwa ajili ya operesheni ambayo inaweza kuanza wakati wowote kuanzia sasa.

Alisema kwamba wizara yake ilishindwa kutoa taarifa rasmi kwa umma kuhusiana na kushiriki kwa Tanzania katika jukumu hilo kwa kuwa kiutaratibu ilihitaji kwanza Rais Jakaya Kikwete aliarifu Baraza la Mawaziri na uongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kabla ya kuvitaarifu vyombo vya habari.

Waziri Membe alisema kwamba jeshi hilo limepangwa kuwa na jumla ya askari 1,800, ambapo Tanzania inatarajia kupeleka askari 750, Senegal na Sudan (750) na Comoro yenyewe 300.

Alisema tayari Tanzania ina askari 200 waliopo Comoro kwa ajili ya kulinda amani.

Alisema kwamba jeshi hilo limepewa majukumu makuu matatu ambayo ni kumtia mbaroni Kanali Bacar ili ashtakiwe, kuhakikisha kuwa wanamgambo wanaomuunga mkono Bacar wanaporwa silaha na kulinda amani kisiwani Anjouan hadi kutakapofanyika uchaguzi halali utakaoitishwa na AU.

``Majeshi yetu hayatarudi nyuma hata kidogo kwa kuwa tumedhamiria na operesheni hii imeandaliwa kisayansi ili pasitokee madhara kwa wananchi,`` alisema.

Alieleza kwamba askari hao wamepangwa kuwepo Anjouan hadi Mwezi Mei mwaka huu ambapo hali inatarajiwa kurejea katika hali ya utulivu.

``Siku 9 zilizopita Bacar aliombwa ili ajisalimishe mwenyewe lakini aligoma tena kwa kiburi kikubwa, na ndiyo maana sasa tumeamua kutumia nguvu za kijeshi,`` alieleza Waziri Membe.

Alisema kabla ya kufikia maamuzi ya kutumia nguvu za kijeshi, AU ilitumia vikao 12 kama njia ya kidiplomasia na baadaye kukiwekea vikwazo kisiwa hicho lakini njia zote hazikufanikiwa.

Alieleza kwamba serikali inaandaa utaratibu ambao utawawezesha waandishi wa habari kutoka Tanzania kuungana na jeshi hilo la AU huko Anjoun ili kuwapasha wananchi matukio yote.

Katika mkutano huo huo, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Hussein Mwinyi, alisema serikali imehakikisha usalama na maslahi ya askari wote ambao wamepelekwa kwa operesheni ya Comoro.

Alikuwa akijibu swali la Mhariri wa gazeti la MwanaHalisi, Saed Kubenea aliyetaka kujua jinsi serikali itakavyowalinda askari watakaojeruhiwa au kufa huko Comoro.

``Tunawahakikishia wananchi kwamba serikali itaendelea kuziangalia familia za askari wote tuliowapeleka Comoro huku tukiwahakikishia usalama wao,`` alisema Waziri Mwinyi.

Kanali Bacar ambaye aliingia madarakani katika maasi mwaka 2001 alijitangazia ushindi wa kuwa Rais wa Anjouan mwezi Juni mwaka jana katika uchaguzi ambao haukuwa halali.

Tangu ajitangazie madaraka hayo, Kanali Bacar amefunga Uwanja wa Ndege, bandari pekee ya Comoro, Anjouan na kumzuia Rais wa Shirikisho la Comoro, Mohamed Abdallah Sambi asiingie kisiwani humo. Sambi ni mzaliwa wa Anjouan na familia yake iko huko.

Shirikisho la Comoro linaundwa na visiwa vya Muheri, Anjouan na Ngazija na mbali na rais wa shirikisho, kila kisiwa kina rais wake.

Kuna kisiwa kingine cha Mayotte ambacho hakijajiunga na shirikisho na hivyo kinatawaliwa na Ufaransa.

