mtoto wa mchungaji
JF-Expert Member
- Oct 24, 2020
- 279
- 480
Matukio ambayo tulishayasahau kitambo sasa yameamza kuibuka upya tena kivingine, kwani zamani majambazi walikuwa hata wanauliza au hata kutishia silaha au kupiga hewani risasi, lakini safari hii wananyonga yaani wamechoka, na kupiga risasi hewani wanaona kama hasara ni mwilini tu.
Kwa mujibu wa taarifa kupitia vyombo vya habari tayari majambazi wamenyonga mlinzi wa benki. Na mpaka sasa tayari kumeanza kuripotiwa matukio mbali mbali ya ujambazi na kupoteza maisha ya watu hata arobaini bado haijaisha.
Aliyekuwa Rais wa awamu ya tano Hayati Dr. Magufuli yeye aliwahi kuwaita wakuu wote wa vyombo vya ulinzi na usalama na kuwaambia kuwa ni bora niendelee kusikia majambazi wameiba au wameua lakini sitaki kusikia jambazi kafikishwa Polisi au Mahakamani naomba muwanyang'anye silaha, mwisho wa kunukuu. (na hapo hata mimi sichangii zaidi).