Maisha yangu nimeyaharibu mwenyewe

Maisha yangu nimeyaharibu mwenyewe

SEHEMU YA 13

Tulipoishia….

Nilitambulishwa na shemeji yangu na mimi nikaishia kusema karibuni ndani.
Tulielekea room kwangu tukiwa jumla wanne, Mimi, Annabellah, rafiki yangu na mwanamke wake yaani shemeji.

Kama unavyojua room za wanafunzi hakunaga makochi (wengi wao). Tulikaa kwenye kapeti la manyoya pale chini tukawa na story nyingi huku tukitazama movie.

Baada kama ya nusu saa, rafiki yangu na girl wake wakasema wanatoka kidogo

Tuendelee sasa…

Nilibaki na Annabellah pale tukiangalia movie na story za hapa na pale, nilikua najaribu kumuuliza yuko Course gani na mwaka wa ngapi maana sikua namjua kabisa na sikuwahi kumwona kabla pale chuoni.

Annabellah alikua anasoma Certificate (kiukweli course yake siikumbuki vizuri) na alisema anakaa In-campus (Hostel za ndani ya chuo) na alisisitiza yeye sio mtu wa kutoka toka ndo maana sikua nikimjua.

Tulizungumza mengi pale kikubwa ilikua ni kufahamiana na baada kama ya lisaa hivi, rafiki yangu alirudi na girlfriend wake, kisha wakasema wanataka kurudi hostel kabla ya saa nne (hostel za ndani ilikua wanalimit muda wa kurudi)

Tuliwasindikiza kwa pamoja, nilipata muda mdogo wa kuzungumza na yule dada anayedate na rafiki yangu na mazungumzo yalikua hivi

Her: vipi unamwonaje rafiki yangu?
Me: Kwakweli ni mzuri sana na anaonekana hana mambo mengi
Her: Yea ni mzuri, we subiri mjuane vizuri utafurahi
Me: Usijali wala sina haraka

Basi baada ya mazungumzo hayo tuliagana na mimi nikarudi hostel nikiongozana na rafiki yangu. Tulikua tukuongea mambo mengi ila mi tayari akili yangu ilikua inawaza namna ambavyo ntakua mwenye bahati nikimpata Annabellah.

Kesho maisha yaliendelea kama kawaida, nilienda chuo kama kawaida na jioni nilipita kijiweni kucheza kamali kama kawaida (nilikua najificha sana kuhusu huu mchezo)

Hiyo wiki nayo Boom lilitoka, kama mnakumbuka hapo nyuma baada ya kuachana na Nelly niliingia kwenye “Friend for Benefit” na dada mmoja (tumwite Cutie)nilikua nasoma nae.
Hii siku nilikula beer zangu kadhaa kisha nikamtext “Kama uko free leo jioni tutoke” nae alinijibu fresh. Si unajua tena nilikua na jeuri ya Boom hivyo sikua na wasiwasi


Cutie alikua na mahusiano na jamaa flani ambaye tayari ana familia na sio mwanachuo. Jamaa ndo alikua sponsor wa Cutie kwa mambo mengi, cutie alikua anakaa kishua sana sababu ya Sponsor wake na tulipeana code ya kutotafutana kwenye simu jamaa akiwepo, so Cutie alikua ananitext “He’s coming today” hapo nilikua sitakiwi hata kujibu chochote kwani tayari tulishapeana code.

Huyu Cutie ni miongoni mwa wanawake wanajua ku-make love asee. Yani ilikua show show.

Basi usiku tulitoka na cutie tukaenda Club flani ilikua inaitwa Rock Bottom (sijui kwa sasa inaitwaje) ila ilikua kwenye lile jengo refu pale city center Mwanza.
Tulilewa sana hii siku na tulianza romance mule mule club. Tulikiss sana na kucheza sana.
Wakati yote yakiendelea mimi sikua najua kama kuna wanafunzi wenzetu mle ndani.

Mida ilisogea sana na wote tulikua tayari tumelewa na tulikua tunatamaniana tu, Cutie alikua horny tayari hivyo alisema leo tusirudi chuo. Tutalala mjini, kuhusu pa kulala nimwachie yeye.

Saa 11 asubuhi tuliondoka pale club tukaenda mtaa flan hapo hapo mjini, kulikua na ghorofa lina apartment kadhaa. Tulipanda hadi ghorofa ya 4 na tukaingia kwenye hiyo apartment. Cutie alikua na funguo ma sikujua pale ni kwa nani (hadi leo sijui pale ni kwa nani)
Ilikua apartment kali na iko full furnished. Sikujiuliza maswali mengi as long as alinihakikishia kuwa ni salama na nisiwe na wasiwasi.
Tuliishia kusex pale hadi jua linachomoza, ilikua siku nzuri sana maana ile show ya pale haikua ya kawaida. Cutie anajua mapenzi kwelikweli na hachoki, mostly mimi ndo nilikua nikichoka namwambia tupumzike.
Wakati wote huo nasex na Cutie sikuwahi kutumia condom.

Tuliamka mida ya saa saba mchana. Tukaoga kisha mi nilimwambia Cutie nataka kurudi chuo nae hakuwa na shida alisema mi nitangulie then yeye atapumzika hadi jioni ndo arudi chuo na alisisitiza amechoka sana.

Nilirudi chuo na nakumbuka wakati nashuka kwenye daladala pale chuo nilikutana na rafiki yake Annabellah, tulisalimiana kisha nikailiza kuhusu Annabellah, baadae nikamwambia yule dada amwambie Annabellah naomba namba yake (sikuwa nimechukua namba ya Annabellah siku ya kwanza)

Alinijibu sawa na tukaachana pale nikaenda zangu hostel kulala kwani nilikua na hangover plus kuchoka.
Jioni niliamka na kukuta sms yenye namba za simu kutoka kwa yule dada, nikajua tu Annabellah kakubali kunipa namba.

Nilimtext mambo nae hakuchelewa kujibu, tulichat kidogo kisha nikaomba kumwona tena kama hatojali, akanambia atakuja kwangu kesho jioni. Basi tukaachana hivyo

Moyo wangu ulikua na furaha na nilijisemea “Nikimpata huyu binti basi Nelly ataisoma namba”
Annabellah alikua mzuri sana kuliko Nelly, Nelly alikua haingii hata robo kwa mtoto yule wa kichaga. Kwa kifupi sikuwahi kuwa na mwanamke mzuri kama Annabellah pale chuoni.

Kesho jioni Annabellah alikuja hostel kwangu na alikua peke yake.
Nilishuka chini kumpokea kisha tukapandisha ngazi kuelekea room kwangu, njiani nilipishana na rafiki yangu flani na aliishia kusmile kwa ishara.
Tulipiga story sana na Annabellah na tulikua tunaangalia movie, hii siku nilijua kuwa alikua single. Nilimwambia natamani sana awe rafiki na mtu wa karibu kwangu na akasema hamna shida muda utazungumza.

Ilifika majira ya saa 3 usiku na aliomba kuondoka baada ya kupigiwa simu na rafiki yake kuwa wana birthday party. Wakati namsindikiza tulikutana ma yule dada rafiki yake Annabellah na alionyesha kama kumind hivi kwamba tumeanza kukutana bila yeye kujua.

Baada ya siku kama 4 hivi za mawasiliano mazuri na Annabellah basi alinikaribisha hostel kwake. Ilikua ni hapo hapo chuo karibu kabisa na viwanja vya Raila Odinga (waliosoma SAUT wanajua)
Siku hiyo nakumbuka nilitoka kwenye darasa la Tv nikaenda moja kwa moja kwake. Alinipokea kwa upendo sana na alikua na rafiki yake flani mule ndani (Room mate) na baada ya dak kama 20 yule dada alitoka na kutuacha wenyewe.
Hii ndo ilikua siku ya kwanza nakiss na Annabellah. Sikuamini kabisa kutokana ma uzuri wa yule binti. Tulikiss bila kutarajia kabisaa lakini baada ya lile tendo hata mazungumzo yakabadilika, tulikubaliana kuanza mahusiano siku hiyo.

Annabellah alinambia kuwa ana wivu sana hivyo niwe makini na moyo wake. Nikamwambia usijali mamie, we goona make a good couple.

Niliondoka pale kwake na furaha ya hali ya juu na nilijiona mwenye bahati sana. Ilibidi nimpe story nzima mshikaji wangu sana (Tumwite Fredy)
Huyu jamaa alitokea kuwa rafiki yangu sana nikiwa 3rd year na tulikua tunasoma course moja na tunakaa hostel moja ila kila mtu na room yake.
Alikua anapenda sana picha na mimi nilikua na camera so ilikua ni picha juu ya picha.

Nilimpa mkasa mzima Fredy na alifurahi sana kwani alikua anajua napitia wakati mgumu sana baada ya kuachana na Nelly.


Maisha ya chuo yaliendelea na nilikua napambana na Research na nilikua Tv room siku hii. Annabellah alinipigia na aliomba kuniona , ilikua ijumaa na nilimwambia sawa ntakuja kwako. Akasema anataka kuja kule kwangu, nikamwambia hamna shida.
Sasa nilivyokata simu tu kuna jamaa angu flan akanitania, mzee unaongea na simu hadi unalegea, nikamwambia eb angalia kwanza picha yake alafu nambie kwanini nisilegee kwa hiyu binti.
Nikamwonyesha picha jamaa, kumbe mwalimu wangu wa Tv production alikua kwa nyuma akaona ile picha.
Nilisikia tu sauti inasema, huyu si mdogo wangu Annabellah, umetoa wapi picha zake.
(Huyu Ticha alikua kijana kijana hivi)
Nilimjibu tu kuwa namjua na nikakatisha story na kuondoka eneo lile.

Usiku mida ya saa 2 Annabellah alipiga simu na akanambia amefika pale hostel kwangu. Mimi nilikua ndani, nilishafanya usafi na kuweka mazingira vizuri kabisaaa.
Nilishuka kumpokea na this time alikuja na mkoba flani hivi ambao nilimpokea na kuubeba mimi.

Tulipofika room nilimuiliza kama atakunywa chochote akasema hapana. Tuliangalia movie pale huku story za mahusiano zikinoga, utani mwingi na tulijikuta tumeanza romance pale pale.
Kwakweli sikuweza kuvumilia tena nilijikuta natoa nguo yake moja baada ya nyingine, japo alinikazia mwanzoni.

Annabellah alikua mzuri sana asee, ile shape yake isiyoumiza niliishuhudia live akiwa amebaki na nguo ya ndanj peke yake. Alikua msafi yule dada asee.
Hii siku ndo mara ya kwanza tulisex na ilikua sex ya slow isiyo na fujo ila ndefu sana.
Ilikua ni miongoni mwa siku nilikua na furaha na Annabellah alisema ananipenda sana na alianza kunifahamu hata kabla hatujaonana (alikua amenifollow instagram) niligundua alikua na picha zangu kadhaa kwenye simu yake ambazo alizitoa instagram.


Ilikua mida ya saa 4 hivi usiku wote tukiwa tumechoka na nilikua nahisi njaa, nikamwambia ngoja nikanunue msosi nakuja. Annabellah alisema ngoja nioge na mimi twende wote. Moyoni nikawa najisemea, huko mtaani watakoma, nilikua navimba sababu ya uzuri wa Anna.

Tulienda kununua msosi na Annabellah na kiukweli nilikua ma confidence sana, Annabellah alikua romantic hata njiani, mtu angetuona tu hakua na haja ya kuuliza kama sisi ni wapenzi.
Nilipishana na rafiki yangu flani njiani wakati tunaenda kununua Msosi na jamaa nilimtambulisha kuwa yule ni shemeji yake, akaishia kusema hongereni sana (huyu jamaa alikua akinisema na kunicheka wakati nimeachwa na Nelly)

Tulinunua msosi na kurudi ndani,na hii siku Annabellah alilala kwangu. Usiku tulipiga show moja tena ya maana kisha tukalala.


NITAENDELEA
Oya mbona hujamalizia story
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom