Maisha yamenishinda!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maisha yamenishinda!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by FUSO, Feb 23, 2011.

 1. F

  FUSO JF-Expert Member

  #1
  Feb 23, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,844
  Likes Received: 2,319
  Trophy Points: 280
  Wakuu Maisha ya Mjini yamenishinda, yaani nikiangalia kipato changu na majukumu niliyonayo naona siwezi kabisa.

  Maisha kama haya naona afadhali yale maisha niliishi kwa wazazi wangu enzi za mwalimu pamoja na kuwa babangu alikuwa mkulima lakini tulienda shule na tuliishi maisha mazuri.

  Mimi sijui wenzangu mnaishije? mnapata haya machungu nayoyaona mimi? nasimama asubuhi kituoni kwenda kazini naona magari yanapita tu huku mmefunga vioo hivi kweli mna matatizo kama yangu kweli? Hivi nyie pesa mnazipata wapi? mbona najiona mpweke katika nchi yangu hii?

  Wakuu siyo siri natafakari kama mambo yakizidi kuwa magumu basi nitafute nauli nirudi kwetu angalau huko nitakuwa na uhakika wa kusogeza siku.

  Kipato changu wakuu ni Tshs 542,000/- Nina Mke na mtoto mmoja (5), nimepanga nyumba viwili na sebure - Mambo yamegoma kabisa.

  Nipeni ushauri nateketea mtanzania mwenzenu.
   
 2. semango

  semango JF-Expert Member

  #2
  Feb 23, 2011
  Joined: Aug 24, 2010
  Messages: 532
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  daaaah!pole sana kaka ila umeuliza maswali ya msingi sana ambayo hata mimi nangoja majibu yake.wenzetu waseme wanafanya maujanja gani.
   
 3. mbuvu

  mbuvu Member

  #3
  Feb 23, 2011
  Joined: Jul 3, 2009
  Messages: 62
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Hicho ni kilio kwa wengi wanaotegemea mshahara maisha ni magumu sana kwa sasa.
   
 4. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #4
  Feb 23, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Nimelipenda bandiko lako kutokana na:
  -mpangilio wa maneno ..ni mzuri sana.
  -Ujumbe uliopo kwenye sentenso zako...ni murua na unafundisha.
  -Hitimisho la bandiko lako kinajieleza vizuri, kwamba unarudi kijijini!

  Lakini ngoja nikwambie, kama unaona kijijini mambo yatakuwa safi, kwanini umekaa mjini all those years?
  Fanya haraka urudi kijijini, lakini usiwe kama Dr Remmy ambaye aliimba anarudi SONGEA, ambapo hakuwahi kwenda huko daima!
   
 5. Elizaa

  Elizaa Senior Member

  #5
  Feb 23, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 160
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Inabidi pia mke wako naye atafute shughuli ya kufanya msaidiane, maisha ya sasa familia haiwezi kutegemea kipato cha mmoja.

  Hivi maisha yamependa sana naona hata wenye magari wengi wanatafuta wa kumuuzia

  maana hata mafuta na spare ziko juu sana
   
 6. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #6
  Feb 23, 2011
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,120
  Likes Received: 615
  Trophy Points: 280
  Hapo kazini hakuna chance ya kuiba? :usa2:
   
 7. L

  Leornado JF-Expert Member

  #7
  Feb 23, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,534
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Pole sana, jaribuni kubana matumizi sana, mwambie wife asione aibu ajaribu kutengeneza hata karanga, aisikrimu au maandazi aweke hapo dukani kwa mangi ili yeye awe ananunua msosi halafu wewe unadili na matumizi mengine.

  Muhimu, baneni matumizi acha kuchangia harusi, birthday nk.

  I feel ur pain, wengine hapa tunasomesha wadodo vyuo, bado wazee nyumbani yaani acha tu ndugu yangu tupo wengi wala hauko peke yako.
   
 8. Makindi N

  Makindi N JF-Expert Member

  #8
  Feb 23, 2011
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 1,068
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Unamfanyia kazi JK au?
   
 9. K

  Kitangawizi Member

  #9
  Feb 23, 2011
  Joined: Feb 18, 2011
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  we ucmfundishe mwenzio vibaya.
   
 10. Linamo

  Linamo JF-Expert Member

  #10
  Feb 23, 2011
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 9,060
  Likes Received: 21,275
  Trophy Points: 280
  Pole member!
  Umekosea sana kuwaza hali ya maisha haya tulio nayo!
  Jiweke kama mwendawazim utaona maisha yanaenda tu!
  Kumbe unawaza uishi maisha mazuri humu (....)
  Tangaza nawewe ni karumanzira ila dawa zako usihitaji pesa uwe unaomba kuku na vitu vingine. Hapo mambo yatapungua.
  Au urejee huko huko kijijini kwako.
  Pia ungetaja jina ya kijiji chako isiwe ni mjomba wangu bure!
   
 11. Seto

  Seto JF-Expert Member

  #11
  Feb 23, 2011
  Joined: Jan 15, 2011
  Messages: 961
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  ndugu yangu kwa mshahara tu bongo life haliendi hata siku moja, vyanzo vingine lazima viwepo...
   
 12. M

  Matarese JF-Expert Member

  #12
  Feb 23, 2011
  Joined: Aug 30, 2009
  Messages: 519
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Da mwanangu pole sana, ila tuko wengi, hata mm ni hivyo hivyo, yaani kama unafanya kazi serikalini na unategemea mshahara tu kwa kweli ni mateso na matatizo. Cha muhimu, kama alivyosema mdau, punguza bajeti usishindane na bei. Kama ulikuwa unakula nyama mara tatu kwa wiki sasa kula mara moja, acha kabisa biashara ya kuchangia harusi, ubarikio, kipaimara na kitchen parties. Ondoa kabisa safari za kutembelea mjomba, shangazi, binamu etc. Pia kwenye viti virefu punguza au ondoa kabisa. Ikiwezekana beba msosi unaowezekana toka home ule mchana. Nunua pasi ya mkaa ili kusevu luku yako. Kwa ufupi bana bajeti kila angle, usijaribu kushindana na bei.
   
 13. roselyne1

  roselyne1 JF-Expert Member

  #13
  Feb 23, 2011
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  pole sana,jitahidi usave pesa kidogo umfungulie mkeo biashara ya kufanya..mie sikushauri urudi kijijini,mnh huko ndio utakuwa frustrated zaidi nahisi...
   
 14. P

  Pokola JF-Expert Member

  #14
  Feb 23, 2011
  Joined: Jul 16, 2010
  Messages: 717
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  The best years of your life are the ones in which you decide your problems are your own. You don't blame them on your mother, the ecology, or the president [not in Tanzania]. You realize that you control your destiny!

  Kaka, pole sana. Tunaoendesha vimutukari usidhani tuna raha. Yaani vinatuzeesha kwa jinsi vinavyotafuna kila senti, na pia usifikiri kuwa na gari ndiyo mafanikio. Jitokeze tuulaani mfumo. Maandamano makubwa yanakuja. Kwanza Mwanza, subiri tupulize kipenga!! But in the mean time, jibane sana, wacha ulimwengu ukuite bahili, but potelea mbali. USICHANGIE HARUSI, K.PARTIES, na UJINGA WA NAMNA HIYO.
   
 15. m

  mamakunda JF-Expert Member

  #15
  Feb 23, 2011
  Joined: Jul 4, 2010
  Messages: 371
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mbona wewe mshahara wako ni mkubwa sana? wenzako tunapata ndogo zaidi ya hiyo, kinachotakiwa tu ni kuchakalika baba na mama, hata maandazi mama auze tu kwani kuna shida gani bwana.
   
 16. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #16
  Feb 23, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Huku kijijini na mimi maisha yananishinda.
  Nataka niuze mahindi nije mjini, mjini kuna nyumba nzuri na magari. Nasikia magari madogo ila yanakimbia hayo. Yakikua makubwa ndio yanazidi kukimbia. Nikiyaona nitahamasika kutafuta vyangu.
  Huku kijijini tunacheza na ngedere tu.
   
 17. M

  Mandago JF-Expert Member

  #17
  Feb 23, 2011
  Joined: Feb 8, 2008
  Messages: 238
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 45
  Pole ndugu yangu,

  Jitahidi zaidi kufanya kazi na mwombe Mungu akupe riziki zaidi Inshallah atakubali dua yako,

  Na mimi nakuombea Mungu akupe riziki zaidi na akupe furaha nyingi wewe pamoja na familia yako, Amin.

  Mimi nitakupa siri ya maisha ya furaha, siri ni hii.

  Daima ridhika na yale uliyo pewa na Mungu lakini endelea kuchapa kazi, yote yalio baki mwachie Mungu.

  Hakuna furaha kubwa kuliko kuridhika.
   
 18. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #18
  Feb 23, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Tafuta vyanzo vingine vya pesa.
   
 19. BLUE BALAA

  BLUE BALAA JF-Expert Member

  #19
  Feb 23, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 899
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Kwa kipato cha shs 542,000 hutakiwi kulalamika. Kuna watanzania kama 85% ambao wanapata 1/4 ya unachopata (135,000) na wanaishi na familia zao watoto wa3 and above na bado utakuta ana kibanda chake Charambe, Kongowe, Kitunda au Kipate.

  Wewe una mke na mtoto mmoja na unatumia daladala unalalamika nini. Nakushauri kuwa na vipaumbele, acha makundi ya starehe kama ulevi. uzinzi then hicho kipato kinaweza kukutoa. Hebu tufanye mchanganuo hapa chini.

  Tshs 542,000/=

  1. Kodi ya nyumba shs 100,000
  2. Chakula nyumbani shs 150,000
  3. Chakula kazini shs 60,000
  4. Nauli ya dala dala 30,000
  5. Mengineyo shs 100,000

  Jumla ya matumizi ni shs 440,000 hivyo unabaki na akiba ya 102,000. Ukitunza hii akiba kwa miezi sita unaweza ukampatie mke wake mtaji wa shs 612,000 baada ya miezi sita na mkaanza mkakati wa kununu ka plot Gongolamboto.

  Chukua huo ushauri na usirudi kijijini utajuta.
   
 20. F

  Future Bishop Member

  #20
  Feb 23, 2011
  Joined: Dec 4, 2009
  Messages: 75
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  FUSO, Nakubaliana na wewe kwamba mshahara wa laki tano haukidhi mahitaji muhimu kwa hali ya sasa ya maisha yalipoTanzania. Lakini sikubaliani na wewe kwamba ufumbuzi wake ni kwenda kijijini ukifikiri kwamba huko ndiko maisha yatakuwa nafuu. Kama wenzangu walivyosema wapo watanzania wengi (naamini zaidi ya asilimia 50) ambao wanapata chini ya kiwango unachopata na bado wanaishi mjini.

  Ukifanya utafiti wa je wanawezaje kuishi mjini na vipato hivyo vidogo utagundua kuwa wapo walio na njia zingine mbadala za kuwaingizia fedha (halali na haramu) na wengine wanaamua kuishi kulingana na kipato wanachopata.

  Uzoefu wangu unanionyesha kwamba hakuna siku utapata kipato/mshahara utakaokutimizia mambo yote/mipango yote unayotaka kwa wakati huo. Kinachotakiwa ni kujitahidi kuishi kulingana na kipato chako kwa kuweka vipaumbele vitakavyokuletea maendeleo huku ukiepuka matumizi yasiyo ya lazima/anasa. Najua kwa kufanya hivyo unaweza usipendwe na jamii inayokuzunguka kwani itakulazimu kupunguza michango ya arusi/ubarikio/birth day n.k. Sambamba na hili unapaswa kujitahidi kutafuta njia mbalimbali za kuingiza kipato, usikubali mtu akakaa kwako hata kama ni mkeo/mmeo , au ndugu, rafiki akawa anashinda nyumbani kwenye kochi/sofa akiangalia TV na huku akisubiri saa ya kula chakula. Kwenye hili lazima useme hapana na mtu awe tayari kufanya kazi yoyote ya halali ili mradi mwisho wa siku analeta kilo ya sukari nyumbani. Biblia inasema "ASIYEFANYA KAZI NA ASILE".

  Jambo lingine, nakushuri usitamani kuishi, kula au kuvaa kutokana na jirani/rafiki/mfanyakazi mwenzako anavyoishi, kula and kuvaa wakati vipato vinatofautiana. Ishi kulingana na kipato chako (Live within your means). Endelea kuwa maono ya kuwa na hatua nyingine zaidi na fanyia kazi maono yako lakini maono hayajatimia ishi ndani uwezo wako.

  Barikiwa.
   
Loading...