Majamaa majanja sana haya... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Majamaa majanja sana haya...

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Nyani Ngabu, Sep 8, 2010.

 1. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #1
  Sep 8, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,650
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Tayari yamesha divert attention kutoka kwenye madhambi yao ya ufisadi na kushindwa kuongoza na sasa tupo hapa tunamzungumzia Josephine na "kuibwa" kwake NA Dkt. Slaa.

  Nimekoma nayo haya majamaa ya CCM....SALUTE!!
   
 2. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #2
  Sep 8, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Dawa ni kujiuzulu kwa Slaa hakuna jingine na majeshi yaelekezwe kwengine itakuwa hapajaharibika kitu ,kwani kwa hili tayari Slaa ameshakuwa hafai na sio siri au kuwalaumu wengine ,Slaa ameonekana kwenye vyombo vya habari akijilabu kwa mke wa mtu mwengine ,hapa ameharibu kabisa ,hivi tuseme Slaa alimuokota tu huyu na hakumuuliza masuali masuali na kumhoji kwa undani ,je kama alitumwa kumharibia na ndio Slaa akavamia na sasa amenasa.
   
 3. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #3
  Sep 8, 2010
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Nyani,
  That is an old trick. Ukiona unazidiwa change the subject. Let us see how much shelf life it will hold. Namshauri Dr Slaa aendelee kukata issues, regardless the diversion.
   
 4. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #4
  Sep 8, 2010
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Wakati sisi tunapigana na UFISADI, Wazenji wanashangilia. Si unamuona MWIBA?

  Kuna haja tulivunje li Muungano na Wazenji warudi kwenye Vibanda vyao walivyoacha Zenji.

  Kwa hali ilivyo, sioni haja kwa huko mbeleni kuja kuwa na Rais kutoka Zanzibar.
   
 5. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #5
  Sep 8, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  :mad2:Deep green nao wajiuzuru
   
 6. Tusker Bariiiidi

  Tusker Bariiiidi JF-Expert Member

  #6
  Sep 8, 2010
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 4,757
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  Dr.Slaa ndio propaganda za CHECHEMEEE... Inanikumbusha hadithi ya jamaa ambaye amechelewa kurudi nyumbani... Akifunguliwa Gate na Mlinzi... Anaanza kuhoji "Mbwa wanaonekana kama wana njaa!" mbona umechelewa kufungua Gate...
   
 7. O

  Ogah JF-Expert Member

  #7
  Sep 8, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Namkumbuka sana yule mwanamke alivyokuwa akifundishwa jinsi ya kumpaka Mrema kipindi kile cha uchaguzi............thats CCM old trick kama alivosema Mkuu Jasusi
   
 8. B

  Binti Maria Senior Member

  #8
  Sep 8, 2010
  Joined: Jun 26, 2007
  Messages: 159
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Msome Tundu Lissu, interesting episode:

  Josephine Mushumbusi, amezungumza kupitia Mwanasheria Mkuu wa Chadema, ambaye pia ni wakili wa Dk Willibrod Slaa, Tundu Lissu, akaviambia vyombo vya habari kuhusu tuhuma zinazowakabili yeye na Dk. Slaa kuwa kwa mara nyingine, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimerejesha mfumo wa uchaguzi unaobadilishwa kuwa mfumo ya kijinga (a silly season). Akasema kwamba CCM wamekuwa wakikishambulia Chadema kuwa ni chama Wachagga; kwamba baadhi ya viongozi wake ndio walimuua Chacha Wangwe; na kwamba Dk Slaa ametumwa na kanisa Katoliki kugombea urais; lakini baada ya kuona hadithi hizo zimepuuzwa, sasa wameibuka na suala jipya na "ndoa za Dk. Slaa" wakidhani zitawasaidia kugeuza macho ya umma kutoka kwenye masuala muhimu ya wakati huu.

