Kada wa CHADEMA akutwa amefariki Igunga!

Kada wa CHADEMA akutwa amefariki Igunga!

Ni simanzi kubwa; Wa-Tanzania sasa tutambue kwamba mauaji ya kisiasa yamefika katika nchi ya Mwalimu Nyerere ambako mambo kama haya yalikua ni ndoto kubwa.

Wa-Tanzania, huo hapo chini ni mwili wa marehemu Ustaadh Masoud Mbwana pale alipoonekana akiwa mfu tangu watu wanaosadikiwa kuwa ni MAAFISA USALAMA wa CCM walipomdaka mbele ya watu wengi hadharani akiwa hai, ndugu huyu hakuonekana tena wala kuweza kutekeleza azma yake ya kulinda kura za chama chake CHADEMA kama ambavyo alivyoinuia kufanya huko Igunga. Kifo cha huyu Kada wa CHADEMA inajulikana wazi takriba wiki moja tangu ratiba ya uchaguzi Igunga ikamilike lakini bila uchaguzi.

Ni vema CHADEMA kikatafuta msaada wa Scotland Yard ya Uingereza kuja kufanya uchunguzi juu ya mauaji haya ya kutisha kisiasa na mwili ule kufukuliwa upya. Taasisi hiyo ya Uingereza au FBI ya Marekani wanao uwezo mkubwa wa kuweza kutumia Satelite picture (ambazo CCM hawana uwezo kuzibadilisha) hata wakanasa mienendo mizima sekunde kwa sekunde mpaka kukaungwa mkanda wa kutisha juu ya mauaji hayo, wahusika wake, utekelezaji na kutupa dira zaidi huku tuendko ili haki itendeke kwa marehemu na familia yake. Kazi ianze mara moja bila kulaza damu.

Pumzika kwa amani!!!!!!!!!!!


11th October 2011 19:26

nawashangaa humu nyote siwaelewi mtu aliye mwagiwa tindikali mna sema CCM lolote baya mnasema ccm tuache huu unafiki. Sasa hili laleo mna sema CCM, kama si unafiki mnauendeleza.

Nini tuwe wakweli penye ukweli tuwe wakweli. Huyu mtu katoka dar es salaam mpaka tabora igunga. Chama kilichompeleka kama wakala ndicho kimehusika na mauaji ya kijana wetu ndugu yetu kwa maslahi ya chama chao kwani wao hawaoni shida kupoteza mtu kwa maslahi ya chama.

Kwani igunga kulikuwa hakuna mawakala. Inaonesha dhahiri chama hicho kisivyo waamini raia waeneo husika la uchaguzi. Lazima viongozi chama hicho wawajibishwe kwani ndio wamesababisha kifo cha marehemu mbwana.

Taarifa rasmi inaeleza kuwa Marehemu Mbwana Masoud, aliekuwa Wakala wa CDM kutokea Ubungo DSM, alipotea tar 2/10/2011, siku ya uchaguzi, lakini ukweli ni kuwa siku hiyo ndiyo ilipogundulika kuwa amepotea baada kuhitajika kupelekwa kituoni kwake na kukosekana.

Hali halisi ni kuwa Mbwana Masoud usiku wa tar 1/10/2011 (Mkesha wa kuamkia siku ya uchaguzi) baada ya kula chakula cha jioni alitoka kunyoosha miguu, ingawa palitolewa Hali ya tahadhari lakini hali ilionekana iko shwari.

Kumbe kulikuwa na kundi la mabaunsa wanne wa CCM wakimfuatilia, na inaelekea walikuwa wakiwasiliana kwa simu na gari lao, kwani mara walipomvamia, tena mbele za watu, gari hilo aina ya L/Cruiser Hardtop jeupe lenye namba T***ARD, mali ya CCM, Mara nyingi katika kipindi cha kampeni hizi lilikuwa likitoka usiku na mchana huwa linapaki, dereva wake ni yule alieshiriki kuwapiga mabapa ya mapanga wana CDM waliokuwa wakidai matokeo ya uchaguzi yatangazwe.

Ingawa Mbwana alijitahidi kujitetea asichukuliwe lakini alizidiwa nguvu, alijaribu kupiga kelele kuomba msaada lakini alipigwa kabari ya nguvu, kabla ya watu waliokuwa karibu hawajajua la kufanya (kwani tukio lenyewe lilifanywa kwa kasi, pia walijifanya kama ni watu wanaofahamiana ila wana mzozo fulani) walimtia kwenye gari Hilo na kuondoka nae kwa kasi kuelekea upande wa Mwanzugi.

