Maiti zaidi za wana CHADEMA zaokotwa Igunga!

Ingawa inasikitisha wakati wowote uhai wa binadamu unapotolewa, lakini wana JF kuna umuhimu wa kutokukimbilia conclusion ambazo zinaweza kupeleka nchi kwenye machafuko.

Ukisoma hiyo habari vizuri, utaona mwandishi kaweka angalizo la Taarifa za awali...

Halafu akaja kusema watoto wa diwani ambao ni maarufu kwa ujambazi...

Tukiweka ushabiki wa vyama pembeni. Pamoja na vile mwandishi anavyopenda wasomaji wake walitazame.
Inawezekana taarifa isiwe sahihi, inawezekana ikawa imeongezwa chumvi ili ikamilishe malengo ya kisiasa au
inaweza kuwa ni tukio ambalo ni purely la uhalifu kama uhalifu mwingine wowote
. Kwani naamini ili mtu uwe
maarufu kwa ujambazi lazima utakua na historia ya matukio ya kutisha siku za nyuma.

Ni vyema chombo huru kifuatilie na kutoa taarifa iliyo kamili, kuliko vyama vya siasa kuingilia uchunguzi.


This is lazy thinking Alwatan. Funguka akilini mwako. Majambazi wanauwaga watu wasio na mali??/ What for?? Majambazi wangevamia kwenye hotel ya CHADEMA au hata ya CCM na kuiba hela za kampeni etc. BUT This is Planned Murder
 
Green guards siku ya kufa kwao lazima kila moja aliwe tigo halafu akikata roho anachomwa moto
Hapana.
tusifikirie kulipiza kisasi tutachafua nchi. hizi ni dalili kwamba hata wao wametambua their end jad just come.
wamechanganyikiwa ndio maana wanafanya mambo ya kihayawani.

tuombe Mungu wakatiliwe kila kona ya nchi
 
Dah!!!! Mauaji tena!
Nape Nnauye inabidi ahojiwe kwa ili tukio kwani kauli aliyoitoa wakati kijana mmoja akisemekana amemwagiwa tindikali wakati kampeni za uchaguzi mdogo Igunga ilikua na utata.
 
This is lazy thinking Alwatan. Funguka akilini mwako. Majambazi wanauwaga watu wasio na mali??/ What for?? Majambazi wangevamia kwenye hotel ya CHADEMA au hata ya CCM na kuiba hela za kampeni etc. BUT This is Planned Murder

With all due respect, nafkiri wewe ndio mwenye lazy thinking kwa kumezeshwa kizima kizima chochote kinachowekwa kwenye bango la JF without further analysizing the story and reading carefully, provided kina attack CCM.

Majambazi wa vijijini kwanza wanawaogopa wenye mali, wanabaki kuumizana masikini kwa masikini...

Ninachoshauri siasa iwekwe pembeni, kazi ya uchunguzi ifanywe na chombo huru kitakachotoa taarifa kamili.
 
Sasa hili si jambo la kunyamazia wachukueni watu wa haki za binadamu na viongozi wa CDM waende kusimamia hili ili wananchi wasema yote wanayoyajua pia dunia lazima ielewe na lazima lipigiwe mbiu kubwa

Kamanda! Naunga hoja mkono,magamba wamekuwa sumu kwa Watanzania wasio na hatia.
 
mm ni mwana ccm damu ila kwa tunapoelekea ........

AWAMU YA PILI YA MAITI YA MA-KADA WA CHADEMA IGUNGA:
WA-TANZANIA TUNADAI MAJIBU YA KINA, HURU, HARAKA NA WATU KUWAJIBIKA UPESI BILA MZAHA!!!


Hakuna mtu au kikundi kilichowahi kushinda vita dhidi ya Umma. Hakuna mahala ambapo wauaji hawa watakapoweza kujificha wasionekane.

Hakuna hata mfadhili mmoja wa mauaji haya ya kinyama (mtu, kundi au taasisi) itakayoteleza mbele bila damu hizi zilizotapakaa mikononi kuwaumbua mbele ya kandamnasi. Hakika hakuna atakayeweza kuitawala Tanzania kwa njia ya kumwaga damu za raia kwa sababu tu ya itikadi tofauti kichama.

Viongozi wetu wa dini zote nchini, sisi vijana tunasema mauaji haya KAMWE HAYAKUBALIKI. Enough is enough CCM. Mwenye kubahatika picha nyinginezo za hawa marehemu wetu wapia pamoja na taarifa nyinginezo muhimu atumwagie hapa tafadhali.