SOURCE: Nipashe
 
Bahati mbaya Rais hajui anwani yako ilikuwa akuite Ikulu akuombe ushauri kuhusu kupeleka majeshi ya Tanzania Comoro!!Nafikiri next akipata address yako atakuita umpe ushauri
 
sioni tatizo, wacha waende wachangamke kidogo na siyo kukaa tu na kuharibu magari, kucheza golf na kupiga raia. good excercise for them
 
Bahati mbaya Rais hajui anwani yako ilikuwa akuite Ikulu akuombe ushauri kuhusu kupeleka majeshi ya Tanzania Comoro!!Nafikiri next akipata address yako atakuita umpe ushauri

Ajiunge na JF, after all watu wake si wapo hapa.

La Muhimu hapa, ni kuwa na taratibu zinazoeleweka za kufikia maamuzi fulani yanayohusu nchi, na sio nchi iendeshwe na mtu mmoja na marafiki zake kama vile ni nyumba yake ndogo.
 
Kubwajinga,

Bwana unadhani majeshi yanapelekwa!!! system nzima ya jeshi, wizara ya ulinzi, wizara ya mambo ya nje inajadili kwanza... Rais hakurupuki tu!
 
Kubwajinga,

Bwana unadhani majeshi yanapelekwa!!! system nzima ya jeshi, wizara ya ulinzi, wizara ya mambo ya nje inajadili kwanza... Rais hakurupuki tu!

Kasheshe,
Nafikiri hao uliowataja hawatoshi kuiingiza nchi nzima ya watu millioni 40 vitani. Haya ni maamuzi makubwa sana kufanywa na mtu mmoja hata kama atashauriwa hao uliowataja. After all sidhani kama Membe na Mwinyi wana ujuzi wowote wa mambo ya kijeshi maana hata wao vyeo vyao ni sehemu ya shukhrani za uchaguzi kama FMES alivyotufahamisha. Mwinyi ni MD, Membe ingawa amesoma Intern. Reltn, hajawa na uzoefu wowote wa kuwa full minister let alone kutuingiza vitani.
 
Bahati mbaya Rais hajui anwani yako ilikuwa akuite Ikulu akuombe ushauri kuhusu kupeleka majeshi ya Tanzania Comoro!!Nafikiri next akipata address yako atakuita umpe ushauri

Dude!

Kama huelewi kilicho andikwa si uulize? Au unadhani kuuliza ni ujinga?
 
Anaonyesha Ubabe wake naye.

Juzi tu hapa si katembelewa na Mnene Bush, kuonyesha dunia kwamba siku 4 za ujio wa Bush zimempa nguvu ya uninja naye anajaribu kwenda kuikalia nchi.
Sijui kwa nini hakuyapeleka Kenya kuzuia kuchinjana?
Au ndo umamluki wenyewe?
 
Mkuu naona finally, uananza kuelewa kuwa kama tuna tatizo ni katiba yetu na sio rais,

Halafu kama ninavyosema mnachanganya sana bongo na majuu, ukweli ni kwamba hata rais wa US anaweza kupeleka majeshi bila ruhusa ya Congress, tatizo litakuja kuwa kwenye kuomba pesa za kuendesha operation,

viongozi tulionao, kina Mwinyi, na Membe, wanataimiza sharti muhimu sana la uongozi walionao, nalo ni kuwa wabunge waliochaguliwa na wananchi, the rest ni kelele za mlango.
 
Mkuu naona finally, uananza kuelewa kuwa kama tuna tatizo ni katiba yetu na sio rais,

FMES,
Hapa nakubaliana na wewe kuwa katiba yetu haifai. Inabidi tuunde tume huru ya kurekebisha hii katiba. Ila kama raisi wetu ameamua kuifuata hii mbovu mbovu, ina maana na yeye ni mbumbumbu pia.


Halafu kama ninavyosema mnachanganya sana bongo na majuu, ukweli ni kwamba hata rais wa US anaweza kupeleka majeshi bila ruhusa ya Congress, tatizo litakuja kuwa kwenye kuomba pesa za kuendesha operation,

No! Hii sio kweli. Kuendesha vita right, kuanzisha vita no!. Congress peke yake.

viongozi tulionao, kina Mwinyi, na Membe, wanataimiza sharti muhimu sana la uongozi walionao, nalo ni kuwa wabunge waliochaguliwa na wananchi, the rest ni kelele za mlango.

Mwinyi hana sifa zozote za kuwa waziri wa ulinzi. Hiki ni kichekesho kinachowezekana TZ peke yake. Membe ninaweza kumpa benefit of the doubt, lakini kwa jinsi tulivyo na watu wazuri kuliko yeye inashangaza kwa nini JK akamchukua yeye. Labda kama ulivyosema, analipa waliomsaidia na si ubora wao.


Tukumbuke tu kuwa, tuna katiba mbovu na raisi bomu.
 
FMES,
Hapa nakubaliana na wewe kuwa katiba yetu haifai. Inabidi tuunde tume huru ya kurekebisha hii katiba. Ila kama raisi wetu ameamua kuifuata hii mbovu mbovu, ina maana na yeye ni mbumbumbu pia.




No! Hii sio kweli. Kuendesha vita right, kuanzisha vita no!. Congress peke yake.



Mwinyi hana sifa zozote za kuwa waziri wa ulinzi. Hiki ni kichekesho kinachowezekana TZ peke yake. Membe ninaweza kumpa benefit of the doubt, lakini kwa jinsi tulivyo na watu wazuri kuliko yeye inashangaza kwa nini JK akamchukua yeye. Labda kama ulivyosema, analipa waliomsaidia na si ubora wao.


Tukumbuke tu kuwa, tuna katiba mbovu na raisi bomu.

Kubwajinga,
Nimefurahi kuwa umeingia hapa kuchangia hii thread.

Nadhani umekuwa na mawazo ambayo hayajazama sana katika kufanya uchanbuzi na kuleta hoja zako (sina maana ninadharau hoja zako, ninaziheshimu sana tu) isipokuwa unasahau kuwa kila jambo ambalo linafanyika sasa kama limo ndani ya uwezo wa Rais kikatiba ni halali kabisa kwani huo ndiyo utaratibu na gharama za demokrasia.

Pili, usisahau kuwa rais kikatiba ndiye mtu wa mwisho kimamlaka juu ya vyombo vya ulinzi na usalama, na hii ni muhimu kwa Rais kupewa uwezo huo, lakini hata hivyo tunapomtaja Rais huwa tuna maanisha Rais kama taasisi na wala hatumwangalii JK usoni. Juu ya kwamba katiba ibadilishwe ili kuepuka kufanywa maamuzi na Rais kichaa, nadhani hiyo haijakaa vizuri labda ufafanue Rais kichaa kwa maana ya ugonjwa? kama ni ugonjwa katiba iko wazi inaelekeza kuwa kama rais incapacitated ni hatua gani za kuchukuliwa.

Tatu, kuhusu teuzi za mawaziri kushika nyadhifa kwenye wizara, hapo hakuna tatizo kama unavyofikiria wewe, Uwaziri siyo kazi au fani inayosomewa. Kazi kubwa za mawaziri ni kusimamia na kumsaidia Rais katika kuendesha serikali na hii ni political position kama alivyo Rais. Kinachotakiwa ni uwezo wa Waziri anayeteuliwa kuwa na uwezo wa kuongoza na kusimamia yale serikali iliyoko madarakani inataka kuyatimiza.

Kawaida shughuli za kiutendaji zingine za wizara husimamiwa na viongozi wakuu wa wizara husika (ambao ni wasaidizi wa waziri), baada ya hapo huwa ndiyo kuna timu za wataalam kulingana na mpangilio wa wizara husika.

Nadhani nimejitahidi kukuelezea ili tufaidike wengi kutokana na hoja zako.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom