kukumsela
JF-Expert Member
- Oct 13, 2018
- 721
- 907
Ameandika Ahmed Ally
===
Mara kadhaa utasikia shabiki anasema sisi tunaumia kuliko Wacheza ji au Viongozi.
Ndugu zangu ilimradi sote tuna damu ya Simba basi wote tunapitia maumivu, kinachotokea ni tofauti ya mtu na mtu kuhimili maumivu.
Ndo maana wengine wanalia, wengine wanazimia, Wengine wanashindwa kula, Wengine wanakasirika yote ni maumivu.
Leo tumezomewa kutoka Mtwara hadi Dar Es Salaaam hali ambayo nawaumiza zaidi wachezaji, hakuna mchezaji anaetaka kufungwa makusudi ili azomewe kuzomewa ni kitendo cha aibu sana.
Katika nyakati hizi ni vema kila mmoja akaheshimu maumivu ya mwenzie kwani hakuna anae jua mwenzie anaumia kiasi gani.
Tufanye yote lakini tuwaache viongozi wamalize kuugulia baada ya hapo wa je watutengenezee timu madhubuti kwa ajili ya msimu ujao.
Hakuna mtu anaekubali kuharibikiwa katika kazi yake, viongozi wetu wanapambana usiku na mchana kuhakikisha sisi mashabiki tunapata furaha.
Tuwaunge mkono kwenye kipindi hiki kigumu kwao kwani na wao wanaumia kama sisi na hawana mahala pa kupeleka lawama zao, lakini pia pamoja na kuumia kwao wanatakiwa warudi kazini kututengenezea Simba imara.