11th October 2011 19:26

Hata kama wauaji hawa wako juu ya sheria za nchi yetu ya Tanzania, naamini kwamba HAWAKO JUU YA SHERIA ZOTE DUNIANI. Marehemu wetu laleni kwa amani; haki yenu haitopotea hata kabla ya jua ya UTAWALA WA KISHERIA DUNIANI kuzama.

(1) CHADEMA yetu nendeni kwenye maeneo yote ya tukio Igunga,

(2) Wanaharakati rudini Igunga kwa kila kitongoji,

(3) Kaamati ya Haki za Binadamu CDM andikeni barua rasmi kwenda ICC kuelezea hofu yetu kwamba kuna wasiwasi mkubwa

(i) mauaji ya raia,
(ii) vitendo vya ubakaji,
(iii) utekaji,
(iv) uchomaji mali zinazotiliwa shaka kufanyika na KIKUNDI CHA KIGAIDI nchini kwa kile kinachoelezewa kuwa ni msaada wa taasisi nyeti za kiserikali na pia ambacho wafadhili wake hudhaniwa kuwa wamo ndani ya serikali ya sasa.

(4) Wananchi TUOMBE TAASISI HURU isiyokua na uhusiano wowote na utawala huu wa CCM kuja kuchunguza mauaji haya - FBI na Scotland Yard au ICC.

(5) Usiku ule wa 'Matokeo ya Nape' Igunga, nilipata kuwaandikieni humu kwamba HAKUNA UCHAGUZI WOWOTE ULIOFANYIKA IGUNGA kama vigezo ni 'HURU NA WA HAKI'.

Na leo nawaambieni kwamba
kuna tetesi zinazokwenda hewani hivi sasa toka Igunga kwamba kuna miili ya Wa-Tanzania, hasa waliotokea mikoa mingine kuja kulinda kura Igunga na wengine wengi wakiw ni Ma-Kada wa CHADEMA waliopolewa majumbani usiku wa kuamkia uchaguzi ule mdogo, kibao imezikwa chini ya ardhi kwenye kwenye pori kaburi la pamoja Igunga.

Hayo maafa yote yadaiwa kutokea usiku wa kuamkia uchaguzi Igunga kufuatia matangaza ya afisa mwandamizi wa Chama tawala kwenye vyombo vya habari huku wakionyesha kupinga ujio huo hivyo kuamua kupambana nayo hadi umautini. Kama ni kweli au la, hilo litakua ni jukumu la chombo huru ya uchunguzi usiotokana na serikali kutoa majibu hayo.

Vile vile vyanzo hivyo vitakavyohitajika kupewa ulinzi wa kisheria huko Igunga vinaelezea kwamba huo hasa ndio sababu kubwa ya mambo mazito yaliotokea usiku huo ndio uliochangia watu wengi mno kutokuonekana vituoni siku ya siku watu kupiga kura.

Wakati kunaelezwa kwamba idadi ya waliojiandikisha kupiga kura Igunga ni 171,000, ni wati chini ya 60,000 tu ndio wanaosadikiwa kushiriki uchaguzi huo; tafakari!!!!!!!

Japo uchaguzi Igunga haujamridhisha hata Dr Kafumu mwenyewe na Damu hizi zote mikononi mwake na Wa-Tanzania kumlilia na chama chake, ishara ya alama hizi ni za hatari zaidi ZISIZOWEZA KUACHIWA KWENDA HIVI HIVI na taswira zake hasa tukielekea uchaguzi mkuu 2015.

Wa-Tanzania TUNATAKA MAJIBU YA KINA TENA YA HARAKA ZAIDI ZENYE HAKI NA MIKONO HURU.
 
Duh,kama ndo hivi basi alo onekana na bastola Igunga atakua kaua wengi sana
 
Ndugu zangu Wa-Tanzania ambao kura zetu hzikutuendea sawasawa na matarajio yetu hapo mwaka jana na tena majuzi tu Igunga,

Pindi tu unapoona chombo chochote kinachoitwa SERIKALI, hata kama hakina uhalali wa kupata kuitwa hivo, pale kinapoonekana na kuanza kutiliwa shaka na waongozwa wake kwamba
ndicho hasa kinachohusika na UMWAGAJI WA DAMU ZA NDUNGU ZAO NA KUZALISHA MI-YATIMA KIBAO, chombo hicho mpaka hapo, kwa watu wenye akili wanajua fika kwamba anguko laki si mbali hata kidogo, ni swala la muda tu sehemu kubwa ya wafwasi wake kuanza kukitoka mmoja baada ya mwingine mara baada ya wenginewao kuamua kugeuka wauaji.

