Majambazi wamerudi upya, sasa hivi wananyonga hawaulizi

TUJITEGEMEE

JF-Expert Member
Nov 6, 2010
17,408
2,000
Ndo ujue kwamba ... alikuwa ni rahisi wa ..., aliendesha nchi ktk namna ya watu kumuogopa yeye pasipo kujenga mifumo imara.

Angejenga mifumo imara suala la majambazi kutoweka lingekuwa la jumla jumla.
Nimerudi
===
Asante sana kwa bandiko lako murua.

Nina maswali kadhaa kutokana na bandiko lako hili.

1. Mfumo imara ni nini hasa? Yaani ni kitugani, jambo gani, hali gani na kiko, liko, ikoje?
2. Naomba unipe na kunifafanulia kinagaubaga tabia/desturi/tamaduni za "mfumo imara". Naomba pia katika kufafanua hili utumie mifano halisi ili kunirahisishia uelewa wa hii " mfumo imara"
===
Natanguliza shukrani kwa majibu ya maswali yangu.

Nakutakia asubuhi njema.

Nimebaki nikiwa TUJITEGEMEE.
 

Alistalikopaul

JF-Expert Member
Feb 2, 2019
402
1,000
System hata iwe bora vipi, kama hakuna utashi wa ku-inforce hiyo system hata iwekwe na nani haiana maana. enforcers wetu hawapo. PoliCCM
Ni hilo lilikua jukumu lake kuhakikisha polisi wanafanya kazi kwa weledi bila hata uwepo wake. Angefanya marekebisho ya sheria kuongeza weledi kwenye jeshi letu.
 

peno hasegawa

JF-Expert Member
Feb 24, 2016
3,687
2,000
Hivi hizi maneno za mfumo aka system ni zipi bandugu munieleweshe. Yaan twende Kwa mifano. Kua kuteketeza ujambazi mfumo gani uwepo. Maana naona watu tuko general Sana.
Cha kufanya na cha kuanzia,ni katiba, IGP asichaguliwe na mtu mmoja nafasi ya IGP itangazwe na watanzania wajitokeze kuiomba.na IGP sio lazima awe ni Polisi.
 

Lupweko

JF-Expert Member
Mar 26, 2009
14,713
2,000
Na mpaka sasa tayari kumeanza kuripotiwa matukio mbali mbali ya ujambazi na kupoteza maisha ya watu hata arobaini bado haijaisha.
Ukiondoa hilo la Tanga, nitajie tukio lingine la ujambazi hivi karibuni, ili tuhalalaishe kuwa 'wamerudi'
 

Crocodiletooth

JF-Expert Member
Oct 28, 2012
12,068
2,000
WAKUU WA VYOMBO HIVI HAWANA BUDI KUKAA NA WAKUU WA IDARA ZOTE KUONA KWAMBA NCHI INAENDELEA KUWA NA UTULIVU DHIDI MATUKIO YA KIJAMBAZI WIZI UKABAJI NA YOTE YA KIHALIFU, THE QUEST ARISE IS WHY THIS HAPPEN NOW?

MAGUFULI PRINCIPLES SHOULD BE TAKEN QUICKLY ON THIS SIDES.
 

kamituga

JF-Expert Member
May 31, 2019
1,169
2,000
Inabidi tumlaumu magufuli yeye kama kiongozi Bora alitakiwa kuandaa system ambayo itafanya kazi kwa weledi bila hata uwepo wake maana siku za mwanadamu duniani ni chache zinahesabika.

Watu wa maana siku zote wanaandaa mfumo ambao utajiendesha bila hata uwepo wake sio mfumo tegemezi ambao hauna ufanisi bila uwepo wake.


Alaaniwe yeyote yule amtegemeae mwanadamu.
Wew unaejiandaa kumlaumu mwenzako wew umeandaa nin? Au mfumo gan? Wa kuisaidia tanzania na Taifa kwa ujumla au ata familia yako sio kila kitu kulaumu tu wew ni binadamu km wao sasa jitafakari !!!!
 

Alistalikopaul

JF-Expert Member
Feb 2, 2019
402
1,000
Wew unaejiandaa kumlaumu mwenzako wew umeandaa nin? Au mfumo gan? Wa kuisaidia tanzania na Taifa kwa ujumla au ata familia yako sio kila kitu kulaumu tu wew ni binadamu km wao sasa jitafakari !!!!
Samahani kama umekwazika mkuuu.

Ila huo ni mtazamo wangu binafsi.

Kuhusu taifa itoshe kusema sijalisaidia chochote na wala familia yangu sijaiandaa kwa lolote.
 

Tlg

JF-Expert Member
Apr 3, 2017
789
1,000
Una toa takwimu zako za majambazi au wezi kutoka wapi?

Unajuaje walipungua umefanya research?

Je kwanini walipungua kama ni kweli ?

Na kwanini waongezeke sasa kama ni kweli?


Afterthought: huoni kuna tatizo kama ni kweli walipungua na sasa wameongezeka maana yake vyombo vya ulinzi viliendeshwa na utashi wa MTU mmoja ambaye Mungu anaweza mchukua anytime huoni ni utaratihu hatari sana kwa mustakabali wa taifa letu?

Afterthought 2: may be pia matukio yalikuwepo hayakupata airtime? Sasa yanapata airtime or may be ni kweli pesa ziliadimika mtaani kama baadhi ya watu (wapinzani hawa) wakakosa potential area za Ku robe ??? A lot of may be'z unless uje na proof isiyopingika kuhusu madai yako haya katika thread hui..
 

Kiboko.

JF-Expert Member
Jul 31, 2013
2,842
2,000
Matukio ambayo tulisha yasahau kitambo sasa yameamza kuibuka upya tena kivingine, kwani zamani majambazi walikuwa hata wanauliza au hata kutishia silaha au kupiga hewani risasi, lakini safari hii wananyonga yaani wamechoka, na kupiga risasi hewani wanaona kama hasara ni mwilini tu. Kwa mujibu wa taarifa kupitia vyombo vya habari tayari majambazi wamenyonga mlinzi wa benki. Na mpaka sasa tayari kumeanza kuripotiwa matukio mbali mbali ya ujambazi na kupoteza maisha ya watu hata arobaini bado haijaisha.

Aliyekuwa Rais wa awamu ya tano Hayati Dr. Magufuli yeye aliwai kuwaita wakuu wote wa vyomboa vya ulinzi na usalama na kuwaambia kuwa ni bora niendelee kusikia majambazi wameiba au wameua lakini sitaki kusikia jambazi kafikishwa polisi au mahakamani naomba muwanyang'anye silaha, mwisho wa kunukuu. (na hapo hata mimi sichangii zaidi).
mtamkumbuka sana JPM
 

Tripo9

JF-Expert Member
Sep 9, 2009
4,106
2,000
Cha kufanya na cha kuanzia,ni katiba, IGP asichaguliwe na mtu mmoja nafasi ya IGP itangazwe na watanzania wajitokeze kuiomba.na IGP sio lazima awe ni Polisi.
mmmh Acha niendelee kutafakari ulichoongea. Wabunge wanachaguliwa na wananchi. Kuna wezi na walafi na wabadhirifu kuwashinda wabunge nchi hii. Mawaziri nao ni wabunge kutwaa tunaskia wamepiga dili wanatumbuliwa.
Acha niendelee Tu kutafakar manenoyo
 

nosspass

JF-Expert Member
Mar 7, 2013
5,441
2,000
Hivi hizi maneno za mfumo aka system ni zipi bandugu munieleweshe. Yaan twende Kwa mifano. Kua kuteketeza ujambazi mfumo gani uwepo. Maana naona watu tuko general Sana.
hahahhaaaa....mbinu za vita hazitolewi kwenye mijadala mangi!!( yaani hadharani) intelijensia.....
 

Bambushka

JF-Expert Member
Jan 9, 2020
2,656
2,000
Mfumo mfumo mfumo, huyo Magu hata kama asingekufa mwaka huu, iko siku angekufa, hakuna binadamu anayeishi milele.

Ujambazi haujawahi kuisha, sema kuripoti matukio kwenye media ndiyo kulistopishwa.

Everyday is Saturday............................... :cool:
 

Liwagu

JF-Expert Member
Jan 25, 2017
2,568
2,000
Inabidi tumlaumu magufuli yeye kama kiongozi Bora alitakiwa kuandaa system ambayo itafanya kazi kwa weledi bila hata uwepo wake maana siku za mwanadamu duniani ni chache zinahesabika.

Watu wa maana siku zote wanaandaa mfumo ambao utajiendesha bila hata uwepo wake sio mfumo tegemezi ambao hauna ufanisi bila uwepo wake.


Alaaniwe yeyote yule amtegemeae mwanadamu.

Magu alisha waonyesha njia za kukabiliana na hao wazulumu roho za watu " majambazi"

Sasa nijuu yao kuzitumia ama kuziacha.
Unaweza kumpeleka ng'ombe kisimali lakini huezi kumlazimisha kunywa maji.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom