Kagera: Polisi waua watatu waliodhaniwa kuwa Majambazi

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,377
8,121
Kamanda wa Polisi Mkoa, ACP William Mwampagale amesema tukio lilifanyika kwenye operasheni maalumu baada ya kupata taarifa kuwa kuna kundi la watu waliopanga kufanya uhalifu.

Amesema kundi lilikuwa na wanaume 5 na katika uchunguzi wa awali walibaini wamekuwa wakifanya matukio ya unyang’anyi wa kutumia silaha tangu Septemba 2022.

Kamanda Mwampagale ameongeza kuwa wamefanikiwa kupata silaha moja aina ya AK47 isiyokuwa na namba na magazine moja yenye risasi 12.
===

JESHI la Polisi mkoani Kagera limesema limeua watu watatu wanaodhaniwa kuwa majambazi katika mpaka wa Wilaya ya Ngara na Biharamulo mkoani Kagera.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, ACP William Mwampagale amewaambia waandishi wa habari tukio hilo lilifanyika wakati wa operashani maalumu baada ya kupata taarifa kuwa kuna kundi lililokuwa linapanga kufanya uhalifu.

“Tulipata taarifa za kiintelijensia kuwa kuna kikundi cha majambazi kimepanga kufanya uhalifu kwa kutumia silaha Novemba 15, 2022. Tuliweka mitego katika maeneo hayo ambapo baada ya kuwanasa nakuanza majibizano ya risasi walijeruhiwa na kukimbizwa hospitali ambapo walipoteza maisha,” amesema.

Miili yao imehifadhiwa katika hospitali ya wilaya ya Ngara Nyamiaga” amesema Mwampagale

Amesema majambazi hao walikuwa watano wote wanaume waliokuwa wanakadiliwa kuwa na umri wa kati ya miaka 25 na 35 na katika uchunguzi wa awali uliofanywa na jeshi hilo umebaini kuwa kikundi hicho kimekuwa kikifanya matukio ya unyang’anyi wa kutumia silaha tangu Septemba mwaka huu katika maeneo ya kijiji cha Bugarama,Muganza na Murusagamba.

Hata hivyo Mwampagale ameongeza kwa katika operashani hiyo wamefanikiwa kupata silaha moja aina ya AK47 isiyokuwa na namba pamoja na magazine moja ikiwa na risasi 12 na hivyo kutumia nafasi hiyo kuwaonya wale wote wanaojihusisha na vitendo hivyo.

HABARI LEO
 
Ukweli nachukia sana taarifa kama hizi na sijui zitakoma lini hizi!! Kwanini polisi waruhusiwe kuua watu hovyo na vyombo vya sheria haki za binadamu nk vinakaa kimya au kwa sababu si lao basi wafe tuu?!

Huyo aliyeleta taarifa za kwamba kuna mipango ya kufanya uhalifu kwa kikundi hicho mlimuamini vipi? Je mlithibitisha tuhuma hizo kwa kuwahoji watuhumiwa? Vipi kama hiyo bunduki isiyo na namba iliwekwa na huyo mtoa taarifa au ni polisi nyinyi mliitoa stoo kwenu kuhalalisha mauaji hayo?

Kumbuka mnao waua wana familia zinawategemea wana ndugu na jamaa zao wanaowapenda, hata baada ya matukio ya Ifakara na Mtwara kuthibitika wazi kuwa mnaua wasio hatia bado serikali ya rais Samiah Suluh Hassan inakubali watu wauawe kweli?! 😭😭😭😭
Mimi binafsi nimewahi kufika kituo cha polisi tukahitirafiana kidogo na occid akanitishia kunipa armed robbery! nilimshangaa sana anasema hivyo bila woga wala haya na hakujua kama nilikuwa namrecord hayo matamshi yake.
TUPINGE KWA NGUVU ZOTE MAUAJI YANAYOFANYWA NA POLISI HATA KAMA NDIO WANAWAWEKA WALIO MADARAKANI.
 
Back
Top Bottom