Tetesi: Rais wa zamani wa Gambia, Yahya Jammeh apigwa marufuku kuingia Marekani

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Apr 29, 2016
20,744
25,445
lead_720_405-1.jpg
SERIKALI ya Marekani imempiga marufuku Rais wa zamani wa Gambia, Yahya Jammeh kuingia nchini humo kutokana na historia mbaya ya utawala wake iliyohusisha vitendo vya rushwa na uvunjifu wa haki za binadamu.



Uamuzi huo umetolewa Disemba 10 ikiwa ni miaka miwili tangu Jammeh alipolazimishwa kukimbilia uhamishoni nchini Equatorial Guinea. Aliondolewa kwa nguvu madarakani na Jeshi la Umoja wa Afrika baada ya kukataa kuachia madaraka kufuatia kushindwa kwenye uchaguzi mkuu na Adama Barrow.



Marekani imeeleza kuwa Jammeh amezuiwa kuingia nchini humo pamoja na familia yake yote, na kwamba uamuzi huo unatokana na sheria za nchi hiyo kwa maafisa wa Serikali za nchi nyingine ambao wanaaminika kujihusisha na vitendo vya ufisadi na uvunjifu wa haki za binadamu.

Yahya-Jammeh.jpg


Kwa mujibu wa Serikai ya Gambia inayoongozwa na Barrow, Jammeh aliiba zaidi ya $50 milioni za umma alipokuwa madarakani.



Kwa mujibu wa ripoti, Jammeh anamiliki majumba katika eneo la Potomac, Maryland nchini Marekani, Kilometa 24 tu kutoka Washington. Alinunua majumba hayo mwaka 2010 kwa $3.5 milioni kutoka kwa mwanamichezo wa Marekani, Calbert Cheaney.

2-20.jpg
 
Kwahiyo hayo majumba yake huko US yatamilikiwa na nani? yauzwe ili pesa irudi kwa wananchi.
 
Imekula kwake, huyu jamaa alikuwa bogus sana alipokuwa madarakani. Ni wale wale wanaotaka wasujudiwe na kulambwa matako wawapo ikulu.

Kuna watu walipotea kipindi akihudumu hadi leo hawajulikani walipo. Hakuna lolote la maana alichofanya akiwa rais kando ya kuwaua wapinzani wake na wengine kuwasondeka gerezani akifikiri angetawala milele.

Ngoja wazungu wamlalie tu hizo mali alizopora. He is very hopeless indeed. Ni muda kwa madikteta wengine kula darasa hapo kwani mwenzako akinyolewa, wewe tia ...............
Nakumbuka enzi hizo mke wake akiingia Supermarket jijini Banjul kufanya shopping, watu wote waliamurishwa kutoka kwanza nje.
 
Back
Top Bottom