Mafedhuli hao wa CCM, Mateso waliyomtesa Mbwana Masoud kabla ya kumtoa roho ni Mungu na wao wenyewe ndio wanajua, lakini kwa jinsi Hali ya maiti yake ilivyokutwa baada ya kutupwa kwenye vichaka karibu na Magereza siku ya tar 9/10/2011 inaonesha dhahiri unyama aliofanyiwa hata huko Somalia walikozoea kuuana hakuna unyama wa aina hii.

Alikutwa na suruali tupu bila shati, SHINGO YAKE ILIKUWA IMEVUNJWA KWA NGUVU, MACHO YAKE YAMETOBOLEWA NA HAYAONEKANI, KICHWA CHAKE KIMEPASULIWA KWA NYUMA CHINI YA KISOGO, KIFUA CHAKE KIMEBABUKA KAMA VILE AMEMWAGIWA AINA FULANI YA TINDIKALI, mwili wake unaonesha alipigwa sana kabla kuuawa kinyama.

Kilichotushangaza ni kuwa mwili huo uliotupwa hapo unaonesha dhahiri hakuuliwa siku hiyo ya tar 9/10, lakini haukuwa umevimba Kama kawaida bali ulikuwa unaonesha dhahiri kuwa ulitiwa dawa ya kuhifadhia maiti, kwa vyovyote vile wauaji wake hawakuwa majambazi wa kawaida wa mtaani ambao huua na kuishia zao, bali ameuliwa na Organization kamili yenye motive ya kuua wakala wa CDM.

Ikumbukwe kwamba Serkali ya CCM awali ilitangaza kukataza mawakala kutoka nje ya jimbo, baada Wakili Tundu Lisu kwenda kumfundisha sheria Msimamizi wa Uchaguzi Igunga, ndipo wakaruhusiwa kwa shingo upande, lakini njiani walisumbuliwa sana na maaskari kwa maelekezo ya wakubwa w CCM.

Alitekwa ili kuwatisha mawakala wengine waogope kuwajibika, uongozi wa CDM ulitumia busara kutopiga kelele na badala yake kwenda kutoa taarifa Polisi kimyakimya, ingawa Polisi yenyewe haikuchukua hatua yoyote ya msako, mawakala w CDM waliwajibika vilivyo vituoni na hakuna kura iliyoibiwa.

Ikabidi Serkali iisaidie CCM ishinde kwa nguvu kwa kuwazuia maelfu ya Vijana waliofika vituoni kupiga kura ingawa walipoteza shahada zao, kwa kujaza form No 17, mwanzo waliwaruhusu kupiga kura Kama sheria inavyotaka, lakini walipoona wanazidi kuwa wengi, ilipofika saa 4 asubuhi Mkurugenzi aliagiza wasiruhusiwe kupiga kura, wakafukuzwa, wengine hawakukuta majina yao kwenye daftari, wengine walikataliwa kupiga kura kwa kuwa waliorodheshwa kuwa wamekufa!

Just imagine unaenda kituoni na shahada yako kupiga kura unazuiwa usipige kwa sababu wewe umeshakufa! Haya pamoja na kutumia vibaya mahindi ya msaada kama Rushwa siku moja kabla uchaguzi, na kampeni potofu siku ya uchaguzi kuwa mgombea wa CDM amejitoa kwa hiyo haina haja kumpigia kura, ndiyo yalichangia ushindi kiduchu wa CCM.

Nirudi kwenye mada ya msingi ya mauaji, nisameheni najichanganya kwani Nina machungu mengi, Maiti ya Mbwana Masoud ilipookotwa, ilikutwa na kipande cha karatasi ambacho wauaji walitaka iaminike kuwa marehemu aliiandika baada ya kuuawa akitaja majina ya waliomuua, Polisi waliipuuza karatasi hiyo ingawa bado wanaishikilia, inazidi tu kuthibitisha kuwa wauaji wamejaribi kuficha kitendo chao na hivyo kukamilisha misingi ya First Degree Murder!

