Simiyu: Majambazi wavamia maduka Bariadi, Walinzi wakimbia

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,802
11,961
Watu kadhaa wanaodaiwa kuwa ni majambazi wakiwa na silaha mbalimbali wamevamia maduka yanayofanya biashara za miamala ya kifedha katikati ya Mji wa Bariadi usiku wa kuamkia Juni 8, 2023.

Wahalifu hao wamevunja milango lakini wakashindwa kuvunja boksi za kuhifadhia fedha ambazo ndizo walikuwa wamezilenga.

photo_2023-06-08_22-09-10.jpg

Inadaiwa walifunga Barabara zote zinazoingia eneo ambako maduka yalipo, huku walinzi wakikimbia baada ya kutishiwa kuuawa.

Baadhi ya Wananchi ambao ni majirani kwenye maduka hayo, wamesema walisikia milio ya risasi kati ya askari pamoja na watu hao waliosadikika kuwa majambazi.

Mmoja wa walinzi Msobi Mbelya ambaye aliumizwa wakati akipambana na wahalifu amelazwa Hospitali ya Halmashauri ya Mji (Somanda) amesema baada ya watu kufika walimtishia kwa kusema akamatwe kisha apigwe.

"Baada ya kusikia wakisema hivyo, nilianza kukimbia, ndipo nilipoanguka kwenye mtaro, baadaye nikasikia wanaanza kuvunja milango ya maduka kwa kutumia shoka," amesema Mbelya.

Aidha, mlinzi huyo amesema Polisi walifanikiwa kufika haraka na kuanza kurushiana risasi lakini baadaye Polisi walikimbia kurejea kituo cha Polisi na waliporudi mara ya pili walikuta majambazi hao wamekimbia.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Sokoni Joseph Mula amesema kuwa watu hao hawakufanikiwa kuiba kitu chochote na badala yake walifanya uhalibifu wa kuvunja maboksi ya kuhifadhia fedha pamoja na milango ya maduka.

Mula amesema maduka yaliyovamiwa ni mawili yanayofanya Biashara ya miamala ya kifedha huku duka la tatu likiwa linafanya Biashara ya kuuza Dawa Muhimu ambapo nako walivunja lakini hawakuingia ndani.

Diwani wa Kata ya Sima ambako tukio limetokea Zebedayo Kingi amesema wahalifu hao walifunga Barabara zote zinazoingia na kutoka kwenye maduka hayo.

Amesema "Tayari Jeshi la Polisi limeanza uchunguzi wa tukio, ni tukio baya ingawa hawakuchukua kitu, tunawaomba Wananchi wawe watulivu, ingawa tunawashauri wenye maduka kutafuta walinzi wenye vifaa imara."

"Nilifika dukani nikakuta boksi ya kuhifadhia fedha nilikiwa limebomolewa lakini walishindwa kulivunja kabisa, ndani kulikuwemo na Sh. Milioni tano, simu za miamala pamoja na mashine za Benki,” amesema Rebeca Masunga.

Naye, Juda Sayi mmoja wa wamiliki wa Duka lilibomolewa, alisema kwenye dula lake hilo ni tukio la pili, ambapo miezi miwili iliyopita walimwibia Sh. Milioni 24.

"Tunaomba ulinzi uimarishwe kwenye huu Mji wa Bariadi, matukio yanaanza kuongezeka haya sasa, tunaomba Serikali itusaidie maana tunashindwa kufanya biashara," amesema Juda.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Simiyu halijatoa taarifa yoyote juu ya tukio hilo, licha ya Kamanda wa Polisi kuombwa taarifa lakini hakujibu.
 
Kichekesho ni polisi kuja na baadae kukimbia.

Yaani umeitwa kuwa kuna majambazi yenye silaha, unakurupuka na virisasi vyako 6. Unafika unaona zengwe, unakimbia. Kulikuwa na haja gani ya kuja?

Mtu akihisi polisi wamekula njama atakuwa anakosea? Pumbavu.
 
Back
Top Bottom