Polisi yatangaza kuwakamata wanaodaiwa kufanya Ujambazi maeneo ya Goba, wajeruhiwa kwa risasi

Idugunde

JF-Expert Member
May 21, 2020
6,273
6,637
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, tarehe 08/1/2023 saa 6 :30 mchana eneo la Mabibo External Kinondoni lilifanikiwa kuwakamata majambazi sugu wanne wakiwemo Athuman Yusuph Mbalilo SOTI (50) Mkazi wa Kimara Temboni, Mpoki Raphael @ Mwangwisya (41) mkazi wa Mbezi Luis na wengine wawili kwa tuhuma nzito za kujihusisha na vitendo vya kihalifu vya unyang’anyi wa kutumia silaha na kupora pesa katika maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam na mikoa ya jirani.
Muliro.JPG

Kamanda Kanda Maalum ya Polisi Dar es Salaam, Muliro J. MULIRO – ACP amesema ukamataji huo umetokana na taarifa fiche ya kuwepo kwa kundi hilo la kihalifu ambalo lilionekana kuanza kufanya matukio mbalimbali ya uhalifu wa kutumia silaha kuanzia tarehe 01/01/ 2023 hadi tarehe 07/1/2023 katika Jiji.

Amesema Watuhumiwa hao wanne walikutana kupanga na kujiandaa eneo la kufanya uhalifu na walipobaini kuzingirwa na askari Polisi mmoja wao alitoa bastola yake na kupiga risasi kuwashambulia askari, na katika mazingira hayo askari walijihami na kuwajeruhi watuhumiwa wote wanne kwa risasi na kufanikiwa kuwakamata.

“Mahojiano ya awali na watuhumiwa hao na kumbukumbu za kihalifu za Polisi zimeonesha kuwa miongoni mwao waliwahi kukamatwa na kukaa kwenye mahabusu za Keko kwa tuhuma za mauaji na unyanganyi na walitoka Mwaka 2017 na mmoja wao akakimbilia nchi jirani na alirudi 2022 na kushiriki matukio yakiwemo jaribio la uporaji eneo la Mtaa wa Tandamti Kariakoo, kupora pesa huku wakitishia bunduki eneo la Kunduchi Mtongani, Goba walitishia silaha na kupora pesa, Keko, na Vikindu Wilaya ya Mkuranga pia walipora pesa,” amesema Kamanda Muliro.

Ameendelea kueleza kuwa baada ya kukamatwa waliwaonesha askari bunduki aina ya AK 47 yenye namba za usajili UC 3889 1998 ikiwa na risasi 24 ndani ya Magazine, Bastola moja aina Star iliyofutwa namba ikiwa na Risasi nne (4) ndani ya magazini na zilikamatwa pia pikipiki mbili aina ya Boxer nyeusi, MC 665 DMD na MC 475 DPH ambazo zimekuwa zikitumiwa kwenda na kutoka kwenye maeneo ya matukio yaliyotajwa.

Kutokana na majeraha waliyoyapata wakati askari wakijihami kwa risasi wahalifu hao walipelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu lakini hali zao sio nzuri. Juhudi za kuwatafuta majambazi wengine ambao hawajakamatwa zinaendelea na lazima watakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vingine vya kisheria.

Kamanda Muliro amesema “Jeshi la Polisi linachukizwa sana na halitavumilia hata kidogo kuona wahalifu wakiwasumbua wananchi kwa vitendo vya kihalifu.Jeshi halitakuwa na huruma lakini litazingatia sheria kuwashughulikia kwa haraka sana kila atakaye jihusisha au kutenda vitendo vya ovyo vya kihalifu.

“Jeshi la Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam linatambua Dar es Salaam ni mji wa kibiashara na uwekezaji na mtaji mkubwa ni suala la usalama. Jeshi la Polisi litaendelea kutimiza majukumu yake na kuhakikisha usalama unaimarika zaidi na hakutakuwa na mwanya wawahalifu kulazimisha kurudi tulikotoka. Wito, wananchi waendelee kutoa taarifa na tunaahidi kuzitunza na kuzifanyia kazi haraka iwezekanavyo.”


==========

Jambazi.jpg
 
Wangekua wanawekwa hadharani itasaidia kujua mtandao wao
 
Wangekua wanawekwa hadharani itasaidia kujua mtandao wao
uko sahihi.
mara baada ya uchunguzi kukamilika picha za majambazi wawe wanaonyeshwa hadharani kwenye TV na magazeti hii itasaidia ndugu na jamaa kuwakanya baadhi yao wenye tabia kama hiyo.
 
Ushauri wangu ili kupunguza hili Jambo wawe wanamalinzwa kimya kimya
Style ya enzi za Mwendazake. Wale wa Kibiti na wale waliokuwa wanavamia vituo vya polisi kisha kuua na kupora silaha wengi wao waliishia kuokotwa kwenye viroba...problem solved!
 
Wanatakiwa kukatwa mikono ili kutengeneza displine kwa vizazi vijavyo .ukishamuona mtu hana mkono ukapewa historia yake kuwa alikatwa kwasababu ya wizi huwa inaongeza displine na uoga
 
Wanatakiwa kukatwa mikono ili kutengeneza displine kwa vizazi vijavyo .ukishamuona mtu hana mkono ukapewa historia yake kuwa alikatwa kwasababu ya wizi huwa inaongeza displine na uoga
kumkata mkono? !!!
acha huruma kwa hawa fisi maji, dawa yao ni kifo tu.
 
Hawa mbwa wajinga sana. Yaani wenzao tunatafuta kwa jasho, halafu wenyewe wanataka kula kwa ulaini tu.
Mkuu,nani kakuambia majambazi wanakula kiulaini? Kazi ambayo unabeti maisha,huko unakoenda kufanya kazi (kuiba) hujui utakutana na kizingiti Cha aina gani chenye kuweka rehani uhai wako,hiyo kazi haiwezi kuwa rahisi kamwe.

Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
 
Yalishatukuta mimi na jamaa zangu, imagine nimetoka 0 level, nimepata kibarua jamaa wakatujia front ofisini, sitasahau. Ila kuna maafande waliwafatilia ndani ya muda mfupi wakawadaka.mbaya ni kwamba waliwaachia baadhi ya jamaa zetu makovu ya usoni kwa vitako vya bunduki mpaka leo wanayo, sitasahau kamwe
 
Naona Kiswahili kimepata vocabulary mpya; taarifa "fiche". Sio za kiintelijensia tena.
 
Back
Top Bottom