CCM Arusha iliua kwa kutumia Polisi wa serkali yake, lakini Igunga CCM imeua kwa kutumia Mungiki wake iliowalipa na kutumia gari lake, gharama zitokanazo na kodi zetu, Masoud akiwemo.

Salaam kwenu enyi Wauaji CCM, mnahubiri Amani na Utulivu majukwaani lakini Mikono yenu imetapakaa Damu ya wasio na Hatia, hakuna waliofanya hivyo wakafanikiwa mafanikio ya kudumu, mmepata Spasmodic Victory lakini Hakika mtaSuffer Eternal, Shameful Defeat!

Enyi wauaji CCM, Salaam kwenu kutoka kwa maelfu ya vijana wa Igunga waliodhulumiwa haki Yao ya kupiga kura kwa makusudi, Tunawaambia, Sukilizeni Vizuri enyi Mafedhuli, Haki itatendeka Igunga, however long it might take, lakini HAKI LAZIMA ITATENDEKA TU!

Tunajua hamuamini Mungu Enyi Wauaji na Wazinzi wa Wake za Watu, lakini Mungu alishasema " HAKI IKIDHIHIRI, BATILI HUJITENGA, HAKIKA BATILI NDIO HUJITENGA!" Kama mnajidai hamumuamini wala kumuogopa Mungu basi Hakika Mtakumbana na Nguvu za Umma ambazo ni Kubwa kuliko nguvu za Dola!

Umma wa Igunga una Hasira na Nyie Mafedhuli wakubwa, mnajua, Mbona hamkusherehekea vilivyo ushindi wenu hapa Igunga? Mlilipua fastafasta mkaenda kusherehekea Singida na Dar ambako mlifanya sherehe kubwa na maandamano ya kumpokea Mbunge wenu wa huko mliekuja kumtengenezea Igunga.
 
Mungu akulaani, hujafa hujaumbika.....wewe huoni huruma binadamu kufa tena kwa mateso makali"....DC mkafanya siasa za udini? Mke wa ustaadhi Rajab kutiwa pande zote na Mchemba mkaa kimya, nasasa mtu ameuliwa (kwa kukataa kushiriki uchakachuzi) kimya......ubinadamu wenu uko wapi...j.

jamaa nitakushanga sana kama yaDC wamefanya ccm wenyewe kumvuta nguo yake na ilikuwa hakuna haja ya ccm kumsumbua ndugu yao kama mnavyo sema ccm imefanya yenyewe yani imetumia kivuli chake basi hata hicho chama kilichompeleka huyo kijana igunga kimempotezea maisha ndugu yetu kama kafara. Mungu ailaze roho yako marehemu mahala pema peponi amin. Kwani ulienda bila yakutambua kuwa kama utapoteza maisha kwa kuwanufaisha hao kisiasa nawe utakufa nahatimae hutokuwa nathamani kwao ndipo vijana wengi wanaingia kwenye mitego kama hii ya kijana mbwana mungu amlaze mahala pema. Wanapigania jambo wasilolijuwa wao wakidhani wanatetea nchi na wananchi na haki. La kumbe wanapigania maslahi ya watu binafsi. Tena maslahi ya akina freeman son haya ni hatari sana freemanson hawa hawaoni hasara ya kumwaga damu ya mtu mbele ya maslahi ndivyo walivyo akina bush walker na akina mahafidhina wa uingeraza. we unae tetea uovu kwa misingi ya kuwapa watu makosa wasiosika umepotea
 
Ni kawaida ya hiki chama cha majambazi,hatua stahiki zichukuliwe haraka bila upendeleo.......
 
Ni simanzi kubwa; Wa-Tanzania sasa tutambue kwamba mauaji ya kisiasa yamefika katika nchi ya Mwalimu Nyerere ambako mambo kama haya yalikua ni ndoto kubwa.

Wa-Tanzania, huo hapo chini ni mwili wa marehemu Ustaadh Masoud Mbwana pale alipoonekana akiwa mfu tangu watu wanaosadikiwa kuwa ni MAAFISA USALAMA wa CCM walipomdaka mbele ya watu wengi hadharani akiwa hai, ndugu huyu hakuonekana tena wala kuweza kutekeleza azma yake ya kulinda kura za chama chake CHADEMA kama ambavyo alivyoinuia kufanya huko Igunga. Kifo cha huyu Kada wa CHADEMA inajulikana wazi takriba wiki moja tangu ratiba ya uchaguzi Igunga ikamilike lakini bila uchaguzi.

Ni vema CHADEMA kikatafuta msaada wa Scotland Yard ya Uingereza kuja kufanya uchunguzi juu ya mauaji haya ya kutisha kisiasa na mwili ule kufukuliwa upya. Taasisi hiyo ya Uingereza au FBI ya Marekani wanao uwezo mkubwa wa kuweza kutumia Satelite picture (ambazo CCM hawana uwezo kuzibadilisha) hata wakanasa mienendo mizima sekunde kwa sekunde mpaka kukaungwa mkanda wa kutisha juu ya mauaji hayo, wahusika wake, utekelezaji na kutupa dira zaidi huku tuendko ili haki itendeke kwa marehemu na familia yake. Kazi ianze mara moja bila kulaza damu.

Pumzika kwa amani!!!!!!!!!!!


11th October 2011 19:26

nimekuelewa kwa hali ilivyo unavyoona haya ndo mauaji pekee hayo ya arusha na igunga yana yofanywa na usemavyo wewe ni ccm ndo wanauwa.leo hii ndo mnayaona mauaji hayo uliyo yataja inadhi hirisha jinsi ulivyokuwa huna ukweli kuna unafiki ndani ya moyo wako hufai. Mungu awalaze mahala pema wote waliofikwa na umauti wakitetea haki kwa moyo kuanzia chaguzi zote zilizo shirikisha vyama vingi. Kama ni hivyo vifo vya wapemba wa unguja, dar es salaam, arusha vifo hivi ni vya maksudi na vya silaha za moto, kuna vifo kama cha igunga huu mtindo huu mpya.na hatuwezi sema kwa hakika mtu fulani kahusika. Na kuna vifo vya viongozi kama kolimba, kighoma ali malima vifo vyao vya njama na kisayansi vina siri . Na kifo cha miaka ya karibuni cha mh chacha wangwe hawa vifo vyao vya kupangwa kutokana na kusema ukweli nakutaka haki ya kweli ktk jamii watu wakweli hawadumu mungu azilaze roho zao mahala pema. Waliobaki wengi wao ni wanafiki na pia kuendekeza maslahi binafsi ama maslahi ya kundi fulani ndio siasa zilivyo sasa hatuamini na vijana wengi wanatumiwa pasina kuelewa nini wanacho kipigania. Nikweli vijana wenzangu niwasomi bahati mbaya mtazamo wawengi ni one side. Hufuata bendera leo kikitokea chama kingine chenye kuleta matumaini hewa basi watafuata bila kipimo ndio mtindo uliopo tunakurupuka na papara hali hii inajidhihirisha hata ktk shughuli za kimaisha watu wengi navijana wasasa wanataka utajiri waharaka ndipo utaona kama anafanya kazi kampuni yoyote atahakikisha anafanya udanganyifu ilimradi afanye uhalifu nakupata anachokitaka. Kama ni benki ataibia wateja. Hii ndo hali tulionayo chini mpaka juu. Fisadilazition. Imetawala tena wizi wakupora. Watu wana kurupuka hii itatugharimu sana mbali na itikadi zetu. So ndomana imekuwa nirahisi na kawaida sasa kusikia vifo hivi kama cha igunga sema ili limetokea kwenye kivuli cha siasa. Mungu alaze roho ya marehemu mahala pema
 
CHADEMA TUTAFUTE MSADA WA UCHUNGUZI WA KITAALAM ZAIDI TOKA SCOTLAND YARD YA UINGEREZA AU FBI YA MAREKANI KUTOA MAJIBU JUU YA MAUAJI YA NDUGU MASOUD MMBWANA IGUNGA

umma wa Tanzania umepigwa butwaa na kazi ya vijana wa Nape Nnauye, GREENGUARD MUNGIKI, na mauaji ya kinyama ambayo haijawahi kufikiriwa nchini.

Mpaka hapa, kwa kuwa ushahidi wa mazingira unaashiria kwamba mtuhumiwa wetu ni CCM, serikali yake na vyombo vyake, basi tangia hapo penye nukta ya kutiliwa shaka ni wazi kwamba CCM na vyombo vyake vya ulinzi tayari vinapoteza sifa za kuchunguza au kudai kuchunguza chochote kuhusiana na kifo wa kada wa CHADEMA huko Igunga.

Taasisi huru ya uchunguzi ni muhimu sasa hivi ili Wa-Tanzania tujue ukweli wote. Lakni, wakati tukisubiri hayo yote hebu tutafakari mambo haya:

1. Je, ni kitu gani kilipoozesha ghafla utangazaji wa Matokeo Igunga,

2. Kulikua na udharura wa aina gani uliomfanya January Makamba, MWENYEKITI WA KAMATI YA USALAMA CCM, kuzungumza yale aliyoyazungumza dhidi ya ujio wa mawakala kutoka nje ya jimbo la uchaguzi Igunga na kule CHADEMA kuchukua uamuzi wa kuleta mawakala wapya dakika za majeruhi, ikiwa ni pamoja na ujio wa marehemu Maasoud Mmbwana, kukaonekana TISHIO kwa huyo afisa mwandamizi wa usalama CCM?

3. Je, ule ugeni wa UVCCM kwenda makao makuu CHADEMA siku chache zilizopita ulisukumwa na nini nyuma ya pazia???????? Ni ujembe gani waliuwashilisha CDM na ni upi huo amba huenda walishindwa kuwashilisha kwa viongozi wetu???????????

4. Ni kitu gani kilichoifanya BAKWATA kunyweya ghafla Igunga mara baada kudandia sakata la Bi Fatuma Joseph Kimario ambaye pia ni DC wa Igunga????

5. Hiyo story ya gari 'jeupe', 'hardtop' iliombeba Masoud kwa safari yake ya mwisho kwenda ahera, mbona maelezo yake hayatofautiani sana na yale maelezo ya Mhe Dr Harrison Mwakyembe na yale magari ya akina 'Master' na ugeni wao wa Al-Shaabab????????

Tafakari, sana!!!!!!!!!!!!
 
Hili jambo linakuzwa mno. Gazeti la Rostam la MTANZANIA leo limeiandika habari hii kwa "mbwembwe" ili ionekane ameuawa na CCM. Gazeti la CHADEMA ambalo ni TANZANIA DAIMA lenye uhusiano na EL na RA nalo limetoka na habari kuhusu Benno Malisa akimshutumu NAPE. Ni kampeni na propaganda zinazopikwa. Tunafahamu namna baadhi ya waandishi wa habari wa magazeti haya wakiwemo baadhi ya wahariri wao walivyowekwa mfukoni na akina EL na RA. Ikumbukwe hakuna mahali popote duniani mafisadi na majambazi walishinda vita. Wanaweza wakashinda kwa muda lakini mwishowe haki hutendeka.
 
Nimekosa la kusema kwa hali hii tuelekeako ni Mungu pekee mwenye majibu na wala sio sisi wanadamu. Pumzika kwa amani ndugu damu yako iwahukumu wale wote waliohusika.!
 
mkuu jitahidi urudi haraka!
kwani kuna watu walikuwa gerezani? nahuyo mtu wamejuaje kama alikuwa wakala wa chadema mkuu?
dah mambo magumu sana!

Nilivyomuelewa mleta habari hajamaanisha kuwa marehemu alikuwa jela, au mahabusu. Anasema alitoweka kwa maana ya kuwa alikuwa hajulikani alipo mpaka mwili wake ulipokutwa katika msiku unaojulikana kwa jina la pori la magereza. Tofauti kidogo, ponti ya msingi hapa ni ilikuwaje taarifa za kupotea kwa wakala huyo hazikutangazwa sana?
 
Hili jambo linakuzwa mno. Gazeti la Rostam la MTANZANIA leo limeiandika habari hii kwa "mbwembwe" ili ionekane ameuawa na CCM. Gazeti la CHADEMA ambalo ni TANZANIA DAIMA lenye uhusiano na EL na RA nalo limetoka na habari kuhusu Benno Malisa akimshutumu NAPE. Ni kampeni na propaganda zinazopikwa. Tunafahamu namna baadhi ya waandishi wa habari wa magazeti haya wakiwemo baadhi ya wahariri wao walivyowekwa mfukoni na akina EL na RA. Ikumbukwe hakuna mahali popote duniani mafisadi na majambazi walishinda vita. Wanaweza wakashinda kwa muda lakini mwishowe haki hutendeka.
Nini? Inakuzwa!! Hii ni habari ndogo? Unawatafutia watu ban humu,kama 1954 ndio mwaka uliozaliwa una miaka 57! Miaka 57 kwa upupu kama huu ni aibu kwako na familia yako! Huna utu wala maadili na pengine kwako ni jambo dogo sana! we ndo hao Mungiki nini? Hujali damu hii isiyo na hatia! Unajua impact ya mauaji ya kisiasa kwa nchi mpuuzi wewe!
 
Hata ile percent ndogo niliyokuwanayo kwa CCM sasa imenitoka CCM ni wauwaji wakubwa mateso waliyompatia kijana huyu hadi mauti yake hakika damu yake itakuwa juu ya viongozi wote wajuu wa CCM nao watakufa kwa mateso ikiwezekana zaidi ya haya Mungu na atimize, anayesadiki na aseme Amina.
 
nawashangaa humu nyote siwaelewi mtu aliye mwagiwa tindikali mna sema CCM lolote baya mnasema ccm tuache huu unafiki. Sasa hili laleo mna sema CCM, kama si unafiki mnauendeleza. Nini tuwe wakweli penye ukweli tuwe wakweli. Huyu mtu katoka dar es salaam mpaka tabora igunga. Chama kilichompeleka kama wakala ndicho kimehusika na mauaji ya kijana wetu ndugu yetu kwa maslahi ya chama chao kwani wao hawaoni shida kupoteza mtu kwa maslahi ya chama. Kwani igunga kulikuwa hakuna mawakala. Inaonesha dhahiri chama hicho kisivyo waamini raia waeneo husika la uchaguzi. Lazima viongozi chama hicho wawajibishwe kwani ndio wamesababisha kifo cha marehemu mbwana.

Kwahiyo kama CDM hawawaamini watu wa Igunga ndio sababu wamtoe mtu innocently kutoka Temeke wampeleke Igunga wakamwue? What's the motive? Mbona watu wanakuwa na akili ndogo hivi? Hivi TOT nao wanatoka Igunga? Na Green Guard nao wanatoka Igunga? Your hands are tainted with blood. Shame on you! Hili hamtaweza kulikwepa. Malipo ni hapa hapa duniani.

http://youtu.be/uERcp_9Obzc

CCM imeua, inaua na itaendelea kuua kwa maslahi ya mafisadi wachache. CCM inang'ang'ania kukaa madarakani kwa gharama yoyote ile. Na haya ndio matokeo yake.
 
Very sad.Kama ni kweli wengi watawajibishwa.

hakuna atakaye wajibishwa hapo, waliotenda wametenda na malengo yao wametimiza, cha msingi ni kuomba Mungu aiongezee ujasiri ktk iki kigumu familia ya marehemu
 
mbaya sana madaraka ya kupatikana kwa njia hii yana laana,,,,hakika mungu atawaadhibu waliohusika na malipo ni hapahapa duniana,ukiuwa kwa upanga na wewe utakufa kwa upanga
 
Najali saana maisha ya binaadamu.
Hata hivyo huyu inaonekana ameponzwa na kimbelembele na umbumbumbu wa kutojua ufedhuli na usanii wa CDM.
Aliponzwa na uhuni wa chama chake. Nawahurumia ndugu zake manake watafanyiwa usanii wa ki-magwanda huku wakiwa mamempoteza mtu wao.

Mungu akirehemu kiumbe chake.

Wewe mi nshasema wewe na we ni Chakla,
 
Kama JK jana tu amewaachia huru wauaji (convicted before the court of law) wa Imran Kombe (FYI the murder was political motivated). Hivi mnafikiri JK atapata wapi moral authority ya ku-insitute uchuguzi huru wa Kijana Masoud Mbwana. This was a deliberately killing to send a clear message to others kwamba if you will dare to stand to our election victory we are going to murder you with impunity. Hence kuwatisha vijana wasiendelee kujitolea tena kuwa wakala wa CDM.

CCM and JK they are mumiani, wataua na wataendelea kuua, kwasababu CCM USHINDI WAO NI LAZIMA, CDM lazima hili mlisema kwa nguvu zote ili dunia ijue u-mafia wa CCM.
 
Uchunguzi unaweza usifanyike, ikaonekana wameshinda kwa sasa. Ila ikumbukwe damu ya mwanadamu haimwagwi bure. They will pay for it the evil they have done for Masoud and his family.
 
Back
Top Bottom