Mambo mremboKweli... japo me sio "bro" kiongozi
KabisaFunguka zaidi mkuu, magumu huya pitii peke yako.
mbeya ulisoma lufilyo,rungwe sec au mwakaleli mzee wanguSEHEMU YA SITA (6)
Tulipoishia…
Kipindi hicho matokeo walikua wanaandika majina kama sikosei (mtanirekebisha kama nimekosea) . So yule mtoto wa aunt alikua anajua namba ya shule ya BK SEC, nakumbuka ilikua S.0307/….. ndo namba ya mwanafunzi inafuata.
Nilipokea simu ya aunt na alikua akinipa taarifa za matokeo yangu
Tunaendelea…
Aunt alianza kwa kunisalimia “Hujambo” Mimi: Sijambo shikamoo aunt
Aunt: Nasikia matokeo yametoka
Mimi: (Kwa unyonge sana)ndio nimesikia
Aunt: Hongera mwanangu umefaulu
Baada ya hii kauli nilinyanyuka kitandani kwanza nikaweka bible pembeni,
Mimi: Umejuaje na nimepataje aunt
Aunt: una three (3) ya 24
Mimi: Asante Mungu…
Maongezi mengine yaliendelea pale na aunt na baada ya kunipongeza nilikata simu nikatoka nje speed kwenda kwa rafiki yangu.
Chaaap hao internet cafe… V alipata 3 ya 24 kama mimi na yule rafiki yetu mwimgine alipata 4 ya 26 ila combination zilibalance
Nilipokea simu kadhaa za hongera kutoka kwa Aunt wa Dar, Baba, Bro na wengineo wengi maana tayari hawakua na imani na mimi. Kwa upande wa marafiki zangu Mwanza kule hakuna hata mmoja aliyepata Div 1-3. Wengi walipata 4 wengine walipiga zero.
Nilimshukuru Mungu sana na nikakumbuka kauli ya V kuwa tukaze humu humu Arts.
Wakati nasubiri selection za shule, aunt alinipeleka kijijini kuna shule inaitwa KADEA, nilienda kufanya interview ya kujiunga na kidato cha 5. Na baada ya kuona matokeo yangu walisema nimechaguliwa kujiunga na shule hiyo.
Kwakweli sikutaka kabisa kusoma Bukoba tena, nilikua sijui naonaje mbaya zaidi nikasome bush… Noooh, nilijiambia mwenyewe.
Aunt bado hakunipa ruhusa kurudi Mwanza hivyo niliendelea kukaa pale pale kwake na maisha yaliendelea.
Selection zilitoka na nilipangiwa shule moja iko Mbeya Tukuyu huko ndani ndani (Sitoitaja jina). Sasa changamoto ikawa ni kumshawishi aunt niende Mbeya na sio Bukoba hapo.
Niliwasiliana na bro wa tabora boys, then yule bro mtoto wa aunt wa UDSM. Nikawapanga kabisaa wamwambie aunt faida za kusoma advance shule za serikali.
Maelezo yangu yalijificha kwenye sababu ya mikopo ya chuo. Kwamba nikisoma private chuo sitopata mkopo. Pia tulifuatilia ufaulu wa shule ya mbeya na hiyo KADEA ikaonekana ile shule ya Mbeya wanafaulu sana.
Baada ya siku kadhaa aunt alikubali na mchakato ukaanza. Form 5 nilichaguliwa mchepuo wa HGK.
Wakati wote niliokaa bukoba, nilikua nikipata nafasi naenda kijijini pale kwenye kaburi la Mama kumsalimia🙏🏾. Hata kabla ya kuondoka Bukoba nilienda tena pale alipolala mama.
Kipindi nimemaliza form 4 Aunt alinipa hela nikafungue Acc bank. Hivyo acc yangu ya kwanza ya Bank nilianza kuitumi 2010, ilikua CRDB.
Aunt wa Dar alinipigia na kuniuliza nini nahitaji ili viniwezeshe shuleni, Nilimwambia vitabu.
Niliondoka Bukoba kwenda Dar lakini aunt safari hii aliniruhusu nipite Mwanza kumsalimia Baba na alinipa siku 2 tu then niende Dar
Ilikua 2011 tayari na nilirudi Mwanza kwa mbwembwe sana, safari nzima nawaza namna ntamwona Crush wangu wa tangu utotoni.
Niliwasili Mwanza mapema tu na shughuli kubwa ilikua ni kutembelea marafiki zangu. Jioni yake nilionana na Crush wangu ( Clara tumwite hivyo) na tulikubalina siku nnayoondoka nikalale Lodge pale Nyegezi na yeye angetoka kwao ili tulale wote. Nami nilikubali ukizingatia nilikua na visent kwenye Acc yangu.
Mzee alifurahi sana na hakuna mkali tena hadi leo hii. Kesho mchana nilinunua simu mpya ya mchina nakumbuka niliweka ringtone nyimbo ya 20%.
Jioni nilijiandaa vyema na safari kwenda Nyegezi ikaanza, tulipanga kukutana na Clara maeneo ya Ghana then tuondoke wote na ilikua hivyo.
Nilimpend Clara ila Jane alikua mzuri sana. Basi tulipata Lodge pale Nyegezi na tukaenda kununua vyakula tukarudi ndani.
Clara alikua Bikra kabisaaa na hiyo siku ndo nilitoa usichana wake.
Alimia sana ila hatukua na namna maana alikua tayari kwa kile kilichokua kinaendelea.
Asubuhi niliondoka na Clara alisubiri hadi bus liondoke ndo akaondoka ila alikua na maumivu makali mno na hata tembea yake haikua kawaida.
Wakati niko njiani tulikua tukichat na alinijulisha kuwa anaumwa sana, amepata hadi homa. Nilimpa pole nyingi na kumwambia ajikaze home wasijue.
Kwa upande wa Jane baada ya kumaliza form 4 alienda Dar kwa mpenzi wake baadae akaenda mwanza kwa dada yake (niliambiwa na mwenzake) lakini taarifa niliyokuwa nayo wakati naenda Advance ni kuwa Jane tayari ana mimba kubwa tu.
TUTAENDELEA…..
Kama bado tuko active niandike epsode moja ya mwisho kwa leo
NB: This is my true story, sijacopy mahali… Nimeileta hapa maana huko mbeleni nahitaji ushauri wenu muhimu
hapa ni lufilyo boys kabisa mshkaji wangu sioSEHEMU YA SABA (7)
Tulipoishia…
Asubuhi niliondoka na Clara alisubiri hadi bus liondoke ndo akaondoka ila alikua na maumivu makali mno na hata tembea yake haikua kawaida.
Wakati niko njiani tulikua tukichat na alinijulisha kuwa anaumwa sana, amepata hadi homa. Nilimpa pole nyingi na kumwambia ajikaze home wasijue.
Kwa upande wa Jane baada ya kumaliza form 4 alienda Dar kwa mpenzi wake baadae akaenda mwanza kwa dada yake (niliambiwa na mwenzake) lakini taarifa niliyokuwa nayo wakati naenda Advance ni kuwa Jane tayari ana mimba kubwa tu.
Tunaendelea….
Nilifika dar majira ya saa tano usiku, na hii ndo ilikua mara yangu ya kwanza kuja Dar. Aunt alituma mtu aje kunipokea na joto ndo lilinipokea vizuri.
Aunt wa Dar ana maisha yake mazuri tu na sitotaka kuongelea chochote kuhusu maisha ya kwa Aunt ila kwa ufupi sana ni maisha poa na kila mtu na time zake, mtakutana jioni muda wa kuangalia habari na kula labda
Kesho yake kuna Dada yangu alinipeleka Mwenge na Kariakoo kununua vitu vya Shule. Nilikaa Dar kama siku 4 then safari ya Mbey ikaanza.
Wakati natoka Dar nilikua na kila kitu cha shuleni. Aunt wa Dar alininunulia ( aunt wa Dar tumwite B. Mkubwa ili kutofautisha na wa Bukoba)
Account yangu ya CRDB iliwekwa laki 2 na B. mkubwa kama Pocket money ya shule then nikapewa nauli na pesa ya kula njiani. Nilinunuliwa counter Book 12, vitabu 6 na kila hitaji nilipewa. Mzee mwanza pia alinipa hela ila nilikula bata yote nilivyofika Dar ikiwemo kununua nguo mpya.
Safari ya Mbeya ilikua safi tu na nilifika Mbeya Tukuyu majira ya saa nne na nusu hivi usiku. Wakati niko njiani kuna mbaba nilikaa nae alikua ni doctor huko Kyela na alitokea kunikubali sana na tulibadilishana namba.
Changamoto ilikuja pale nilipofika Tukuyu na kujikuta nimebaki na Cash kama elfu 17 tu. Sasa nikauliza bank iko wapi, Dreva tax alinijibu “huku hakuna CRDB, kuwa linakuja gari (Mobile Bank) sijui kama niko sahihi linavyoitwa. Hilo gari huwa linakuja siku ya jumatatu tu na linatoa huduma na kuondoka”. Asee nilichanganyikiwa na sikuwa na mwenyeji yoyote Mbeya kwa wakati huo. Niliomba dreva Tax anipeleke lodge yoyote ya bei ndogo. Jamaa alinifanyia uhuni, Lodge ilikua sehemu ya kutembea kwa dak 2 tu ila jamaa akanizungusha njia ya mbali na akanipela hapo Lodge nikampa buku 3. Pale Lodge nililipa elfu 10 nikalala huku nikiwaza asubuhi naendaje Mbeya mjini maana nilikua mgeni kabisa na mfukoni nna kama elfu 4 tu.
Niliamka asubuhi nikajiandaa then nikaenda mapokezi nikamwomba jamaa aniangalizie mizigo yangu.
Nilipanda costa za Tukuyu - Mbeya nauli ilikua buku 3 kama sikosei. Safari ikaanza nami macho yangu yote yalikua barabarani nikijisemea ntakapoona ATM ya CRDB basi nashukua.
Nilishuka Mwanjelwa pale baada ya kuona ATM then nikatoa pesa kama laki hivi. Nilinunua godoro, blanketi na koti jeusi. Ile shule tulikua tunavaa full black… Yani shati white, suruali black na koti Black… suit kabisa yani.
Nikarudi Tukuyu na kubeba vitu vyangu tayari kwenda shule. Yule dreva tax nilichukua namba yake na tulikuja kuwa washkaji baadae. Alinipeleka hadi stand ya kwenda huko ndani ndani (Mbambo, Itete hadi shuleni penyewe)
Sasa pake stand nilikutana na wanafunzi kibao wanaoenda shuleni ila cha kushangaza usafiri ulikua Canter na sio mabasi… Yani mnaning’inia huko juu kwenye canter.. wanawake ndo wanakaa chini. Asee niliishiwa nguvu baada ya kusikia hivyo.
Canter inajaza balaa na mizigo ni mingi mnoo kwani watu huja Tukuyu kununua mahitaji mengi na wengi ni wafanyabiashara kule kijijini.
Safari ilianza kama baada ya masaa mawili hivi na wanafunzi tulikua tunapiga story nyingi mnoo na swali kubwa ilikua ni kuulizana we umetokea wapi. Peke yangu ndo nilikua natoka Bukoba.
Ile safari ilikua ya mateso sana. Barabara ni vumbi, madaraja ya mbao alafu barabara ina milima na kona balaa (watu wa Mbeya hususani Tukuyu wananielewa vizuri hapa)
Ilikua Gari ikilalia upande wetu nasali sana maana ukiachia zile bomba ndo uko chini hivyo
Nilianza kujuta kwanini sikusoma Bukoba tu. Baada ya masaa matatu na nusu hivi tulifika shuleni… Asee nilihisi kuna kitu kimenikaba kooni kama nataka kulia kama nimebanwa (hii hali mnaijua wengi) kwa ufupi ningekua mtoto ningelia
Shule ilikua mwisho kabisa. Yani kata ya mwisho kabisaa baada ya hapo kuna Mlima Living stone so hakuna namna utaenda kokote.
Tulipokelewa shuleni tukaonyeshwa mabweni then tukaenda kula mtaani siku hiyo maana tulifika watu washapewa chakula cha jioni shuleni pale.
Nilifanikiwa kupata marafiki wengi na maisha ya kuishi mbali na wazazi yakaanza rasmi
Tuishie hapa kwa leo
See you kesho
Amina.Pole kwa kwa kupoteza mama..huwa naumia mama akifa akiacha wtt wadogo..Mungu atujalie afya njema tuwalee watt wetu..
[emoji23][emoji23][emoji23]Dogo ameshalewa kazima tena mda huu katundikiwa drip
Leta kwa summary acha upumbafu wakueleza kila takatakaSeHEMU YA TISA (9)
Tulipoishia…
Tabia ya kwenda porini ikakua na tukaanza kucheza kamali kule. Tulikua tukicheza kamali ya karata na dau nakumbuka lilikua 100 au siku nyingine 200. Ilikua pesa nyingi kwa maisha ya shule kwani ukipigwa kama elfu 3 hivi basi wiki nzima utakunywa uji mkavu…
Nikawa na ukaribu wa mdada flani (tumwite Tina) alikua mwanafunzi wa O-level… Asee kumbe yule dada kuna mwalimu anamtaka…. Hapa nikawa nimeyatimba
Tuendelee sasa…
Tina alinijuza kuwa kuna mwalimu huwa anamtaka sana na sasa ananiulizia.
Ngoja nipunguze maelezo naona watu wamesema hayana umuhimu
Huyu Tina alinipa msala, alikuja kupata mimba shuleni alafu kila mtu akawa anasema lazima mimba ni yangu. Tulikua form 6 tayari hapo na maisha ya kucheza kamali na kutoroka shule nilishayazoea
Nilishauza zile counterbook zote 12, nilibaki na moja tu la masomo yote. Niliuza vitu vyangu vingi mnoo
Katika yooote sikuacha kwenda kanisani jumapili. Na kuna mzee mmoja alikua na mwanae yuko form 4 pale shuleni. Yule mzee alinipenda sana, akawa kila jumapili lazima aniletee matunda pale kanisani, sikunyingine samaki au dagaa. Mzee alikua akinisisitiza nisome lakini mwanae pia asome kwani wana maisha duni na ni mtu pekee kwao walikua wakimtegemea (huyu dogo nilikuja kutana nae baada ya miaka 6 hivi mbele, pia story yake nimeiachia hapa)
*Kuna kipande muhimu sana cha dada kiongozi wa Dini haswaaa, nilijikuta kwenye mahusiano nae na hata nilivyoenda chuo bado nilikua nae. Huyu Dada nilimfanyia vitu vya ajabu sana kwakweli na niseme nilipoteza mtu muhimu basi tu. Ila sasa nikileta story yake watu watasema najizungusha story iwe ndefu.
Tuendelee kwa ufupi yule Tina alikuja gundulika ana mimba na mwenye mimba sio mimi, kuna jamaa flani alipewa msala huo. Maisha yakaendelea
Mtahani wa mock wa form 6 nilifeli tena… Nilipata 3 ya mwisho…
Kwa kipindi kilichobaki niliona nikomae na shule tu. NECTA ilifika nikafaulu na baadae nilichaguliwa kwenda SAUT Mwanza
TUENDELEE, NTASOMA MAONI YA WENGI KAMA TWENDE NA SUMMARY AU NIELEZE KWA KINA MATUKIO MUHIMU HADI NIMALIZE MKASA WANGU
ASANTENI
Huyu atakuwa ameyakanyaga mawaya.Muendelezo please sijapata picha bado wapi umeharibu maisha.
Pole moyo wakoEpisode ya kwanza imeniumiza Moyo wangu❤️🩹❤️🩹❤️🩹