Majanga kama hili la Moto Kariakoo yanazidi kutukumbusha umuhimu wa Sekta Binafsi kwenye Uchumi

Naanto Mushi

JF-Expert Member
Oct 16, 2015
6,236
15,603
Najua bado itatuchukua muda sana kwa watunga sera kulielewa hili suala, maana ni suala la kifalsafa zaidi.

Fikiria kama ungekuwa na huduma ya Fire ambayo ni ya binafsi, ambao wana kandarasi ya kuzima moto kwenye jiji, utendaji wake ungekuwa wa tofauti sana. Private sekta ipo efficient sana maana wanawajibika kwa shareholders ambao ni watu binafsi tofauti na zima moto ya sasa ambao wabawajibika kwa serikali. Ni ukweli usiopingika wafanyakazi wa serikali ni wavivu mnooo..

Fikiria kama soko la kariakoo lingekuwa kinaendeshwa na Sekta Binafsi, hali ingekuwa tofauti sana, ukitaka kuthibitisha angalia performance ya taasisi za kifedha za Serikali na za Binafsi.

Kwa kifupi kabisa, mambo mengi tunayoyashuhudia sasa yanachangiwa zaidi na nchi kuendelea kukumbatia ideology za kikomunisti za serikali kufanya kila kitu, ambazo sio efficient.

Ni moja wapo ya sababu ni kwanini mimi N.Mushi nahitaji katiba mpya kwenye hii nchi, lazima tubadili ideology, kutoka hii ya sasa ya kikomunisti na tuende kwenye market economy ambayo itaelemea kwenye Private Sekta zaidi.
 
Jibu ni moja tu serekari ya ccm majanga sio vipaumbele vyake, dawa ni kuindoa madarakani.
Hizi lawama wanazopata ccm pamoja na dua mbaya Lau zingekua zinafanya kazi leo hii hio ccm isingekuwepo.

Nikama vile dua la kuku kwa mwewe!
 
Mkuu wala usiende mbali; jiulize KNIGHT SUPPORT waliokuwa wametanda maeneo yote ya jiji standby 24/7 na magari yao ready for anything siku hizi wako wapi? Uliingia utawala uliochukia private sector matokeo yake ndio kama hivi!

Eneo mojawapo walilokuwa muda wote wamepaki kusubiri matukio ni pale Shekilango; very strategic area kwa jiji la Dar. Kupitia njia ya mwendokasi kufika Kariakoo ingekuwa ni within minutes. Bahati mbaya kwenye hili maono yalikosekana.

Mojawapo ya ToR's za kamati iliyoundwa iwe ni kuja na majibu ilikuwaje makampuni mengine ya kupambana na majanga hayakushiriki kwenye tukio hili zito la kitaifa. Kama hayapo wakati yalisajiliwa kufanya kazi nchini basi itafahamika ni sababu zipi ziliyaondoa.
 
Awali ya yote ndugu mleta mada, umewahi kufikiria side effects ya hii hoja yako pengine?

Umewahi kufikiria Kama kungelikuwepo na kitu Kama hiko Kisha kutokee hakuna kazi hizo taasisi zingekua zinajiendeshaje?

Matukio ya Moto sio ya kila wakati, unaweza kupita hata mwaka mzima kusitokee hata kichaka kuungu!

Unadhani hizo taasisi zinajiendeshaje, uoni kwamba wanaweza kutengeneza matukio ya Moto kwa maksudi ili waweze kupata kazi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu wala usiende mbali; jiulize KNIGHT SUPPORT waliokuwa wametanda maeneo yote ya jiji standby 24/7 na magari yao ready for anything siku hizi wako wapi? Uliingia utawala uliochukia private sector matokeo yake ndio kama hivi!

Eneo mojawapo walilokuwa muda wote wamepaki kusubiri matukio ni pale Shekilango; very strategic area kwa jiji la Dar. Kupitia njia ya mwendokasi kufika Kariakoo ingekuwa ni within minutes. Bahati mbaya kwenye hili maono yalikosekana.

Mojawapo ya ToR's za kamati iliyoundwa iwe ni kuja na majibu ilikuwaje makampuni mengine ya kupambana na majanga hayakushiriki kwenye tukio hili zito la kitaifa. Kama hayapo wakati yalisajiliwa kufanya kazi nchini basi itafahamika ni sababu zipi ziliyaondoa.
Japo matukio ya moto yamekuwa yakisumbua miaka kadhaa, lakini yule jamaa aliua kabisa private sector.
 
Najua bado itatuchukua muda sana kwa watunga sera kulielewa hili suala, maana ni suala la kifalsafa zaidi.

Fikiria kama ungekuwa na huduma ya Fire ambayo ni ya binafsi, ambao wana kandarasi ya kuzima moto kwenye jiji, utendaji wake ungekuwa wa tofauti sana. Private sekta ipo efficient sana maana wanawajibika kwa shareholders ambao ni watu binafsi tofauti na zima moto ya sasa ambao wabawajibika kwa serikali. Ni ukweli usiopingika wafanyakazi wa serikali ni wavivu mnooo..

Fikiria kama soko la kariakoo lingekuwa kinaendeshwa na sekta binafsi, hali ingekuwa tofauti sana, ukitaka kuthibitisha angalia performance ya taasisi za kifedha za serikali na za binafsi.

Kwa kifupi kabisa, mambo mengi tunayoyashuhudia sasa yanachangiwa zaidi na nchi kuendelea kukumbatia ideology za kikomunisti za serikali kufanya kila kitu, ambazo sio efficient.

Ni moja wapo ya sababu ni kwanini mimi N.Mushi nahitaji katiba mpya kwenye hii nchi, lazima tubadili ideology, kutoka hii ya sasa ya kikomunisti na tuende kwenye market economy ambayo itaelemea kwenye private sekta zaidi.
Una hoja sahihi ila la kujiuliza ni kwanini Sekta binafsi haijawekeza kwenye hiyo sekta? Labda unalo jibu
 
Nakupinga kwa hali zote. Nchi luluki fire Brigades zinaendeshwa na serikali au majiji na ziko vizuri mno mno. Pia kuna mashirika, masoko, nk yanaendeshwa na serikali na yako vizuri mno. Tatizo ni utendeji tu. Ukishaona unafikiria mpaka kuanzaisha huduma za fire za binafsi eti kwa sababu serikali kuu au serikali za mitaa zinazembea ujue unaikoroga nchi kichwa chini. Unafikiri unaweza kulipia huduma ya kuzima moto wewe? Kodi zako zinafganya kazi gani. Uzembe wa serikali unatakiwa ushughulikiwe.
 
Najua bado itatuchukua muda sana kwa watunga sera kulielewa hili suala, maana ni suala la kifalsafa zaidi.

Fikiria kama ungekuwa na huduma ya Fire ambayo ni ya binafsi, ambao wana kandarasi ya kuzima moto kwenye jiji, utendaji wake ungekuwa wa tofauti sana. Private sekta ipo efficient sana maana wanawajibika kwa shareholders ambao ni watu binafsi tofauti na zima moto ya sasa ambao wabawajibika kwa serikali. Ni ukweli usiopingika wafanyakazi wa serikali ni wavivu mnooo..

Fikiria kama soko la kariakoo lingekuwa kinaendeshwa na sekta binafsi, hali ingekuwa tofauti sana, ukitaka kuthibitisha angalia performance ya taasisi za kifedha za serikali na za binafsi.

Kwa kifupi kabisa, mambo mengi tunayoyashuhudia sasa yanachangiwa zaidi na nchi kuendelea kukumbatia ideology za kikomunisti za serikali kufanya kila kitu, ambazo sio efficient.

Ni moja wapo ya sababu ni kwanini mimi N.Mushi nahitaji katiba mpya kwenye hii nchi, lazima tubadili ideology, kutoka hii ya sasa ya kikomunisti na tuende kwenye market economy ambayo itaelemea kwenye private sekta zaidi.
Watanzania walilishwa ukomonist/ujamaa na wakaumeza haswa. Kasumba ya ujamaa ililemaza kabisa ujasiri wa watu kuona uzuri wa sekta binafsi ndiyo maana hadi leo serikali ni kama inasita kuruhusu sekta hii ichanue na kuendesha uchumi.

Bila mageuzi ya kweli ya mfumo na kufikiri hata katiba mpya haitatusaidia. Watanzania wanatakiwa waachane kwanza na kasumba ya ujamaa ya kudhani Serikali inapaswa kufanya kila kitu.

Kuhusu hizi fire zisiwe centralized kama ilivyo sasa. Kila mji uwe na fire service iliyo independent na iwe chini ya mamlaka ya meya au Mkurugenzi wa sehemu husika. Na hiyo miji au Halmashari ndiyo wawajibike kuwalipa. Hii fire ya sasa hivi inajua mshahara unatoka hazina haiwezi kuwa na ufanisi. Fire iwe localized ili kuleta ufanisi
 
Mkuu wala usiende mbali; jiulize KNIGHT SUPPORT waliokuwa wametanda maeneo yote ya jiji standby 24/7 na magari yao ready for anything siku hizi wako wapi? Uliingia utawala uliochukia private sector matokeo yake ndio kama hivi!...
Umeeleza vyema kwani najiuliza kuhusu hili.
 
Una hoja sahihi ila la kujiuliza ni kwa nini Sekta binafsi haijawekeza kwenye hiyo sekta? Labda unalo jibu
Huduma za zimamoto na uokoaji ni jukumu la serikali. Huwezi kubinafsisha kwa sababu ni wachache mno ambao watafaidika. Imagine nyumba yako inaungua halafu mtu wa fire anataka mkubaliane kwanza gaharama za malipo ndiyo waanze kuzima nyumba. Na wakizima bila kukubalina kwa hali yoyote utakuwa huna fedha za kulipa.
 
Back
Top Bottom