  Akasema CCM hawataki Dk. Slaa na Chadema wajadili wizi, ubadhirifu wa fedha na mali za umma; hawataki wajadili wizi wa Sh. bilioni 772 zilizoibwa katika mwaka 2008/9 tu, kwa mujibu wa ripoti ya Mkaguzi na mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali; hawataki Chadema itaje majina ya wezi wa Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT); hataki Chadema wajadili jinsi JK na rafiki zake, akina Edward Lowasaa, Nazir Karamagi, Andrew Chenge na Rostam Azizi walivyofilisi taifa hili; hawataki Chadema ijadili madai halali ya wafanyakazi wa Tanzania na ahadi za ‘maisha bora kwa kila Mtanzania.' CCM hawataki Chadema kijadili sera mbadala ambazo zinalenga kuwakomboa Watanzania kutoka lindi la umaskini.

  Wanataka kulielekeza taifa zima katika kujadili masuala ya ‘chumbani' kwa Dk. Slaa; analala na nani, ana wake wangapi, kawapata wapi na kadhalika; ili kwa kufanya hivyo mgombea wao awarubuni wananchi kwa ziara mikoani na ahadi kemkem zisizotekelezeka.

  Tundu Lissu amesisitiza kuwa kila wanapoona wamebanwa, CCM huwa wanabuni njama za kukomoa washindani wao, kama walivyofanya huko nyuma. Alitoa mifano ya kilichotokea miaka ya 1995 na 2005.

  Mwaka 1995: Kwa kumwogopa Mrema aliyekuwa tishio kwa CCM, walimtumia mwanamke mmoja, aitwaye Angelina, wakidai ni kimada aliyezaa na Mrema; akawa analala getini kwa Mrema, Masaki, Dar es Salaam. Wakamdhalilisha. Baada ya uchaguzi, Mrema akashindwa, na suala la Angelina halikujadiliwa tena.

  Mwaka 2005 tishio la CCM ilikuwa Chama cha Wananchi (CUF), hasa Zanzibar. CCM wakamtumia Inspekta Jenerali wa Polisi, Omar Mahita, siku chache kabla ya uchaguzi, kudai kuwa amekamata lori lenye mapanga, majambia, visu na silaha nyingine zenye nembo ya CUF. Wakakipaka chama matope. Baada ya uchaguzi, hatukuelezwa lolote kuhusu visu hivyo.

  Mwaka huo huo, katika uchaguzi wa ndani ya chama, baada ya kundi la JK kuona limezidiwa mno, likaamua kumzushia Dk. Salim Ahmed Salim likidai ni Mwarabu, na muuaji wa Rais Abeid Amani Karume. Wakamhujumu, Na baada ya uchaguzi hawakuzungumzia tena uarabu wa Dk. Salim.

  Mwaka 2010: Tishio la CCM ni Chadema na Dk. Slaa. Baada ya kuona upepo unawaendea vibaya, CCM wameamua kufanya siasa za mtaro wa maji taka; hizi wanazotumia watu kumwandama Dk Slaa.

  Tundu Lissu alisema kuwa Chadema hawako tayari kufanya siasa za majitaka; na kwamba Watanzania hawako katika kujadili mambo hayo, kama hali ya afya za wagombea, ambao baadhi wanadaiwa kuwa na virusi vya ukimwi kiasi cha kubadili damu kila baada ya miezi, na kwamba kwa sababu ya unyonge huo, baadhi yao waanguka mara kadhaa jukwaani.

  Akasema wao hawatazungumzia baadhi ya wagombea urais wana wake wangapi, mahawara wangapi, na wamewaweka katika ofisi gani za umma, wapi wamepewa mikataba minono ya fedha kwa upendeleo, na kadhalika. Akasisitiza kwamba Chadema haitajibu uchafu unaosambazwa na vyombo vya habari, lakini akasema, "sauti yetu itasikika iwapo wataenda mahakamani."
  Akasema Chadema itazungumzia umaskini wa Watanzania na namna ya kuupunguza au kuuondoa; jinsi Tanzania ilivyo nchi ya tatu katika Afrika lakini wanakijiji wanalazimishwa kujenga shule za kata huku serikali ikifuja mabilioni ya pesa (kama hizo bilioni 772/- zilizotafunwa ndani ya mwaka mmoja.

  Akasema Chadema itajadili malipo ya anasa kwa mawaziri, maisha duni ya polisi, walimu, wauguzi na makundi mengine yanayonyonywa katika jamii. Akasema Chadema itajadili jinsi ya kuboresha afya za wananchi.


  Akasema, "hatutaki siasa za chumbani, bali za hadharani."

  Kwanini wamshambulie Dk Slaa? Kwa sababu ni Dk. Slaa.

  - Ana rekodi ya kuwashinda CCM mara tatu, kwa miaka 15 mfululizo
  - Amekuwa sauti kuu ya wananchi Bungeni, inayotetea masilahi ya umma
  - Kuliko kiongozi yeyote aliyewahi kuwapo Tanzania ndani ya miaka 50, ni Dk Slaa pekee aliyetaja hadharani mafisadi 11 bla woga wowote. Walioathirika kwa ujasiri wake ndio hao wanaomsakama sasa kwa mambo ya chumbani badala ya mambo ya hadharani.
   
 9. TzPride

  TzPride JF-Expert Member

  #9
  Sep 8, 2010
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 2,423
  Likes Received: 395
  Trophy Points: 180

  Imekaa vizuri hiyo!!! safi sana mbunge wangu mtarajiwa, kichwa hiki kinatakiwa pia mjengoni kikate issues.

  Amucha munyampaa Lissu!!!
   
 10. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #10
  Sep 8, 2010
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Hawana lolote, vichwa maji... Wanadhani hii itampunguzia Slaa umaarufu! Thubutu!!! kama ingekuwa hivyo leo Zuma asingekuwa raisi au Silvio Belusconi asingekuwa waziri mkuu...
   
 11. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #11
  Sep 8, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Hapa JF mtashinda yaani hata Uraisi chati inaonyesha tayari mmeshashinda bado kututangazia Mawaziri ,sasa hao mawaziri sijui mtawatoa wapi au ndo mtawahitaji akina Juma Duni na wenzake !!!

  Mlala hoi ameshatinga kortini ,tuone huyo Slaa na genge lake linalomtetea. Na hata hapa nawaona mpo watu wa ajabu sana ,kuweza kumtetea Slaa kwa jambo hili ambalo lipo wazi ,hamna tofauti na wanaoitetea CCM ,ila tutaona mwisho wake ,ambao naamini kabisa Slaa hana au hapati tena usingizi , tunasema kibao kimegeuzwa.

  [FONT=ArialMT, sans-serif]Dk Slaa afunguliwa kesi mahakamani[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif] Wakati huo huo, shauri la madai limefunguliwa jana Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam na Aminiel Chediel Mahimbo, akimtaka Dk. Willibroad Slaa amlipe fidia ya Sh. bilioni moja. Mahimbo anamtuhumu Dk. Slaa ambaye ni mgombea urais kupitia Chadema, kuwa amemnyang'anya' mke, Josephine Mkatunzi Mushumbusi.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]
  [/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif] Kesi hiyo ilifunguliwa jana kwa niaba ya Mahimbo na kampuni ya uwakili ya Amicus kupewa namba 122 ya mwaka 2010.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Mahimbo alifafanua katika madai yake kwamba katika fedha anayodai, Sh. milioni 200 ni ya maumivu maalumu na Sh. milion 800 ni ya kufidia kitendo cha mlalamikiwa kumpunguzia hadhi na heshima mbele ya jamii.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]
  [/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif] Aidha, Mahimbo alidai kuwa, Septemba 7, 2002, alifunga ndoa ya Kikristo na mwanamke huyo katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT), usharika wa Kijitonyama na waliishi sehemu mbalimbali hapa Dar es Salaam ikiwemo Kimara Baruti.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Alidai kwamba ndani ya ndoa yao, walifanikiwa kupata watoto wawili, Upendo aliyezaliwa Mei mosi 2003 na Preciuos aliyezaliwa Machi, 14, 2007.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]
  [/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif] Vivuli vya vyeti vya ndoa na vile vya kuzaliwa watoto hao vimeambatanishwa.Pia alidai kuwa ndoa yao bado ni halali kwa kuwa haijawahi kutenguliwa.Aidha alifafanua kuwa mwanzoni mwa mwaka huu, mkewe alianza safari za mara kwa mara, kitendo kilichosababisha asiwepo nyumbani kwao kwa muda mrefu.Mahimbo alidai kwamba aliamini kuwa safari hizo zilitokana na kuongezeka kwa shughuli za mkewe, kwani ni mfanyabiashara anaeendesha kampuni iitwayo Green World Clinic.Aliendelea kudai kwamba, mlalamikiwa amemtambulisha Mushumbusi kama mkewe kwa tarehe na sehemu tofauti.Vivuli vinavyoihusu habari hiyo katika magazeti mbalimbali vimeambataishwa.Pia alidai kuwa mahusiano ya kingono kati ya mlalamikiwa na mke wake yamemdhalilisha, yamemhuzunisha, yamemshushia hadhi mbele ya jamii, hivyo kupata maumivu maalum.[/FONT]
   
 12. kilemi

  kilemi JF-Expert Member

  #12
  Sep 8, 2010
  Joined: Mar 13, 2009
  Messages: 520
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Hivi huyo anayeahidi hata visivyotekelezeka, hajawahi kabisa kuzini na mke wa mtu?
   
 13. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #13
  Sep 8, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Kusema kweli WaChadema mnatia huruma sana ,yaani ndio mnalitetea jibaba ?? :confused2:
   
 14. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #14
  Sep 8, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  mijamaa inaakili ya wizi hiii balaaaa!!! nawavulia kofia kwa fitna!!!
   
 15. k

  kiparah JF-Expert Member

  #15
  Sep 8, 2010
  Joined: Sep 7, 2010
  Messages: 1,176
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Hiyo, bold nyekundu inaonesha kidogo thinking capacity yako ina matatizo. Hivi kuna kiongozi yeyote wa CCM (chama cha mafisadi) hajawahi kulala na mke wa mtu kama si girl friend wa mtu. Na Kwa upande wako wewe 'kama huna matatizo' hujawahi kutembea na mwanamke asiye wako????

  Tafakari, chukua hatua. Then changia mada!
   
 16. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #16
  Sep 8, 2010
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135

  alieanza ni nani? siasa sawa na mchezo wa draft rusha kete ni rushe kete.

  mlionywa acheni michezo michafu mkajiona ooh sisi ni magwiji wa fitna tuna marando, tuna shibuda, basi CCM kwisha


  sasa mnalia na nani, lenu hili mtahangaika nalo
   
 17. Mpambalyoto

  Mpambalyoto JF-Expert Member

  #17
  Sep 8, 2010
  Joined: Mar 26, 2010
  Messages: 752
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mtu wa Pwani umesoma hii?
   
 18. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #18
  Sep 8, 2010
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135

  nimeisoma ila nimeiona rubbish tu, sasa hizo siasa zao maji taka, wakijibiwa kwa mfano wenye kufanana walie ooh tumeonewa.


  hawa wepesi hawana ngozi ngumu mgombea wetu ni kiboko ana ngozi ya tembo
   
 19. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #19
  Sep 8, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Wapo wengi tu ,ila hili halikutegemewa kwa mgombea Uraisi ,hii ni nafasi nyeti ,ndugu yangu ,naona unafananisha fenesi na shokishoki ,eti yote yana miba au !
   
 20. jaxonwaziri

  jaxonwaziri JF-Expert Member

  #20
  Sep 8, 2010
  Joined: Feb 17, 2010
  Messages: 378
  Likes Received: 54
  Trophy Points: 45
  Mnataka taifa lingie katika kilio? Mbona hamuwi wawazi kuhusu afya za wagombea wenu?
   
Loading...