Majenerali Wamgeuka Yahya Jammeh, sasa kwenda uhamishoni

Good. Ninalipongeza jeshi kwa uamuzi imara.wasijubali damu zao zomwagike kwa ajili ya mtu mwenye maslahi binafsi.
 
Jammeh amejisahau sana...hataki kujifunza nini kinaweza kutokea kama wafadhili wake na waliokuwa wanambeba wakimchoka....He will go down ashamed.
 
Huyo Jemmeh hayupo vizuri upstairs
Viongozi wengi wa Afrika hawako sawa upstairs. Huwezi kuiba mabilioni ya watu masikini ukajitajirisha kupita kiasi huku watu wako masikini kabisa kabisa wakifa kwa njaa, huduma mbovu na kukosa hata aspirin mahospitalini halafu ubakie salama upstairs. Madhambi haya yana gharama sana ndiyo maana wengi wa mafisadi hawa hata mwisho wao huwa siyo mzuri. Inavyoonekana hata huyu naye mwisho wake hautakuwa mzuri na yatakuwa yale yale ya kufia uhamishoni kama akina Mobutu Seseseko Kuku Ngbendu Wa ZaBanga.
 
Kweli kabisa, wange kuwa na akili ya kiarabu na ya mtu mweusi, wangeburuzwa na kutii amri za kijinga kama walivofanya MAJENERALI wa LIBYA na Avery cost, mwishoe nchi zao zikatumbukia kwenye matatizo
 
Na huku kwetu wangefanya hivyo kule katikati ya maji jeshi letu lingeheshimika,ila yule aliyekunywa sumu atakuwa kasikia izo salamu,kuwa angejua nae afanye hivyo ili heshima iwepo,hongera jeshi la Gambia mmetenda haki,majeshi ya Afrika yajifunze raia anasababishaje watu wafe kisa anaitwa Raisi, kwani uyo atakaekuja nae c atawalipa mshahara ilimladi msimamie haki,tukomeshe tabia za kina Jechachachaaaaa,mungu ibariki Gambia mungu ibariki Afrika
 
Kuna watu wanafikiri nchi ni miliki zao na familia zao.
Hao majenerali wameonyesha uzalendo wa kweli kwa nchi yao.
Kwa fikra hiyo hiyo kuna mmoja aliwahi kujenga ofisi za bunge nyumbani kwao!!!!

Mwingine kaanza na uwanja wa ndege haoni hata aibu!! Nyerere zaidi ya miaka 25 madarakani lakini kwao hapakupendelewa kwa namna yoyote.
 
Mkuu uko sawa mm mwenyewe ni muumin wa udikteta naamin kwa nchi ambazi bado hazijaendelea udicteta unahitajika ili maendeleo yakifikia level fulan nzur ndio tuwaachie wapayukaji wa kisiasa waanze mambo yao maana huwa nakereka nchi INA matatizo lukuki halafu kila mtu anataka asikilizwe badala ya kutatua changamoto huku wengine wakitaka maandamano ni upuuzi tu. Angalia mifano kutoka China hakuna pure democracy anayoihubiri mmarekan still jamaa wako juu kiuchumi kuishinda ulaya na democrasia yao
Miaka 55 ya uhuru bado unajipanga kuleta maendeleo? Kweli tumerogwa vibaya mkuu.
 
Hawa Majenerali wana akili sana.

Nchi haiwezi kuingia machafukoni na kutesa raia wasio na hatia kisa kuna mtu kanogewa na kiti cha ofisi kubwa.
 
Jenerali MUSA SAVAGE na Jenerali Badjie wamemgomea Rais wa Gambia Bwana Yahya Jammeh, wakisema tarahe 19 January 2017 wataanza kumtii Rais mteule ADAMA Barrow, linataarifu Gazeti la FREEDOM la Nchini humo.

Taarifa zinasema, Jana Alhamis Ikulu ya Gambia kulikuwa na Kikao cha " SECURITY BRIEFING" ambapo Rais Yahya Jammeh ametaarifiwa kuwa wakuu wa Battalions zote wamekubaliana kutoruhusu Jeshi kupigana ikiwa itatokea uvamizi wa Nchi za ECOWAS ili kumuondoa madarakani.

Jenerali MUSA SAVAGE tayari amewaarifu wenzake kuwa hataruhusu Battalion yake ipigane na kwamba ni lazima maamuzi ya wananchi wa GAMBIA yaheshimiwe.

Hali ilibadilika jana ndani ya ikulu punde baada ya Yahya Jammeh kuarifiwa hivyo ambapo alibadilika na kuondoka ndani ya kikao asiamini kile alichoelezwa na mtu wake wa karibu Jenerali Badjie.

Taarifa mpya zinasema, Tayari mazungumzo yameanza ili Rais Yahya Jammeh aende uhamishoni katika moja ya nchi za AMERICA KUSINI ambapo nchi hizo hazina utaratibu wa kutekeleza amri za ICC za kumsalimisha mtu kwenye mahakama hiyo.
Huu sasa ndiyo uzalendo kama haya ni kweli Africa tunajikomboa.
 
Mkuu Libya, Iraq, Saudi Arabia, UAE, China nk. Pia mataifa ya ulaya yalipiga hatua kipindi cha kina Hitler. Nimesema mambo yakikaa sawa kwenye nchi ndio democracy irudishwe kwa mfan kwa level ambayo Libya ilifikia kiuchumi na Huduma za kijamii Gadaffi alipaswa kurejesha utawala wa kidemokrasia kwa kuwa alishainyoosha nchi
Libya Saudi arabia iraq na uae ni nchi zilizo piga hatua kwasababu ya hela za mafuta sio kwasababu ya udikteta. Libya hata bila gadafii bado wangekua na uchumi mkubwa tu kwasababu mafuta sio ya gadafii ni ya libya na wananchi walijua hilo ndio mana waliona hakuna haja ya kumfanya gadafii kama mungu.
 
Libya Saudi arabia iraq na uae ni nchi zilizo piga hatua kwasababu ya hela za mafuta sio kwasababu ya udikteta. Libya hata bila gadafii bado wangekua na uchumi mkubwa tu kwasababu mafuta sio ya gadafii ni ya libya na wananchi walijua hilo ndio mana waliona hakuna haja ya kumfanya gadafii kama mungu.
Lakini licha ya utajiri wa mafuta wa mataifa hayo bado viongoz hao wangeweza kumissuse mapato ya mafuta kwa kuwa wana madaraka yote ila wamesaidia mataifa yao kupiga hatua tofauti na mataifa mengine ambayo yana rasilimali nyingi ila kwa sababu ya rushwa na ubinafsi yameingia mikataba mibovu na wawekezaji na kusababishia nchi zao umaskin kutokana na kukosa mapato stahiki
 
Back
Top Bottom