Mudawote
JF-Expert Member
- Jul 10, 2013
- 11,569
- 16,027
GTs,
Hebu fikiria tu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amekemea vikali hatua ya kufungiwa kwa Kanisa la Ufufuo na Uzima inayoongozwa na Askofu Josephat Gwajima, akieleza kuwa ni ukiukwaji wa haki ya kuabudu inayolindwa na Katiba. Hebu fikiria tu akizungumza haya yote akiwa katika ziara ya kikazi jijini Dar es Salaam, Rais Dkt Samia alieleza kushangazwa na uamuzi huo wa mamlaka bila kujumuisha majadiliano ya wazi na viongozi wa dini. Rais alisisitiza kuwa serikali yake inaheshimu uhuru wa kidini na haitavumilia matumizi mabaya ya madaraka kwa kuzuia watu kushiriki ibada zao kwa misingi isiyoeleweka.
Katika hatua nyingine, Rais Dkt Samia ametengua uteuzi wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi kufuatia kushindwa kwake kushughulikia matukio ya utekwaji wa watu yanayoendelea kushika kasi nchini. Dkt. Samia alisema serikali haiwezi kufumbia macho vitendo vya kihalifu vinavyohatarisha usalama wa raia na kuvuruga amani ya nchi. Aliahidi kuchukua hatua kali kwa watendaji wote wa umma wanaoshindwa kutimiza majukumu yao ipasavyo, akisisitiza kuwa suala la utekaji halitavumiliwa na linahitaji hatua za haraka na za kimkakati kutoka kwa vyombo vya usalama.
Wadau nimewaza hivyo, je ikitokea Rais Dkt Samia kafanya hivyo CCM viherehere hawataitisha press kumsifia Rais Dkt Samia? Je wana JF tutamsifia?