Hili nalo haliko mbali sana hapa nchini mwetu.
 
Me mwenyewe nilinusulika..Nilikuwa kijiji cha Bulumbela kata ya Ziba na hao vjana wakawa wanaongea na viongoz wao huku wananinyooshea vdole.Na waliningea sana hata hvyo walikuwa wananiogopa coz walidhan me ni komando coz kuna cku niliwacha magamba na polic bila woga so wakaanza kuniita komando kwan m2 wa kawaida hawezsema hvyo.Pil kombat yangu mimi umekaa kijesh zaid so hlo lilifanya niogopwe ila nilikuwa nawindwa sana...Mungu azilaze roho za marehem pema.
 
Jambo hili halivumiliki tena na halina tena subira, naomba mwongozi wa viongozi wangu wakuu wa CDM maana hawa ni wanachama wenzetu wameuawa na hili lisipopata makaripio makali yataendelea na yatatuathiri. Ee Mungu utusaidie
 
Siku za mwisho za kitu chochote zinadhihirika kwa staili mbalimbali, ccm kwisha habari
 
Nahisi watu wengi wamepotezwa kwny uchaguzi wa igunga! Mtunza mochware wa hosptl ya wilaya atakuwa na siri nzito CHADEMA MNALO JUKUM LA KUFUNUA UKWELI
 
Maiti za wanawake wawili zimeokotwa jana katika msitu wa kijiji cha Ulaya, Kata ya Nkinga wilayani Igunga zikiwa zimeharibika vibaya.

Wakati uchunguzi unaendelea, taarifa za awali zinaeleza kuwa mmoja wao ambaye ni mama wa makamo, anajulikana kuwa ni shabiki mkubwa wa Chadema na Mhamasishaji maarufu mwenye ushawishi wa kisiasa, alikuwepo siku Helikopta ya CHADEMA ilipotua Nkinga na Mwenyekiti Freeman Mbowe kwa ajili ya kampeni siku ya J'4 kabla J'2 ya uchaguzi, Baada kumalizika mkutano huo muda wa jioni sana, mama huyo alikuwa akirudi kijijini kwake, lakini kuna kikundi cha vijana wa makambi wa CCM walionekana wakimfuatilia, wakiwemo watoto wawili wa Diwani wa kata hiyo ambao ni maarufu kwa ujambazi lakini mara zote wanakingiwa kifua na baba yao kwa wadhifa wake wa udiwani, mama huyo hakuonekana tena hadi maiti yake ilipookotwa jana msituni ikiwa bila nguo (zimetundikwa juu ya mti) na imeharibika vibaya na kuliwa na wadudu.

Upande wa pili wa barabara alipookotwa mama huyo kulikutwa maiti nyingine ya mwanamke mwingine aliyeuawa kwa staili ileile na kuachwa bila nguo, ila kutokana na kiwango cha kuharibika kwake inaelekea aliuawa siku tofauti na kuja kutupwa hapo, pembeni yake wauaji hao waliweka kitambulisho cha mtu wanaetaka ahusishwe na mauaji hayo, dalili zote zinaonesha wauaji ni walewale, inasemekana mwanamke huyo ametokea kata jirani ya Ndembezi.

Polisi zaidi ya kuchukua maiti hizo kwa pamoja na kuondoka nazo haijasema lolote, jitahada kubwa zinafanywa kulifunika suala hili liishe kimyakimya lisije likaleta kashfa kubwa ya mauaji kwa chama tawala, baada ya Nape Nauye kuahidi kuwa watafanya hivyo na wasilaumiwe kwa kuwa kuna kijana wao amemwagiwa tindikali.

Inaelekea kuna maiti nyingi zaidi hazijapatikana maporini na nyingine zimefukiwa huku ndugu zao wakidhani wamesafiri au wako kwenye mihangaiko, lakini kwa kuwa La Kuvunda Halina Ubani, basi kitaeleweka tu!

Acha uchochezi, hivi wanachadema hawafahamiani kama mtu alipotea kwa nini taarifa haikutolewa polisi na wewe kama uliona vijana wa CCM wanamfuatilia huyo mwanamke kwa nini hufanya Polisi Jamii kwa kutoa taarifa Polisi ili waokoe maisha ya mwanamke huyo. Watu wakigombana au kuuana kwa wivu wa mapenzi kama waliachana unahamishia mauaji hayo kwa CCM. Post thread za MSINGI.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom