Maiti yageuka ng'ombe Tanzania

Mpita Njia

JF-Expert Member
Mar 3, 2008
6,998
1,156
Ni kweli hiyo habari ipo lakini ni ngumu sana kuamini. Inachosema, kwa ufupi, ni kuwa mwiliw a Bi Jamida Lucas (27) mkazi wa kijiji cha Igundu wilayani Bunda uligeuka imbo na kuwa na sura ya ng'ombe muda mfupi baada ya kufariki.
Pia, pamoja na kugeuka sura na kuwa kama ng'ombe, mwili huo ulivimba sana jambo lililowafanya ndugu na waombolezaji wautoe ndani na kuuweka nje kwa hofu kuwa unaweza kuvimba zaidi na kushindwa kupita mlango wakatakapokwenda kuzika.

Baadaye ukiwa nje, mwili uliendelea kuvimba huku viungo vingine vikibadilika pia na kuanza kutoa kinyesi cha ngombe...

Nasema ni vigumu sana kuamini habari kama hizi
 

Sabry001

JF-Expert Member
Jun 28, 2011
1,064
353
Buji bhana...! Kilichokushinda kuicopy nini wakati unajua wengne 2na aleji na magazeti km hayo...eti majira! Mwee!
 

Crashwise

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
22,228
8,722
Kawaida siamini ushirikina, lakini kwa hili nafikiria upya!
teh teh...nenda usukumani kunakijiji ukijidaunajua mvua itakuwa inanyesha kwako tu au ulipo, na ukitaka kupika chakula hakiivi au unajikuta unatandikwa fimbo na mtu ambae humuoni...acha mkuu haya mambo yapo ukikataa kuwa haya po basi wewe mbishi tu...
 

Ngambo Ngali

JF-Expert Member
Apr 17, 2009
3,518
1,336
Nasema ni vigumu sana kuamini habari kama hizi

Ningekuwa editor hii habari ingeishia kwenye dustbin. Lakini shauri editors wanapenda sensational newsilimagazeti yauzwe inabidi ipate nafasi tu.

Hadithi kama hii ilitakiwa kuwa angalau na muunganiko wa daktari wa wilaya bunda ambaye angekuwa scientific zaidi kuelezea scientific reason ya kitu kama hicho kutokea kama kweli kilikuwepo.

Labda tuchukue fursa hii kuwakumbusha wahariri kuwa kazi kubwa ya magazeti ni kueleimisha na kutoa habari na katika hilo tutegemee kuwa wakati wa postmoterm leo lazima waliambiana kuwa kuwe na habari ya muendelezo kuhusu habari hiyo na sio kuacha habari hii inaishia kwenye gazeti la leo.

Endapo habari ya muendelezo haitakuwepo basikuna hatari kubwa ya waliosoma leo wabaki na dhana kuwa mtu akifa anaweza kubadilika na kuwa ng'ombe kitu ambacho hakijawa proved scientifically.
 

Kapwani

JF-Expert Member
Nov 17, 2009
672
109
kwa tunaotoka Kilombero hatupati tabu kuelewa jambo hili....baadhi ya koo fulani fulani tukiwa katika misiba yao basi mazishi huarakishwa ili kupesha maiti kugeuka simba, chatu nk........tena utasikia wanasema duuh ameshaanza kugeuka humo ndani anaota kwato basi mtakimbizwa makaburini haraka sana......koo hizo naomba nizihifadhi kwa sasa ila zipo Kilombero na huleta mitafaruku yenye sura hiyo misibani, ili kuepusha hayo basi madawa ya kienyeji huwa yanatumika kuchelewesha maiti kugeuka na wakati mwingine inabidi maiti izikwe na kipande cha ngozi ya mnyama fulani kwenye paji la uso ili hata akigeuka hapo baadae (baada ya mazishi) asiwe na madhara......ninachooamini mpuuzi ibilisi anaweza kufanya jambo lolote ku justify uwezo wake kwa wanaomwamini na kumtii kwani yeye ni mwongo toka mwanzo wala kweli haimo ndani mwake

mix with yours
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom