Majenerali Wamgeuka Yahya Jammeh, sasa kwenda uhamishoni

Ni vzr kuona makamanda wa ngazi za juu wakisimamia UKWELI na kuheshimu maamuzi ya wananchi ,huo ndio uzalendo wa kweli na sio unafiki
Kwa mara ya kwanza kutokea Africa,natamani huo utaratibu ungesambaa sehemu zote
 
Mnaoshangilia miaka miwili ijayo mtaanza kusema walimuonea kama gaddafi, oooh alikua anajua kitakachotokea na lawama kibao.......
Waafrika tuna laaana, demokrasia haijawahi kua mfumo wa kiafrika lakini mtu anashabikia kama ipo kwenye DNA yake, kihistoria hakuna nchi ilioendelea bila dictatorship, either internal or external dictatorship
 
Kazi kweli kweli, kwa hio alimua kubaki madarakani bila kujipanga?
Yawezekana alikua amejipanga, lakini ma-generali wakaamua kufikia mamuzi hayo kutokana na pengine Hali halisi ya kisiasa ndani ya Gambia. Pamoja na hayo, ma-generali hao wametazama hatma ya nchi na wananchi ikiwa wataendelea kumuunga mkono rais alie katalia madarakani.
 
Mungu mwema. Ukisoma kitabu cha Samweli utaona ni namna gani principle ya "King's destiny is in the hands of the host of his captain"! Hawa wafalme huwa hawafurukuti kwa majemerari wao wa jeshi (magenerali). Ndio maana wafalme wengi wasiojiamini na ufalme wao huwa wanajikomba sana kwa majenerali. Chezea generals wewe?
 
Hii ndiyo nidhamu ya Jeshi la wananchi kwa wananchi wake siyo kwa watawala wake.
 
Mnaoshangilia miaka miwili ijayo mtaanza kusema walimuonea kama gaddafi, oooh alikua anajua kitakachotokea na lawama kibao.......
Waafrika tuna laaana, demokrasia haijawahi kua mfumo wa kiafrika lakini mtu anashabikia kama ipo kwenye DNA yake, kihistoria hakuna nchi ilioendelea bila dictatorship, either internal or external dictatorship
Mkuu uko sawa mm mwenyewe ni muumin wa udikteta naamin kwa nchi ambazi bado hazijaendelea udicteta unahitajika ili maendeleo yakifikia level fulan nzur ndio tuwaachie wapayukaji wa kisiasa waanze mambo yao maana huwa nakereka nchi INA matatizo lukuki halafu kila mtu anataka asikilizwe badala ya kutatua changamoto huku wengine wakitaka maandamano ni upuuzi tu. Angalia mifano kutoka China hakuna pure democracy anayoihubiri mmarekan still jamaa wako juu kiuchumi kuishinda ulaya na democrasia yao
 
ECOWAS ina sapoti matokeo ya uchaguzi na kuwalazimisha member wake waheshimu - je EAC wanaweza kufanya hivyo ? Kuruzinza ana haki ya kupata hofu ?
 
Wangenishangaza kujiita wanajeshi walinzi wa katiba.
Kama wasingefanya haya.
 
Lakini lazima ujue ECOWAS wakiongozwa na Senegal wanafua misuli kwa ajili ya kumtia adabu, kwa jiografia ya Gambia mpiganaji yeyote mwenye akili lazima ajue kitakachofuata baada ya vita kuanza kwani uwezi jua Senegal wataanzia pembe ipi. Hivyo uki geu geu nautegemea sana
Nadhani shukrani za kwanza ziwaendee ECOWAS...
Jeshi limeona mziki unaofuata ni mzito...auchezeki
 
Mnaoshangilia miaka miwili ijayo mtaanza kusema walimuonea kama gaddafi, oooh alikua anajua kitakachotokea na lawama kibao.......
Waafrika tuna laaana, demokrasia haijawahi kua mfumo wa kiafrika lakini mtu anashabikia kama ipo kwenye DNA yake, kihistoria hakuna nchi ilioendelea bila dictatorship, either internal or external dictatorship
Kwa hiyo Gambia ni moja ya nchi zilizoendelea Africa?! Ni sawa na Libya?
 
ECOWAS ina sapoti matokeo ya uchaguzi na kuwalazimisha member wake waheshimu - je EAC wanaweza kufanya hivyo ? Kuruzinza ana haki ya kupata hofu ?
ECOWAS wanaweza kuwa mfano wa kuigwa siku za baadae...
Ghana mfano ni nchi ambayo madaraka yanabadilishwa tena kwa amani.... leo chama tawala kesho upinzani...nawa admire sana...watafika mbali wenzetu
 
Yawezekana alikua amejipanga, lakini ma-generali wakaamua kufikia mamuzi hayo kutokana na pengine Hali halisi ya kisiasa ndani ya Gambia. Pamoja na hayo, ma-generali hao wametazama hatma ya nchi na wananchi ikiwa wataendelea kumuunga mkono rais alie katalia madarakani.
wamefanya vizuri...else na wao wangemsindikiza huko uhamishoni....
Sasa hivi wanataendelea kula bata na rais ajae...
Jeshi lazima liwe neutral...
 
Suala la Jameh ni fundisho kwa watawala wapuuzi wa Kiafrika na siyejifunza hapa sijui. Nguvu ya umma imesemwa tangia kuumbwa kwa dunia kuwa haiwezi zidiwa na kitu chochote. Nashindwa kuelewa kuwa alishindwaje kumtanguliza puppet mbele alafu yeye akaonekana amestaafu huki akiwa salama!
 
Mkuu uko sawa mm mwenyewe ni muumin wa udikteta naamin kwa nchi ambazi bado hazijaendelea udicteta unahitajika ili maendeleo yakifikia level fulan nzur ndio tuwaachie wapayukaji wa kisiasa waanze mambo yao maana huwa nakereka nchi INA matatizo lukuki halafu kila mtu anataka asikilizwe badala ya kutatua changamoto huku wengine wakitaka maandamano ni upuuzi tu. Angalia mifano kutoka China hakuna pure democracy anayoihubiri mmarekan still jamaa wako juu kiuchumi kuishinda ulaya na democrasia yao
Sasa kama unataka huo udikteta si wabadili katiba ijulikane kuwa ni udikteta na hakuna democracy, kuliko kutumia pesa nyingi katka uchaguzi halafu kushindwa hutaki, China wao wana mfumo wao wa kuchagua Rais, yani baraza la communist ndo linamchagua fulani kuwa Rais, na sio blah blah za uchaguz akat kushindwa hutaki
 
33 Reactions
Reply
Back
Top Bottom