Maisha yanaenda kasi, kweli timu ya Simba ni yakuzomewa kutoka Mtwara hadi Dar?

Hakuna jipya. Hao viongozi watamleta Manzoki au Adebayor kwenye mkutano wa wanachama halafu watashangiliwa.
  • Kocha wa Wydad katimuliwa kwa sababu tu kaingia nusu fainali kwa taabu sana
  • Kiongozi wa Raja kajiuzulu kwa sababu wameshindwa kuingia nusu fainali.

Kwa Simba kufanya vibaya msimu wa pili mfululizo bila kombe lolote nani kajiuzulu/kawajibika mpaka sasa?
Bongo kujiudhuru ni ngumu
 
Nilimsikia msemaji wa Simba (Ahmedy Ally) akilalamika kuwa wamezomewa na mashabiki kutoka Mtwara mpaka Dar es Salaam.

Situation hiyo ilijitokeza baada ya Simba kuchezea kichapo cha mabao mawili kutoka kwa Zam FC, na hiyo ndiyo ilileta taharuki kwa mashabiki na kuanza kuzomea timu yao.


NALIA NGWENA nipo upande wa mashabiki wa Simba, naona wana haki kabisa ya kufanya hicho walichofanya japo kuwa bwana mdogo Ahmedy Ally aliona kama mashabiki walikosa nidhamu kuwazomea wachezaji la hasha! Mashabiki wanaonesha namna gani wanaumizwa/hawafurahishwi na kitendo cha kitendo timu kukosa hata kombe la kufutia jasho kabatini.

Hii ni kwa mashabiki wa timu yoyote ya mpira hapa Duniani, wanapoona timu yao haifanikiwi/kufikia malengo waliyoyapanga kwenye msimu ni lazima walalamike/wahoji ni kwa nini imekua hivyo?

NALIA NGWENA niliona na kusikia mashabiki Chelsea, Man U, PSG nk, wakipiga makelele nakudhinikiza viongozi ama benchi la ufundi livunjwe kwa kuwa tu timu inafanya vibaya.

Kelele za mashabiki wenye uchu ya makombe kabitini kwao, zikawe chachu/challenge kwa uongozi wa Simba SC na wajue nini kifanyike ili msimu ujao walete furaha kwa kwa mashabiki wao. Shabiki ni mchezaji wa kumi na mbili na ndiye anayechangia kwa kiasi kikubwa kununua bidhaa za timu pamoja na kuingia uwanjani hapo timu inapata kipato.

Kwa hiyo mashabiki kuzomea ni haki yao kabisa na wala siyo utovu wa nidhamu, bwana mdogo Ahmedy Ally usipoangalia/msipofanya mabadiliko na kuleta furaha kwa mashabiki basi utajikuta mtaani na kisipika chako peke yako.
 
Hiyo ndio tofauti ya simba na yanga, simba wakifungwa wanapambana wao kwa wao ila yanga wakifungwa utasikia tutaandamana hadi ikulu
 
Back
Top Bottom